Home
Unlabelled
ambulensi ya kijijini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Yaani mtu huwezi amini hawa ndugu wanaishi katika nchi yenye viongozi wanaoita billions kuwa ni vijisenti. Sijui tumfuate mshikaji Chenge awarushie japo vi-milini 50 kwa ajili ya kununua ambulance na kuweka madawa katika hizooo hospitals. Manake si ajabu hiyo hospital wanayoenda haina dawa nyingine zaidi ya panadol...!!
ReplyDeleteMAFISADI WAMECHUKUA HELA ZOTE WALALA HOI WANAKUFA VIJIJINA KWA KUKOSA JUST BASIC HUMAN NEEDS. I GUESS THAT'S WHAT THEY CALL Chama Cha Mafisadi
ReplyDeleteUmaskini hauwezi kuisha kwa kuwa pesa zipo mikononi mwa viongozi wetu. Vijisenti vinanunua ambulance ngapi?
ReplyDeleteMichuzi hili sio jambo la utani kama uliavyoandika ni jambo la kusikitisha ... tatizo watu wengi huko nyumbani mnafikiria Tanzania ni Dar es Salaam tuu !
ReplyDeleteHayo ndio matokeo yake ...ndungu zangu wa kusini tumieni kura zenu vizuri.
Hapa hakuna cha umaskini wala nini,Serikali imeshindwa kazi.Hawa watu kama wangeachiwa waendeshe mambo yao wenyewe bila ya kuingiliwa na Kunguru yoyote ndani ya mipaka ya eneo lao nakwambia kiwango chao cha maendeleo kingekuwa tofauti kabisa.Serikali Kuu ingekuwa inachukua pasenti ndogo tu toka kwao kwa ajili ya gharama za ulizi basi.Viwango vya kodi wapange wenyewe,mapato wachukue wenyewe,matumizi wapange wenyewe,mipango ya maendeleo wapange wenyewe,ajira za wataalamu wazikadirie wenyewe na kuajiri wenyewe,viwanda waanzishe kwa ubia kwa jitihada zao wenyewe na mambo mengine yote.Pamoja na udhaifu walio nao bado utakuta Pato lao la wastani kwa kila mkazi mmoja litakuwa kubwa zaidi,gharama ya maisha itakuwa nafuu zaidi.Hakuna chama kitakacho pata ruzuku,kila chama kijiendeshe kwa pesa na biashara zake chenyewe.Huwezi kuona wagonjwa wakibebwa katika machela namna hiyo.Kuna vijiji hapa nchini hawajawahi kuona baiskeli toka wazaliwe!utaamini?Republic of Danganyika hiyo!Hizo ni enzi za Dr.Livingstone nakuambia,kada wangu!Mbo tabu!
ReplyDeleteI have seen philanthropists, celebrities, spostmen & women, businessmen & women, well wishers, etc giving back to the society but I have never heard and seen mafisadi giving back to the societies they have robbed.
ReplyDeleteMkapa thats your people in Mtwara you better dig in your pockets and at least do the right thing/ deed sometimes.
Picha za namna hii zitafutiwe utaratibu ili watz wengi waweze kupata fulsa ya kuziona. Bahati mabaya zinaishia hapa kwenye deskitopu. Nafikiri ziwe zinapelekwa bungeni wabunge wawe wanazijadili.
ReplyDeleteMimi nilipita katika kijiji cha Namajani wilayani Masasi nikakutana na jamaa kabeba mke wake kwenye tenga (siyo jina la mtu, wafanya biashara wa matunda wanajuwa hiki ni chombo gani) laivu...halafu akampakia kwenye baiskeli. Nilitaka kupiga picha lakini nikasita kwamba ningeumiza sana nafsi ya jamaa huyo.
Yapo mengi tz ambayo kama yakiwekwa hadharani yangeweza kusisimua hata roho za kigaidi za mafisadi.
Nacheka ila issue inasikitisha nikiangalia ambul...zinavyokimbizana hapa London na vingora alafu sisi ndio hivyo tena kweli wanaokula hela za kodi yetu hawana huruma kabisa kazi ipo sio vicheko taifa lina mambo mengi sana ya kufanya bado changa, maskini illiteracy rate iko juu ila kuna walafi wachache wanataka kutuaribia mambo unaposoma kwamba kuna watu wawili wanapata 140+ mil kila siku alafu hata wilaya zote sijui kama zina ambul...bongo niambieni kazi si bado kubwa sana?
