mdau njili mwakoba wa kasulu katuletea hii tukumbuke tulikotoka na tunakoenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Bro' michu hiyo haijatulia kabisa na huyo aliyekuletea mwambie atuombe samahani. Ana maana gani kuleta jisia kwamba bado siye hatujamaliza evolution. Hicho kikaragosi cha mwisho kinaonyesha ni kizungu.Acheni hizo washkaji

    mdau

    ReplyDelete
  2. Haya mambo ya evolution of man sio wote tunaamini mi nilizaliwa binadam hivihivi na vizazi vyangu vyote sijawahi kuambiwa na wazee kwamba nilikuwa na babu au bibi nyani...sijapitia hayo hebu pelekeni hukooooooooo, huyo jamaa lazima ni crew wa makumbusho tu..mwambie afungue bongo lake hii karne nyingine hatupo kale tena...

    ReplyDelete
  3. Na mbona bado kuna manyani, sokwe kima,mbega, ngedere nk.........hii nayo imekaaje, msifuate tu falsafa za wazungu mnafanywa wajinga nyie nia yao mjione nyie weusi sio binadamu, hebu angali hapo wa kwanza shoto ni mweusi anefuata afadhali kidogo then mpaka wa mwisho kulia ni white mi siikubali hii noooooooo.

    ReplyDelete
  4. Evolution ina ukweli na uzushi kibao.

    Myenyezi Mungu kamsifu binaadamu kwa umbo alilomuumba sasa vipi mutadai tulikuwa masokwe!!

    ReplyDelete
  5. Huyo wa kwanza kulia ni mzungu,akifuatiwa na mhindi na wa mwisho yaani kushota ndio mnyaturu mwenzangu!!!

    ReplyDelete
  6. EHE! Sokwe kageuka MZUNGU!

    ReplyDelete
  7. maana yake wote tunaelekea kuwa wazungu... DISASTER!!! maana ni huko nd'o unakuta "serial killers", "pedophiles", "road rage" na mengine mengi tu. lakini huku kwetu ni ma- "rapist", "abusers" na ma-"wife beaters" tu! kwa hiyo maendeleo yako afrika na tusidanganyike!

    ReplyDelete
  8. alama za nyakati zinaonyesha tunarudi mwanzo hasa kwa ufisadi huu ulivyoota mizizi.

    ReplyDelete
  9. hivi wadau nani alipiga hizo picha au ni imagination tu.Hiyo camera ni kodak,sony au yashika.Naamini kamera hazikuwa zimegundulika.Na kama hiyo ndo evolution whats the next step tutakuwa tunapaa labda kama ndege.

    ReplyDelete
  10. Michu nimefurahi kuona michango yangu umeiweka katika blogu.Leo huyu jamaa amenikumbusha mbali sana na hii picha inayoonesha evolusheni.Kanirudisha shule ya msingi(Histiria),
    Sasa kwa wadau,naomba jibu;
    KWA NINI MASOKWE WA SASA WASIENDELEE KUGEUKA NA KUIJAZA NCHI?

    Mchangiaji,
    Mbeya-Ileje

    ReplyDelete
  11. Ina maana binadamu wa kwanza alikuwa mwafrica?akafuata mzungu?uzushi huo..BINADAMU WA KWANZA ALIKUWA ADAMU NA HAWA...HUO NI UONGO NA UZUSHI..SASA NANI ALIWA ZAA HAO MANYANI?

    ReplyDelete
  12. Bro michu
    u\huu ndio utawala bora!wa kwanza JK,DR ShE,Uncle Mize,Ramadhan Wasso wa watani wa jadi na mzee wa vekeshen Michu

    ReplyDelete
  13. Muwe wakubwa na werevu jamani!
    Hivi nani aliwaamba kuwa watu weusi wako Afrika tu? Ona sasa mmeanza kujifananisha na huyo Nyani, mimi simo. Fananeni wenyewe na huyo Nyani. Mh! Kizazi cha Nyoka.
    Haya, na huyo wa mbele mzungu. Wazungu tu ndio weupe? Hakuna taifa lingine lenye watu weupe? Kazi mnayo.

    ReplyDelete
  14. Jamani eeh, hii ni "Darwin's THEORY". It is a "theory". It is NOT a "FACT".

    Ukiumizwa kichwa na vitu kama hivi basi umetaka mwenyewe.

    ReplyDelete
  15. Sasa Michu kwa alio weusi una maanisha witukuu vyetu vitapauka vije viwe viko waiti kama watasha?

    ReplyDelete
  16. wewe ukubali usikubali bibi na babu zetu walianzia hali hiyo.kama mnaamini kuwa mwanadamu wa kwanza alikuwa ADAMU NA HAWA kutokana na biblia mbona hii unaona vigumu kuubali?hujui hata hao wazungu wako walikuja na utamaduni wao na ukabebewa akili na kuwakubali mpaka leo?kubalini ukweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...