Kaka Michu!


Pole na shughuli za kila siku na tunakushuru pia kwa kuweza kutuburudisha na kutuelimisha Watanzania kwa ujumla walio nyumbani na wa ng'ambo pia.Katika pitapita zangu nilikutana na hii kalenda ya mwaka 2008 ya World Travel na kwenye picha ya mwezi wa pili ikiwa na picha ya Mlima Kilimanjaro na Twiga kwa mbele ikiwa na maelezo ' Mt.Kilimanjaro, Kenya ' hayakuwa madogo nilishikwa na uchungu sana na kuinunua ile kalenda na kwenda mojamoja kuwaandikia email hawa wachapishaji na kuwataka kuwaomba Watanzania msamaha kwa walichokifanya ni mpaka leo sijapata majibu sasa nataka iwe kampeni kwa wana blogu wote kuwaandikia hawa jamaa emails na kuwaonyesha umuhimu wa kosa walillolifanya si dogo kama wanavyofikiria wao, pia ninafanya jitihada niweze kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania hapa Ukerewe nione kama lolote wanaweza kulifanya juu ya hili. Hii kalenda World Travel 2008 imechapishwa na COMDA, The Calendar People branch ya Canada na picha hii walipewa au waliipata hapa sina uhakika kutoka Gallo-Travel Library kwani kuna sifa za pongezi kwa kupata picha kutoka kwao, na chini ya picha hii pia kuna maelezo mengine marefu tu yakielezea mlima huu na sifa kemkem kwa mahasimu wetu kama vile Mt.Kenya (Africa's highest mountain). Nimeambatanisha na picha wadau wapate kuona nini kinaendelea mpaka sasa yaani mwaka huu wa 2008 lakini bado watani wa jadi wanafunga goli kwa mkono. Mdau Ukerwe hapa naomba email yangu iwe kapuni tu.


Asante sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 53 mpaka sasa

  1. Lol watu wakiambiwa hawa jamaa wanatumia nyezo zetu hawataki kuamini haya ona sasa ndio wanachofanya hapa kila siku kazi kwenu wanaharakati

    ReplyDelete
  2. Acheni kuwaonea hiyo picha haisemi Mt Kilimanjaro iko Kenya. Imeandika tu Neno Kenya mbele ya Mt Kilimanjaro.

    ReplyDelete
  3. Sema sasa tuandike wapi, anwani yao iko wapi? Juzi jamaa katueleza kuwa Zanzibar imeoneshwa kwenye habari kana kwamba iko Kenya lakini wapuuzi kibao wakaja juu, bora wewe umetuwekea ushahidi mzuri zaidi, ile ilihitaji bongo kufikiri tukashindwa. Tupatie tuanze kazi.

    ReplyDelete
  4. Tuko na wewe, katika hili haya ndio mambo ya kupigania kuhusu nchi yetu. Hapo ubalozini uliza kama kuna wanasheria ili litazamwe kisheria zaidi, safari hii nafikiri hata kwenye mahakama za kimataifa wapelekwe. Tumechoka na wizi wa wazi wazi usio na haya. Kama kuna mahali pa kusaini ili kuprotest tupe link tutasaini na kuwaforwadia wengine nao ili huu mwaka ndio uwe mwisho wao kufanya hayo madudu yao. Hali hiyo wanatuibia hata hatujaingia hiyo Jumuiya ya Africa Mashariki, tukishaingia si ndio watatumeza kibasa!

    Swali kwa wakenya, hivi nchi yenu haiuziki kwa vitu vya kwenu?

    Unajua kuna siku hawa watakuja kusema kuwa Mlima huo ni sehemu ya nchi yao, mjinga mmoja kwenye You tube alisema eti mlima ni wa Kenya, watanzania wanaung'angania. Hivi wangekuwa na uwezo wa kuuvuta wangeuvutia ukaenda kwao lakini ndio hivyo hola hauvutiki kama kapeti

    ReplyDelete
  5. inauma sana.ila mimi nilikuwa na wazo lingine siku ya siku watalii wanakuja kugundua mlima uko Tanzania kwa jinsi tunavyojitangaza.ombi langu kwa serikali kama wangeweza kufanya tangazo lingine tofauti na lile tumezoea kuliona cnn kila siku.waweke chachandu kidogo..si mnayaona matangazo ya sandals jamani!ukiona tangazo tu unasikia roho imesuhuzika.ushauri tu.