ReplyDeleteLondoner
Aaah maskini,kope zangu zimeshindwa kuhimili vishindo vya machozi yangu. Nimeshindwa kujuwa yametiririka kwa speed gani, kutoka kwenye glands hadi kwenye keybord, kwani nlikuwa kwenye dimbwi zito la mawazo juu ya picha hiii!
ReplyDeleteLoh, inasikitisha, inaumiza, inahuzunisha,inatiasimanzi, inakatisha tamaa!
Huwezi amini kwamba sehemu hiyo ndiko anakotoka rais mstaafu billionea, anaemiliki kampuni ya umeme ya TanPower Resources Ltd, rais mstaafu mwenye hisa kubwa tu kwenye kampuni ya madini, rais mstaafu mwenye kampuni binafsi ya Anbem Ltd! Vyote hivyo vikiwa vimepatikana katika hali tata!
Rais huyu ndo aliekuwa akisimama kwenye majukwa, kwa jeuri na kiburi akijinadi kwamba uchumi wa Tanzania unapanda kwa 7.6%! Kumbe kijijini hata gari la ng'ombe au mkokoteni wa kubebea wagonjwa hakuna!
Maskini Tanzania yangu, maskini wakulima mnaolima kwa jembe la mkono, mvua jua halafu jasho lenu linaishia kwenye matumbo ya mliowapa dhamana ya kuwaongoza, maskini vibarua mnaofanya kazi viwandani, kwenye sumu za makemikali, kwenye mazingira hatarishi ya afya zenu, chini ya kibaraka muhindi anaekusimamia kama askari jela na matusi juu, kisha jasho lako linaishia kwenye account za mabenk ya kisiwa cha jesrsey, maskini waaalimu wangu mnaosomesha wanafunzi zaidi ya 100 kwenye darasa, kisha mshahara wenyewe mbuzi unaishia kwenye nauli za dala dala, tena huupati mpaka tarehe 40 (mna kalenda zenu za pekee eenu),aaah kumbe vijisent vinalipwa kwa viongozi wenu wenye makampuni ya Richmond, maskini wanajeshi wetu, wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu, wanaolinda mabenk na makampuni ya wakubwa wakiwa wamebeba rungu au gobore wakati majambazi wana lmg na smg! wanaishi kwenye nyumba za mabati "full suit", mlango mmoja, wanalipwa mshahara unaoishia kwenye kununuwa dona tu! Ah maskini wafanyakazi wote msiojuwa lini mtafaidi matunda ya uhuru wa Tanzania....!
Sijui mafisadi hawa ujasiri wanautoa wapi wakwenda vijiji nyakati za uchaguzi kuomba kura?!
Sijui wanatumia mashairi ya malenga gani mpaka wanyonge wavijijini wanawasikiliza wakati wa kampeni zao?!
Sijui limbwata lao wanatengenezewa na nani, mpaka wanafanikiwa kuwahadaa wanavijiji na kupata kura?!
Iko siku bubu atasema...!
HAKI YA MUNGU KWA MTAJI HUU ACHA NIBEBE BOX MPAKA NIFE. YAANI WAKATI MWINGINE UNAWEZA FIKIRI BONGO HAPAFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU.HIVI NI KWELI SISI NI MASKINI MPAKA HATUJIJARI ? ZIKO WAPI HAKI ZA BINADAMU ? TUNAAMINI MUNGU KWELI SISI,KUNA DINI NCHI HII KWELI,VIONGOZI,WALIMU AU HATA WAZAZI ? PESA ZA WALIPA KODI HUWA ZINAKWENDA WAPI AU ZINATUMIKA VIPI ? HAWA WATU WA KIJINI TUTAENDELEA KUWAKANDAMIZA MPAKA LINI ? TUNA WAKANDAMIZA KUANZIA KUWANYIMA ELIMU,HAKI ZA KIKATIBA(MFANO MBUNGE WA VIJIJINI KUTOKEA MJINI),BEI NDOGO ZA MAZAO MPAKAKA HILI LA HUDUMA MUHIMU ? UMEFIKA WAKATI WATU WA VIJIJINI NAO WATAMBULIKE KAMA BINADAMU NA RAIA HALISI WA HII NCHI NA SIO KAMA RAIA WA DARAJA LA PILI.NI LINI WATANZANIA TUTAELEWA KUWA HUDUMA MUHIMU KAMA MAJI SAFI NA SALAMA,AFYA,MALAZI NA MIUNDO MBINU MIZURI SIO TU NI MAHITAJI YA MUHIMU BALI NI HAKI KWA KILA MTANZANIA. NATOA WITO KWA WAPIGA KURA WOTE KUWAULIZA VIONGOZI WAO NINI WAMEFANYA NA SIO NINI WATAFANYA WAKATI WA KUOMBA KURA KWANI YOTE HAYA NI MATOKEO YA KUWEKA MAFISADI NA WABABAISHAJI MADARAKANI.NA WATU WA VIJIJINI NAO WAAMKE WAJUE HAKI ZAO KAMA BINADAMU NA WAGOME KULISHWA KASUMBA NA UJINGA KUPITIA DINI(SINA MAANA WASIAMINI MUNGU) NA VIONGOZI UCHWARA. HAYA MAMBO YATAWEZEKANA PALE TU KILA MMOJA WETU ATAKAPO KUWA INDEPENDENT THINKER NA KUKUBALI KUJITOLEA KAMA MZALENDO HALISI WA NCHI YAKE. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA. AKHSANTENI NA SIKU NJEMA.
