
Hi Bro Michuzi!
Pole sana na majukumu makubwa uliyo nayo.
Ninapenda kuuliza swali, kama huko kwetu tayari kuna matumizi ya gesi ya magari, ( picha hiyo hapo nimeonyesha jinsi ujazaji wa gesi) maana nimesikia nchi kama mbili za Afrika tayari wanatumia gesi ya magari.
Pole sana na majukumu makubwa uliyo nayo.
Ninapenda kuuliza swali, kama huko kwetu tayari kuna matumizi ya gesi ya magari, ( picha hiyo hapo nimeonyesha jinsi ujazaji wa gesi) maana nimesikia nchi kama mbili za Afrika tayari wanatumia gesi ya magari.
Kuuliza si ujinga wadau msije mkanimaliza (ninajihami kabisaaaa), maana nimeuliza kwa watu ninao wafahamu huko Bongo, sikupata jibu kamili. Kama kuna mtu anajua kuhusu jambo hili, naomba jibu tafadhali, maana kuna jamaa hapa kila mara ananiuliza kuhusu jambo hili, nisije nikamwambia hakuna kumbe siku hizi Bongo tambarare.
Kwa kweli gesi ya magari ni kitu kizuri sana, hasa matumizi yake ni mazuri sana na ni bei nafuu sana kwa hapa. Ukijaza ful tank unasafiri km nyingi sana. Pia kwa afya ya binadamu ni nzuri haina madhala, kama petroli au diesel wataalamu ndivyo wanavyosema, hupunguza kasi ya magonjwa mbalimbali kama vile kansa n.k, hasa kwenye miji mikubwa kwenye msongamano wa magari mengi.
Kwa kweli gesi ya magari ni kitu kizuri sana, hasa matumizi yake ni mazuri sana na ni bei nafuu sana kwa hapa. Ukijaza ful tank unasafiri km nyingi sana. Pia kwa afya ya binadamu ni nzuri haina madhala, kama petroli au diesel wataalamu ndivyo wanavyosema, hupunguza kasi ya magonjwa mbalimbali kama vile kansa n.k, hasa kwenye miji mikubwa kwenye msongamano wa magari mengi.
Kwa mfano hapa niishipo kuna miezi 4 imepangwa kwa mwaka, kuna kuwa na utaratibu siku ya jumanne na alhamisi huwezi kuzunguka ndani ya mji na gari ya petroli au diesel kuanzia asubuhi hadi jioni saa 12:30, wanasema kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na gonjwa hilo la kansa.
Kama wakikukamata faini yake ni kubwa sana na unapoteza point nyingi kwenye leseni, kwahiyo watu wanaheshimu sana hilo, na jamaa huku huwa hawafanyi utani wakikukamata. Hata mabasi ya mji kuzunguka yanakuwa machache sana siku hizo zilizo panga, kwahiyo usafiri unakuwa mgumu, maana ni mabasi machache yanayo tumia nguvu ya umeme.
Kama jambo hili bado halijafika huko kwetu, basi litakuja kufika tu, taratibu maana nchi yetu bado changa na kuna mahitaji mengi sana tunayo yahitaji ya mhimu kila siku.
Ni katika kuuliza swali tu na kubadilishana mawazo sina zaidi, tafadhali wadau msinimalize.
SALAMU SANAAAA KWA WADAU WOTEEEE BILA KUMSAHAU HATA MMOJA.
Ni mimi yule yule wa siku zote!
B.CHIBIRITI.
SALAMU SANAAAA KWA WADAU WOTEEEE BILA KUMSAHAU HATA MMOJA.
Ni mimi yule yule wa siku zote!
B.CHIBIRITI.


chibiliti! umekaa kimya sana ndugu yangu.
ReplyDeletekatika swali lako ni magari tu au na mashine pia coz mi nimeona fork lift inayotumia gas H, lakini sijaona gari
waambie washikaji waache noma watoe maoni kistaarabu.
hongera michuzi. leo kwenye marathon dar umekuwa wa ngapi?
ReplyDeleteMSAADA TUTANI
HII IKOJE
Kuna picha nimeona kwenye gazeti la mwananchi la leo ya wachezaji wa yanga nalibya. Huyo mchezaji wa libya kwa juu anaonekana mweupe lakini kwa chini hasa miguu anaonekana mweusi kabisa. bro hii inakuwaje? wee ni mtaalamu wa picha jaribu kuichunguza na kutuhabarisha please. au ibandike ijadiliwe.