    ReplyDelete
  6. Nakupongeza sana ndugu yangu kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu. Mimi binfsi nipo nje ya tanzania (ulaya) lakini watu wengi ninaongea nao wanasema mlima kilimanjaro upo Kenya, nami naumia sana ingawa najaribu kuwaeleza ukweli. Kitu cha muhimu ni kwamba kila mtanzania popote alipo awe wakala wa nchi yake ili tuweze kunufaika na rasilimali zetu. Pia naishauri serikali ya Tz kufunga njia zote za kuelekea mlima kilimanjaro kwa kupitia kenya (kama bado hawajafanya hivyo)ili watalii wanaotaka kutembelea huu mlima wapitie njia zilizopo tanzania,hii itasaidia nchi kujulikana na kunufaisha watanzani badala ya wakenya.Pia balozi zetu ziingie mikataba na wanfanya biashara ya utalii waliopo nje ili watusaidie kuitangaza nchi yetu. Tuipiganie nchi yetu ili tuweze kufaidi urithi tulioachiwa: TANZANIA NI KWA WATANZANIA.......ITUNZE ILI IKUTUNZE.....ITANGAZE ILI IKUTANGAZE.

    ReplyDelete
  7. To resolve such issues, someone try to get a hold of responsible authorities to answer questions as why legal actions are not taken:

    The people to contact are, the Minister of Natural Resources and Tourism Ms. Shamsa Mwangunga tel. #s +255 754 278915/+255 784 278915 OR the Attorney General Mr. Johnson Mwanyika tel # +255 713 324854

    ReplyDelete
  8. Wao wamesema mlima Kilimanjaro uko Kenya, lakini kwani wameuhamishia huko? Si bado uko Tz? Sasa kama ninyi mnasema mlima huo uko Tz prove it! Au kama mnasema hauko Kenya, prove it! Wao wanawaambia wateja wao kuwa waende Kenya kupanda mlima Kilimanjaro, na kweli wakienda Kenya wanapata nafasi ya kupanda mlima huo, sasa mnadhani watalii watasimuliana nini? Mlima hawajauhamisha, uko palepale, wao wametumia elimu yao ya publicity vizuri na wamefanya biashara. Kama na waTz wanataka kufanya biashara waache kupayuka tu ooh mlima uko kwetu sijui nini, ndio kweli mlima uko Tz, onesheni hivyo kwa vitendo na biashara makini sio tu kuendekeza maneno miiiiiingi!!!

    ReplyDelete
  9. Tunaomba email ya hao watengenezaji tuwatumie emails nyingi mpaka warekebishe.

    Hawa jamaa walianza kutuibia miaka ya 70 hadi mipaka ya park kati ya amboseli nr kenya na mt kilimanjaro tz na masai mara nr kenya na serengeti national park ikafungwa hivyo hata sasa wanapotangaza sio mbaya coz lazima mgeni akitoka kenya atachukuliwa na kampuni ya tz au watapitia kwenye mipaka official na mgeni atajua kuwa anaingia tz.

    Tatizo letu wabongo hata kwenye trade fairs hatupeleki watu Pro. tunapeleka watu tunaowajua amabao hawajui chochote kuhusu utalii wala national parks wala hawana idea na wildlife knowledge. wako thousands of professional tour guides lakini hawatumiki ipasavyo.

    swala la hiyo picha imepigwa amboseli nr kenya ukikaa amboseli unauona mlima kili vizuri kuliko upande wowote wa tz

    ReplyDelete
  10. JAMANI WATANZANIA, NI KWELI MLIMA KILIMANJARO UPO TZ, ILA NI VIZURI TUKAFAHAMU KWAMBA SEHEMU AMBAYO UNAWEZA UKAPIGA PICHA NZURI ZA WANYAMA PORI NA MLIMA KILI. AT THE BACKGROUND NI AMBOSELI NATIONAL PARK, AMBAYO IPO KENYA KWA HIYO HIYO PICHA ILIPIGWA KENYA NA UKIWA KENYA MLIMA UNAUONA VIZURI KABISA....NIMEWAHI KUFIKA AMBOSELI N.P. NA KINAPA (KILIMANJARO NATIONAL PARK) NI VIGUMU KUPATA PICHA KAMA HIYO UKIWA KINAPA.KWA HIYO WALIVYOANDIKA KILIMANJARO, KENYA..SIDHANI KAMA NI TATIZO KWANI HIYO PICHA ILICHUKULIWA KENYA..., KAMA WATANZANIA TUNA HASIRA SANA, BASI TUKAWEKE PAZIA KUBWA PALE MLIMANI ILI USIONEKANE KENYA!!!!!! by mtanzania muelewa!!!!

    ReplyDelete
  11. Ni uzalendo mzuri sana,sasa anwani yao iko wapi?