ReplyDeletewawekezaji wa ndani, mazee wa uwazi na K'magi, warudishe japo 1% ya hisa zao kwa wananchi kwa kununua gari la wagonjwa huko
ReplyDeleteMr. vijisenti ameiona hii ambulance? Sasa imefika wakati sasa watanzania tuseme ufisadi mwisho kwani haiwezekani watu watanue kwa pesa za walalahoi wakati walalahoi wenyewe wafa
ReplyDeleteHii inaonyesha jinsi watanzania tulivyo katika enzi za ujima. Haingii akilini kabisa kuendelea kutumia machela kama moja ya njia ya usafiri katika karne hii.
ReplyDeleteWatanzania tutafakari kuhusu hali ya maisha yetu na kujiuliza kama hali tuliyofikia sasa ndiyo hasa maisha tunayotaka kuyaishi.
Inatia uchungu kabisa.
Ignorant, Jeremani
Hii inaniumiza tu ninapoona mahangaiko kama haya kwa wananchi wa Tanzania ambao idadi yao si chini ya asilimia 80%; hasa ukizingatia kuwa BWANA Mkubwa mmoja tu sijui jina lake Chenge, chenga, au Chenji akiwa amekubatia zaidi ya billioni moja peke yake. Cha ajabu bwana huyu baado anaendeleza limbeneke lake bungeni kama kawaida tu. Nadhani jamaa anasanifu tu na kusema "kumnyima punda hadesi ni kumpunguzia mashuzi"
ReplyDeleteDAWA IKO JUKONI!!!!!
Yaani hiyo picha inaumiza kweli hasa ukifikiri jinsi pesa za wavuja jasho zilivyotumika vibaya na hasa kutajarisha watu wachache.
ReplyDeleteAnony wa 4:08, tarehe 25, uliyekosa hata chembe ya huruma kwa sababu tu unaishi manzese, VIJISENTI KWA HESBAU YA HARAKA INAUWEZO WA KUNUNUA AMBULANCE 66, hiyo ni bilioni moja tu, JE +EPA+RICHMOND, TICTS,IPTL, nk.k tungekuwa wapi??? lazima viongozi walaumiwe.
ReplyDeleteNajisikia kufa kufa. Unajua tatizo sio Mafisadi, tatizo ni matumizi ya kura zetu. Nchi za wenzetu, mtu anachaguliwa kutoka na ATAKAVYO watumikia watu wake, lakini sisi, ANAWATUMIKIA kwanza kwa rushwa, ananunua kura, ndio anaingia madarakani. Tena, kama mtu atasema wananchi wa kawaida huwa wananunuliwa, ni dhambi na matusi kwa watanzania. Mimi huwa naona wakati wa uchaguzi. Kuna kikundi kidogo huwa kinachaguliwa kinapita nyumba hadi nyumba kuwalaghai wananchi wawapigie Mafisadi, wakishafanikiwa, wanaanza kuiba ili warudishe fedha yao. Mfumo huu bila kubadilika. matatizo haya yataendelea sana na nasikitika sana.
ReplyDeleteJamani mimi siokama sipendi tuendelee kimichezo au nini lakini we spend millions to build a new national stadium . Nivizuri tuna keep lakini nilini serekali itatumia millions or billions ya pesa kuimarisha huduma za afya nchini?? Tuya dhamini maisha ya watu !! When is change going to come ??
ReplyDeleteMD
halafu utasikia mtu anadiriki kusema tanzania imebadilika siyo kama mlioiacha zamani,jamani tanzania siyo dar peke yake tanzania ndiyo hiyo kwenye picha hapo juu.