Sidhani kwamba nitapatiwa jibu rahisi ambalo halitakuwa limefanyiwa uchunguzi mfano 'alikuwa amevaa sokcs nyeusi'
Kila la kheri
we anonym wa 10;34..unajua hao jamaa ni waislamu na wao au mtu anavaa kutokana na imani yake...anyway...kwa waislamu kuvaa nguo fupi inayoonyesha sehemu ya mapaja na magoti ni sawa na kuwa uchi...sasa huyo jamaa amevaa nguo nyingine nyembamba kwa ndani ili asiwe uchi...
ReplyDeleteChbiriti du ilo ndio gari lako kweli ndio maana tulikutafutia MANKA mwenye hela ungekula raha shauri lako.bila kujibu swali lako uliondoka lini uko kijiji(kwa cha chamaki mchanga)nakutakia majibu mema
ReplyDeleteWewe Masa-pare, hiyo fork lift ya gesi umeiona wapi? Ni Tz au!
ReplyDeleteChibiriti (a.k.a chinjiti) kama fork lift ipo, hakika gari zitakuwepo muda sio mrefu. Binafsi sijapata kuona! Hata ya kupikia ni kwa wachache sana mzee. Jamani mabibi na mabwana tukazane, ila kwa standards tuharakishe maendeleo. Tusisahau uzazi wa mpango.
SEV
Magari ya gesi yapo Tanzania ingawa ni machache sana na ni PanAfrican Energy wanayo wanatumia gesi ya Songo Songo, na mwaka jana huko Saba Saba kwenye banda la TPDC walionyesha magari hayo, na gharama za kuwezesha gari yako kutumia gesi. Lakini kwa magari ya ofisi yao yapo yanayotumia gesi hapo Dar, sina uhakika kama ni yote. Jaribu website ya TPDC kama wanayo au yao ya PanAfrican energy au eastcoast energy sina uhakika ni hizi websites, lakini kwa magari nimeyaona kwa macho yangu yakitumika na kwa aliye Dar anaweza kwenda kuwauliza kwenye ofisi zao zilizopo Jengo la Barclays ghorofa ya Tano Ohio street. Nchi nyingine nafikiri ni Msumbiji na Gabon, hao hao PAE na TPDC wana taarifa zaidi. Its simple and cheaper to use natural gas.
ReplyDeleteGas stations hakuna ijekua utumiaji wa magari ya gas?
ReplyDeleteMshika Chibiriti!!!
ReplyDeleteUnatia aibu, mara nyingi unauliza "very awkward and primitive questions" as if huishi katika karne hii.
Ukipiga picha na mzungu...unafikiri umepiga picha na Mungu....ukiona gari zuri..unauliza maswali...kaka "inovation" iko mbali sana na tambua kwamba utandawazi umeondoa mipaka yoyote unayofikiria na unaweza kukuta kabla hilo gari la kutumia gesi halijatoka kuna mkongo wa DRC alisha"order" gari hilo...na ukakuta mutu wa kwanza kuorder hilo gari ni mkongo na hata siyo masikini hao wa ulaya...yaani waitaliano.
Umetoka na "way of thinking" huko kijijini kwenu na unaiendeleza hata huko uliko...try to mature mentally...tumechoka na urembo wako wa kishamba!!! Jitahidi siku nyingine kuongea mambo ya maana.
Michuzi huyu naona anatuibia "space" humu ndani ya kuandika vitu vya maana...tukimwendekeza huyu mporipori Chibiriti atakuja atuaibishe kuuliza vitu ambavyo tutaonekana washamba sana huku Ugaibuni...hawa ndio wale badala ya kutafuta chao ni kuganga njaa tu kwa wazungu na kuwa omba omba na matokeo yake kutumiwa na hawa wazungu kama madodoki.
Siku nyingine bwana Chibiriti tunaomba uwe unatuandikia vitu vya maana na jitahidi kuondoa huo ushamba wako...jifunze kwa wengine na ujue hunatofauti na mzungu yeyote unayemhusudu hapo ila wewe tu ndo adui wa uwezo wako wa kupambanua mambo..."try to emancipate yourself from mental slavely". Ushauri wa bure.
