Mbunge wa Ulanga Mashariki, Dk. Juma Ngasongwa, akiwa peke yake katika viti kadhaa ambavyo viko wazi wakati wa jioni kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma juzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. tambarare, bora wasiwepo tujue moja kuliko kuwepo nakusinzia, kazi kweli kweli...

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa alipitiwa na usingizi wenzake wakaondoka baada ya kikao au?
    Maana nashindwa kuelewa wabunge wengine wako wapi!
    Nadhani sasa wakati umefika hawa jamaa wawe na punch card wakiingia bungeni. Unagonga muda wa kuingia na muda wa kutoka. Maana kuna wabunge wengine huwa wanajongo sana vikao. Jitu unakuta linahudhuria ufunguzi na kufunga tu vikao vya bunge ... lakini analipwa mshahara na marupurupu kamili!

    ReplyDelete
  3. Nyie wabunge najua baadhi yenu mnasoma blogu, hivi mmegoma au? Maana mlikuwa mnadai muongezewe marupurupu hivi kwa kazi gani hasa? Hii ya kutoroka vikao? Sasa nyie mtoroke vikao vya bunge, wafanyakazi watoroke maofisini, wanafunzi watoroke mashuleni, tutafika kweli? Kaazi kweli kweli, inabidi waweke vidude huko chini ukikaa kinarekodi muda uliokaa kwenye kiti chako mpaka muda ulioondoka halafu mwisho wa mwezi mlipwe kwa masaa mliyofanya kazi.

    Yaani hata wikiend bado wameshakimbilia chako ni chako na mnadani kuchoma nyama!

    ReplyDelete
  4. ...hofu yangu hapa ni kwamba mzee Ngasongwa akiipata picha hii ataitumia kuombea kura kwa madai kwamba yeye ndiye ana mzigo zaidi wa watu wa jimbo lake kiasi cha kuhudhuria peke yake kwenye kikao...kwa hiyo apewe tena kura ili akazidi kuwatetea wadau wa jimbo hilo...
    naumia sana maana sina uhakika ni wapiga kura wangapi wanaelewa kinachoendelea ndani ya uongozi, utawala, nk.

    ReplyDelete
  5. Daktari huyu kuwepo peke yake ni kuchapa kazi, ama kaamua kupiga dozi kwa kuwa bi mkubwa nyumbani kamtimua and ndio kutekeleza prescription ya mganga wake?

    ReplyDelete
  6. Wewe Anony wa April 24 5:31 Ni Genius!!! kwa kuongezea hapo hapo ni kwamba hizo punch card ndiyo ziwe zinatumika kuchukulia masurufu(allowance) zao kwenye Automatic teller Machine (ATM)maalumu ambazo zitakuwa zinatoa hela kutokana na asilimia ya muda mbunge aliohudhuria bungeni..kama amehudhuria 40% basi anapata haki yake ya 40% ya allowance iliyobidi apate na kama ana sababu maalumu ya kutohudhuria basi ofisi ya bunge itatoa maelekezo ya nini kifanyike...lakini kila kitu kitakuwa ni electronic...safi sana mdau

    ReplyDelete
  7. WENGI WA WABUNGE WALIKUWA DAR KWENYE MAZISHI YA SHUJAA DITO. HILO KWAO LILIKUWA MUHIMU ZAIDI KULIKO KIKAO KINACHOHUSU WANANCHI WOTE, HATA HIVYO KWA SABABU NI WANACCM BASI NI SAHIHI KUFANYA HIVYO BILA SHUTUMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...