ReplyDeletekama sikosei hapo ndio wamefika zahanati, waangalie maana hata tenki la maji halipo! limebaki zege tu. na hawa ndugu zngu sijui kama wana hela za kununulia bomba la sindano, na mia tano ya kuandikishia cheti, halafu watafute baskeli kwenda mjini kununua dawa.. wataporudi huyo mgonjwa atakuwa bado anawasibiri?!:(
ReplyDeleteBONGO MAVUMBINI SIRUDI NG'O! UMASKINI NA UJINGA UMEZIDI SANA. SASA HII KARNE YA NGAPI?
ReplyDeleteNa hiyo sio machela ndugu zangu. Bali ni kitanda kinaitwa TEREMKA TUKAZE- vile vinavyotengenezwa kwa ukili.
ReplyDeleteNdio vitanda wanavyolalia asilimia kubwa ya wananchi wa huko maskini jamani.
Yaani wamemhamisha na kitanda chake. Si ajabu huko zahanati hakuna hata kitanda cha kulalia ndio maana wamebeba cha kwa kabisa.
Hurumaa!
Mweeh!
INASIKITISHA SANA TZ ALIYE NACHO ANACHO ASIYE NACHO DUUU!HUWEZI AMINI KUA KUNA WATU WANAJITAJIRISHA KWA PESA YA JASHO LA HAWA WALOBEBANA KWA STAILI HIYO INAKATISHA TAMAA KURUDI NYUMBANI KHERI NIWE MTUMWA NA MBWA WA ULAYA KULIKO BIDAMU WA TANZANIA NASIKIA VIBAYA NA HURUMA SAA NYINGINE NA SEMA SIJUI NIACHE KABISA KUSOMA HABARI ZA NYUMBANI KILA NIKIFUNGUA COMPUTER NI MATATIZO HOME IS HOME SIWEZI KUACHA KUJIZUIA KUJUA HABARI ZA KWETU.NASIKIA MKAPA NABONGE LA HOTEL LA KIFAHARI LUSHOTO WATU WAKE HAWANA AMBULANCE!
ReplyDeleteVITU KAMA HIVI UNAWEZA KUTUMA ccn.com/ireport nina huakika watoto wa mafisadi wataona nakuwaambia wazazi wao au balozi zitapata tu message hio.watumie picha nyingi ya uwezo wako tutaweza kuleta mabadiriko/mnaweza kuanza na picha hio kwani inasikitisha sana.na kweli watu wanashindwa kuelewa tanzania sio dar peke yake.
ReplyDeleteNa wengi wakaa dar es Salaam hawajui hali halisi ya m-Tanzania kijijini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHuu ni umaskini kupita kipimo cha umaskini, I don't believe this is happening at this time and age in Tanzania baada ya maendeleo yote ya kiuchumi tangu tupate uhuru.....Sidhani kama huyo mgonjwa alifikishwa anakokwenda hai.....alafu mnasema vifo kama hivyo eti Mwenyezi Mungu kapanga!!! Sikubaliani kamwe na msemo huo, wengi wanakufa huko kwa kukosa huduma haraka au hakuna huduma kabisa. Hapa nilipo nikipiga simu yoyote 911 watafika hapa na ambulances na zima moto (baada ya dakika tatu hadi tano!) JK - T.O.
ReplyDeleteHAPO JUU HASIRA ZIMEFANYA NIKOSEE NI CNN.COM/Ireport
ReplyDeleteMICHUZI HII PICHA INAHUZUNISHA SANA. MIMI NINA ONI NA KAMA KUNA VI/KIONGOZI WA SERIKALI WANASOMA HAYA MAONI TAFADHALI FIKISHA UJUMBE. MIMI NINASHAURI KABLA KIKAO CHA BUNGE HAKIJAANZA, NINAMAANISHA KILA WANAPOINGIA BUNGENI NA MIJADALA KUANZA. PICHA KAMA HIZI, ZA WATANZANIA WANAOISHI MAISHA DUNI, ZINAZOGUSA SEKTA ZOTE AFYA, ELIMU, USAFIRI, KILIMO ZIONYESHWE ON BIG SCREEN NDANI YA BUNGE KWA MUDA KAMA WA NUSU SAA. NA WAKUMBUSHANE SABABU YA WAO KUKAA BUNGENI NA KUJADILI NI ILI KUDUMISHA MAISHA YA MTANZANIA WALIYEMWANGALIA KWENYE HIZO PICHA KWA SABABU IDADI KUBWA YA WATZ WAKO KATIKA MAISHA DUNI. IKIFANYWA HIVYO NAAMINI ITAKUWA CHANGAMOTO, NA IDADI YA WANAOSINZIA BUNGENI ITAPUNGUA. LAKINI YA YOTE KABLA YA UTENDAJI IANZIE KWA VIONGOZI WOTE KUWA NA UTU NA UADILIFU. SIDHANI KAMA KILA MKOA UKIWA NA MIPANGO YAKE YA MAENDELEO NA UFUATILIAJI MADHUBUTI KUNA KITAKACHOSHINDAKANA..TAMAA SIO NZURI KUNA SIKU ITAWATOKEA PUANI, HATA KAMA SIO KWA WAO BALI KWA VIZAZI VYAO... HII INAUMIZA SANA TENA SANA....