    ReplyDelete
  12. Hivi wewe anony wa pili una akili kweli? au wewe ni mkenya nini, naona hata akili za kufikiria huna, picha imeandikwa kabisa Mount Kilimanjaro Kenya au unataka waandike kabisa Mount Kilimanjaro iko Kenya? hebu kuwa mtu mzima bwana, hawa watani zetu wameshatunyonya sana na malizetu, niliona mahali pia wameandika ukija Kenya pia unawaona wanyama wote wa Serengeti, hawa sasa ni kuwakomalia, mdau uliyetuma post hiyo naomba tuandikie website au email za hao watu tuwakomeshe, wasituchezee kabisa, watanzania wa sasa sio wale wa zamani waliokuwa wanaonewa, Iam sure tukiwakomalia sana wanaweza mpaka kulipa fidia.
    pumbafu kabisa. Shime shime shime wadau tuungane katika hili

    ReplyDelete
  13. Yaani haya Makenya Ni majizi ya siku nyingi sana ya rasilimali zetu,hayo ndio mambo ya kuchangia mada michuzi sie wakina manka mushi wanatafuta waumme kwenye blog!!jamani tuchangie naomba email yao dada..asante sana kwa kutuletea mada nzuri

    ReplyDelete
  14. Hata Mombasa na Masai Mara ni mali ya Tanzania,tumeamua kuwaachia tuu..

    ReplyDelete
  15. Yaani ninahasira...nipe email ya hao jamaa haraka sana.

    ReplyDelete
  16. MLIMA WENU SEMA HAMJUI THAMANI YAKE HATA KIDOGO.JUZI TU HAPA JK NDIO KAANZA KUTANGAZA NCHI KWA UMBALI ZAIDI.WATANZANIA TUNAONGOZWA NA MAMBUMBU WASIOJUWA JINSI GANI KUWEZA KUINGIZIA TAIFA MAPATO ZAIDI YA MISAADA NA MADENI YASIOKUWA NA KICHWA WALA MGUU .MBAYA ZAIDI HIO MISAADA NA WAO WANACHOTA KWA MAMBO YAO BINAFSI.WAKENYA WAO KESI NDOGO HIO WANAWEZA KUWAAMBIA WATTALII HIVYO NI JINSI YA MLIMA WA KILIMANJARO UNAVYOONEKANA KWA UPANDE WAKENYA KITU AMBACHO KWELI MTALII AKIWA KENYA ANAONA MLIMA WA KILIMANJARO VIZURI TU NA KURIZIKA/.HUWEZI UKAJENGA UWANJA WA MPIRA KARIBU NA GOLOFA UKAMKATAZA MWENYE GOLOFA ASICHAJI WATU KUKAA GOLOFANI KWAKE KUANGALIA MPIRA UWANJANI KWAKO KWANI KILA MTU ANAMILIKI CHAKE.iTUNATAKIWA KUWASHUKURU KWA~KUUTANGAZA KWANI MTALII AKIAMUA KUTAKA KUUPANDA ATAKUJA TANZANIA/ PEPO YA UJINGA IMETUNASA~VIBAYA KICHWANI/

    ReplyDelete
  17. Nipo nje ya nchi jamaa kibao wasema Mt Kilimanjaro ipo Kenya, hata mnyarwanda ninae ishi nae hapa aliniambia amekua akijua hivyo. Kwa nini iwe hivyo? Mimi ninafikiri tatizo ni kwamba viongozi wetu wapo kimya na hata wahusika katika mamabo ya utalii hawautangazi sana.

    Sis wote tunaweza kuungana na kuutngaza mlima wetu. Nina furahi nimeelimisha jamaa kibao hapa,

    ReplyDelete
  18. Anon wa 9:45pm nakuunga mkono, kwani kutoka Kenya kuna barabara zinazokwenda mpaka Kilimanjaro hata kule Serengeti ipo barabara nzuri tu kutoka Nairobi-Masai Mara na Serengeti ambayo ilifunguliwa kwenye miaka ya karibuni na hii inawapa watani wenu kuimarisha utalii kwa rasilimali zetu...kitu cha kushangaza kuna jamaa walikuja kutalii Tanzania kupitia Dar na walitaka kwenda Mikumi na jamaa wa TTC pale mtaa wa Samora wakadai hawana magari ya kuwapeleka watalii mbugani labda wakodi ya kwao...wakati serikali ina magari mengi kwa wabunge yamejaa Dar...jamaa wakaruka mpaka Nairobi wakadai huku ndiko kuna facilities zote...sasa utamlaumu nani ikiwa njia rahisi zipo za kwenda mbugani bila usumbufu...inabidi serikali mbali na kutangaza utalii kwetu pia waweke facilities za kufika huko...story ndefu nimeikatisha tu nasikitika kuona Tanzania tunajiangusha hivi hivi tu...