Jamani mwenzenu ameuliza swali sasa ndugu zangu badala ya kumjibu mnaanza kukashifu bila hata ya nyie wenyewe kujiuliza faida ya kutumia Natural gas badala ya petrol muda wote ni ipi,na lazima mjiuliza hilo gari likoje na linafanya vipi kazi..., sio kwamba linatumia gas tu! la hasha linatumia petrol vilevile ila matumizi yake yanakuwa kidogo zaidi, ni magari haya haya ya kawaida yanaogezewa tu system ya gas na vingine vinabaki vile vile ukiwasha litatumia petrol then unashift na Gas..., sasa we mdau unayekashifu bila kuelewa unasema hilo gari likitoka ... kwa taarifa yako sio gari jipya ni hayo hayo unayoyaona kila siku .., na ni mazuri kwani hayaharibu mazingira na ni economy zaidi kuliko Petrol... ila ni gharama kuweka hiyo system ya Gas.
ReplyDeleteBango yapo ila sio mengi kwani watu wanaepuka hiyo gharama ya kuweka system ya Gas na vile vile uhifadhi wa mazingira bado ni Kitendawili bongo
Mdau Urusi
Habari za leo Chibiriti,
ReplyDeletehujakosea kuuliza. ni kweli kuna baadhi ya magari yanayotumia gesi bongo, kuna tipper moja maeneo ya tegeta, baadhi ya forklift na TPDC wanategemea kufungua kituo maeneo ya mikocheni na ubungo kwa ajili ya gesi tuu. kuna blogu zinaongelea hayo mambo na pia website ya TPDC.
pia mwezi wa saba kwenye maonyesho ya saba saba kutakuwa na details nyingi kuhusiana na matumizi ya gesi kuanzia majumbani, mahotelini na kwenye magari.
tutakuhabarisha zaidi ikifika wakati, kwa sasa pata hizo kwanza.
THANKX CHIBIRITI LEO UMETULETEA MPYA ILA NAULIZA HIZO GES HAZILIPUKI MAANA ISIJEKUA KIZA ZAA NA MADALA DALA YETU YANAVYOJAZA KUSIJEGEUZWA MISHKAKI YA MAINI BURE, CHIBIRITI UMENUNUA MCHUMA MPYA? HUJACHACHA NAKUSHAURI USIMUACHE HUYO KIKONGWE SI UNAONA TUMAFANIKIO TUNAANZA KUKUJA MWANEGO.
ReplyDeleteAnna,
ReplyDeleteHaya magari ni ndiyo maana gharama zake kuwekwa system ni ghali. Mitungi ya gas inakuwa nyuma na kuna valve kibao za kulinda mara ajali ikitokea basi mtungi unajifunga. Anyway maendeleo yana RISK zake. Ni sawa na ndege zinapopita juu ya mji na hapo unaanza kusema je ikianguka kwenye miji ya watu? Ndiyo huanguka na kuuwa sana tu. Ila huwezi kusema sitaki ndege. Hii gas inayotumia kwenye magari inabidi WAIPROCESS ndipo inaweza kutumika. Si sawa na inayotumika kupikia au kwa wale jamaa wa kuzalisha umeme. NAfikiri kama wameanza basi itakuwa nafuu kwa nchi. Brazil kwa kuwa wanazalisha GONGO na kutumia kwenye magari (kutokana na miwa), wamejenga kiwanda cha magari kikubwa saaana na magari haya yanatumia GONGO tu. Anyway hiyo inaweza kutokea kama MAFISADI wataanza kufikiria waje wakumbukwe kuwa walifanya mageuzi nchini na si tu WALIKUWA VIONGOZI na KUFISADI nchi. Mungu Ibariki Tanzania. Sikonge
hahaha Chibirit ana kigari cha gesi
ReplyDeletehili ni gari lake wadau angalieni bendera ya tanzania pale juu kushoto kwenye trunk/boot
sio mchezo kibiriti bora kufika hahaha
Mjomba Chibiriti inaelekea kweli unatoka bush,mbona bongo kuna baadhi wanatumia magari ya gesi?wakati wa enzi ya mwalimu kj ilikuwa enzi ya Mabaharia walikuwa wakirudi bongo na hayo magari ya gesi na walikuwa wanajaza kwa wadosi hapo dar labda inabidi kuwekwe mitambo kwaajili ya wote ,hivyo usitufanye kama sisi wabongo tuko nyuma na wewe uburudani uko mbele!! by Mlalahoi.
ReplyDelete