ReplyDeleteKinachosikitisha hapa siyo picha ila ni aina ya maisha ya vijijini yalivyo. Mimi pamoja na ufisadi, napenda kutoa lawama zangu kwa wanahabari kwa sababu hawaitendei haki jamii ya watu wa vijijini. Nasema hivyo kwa sababu sehemu kubwa ya matatizo yapo vijijini lakini ni asilimia chache tu ya haya matatizo ndiyo huripotiwa na mara nyingi hayapewi uzito. Pia kinachonishangaza ni kitendo cha waandishi hao hao wa habari kuwa mstari wa mbele kuwanadi wabunge wabovu ambao wapo madarakani miaka mingi lakini huduma za jamii ni kama hizi zinazoonekana huku wakitumia maneno ya kuwatia hofu watu kama vita. Hali vijijini ni zaidi ya hapo na kwa wakati huu unahitajika ujasiri wa hali ya juu ili watanzania wajue kwamba kuna watu wapo tz na wengine wapo Tanganyika. Mimi nashauri kama walivyokwishauri wengine kwamba kwa sasa lianzishwe jarida ambalo litakuwa linazungumzia matatizo na mafanikio ya maisha ya vijijini baada ya zaidi ya miaka 47 ya uhuru kwani hii itaisaidia kuboresha maisha ya kijijini kwa haraka zaidi badala ya sasa ambapo habari za vijijini huandikwa pale viongozi wanapotembelea. Ili tuendelee siyo tuonyeshe mazuri tu kwani tukionyesha na mabaya jamii itaweza kuyatatua kwa haraka. Mataifa yote yaliyoendelea wameanza kwa kuainisha matatizo yao na then kuyatafutia ufumbuzi na siyo kuyaficha. Ni aibu mpaka leo kusikia malaria bado inaongoza kwa vifo, kipindupindu ambacho chanzo chake ni kula mavi bado kinaua watu tena Dar. Tubadilike na siyo tulalamike, tusitegemee mafisadi watabadili hii hali kwani ingekuwa hivyo tangu uhuru mpaka leo matatizo yangeisha.
ReplyDeleteNa nyie wabeba maboxi msiwakemee tu mafisadi. Hata nyie tumeni pesa msaidie wenzenu huku kama wafanyavyo wenzenu nchi za wenzetu. Kama kweli mnapata hizo paundi na dola mnazojisifia. Ebo!
ReplyDeleteJamani Mungu atuhurumie! Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteMZEE WA VIJISENTI NA MAFISADI WENGINE WANAYAONA HAYA???
ReplyDeleteMUNGU YUPO HAKIKA MUNGU YUPO.
MNAUMIZA WENZENU HAPA DUNIANI MKITEGEMEA MTAISHI MILELE NA HIZO PESA?? TUTAONA YATAKAYOWAKUTA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MASIKINI WAKE TU.
Bwana michuzi mimi nikuanza wewe kama mwanahabari.Unapokuwa safarini hasa ulaya unatoa picha nyingi sana lakini picha kama hizi ni aghalabu sana kuzitoa. nakuomba sana kuanzia sasa hizi ndio picha za kuweka maana huu ndio wakati wa mafisadi kugawana nchi labda wataona huruma.Chondechonde ustaadhi Michu lifanyie kazi hili suala
ReplyDeleteNYIE WA ULAYA TUMENI PESA ACHENI KUCHONGA SANA! MANENO MATUPU HAYAVUNJI MFUPA, KUNA BAADHI YENU WAPO ULAYA NA WANATOKEA KATIKA VIJIJI KAMA HICHO HALAFU.UNAWEZA KUJA DIRECT NA KUSAIDIA KIJIJI CHAKO.
ReplyDeletevena, arusha