    ReplyDelete
  19. MLIMA WENU SEMA HAMJUI THAMANI YAKE HATA KIDOGO.JUZI TU HAPA JK NDIO KAANZA KUTANGAZA NCHI KWA UMBALI ZAIDI.WATANZANIA TUNAONGOZWA NA MAMBUMBU WASIOJUWA JINSI GANI KUWEZA KUINGIZIA TAIFA MAPATO ZAIDI YA MISAADA NA MADENI YASIOKUWA NA KICHWA WALA MGUU .MBAYA ZAIDI HIO MISAADA NA WAO WANACHOTA KWA MAMBO YAO BINAFSI.WAKENYA WAO KESI NDOGO HIO WANAWEZA KUWAAMBIA WATTALII HIVYO NI JINSI YA MLIMA WA KILIMANJARO UNAVYOONEKANA KWA UPANDE WAKENYA KITU AMBACHO KWELI MTALII AKIWA KENYA ANAONA MLIMA WA KILIMANJARO VIZURI TU NA KURIZIKA/.HUWEZI UKAJENGA UWANJA WA MPIRA KARIBU NA GOLOFA UKAMKATAZA MWENYE GOLOFA ASICHAJI WATU KUKAA GOLOFANI KWAKE KUANGALIA MPIRA UWANJANI KWAKO KWANI KILA MTU ANAMILIKI CHAKE.iTUNATAKIWA KUWASHUKURU KWA~KUUTANGAZA KWANI MTALII AKIAMUA KUTAKA KUUPANDA ATAKUJA TANZANIA/ PEPO YA UJINGA IMETUNASA~VIBAYA KICHWANI/ na mdau wa 9 14 pm nakuunga mkono kwa maneno yako "ITANGAZE HILI IKUTANGAZE"

    ReplyDelete
  20. we anon wa wednesday 9:01pm hivi hujui kusoma wewe!!!! Au wewe taahira tu, mtu mzima!!
    Wakenya ni wezi sana kila kitu kizuri ni cha kwao at any cost. Hiki kitendo ni cha kukemewa sana, mbaya kuliko yote ni pale baathi ya watanzania wakiangalia na kuwatetea hawa wakenya kwa kitendo hiki.

    ReplyDelete
  21. TATIZO HAPA NI KWAMBA WATANZANIA TUNAWAFAGILIA SANA WAZUNGU .
    DAWA NI MOJA TU . WAZUNGU WAKITAKA KUINGIA TANZANIA KUOTOKEA KENYA WACHARGE BEI MRA MBILI YA ALIYEINGILA TANZANIA, WATAENDA KUWAAMBIA NDUGU ZAO .

    ReplyDelete
  22. NYANGAU!!!hata mlima wetu wanataka kutuibia!

    ReplyDelete
  23. TUNAUBADILISHA JINA SASA UTAITWA mt.tanzania ILI KUWAFUNGA GOLI HAO WANAOFANYA UJANGILI WA WAZIWAZI.WOTE WANAOUNGA MKONO KUBADILISHA JINA LA MLIMA HUO TUWASILIANE KWA KUTUMIA ANWANI IFUATAYO cliffmuga@gmail.com NIPO LADHI KUWA- WAKILISHA KWA GHARAMA YOYOTE.NDIMI MWENYE UCHUNGU NA NCHI.

    ReplyDelete
  24. Jamani hiyo ni view ya mlima kilimanjaro ukiwa kenya,sasa waandikeje kama imepigiwa kenya? ila sometimes hawa jamaa wanatuzidi,niliona magazine ya board ya tuarist ya kenya inasema"Mt kilimanjaro upo Tanzania ila unaonekana vizuri zaid ukiwa kenya"

    ReplyDelete
  25. Sasa weye anon number 2 mwenzako kachukuwa muda wake kutuma hiyo picha na maelezo kibao ili tu uweze kuelewa lakini hujaelewa !!

    Inasikitisha sana wajua kama huna cha kuchangia ni bora ukae kimya lakini watu nakujudge kutokana na mawazo yako na uelewa wako wa jambo.

    Huyo bwana/mke kafanya hivyo kutokana na uchungu wa nchi yake lakini weye waonekana uko ktk kukejeli !! lakini siwezi kukulaumu labda ELIMU haijakaa sawa

    Unaposema acheni kuwaonea... wakina nani ?? na weye ni nani ??

    When you post your comment you have to be careful not to offend anyone. Respect yourself if you wanna be respected.

    ReplyDelete
  26. tunashukuru sana kwa hii kalenda hii inapaswa tuwaonyeshe balozi wetu na pia waziri wa maliasili ajue ili tuchukue hatua madhubuti, maana hawa wakenya sasa wamezidi.mimi nashangaa sana mbona uganda hatuna shida nao sana kama hawa wakenya?
    hili lazima serikali yetu ilivalie njuga

    ReplyDelete
  27. Watu wengi hawajui Jiografia ndio maana wana bwabwaja hapa. Mlima Kilimanjaro uko kote. Sehemu iko Kenya na sehemu iko Tanzania. Kwa kuwa wenzetu wa Kenya wanajitangaza zaidi ndio maana imejulikana zaidi kuwa upo Kenya. Kuhusu kuaindikia kampuni iliyochapisha hiyo naomba muwe makini kwani mnaweza shitakiwa kwa kuwa Mlima Kilimanjaro ni kweli sehemu iko Kenya. Hapo hakuna Ubishi. Na bahati mtoa maada ameficha identity yako wangekupeleka polisi sijui unabeba boksi wapi. Watanzania tu wajinga narudia kuonyesha msisitizo tu wajinga hatujui kupigania haki zetu. Kuhusu hili suala hatuhitaji mabavu bali busara zaidi.

    ReplyDelete
  28. wee anon. wa Wed. March 12, 2008 9:01:00 PM EAT, what the h*^*^!!!
    Nenda kalale kaa usingizi unakuwasha!
    anyways, nakubaliana na wengi, hii ni 2008 noma mambo kaa haya.

    Can we sue whoever printed those calendars? I mean talking about copyrights, s'one had to give Mt. K'njaro pic, right?

    ReplyDelete
  29. VIONGOZI mnaohusika na masuala ya Utalii, MPO??? dO SOMETHING,NOW.
    Tuna hasira saaaaana. SISI Tutajitahidi kutetea nchi yetu,ila tunawataka wanaoshughulika na UTALII na Mambo ya Nje MHUSIKE KIKAMILIFU, You guys do some...

    ReplyDelete
  30. We mtoa maoni wa pili unajua unachokisema??

    ReplyDelete
  31. ebwana kusema ekweli hawa jamaa wamezidi mimi mwenyewe hii Carendar nimeina sehemu ninayo fanyia kazi na jamaa akaniambia kumbe mlima kilimanjaro upo kenya na sio tanzania nikashindwa nimwanzie wapi aelewe but kitu wanachokifanya hawa jamaa si cha kiungwana kabisa wanafaa wachukuliwe hatua ikiwezekana.
    mdau toronto canada

    ReplyDelete
  32. Hakika inakera sana. Binafsi naunga mkono kuchukuliwa hatua za kisheria. na kwa uelewa wangu mdogo, wanasheria wa Ulaya (Wa haki za binadamu, mazingira, n.k)wako tayari kununua kesi kama hizi. Ngugu jaribu kuwasiliana nao huenda tukapata mwarobaini wa tatizo hili.

    ReplyDelete
  33. Huyo jamaa mleta habari hii mbona hakuweka anuani pepe (e-mail address) ya hao MAFISADI wa UTALII na kuiba picha zetu na kisha kuzitangaza kana kwamba huo MLIMA KILIMANJARO huko KENYA ???? Tunaomba utuwekee hiyo anuani ili tuanze kuwapasha kama Wizara husika (Wizara inayohusika na UTALII) itakuwa imeenda likizo. hao watani wetu wanatumia kila mbinu baada ya kuona sisi WABONGO tumelaza BONGO zetu kuitangaza NCHI yao !!! nami nitakuwa siwalaumu sana ILA wa KULAUMIWA ni VIONGOZI wetu ambao walitakiwa kukemea hali hii ili isiendelee !!!!!

    KWA KWELI INATIA UCHUNGU SANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA !!!!!!

    ciao !

    Kichwabuta Mwendantwala

    ReplyDelete
  34. Mi inaniuma sana lakini wa kulaumiwa ni Rais wetu kitendo cha Kenya kutangaza mlima upo Kenya ni sawa tu na Idd Amini aliposema kuwa Kagera ipo Uganda tunajua Mwalimu alichomfanya though ilitucost economically but ilikuwa ni kutambua na kuutetea Utanzania. Jakaya ni amiri jeshi mkuu wa nchi hii kitu lazima aichukulie kwa umakini sana hiki kitendo ni sawa na cha uvamizi hatupaswi kutumbua macho we have to be serious sio kuwa nachochea vita ila ni uzalendo wa nchi yangu.

    ReplyDelete
  35. We anony wa 9:01 huna maana kabisa. Nachelea kusema upeo wako ni mdogo mno! Yani unaona wazi kabisa maneno yanajieleza halafu still unang'ang'ana hawajasema upo Kenya! Hata walimu wako walipata taabu darasani (kama ulisoma), you better go back to school au kaa kimya watu wenye uchungu na uzalendo wa kweli na nchi yao wanapochangia. Nina wasiwasi wewe si mtanzania!

    ReplyDelete
  36. ACHENI USWAHILI HAWAJASEMA MLIMA UPO KENYA NA SIKU ZOTE WANASEMA UKIENDA KENYA UTAUONA MLIMA KILIMANJARO! FANYENI KAZI KWA BIDII ILI MUWEZE KUWALETA HAO WATALII WANAOTAKA KUUONA NA KUPANDA MLIMA. KWA TAARIFA YENU UKIFIKA KENYA UKITAKA KUPANDA MLIMA WANAKULETA TANZANIA NA UTAPANDA MLIMA KWA BEI RAHISI KULIKO UKIJA MOJA KWA MOJA TANZANIA!

    ReplyDelete
  37. WADAU NIELEWESHENI KIDOGO, HIVI ULE MLIMA UONEKANAO UPANDE WA KUSINI MASHARIKI MWA KENYA UNAOFANANA NA WA KILIMANJARO UNAITWAJE? MTALII ALIYEMO KENYA AKIUONA HUO MLIMA NA KUULIZA NI MLIMA GANI HUO, AJIBIWE NINI?

    ReplyDelete
  38. Wakenya wanautangaza sana huu mlima, jana nilikuwa na Mmarekani mmoja tunaangalia hii blog, akashangaa sana na kuwatukana wakenya, Yeye anaijua Afrika Mashariki vizuri sana kwa hiyo alipigwa butwaa kuona eti Mlima unadaiwa kuwa uko Kenya. Hii dawa yake ni kupambana, siyo kukaa kimya. Watanzania wanaowaogopa Wakenya wakafe mbele huko, na hawa wanaoshindwa kubaini matatizo kama haya hawana akili sawasawa. Mimi mpaka sasa bado nawashangaa waliopinga ile Zanzibar. Tumelala mno jamani, na kuwaambia watu wa serikali kwamba uamuzi wa eti mtu akipata viza ya Kenya anaruhusiwa kutalii Tanzania ni wa kijinga mno, na utatuumiza vibaya. Hakuna hata sababu ya kuruhusu mtalii aliyeingilia Kenya kuja Tanzania, aende kwako kwanza, halafu ajipange upya, tuweke jeshi mpakani ingawa rushwa tutaifanyaje sijui? Hii EAC ni ujambazi wa mali zetu, Wakenya watatuchinja hawa mchana mchana, ni wezi.

    ReplyDelete
  39. jamani mmeona hilo tu? mbona ziwa nyasa tumeshaporwa siku nyingi na vyombo husika viko kimya. mawali wanatangaza kama ziwa malawi la lote liko malawi kitu ambacho ni uongo mkubwa. kazi ipo. tumelala sana

    ReplyDelete
  40. jamani wadau, hao wazungu kufikiri kuwa kilimanjaro iko kenya ni udhaifu wao, as inaonyesha jinsi ambavyo jiografia imawapita pembeni. ina maana wao wanaamini kila wanaloambiwa kwenye matangazo ya biashara wala hawasomi kitu darasani.
    anyway, wakenya walishatumia sana hiyo publicity wakati ule sisi tumezubaa. ila kwa wenzangu wanaongalia CNN watakua wanaona tangazo letu la utalii linaloonyesha vivutio vyote vya pekee vya nchi hii, na mwisho linasema, Tanzania, the land of Kilimanjaro and Zanzibar. so tumeshaanza kuamka, hata kama tumechelewa, lakini JK ameonyesha juhudi.

    ReplyDelete
  41. wewe anon wa mach 12, 2008: 9:01.. tena ukome, nani anawaonea hao wanaosema mt kili, kenya?? mimi nafikiri wewe ni mmoja wao.. use ur brain.. not ur head to speak and think before you spit.. hawa watu wanaodai kuwa mlima kilimanjaro uko kenya basi wabadili uraia wao wawe watanzania. inakera sana na inauma sana. nyie mawaziri/ viongozi mnaohusika na mambo ya utalii mko wapi? hebu pigeni miswaki ya macho na mzibue masikio yenu basi and do something. this is too much. kwanini wajisifie kitu kisicho chao, ni majizi na ndio mana wanauana kijinga tu huko kwao, wakati wahusika wanaofanya wao wauane, wanakula kuku tu.. VIONGOZI WAHUSIKA WA UTALII JAMANI.. DOO SOMETHING!!!

    ReplyDelete
  42. Mimi nafikiri hapa hakuna tatizo maana picha hiyo imepigwa kutokea upande wa Kenya. Ndivyo mlima Kilimanjaro unavyooneka kwa upande wa Kenya.
    Sauala la muhimu hapa Tanzania tunatakiwa tuzingatie taaluma. Viongozi husika hatika masuala ya utalii wanatakiwa wawe na ufahamu wa kutosha kuhusu mambo yote yanayohusu utalii na namna ya kuutangaza. Mara nyingi wadau wa tz ukiwaambia kutangaza wataanza kupiga mahesabu na kusema wanasubiri kikao cha bajeti. Lakini ukiangalia tangazo kama hili sidhani kama linagharimu sana kiasi hicho. Hapa kinachokosekana ni utashi na uzalendo.
    Kitu kingine tunatakiwa tuongeza 'chachandu' kama anon mmoja alivyosema hapo juu. Matangazo kama 'Come to Tanzania to see Kilimanjaro' peke yake hayatoshi kueleza kwamba Kili iko Tz. Mimi naona nivyema sasa matangazo haya yaambatane na RAMANI inayoonyesha mpaka wa Kenya na Tanzania na jinsi Kili ulivyo ndani ya Tz. Hapa hapatakuwa na kigugumizi tena.
    Sasa hivi kuna watanzania wengi wanakwenda nje ta nchi ki-michezo, urembo n.k. Hawa nao wakipewa vipeperushi vinavyoonyesha Kili iko wapi itasaidia sana.
    Sasa ni wakati wa matendo na si maneno!

    ReplyDelete
  43. Tena sio kusema kwamba hii Calender ni ya Zamani labda watakuwa wamejistukia wamebadilisha hapana ni ya Mwezi uliopita na ni mwaka huu.

    Hivi haiwezekani kuwashtaki watu kama hawa na watulipe Fine kwa muda wote huo ambao wamekuwa wakiipata fedha ambayo sio HALALI yao.

    ReplyDelete
  44. Poleni sana wadogo zangu Poor sons and daughters of Tanzania!Waswahili wanasema hivi,'Mficha maradhi kifo kitamuumbua'.Hii mara ya pili sasa tunasoma malallamiko haya yanayofanana kuhusu masuala ya Utalii na ndugu zetu wa Kenya.Ningependa kuwaambia hivi,kwamba,HIYO NI DALILI TOSHA JINSI TANZANIA ISIVYOJULIKANA HUKO UGHAIBUNI KWA KIWANGO AMBACHO VIJANA WETU WANAFIKIRIA.common sense tells me that,Iwapo Tanzania ingekuwa inajulikana kiasi hicho ambacho wengi wenu mnafikiri hakuna ambaye angethubutu kudanganya wageni wa nje kwamba Kilimanjaro iko Kenya au Ziwa lote la Victoria liko Kenya au Ziwa lote la Tanganyika liko Congo DRC au Ziwa lote la Nyasa liko Malawi na mengineyo.Ukweli ni kwamba tumekuwa tukipigwa porojo nyingi sana za kisiasa kwa muda mrefu sasa kwamba Tanzania inajulikana sana ulimwenguni kote.Ingekuwa hivyo ni kweli basi tungewakimbia Watalii kwa uwingi wao ambao wangependa kuona maajabu ya Serengeti na Ngorongoro na vivutio vingine hapa nchini.Hata hapa majuzi yalipokuwepo machafuko ya kisiasa nchini Kenya, watalii wengi sana waliokuwepo nchini Kenya walirejea makwao au walielekea nchi zingine na hawakuwa na wazo la kuvuka mpaka na kuja kwetu Tanzania kwenye mbuga za Serengeti na Ngorongoro.Kwanini?Nashawishika kuamini kwamba wengi wao hawakujua kabisa kwamba hata Tanzania pengine ni bora zaidi kwa vivutio vya utalii kuliko hata Kenya.Watalii wengi wanapokuja Afrika ya Mashariki,sehemu kubwa ya malipo yao huifanyia hukohuko makwao au majuu.Na kila mtalii huchagua Tourist Package maalum itakayo mvutia.Package yenye mchanganyiko wa sehemu nyingi za vivutio huuzika zaidi.Na wenye uzoefu na biashara hiyo wanajua.Mtalii ukimchanganyia mbuga za wanyama,mlima mrefu kuliko yote Afrika,Pwani ya marashi,sehemu za kihistoria na mambo ya kale,misitu ya asili kabisa, tamaduni za kikabila ambazo hazitoweka ulimwenguni nk ni mambo atakayo yapenda zaidi kuliko menu ya vivutio vya aina moja.Katika hilo kwa Tourist Operators hakuna mipaka ya nchi madhali sheria za nchi husika zitazingatiwa watalii watakapowasili.Hayo yanayo fanyika hayafanywi na serikali ya Kenya wala hayafanywi na wananchi wa Kenya.Ni wafanya biashara za Utalii ndiyo wanao tumia kila aina ya promosheni ili kuvutia watalii zaidi na kukuza biashara zao.Kwa hiyo watu wasije wakaingiza ujinga hapa wa kuanza kutugonganisha na ndugu zetu wa Kenya.An ordinary Kenyan does not get anything out of this whole tourism quagmire!Watanzania tumezidi sana MDOMO hakuna vitendo.Nani atakaye tutangazia Utalii wetu wa hapa nchini kama siyo sisi wenyewe?Ni aibu ilioje kwa Balozi zetu za nje.Au watu wanapelekana huko kishemeji bila ya kuzingatia sifa za utendaji?Maana sasa inatia shaka kama kweli Balozi zetu zina watendaji wenye sifa zinazostahili na iwapo kuna vigezo vyovyote vya kupima utendaji wao!Tusikimbilie kuwashutumu ndugu zetu wa Kenya.Wenzetu wanajituma zaidi na ni wachapakazi hodari kuliko sisi watanzania kubali usikubali.Kwetu sisi siasa ndiyo kila kitu.Mkielezwa kitu chokonoeni ndani zaidi ujue unachoelezwa ni kweli au ni cahanga la macho!Kazi kwenu.Mtaishia kunawa tu.Haya weee!

    ReplyDelete
  45. Kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha na wa waziwazi then Kenya inaweza kushitakiwa katika mahakama za kimataifa kwa kosa la kutumia maliasili ya tanzania kwa kujinufaisha.na hili linawezekana.Jambo la muhimu hapa ni njisi gani ya kufungua kesi na chombo gani kitafungua na kushughulikia hii kesi ndilo jambo la kusaidiana kwa hapa.

    ReplyDelete
  46. Wadau msikonde kwa Kenya kuweka picha ya mlima wetu uliopo Tanzania. Ni kweli ukiwa upande wa pili wa mpaka yaani nchini Kenya mlima Kilimanjaro unaonekana vizuri sana, kama vile ukiwa kitongoji cha Njiro Arusha au mkoani Manyara Arusha.
    Hivyo basi kwa kuwa watani wetu wanautamani kwa macho kivutio chetu, na sisi basi tuendeleze kampeni ya kufanya ulimwengu kuelewa mlima upo nchini Tanzania.
    Wacheni watani wetu wachapiche majarida na kampeni kibao kuhusu huu mlima.
    Na sisi Tanzania tuunge mkono kampeni hii watalii kuujua mlima huu na pia kujua mlima huu hasa hasa upo nchi gani kama watapenda kuupanda, au kama wanataka kuuona kwa macho wakiwa mbali sana basi watalii hao watauoa kutokea Kenya. Kampeni yenye ujumbe kama huo unatosha kutuletea watalii, maana 'kelele za mlango hazizui mwenye nyumba kulala'.
    Mdau
    SeniorJunior
    London

    ReplyDelete
  47. MNALALAMI KA NINI??? WAKATI HII NI EAST AFRICA COMMUNITY SO MNALILIA JUMUIA YA AFRICA MASHARIKI???? NA BADO HATA MASHAMBA YA VITUNGUU KARATU WA KENYA WANAKUJA KUCHUKUA ,TANZANIA NI BONGO LALA KWA KILA KITU WACHA WAONA MBALI WAFANYE VITU VYAO,HAKUNA UTAIFA HAPA

    ReplyDelete
  48. Ndiyo maana watalii wamepungua mwaka huu kuja kutalii maana wanachanganyikia Kenya wanasema mlima uko kwao Tanzania wanasema mlima ni wa kwetu sasa waelewe vipi watu hawa?

    ReplyDelete
  49. naona mie bora nitumie mstali wa mr.ebo " TUNAOMBA MLIMA WA KILIMANJARO UAMISHIWE KINONDONI".mnatapa tapa tu nyinyi wenyewe MBUGA ZENU HAMZITEMBELEI NA WALA HAMJALI THAMANI YA KILAMANJARO SASA MNATAKA UJITANGAZE WENYEWE? na wewe unayezungumzia tangazo la the land of kilimanjaro limeanza mwaka jana tu haya mambo yameendelea miaka nenda rudi.WENYEWE WANAKWAMBIA MT.KILIMANJARO ILIKUWA B.DAY GIFT MWALIMU NYERERE KUTOKA KWA JOMO KENYATTA LOOOL MIE NAWASHUKURU HAO WATU KWA KUWAAMSHA NDUGU ZANGU WATZ.

    ReplyDelete
  50. unaweza kukuta baadhi ya watanzanai ughaibuni wanawakumbatia wakenya, ndio maana wanasema mlima uko kwao, haya mambo ya kuwapa wakenya nafasi yaachwe kabisa, tuwasaidie kisiasa lakini sio kuwapa nafasi hivyo, watasema vingne vik kwao, tafadhali watanzania msikubali wakenya watushinde, kwanza wamejipaka matope kwa mauaji yaliyotokea, watanzania tusikubali kamwe.

    ReplyDelete
  51. unaweza kukuta hata ofisi ya serikali, iko karibu na chama cha wakenya utafanyaje na ni ofisi ya serikali, hizi balozi zetu zinatakiwa zifanyiwe uchunguzi sidhani kama raisi kikwete anayajua haya, hapewi taarifa kamili za hawa watendaji.

    ReplyDelete
  52. Mt Kilimanjaro Kenya !
    Sawa kama ni enzi za Malkia Victoria na shangazi yake Kaiser

    ReplyDelete
  53. bwana Kithuku kwanza napenda kukupa pole ya kutumia muda wako kwa kutoa comment na hongera kwa kuwa mtu jasiri kwa kutuma comment zako kwani na wewe una haki ndani blog ya mh.issa michuzi kuwa ni mambo ya publicity ila kumbuka kwamba kwenye utalii kuna kitu kinaitwa ito itineraries ambachacho kinamueleza mgeni route nznima kuanzia kupokelewa hadi kurudi kwao kwa mfano fungua www.kileleafrika.com kwa picha halisi na mimi kwenye hiyo website ya utalii ndiye webmaster (mtengenezaji)...hivyo basi unaposema mgeni anatambua au mlima utaendelea kuwa tanzania unakosea kwani mgeni atalipa fedha za kigeni kenya then kampuni ya kenya impitishe kwanza kwenye hifadhi za kenya then finaly ndo kampuni hiyo imlete TZ tena wao ndo watulipe sisi na si mgeni..... (mdau wa utalii Mtanzania halisi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...