Kaka Michuzi,
Binadamu wanafanya makosa, nimefanya makosa, sikutegemea haya yote yanayonipata. 
Hadi sasa hivi nimepokea emails 6,200. Asilimia kubwa ni matusi na mengine ni watu na picha zao, mengine ya kunifanya nionekani kama mbwa. Wengine ni kunitaka bila kujua ya kwamba nina vigezo vyangu nilivyoweka.
Kama nilivyosema, sitaki mtu mwenye hela. Roho safi ndo ilikuwa lengo langu kubwa, bahati mbaya nimejifunza kutokana na kosa langu. Sitarudia tena, alafu naomba uitoe picha yangu.
Sasa hivi Nipo Ujerumani likizo hadi tarehe 9, lakini nashindwa kulala, kutokana na udhalilishaji na matusi niliyoyapata, na kushangaa ni kwa nini watanzania wanatabia kama hizi. 
Hakuna shida, huyo kaka hajaniandikia, lakini hakuna shida, ya Mungu mengi kwani mipango yake hakuna ajuaye.
Ila naomba tuache wivu unaotutawala .Naomba utoe jina lake, lakini hiyo chini ndo moja ya emails nilizopokea. Naomba waache kuniandikia wakizidi, wote nitaanika majina yao kwa maana wengine ni watu wenye majina makubwa kwenye serikali ya Tanzania, hao ni wengi sana wanaoniahidi mihela na maisha mazuri. sitaki hela zao.
Natoa asante kwako na wadao wako ambao wameamua kunitetea na kwa kunipa moyo pamoja na dada mmoja ambaye tumewasiliana vizuri anayeitwa Lilian.
Asante,
Jovinata

Jovina nimefuatilia vizuri sana posts zako na response kutoka kwenye globu.Kwa kweli pole na bad responses lakini najua utakuwa umepata good responses as well.
Kawaida natakiwa kuanza kujitambulisha lakini niliposoma " admission checklist" ya favourate candidate the room for me got a lot smaller lakini nimeamua nikuandikie regardless na hata tukiishia kuwa marafiki itakuwa hapajaharibu kitu. 
Nafikiria namna ya kuandika qualifications zango ili ziwe na good highlight lakini pia najaribu kutokujifagilia.Nitaifanya iwe fupi na clear isiyona majigambo.
Kabla sijaanza girl i really love bi-racial girls tena akiwa ni wakitanzania kama wewe yaani nakuwa hyper na restless dreaming how good of a guy i will be because you will be the best for me.
Haya chini ni resume yangu fupi. 
1.Naitwa David XXXXXXXXXXXXXXXXXXX. 
2.Nina miaka 28 nilizaliwa september 1981 
3.mama mchaga baba ni mhangaza (kabila la kagera). 
4.Ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa uhandisi chuo (kunradhi, hapa jina kapuni - michuzi) columbus.(uhandisi wa umeme). 
5.Maisha hapa Ohio, columbus, ni magumu lakini tunagangamaa hivyohivyo wagumu kama kitenesi.Ila kwangu siyo shida, account zipo nyngi tu nyumbani hapa na uswisi 
6.tutatumiana picha (nimeiona ya kwako aisee uko moto moto kwelikweli. 
7.On the weekend i fly a small plane for fun it costs about $100 per hour its expensive but its worth it. I have a private pilot licence. 
8.siwezi kutoka marekani manake nikitoka nitashikiwa miguuni(najua unajua ninachomaanisha) 
9.Tanzania tukirudi pamoja hakuna shida, mbezi beach tuna nyumba sita na walinzi tu, yaani tafuta wakazi, kwa hiyo wewe ndo utachagua ni wapi tunapozi utapewa dereva na wafanyaazi wa kukutunza
10 baba bado wamo, yaani serikali inamtegemea yeye kwenye maamuzi makubwa tu ya kifedha na pia kichama, kwa hiyo hakuna wa kukugusa pale. 
Na hapa nikitoka, nadhani tutaenda na ndege yetu private i hope hapo mambo ya huyu kaka unayemtaka wewe yamepungua kidogo, he is a good guy kama ninavyosikia kwa wanaomjua ila nafikiri nimemzidi resume kidogo ila tu labda yeye anaonekana anamapesa kwa vile ni investment banker. ila taarifa za ndani ninazopokea ni kwamba yeye ni muhudu kule NY kwa hiyo hakufai, Niandikie . 
cordially, 
David.


lmaolooool david the young millionare..ana mi account kila nchi, nyumba sita unafanya kuchagua tu..baba waziri wa fedha hahaha jama naomba aliyemuelewa aniambie hio #8amemaanisha nini ??
ReplyDeleteDada jovita nenda www.haki-hakingowi.blogspot.com kunajamaa anatafuta mchumba na sifa zake alizoweka ni zile ulizotaja hivyo hivyo.ushindwe mwenyewe sasa achana na huyo david hajui hata kuhesabu ana miaka.eti kazaliwa sept 1981 alafu leo hii ana miaka 28.
ReplyDeleteWewe bwana mi utaanza kuniudhi...nani kasema kisa watu wamekutukana basi umekosea???katika karibu kila kitu majority huwa ghorofani patupu na wachache wamejaaliwa....
ReplyDeleteU did wat u thot was Ok n' it worked,trust me katika hao wote waliokutukana zipo mails hata kama ni kumi lkn za watu ambao wana nia ya kweli na wako tayari kumaliza maisha yao duniani na wewe sasa kujilaumu ni kama kukata tamaa hali ushindi upo upande wako.....
Kama hawa jamaa wanavyosema(not me) cha muhimu kuendeleza libeneke....Usiache kufurahia kisa kuna baadhi ya wapuuzi wanaona umekosea wakati u took the right measure.....
Nway sina la zaidi,zaidi ya kusema happy holidays n' jiandae kukutana na mtu uliekuwa unamngoja(mr anonymous).........
KAKA MICHU/SUPU/DIKO PULIZ WEKA HUU WARAKA KWA BIBIE HAPO....MI MAVIGEZO NNAYO YOTE ILA WACHA NIMINYE PEMBENI.....
Mwishimiwa David, nnapenda kukuambia kuwa huwezi kumsaga mwenzio kwa sababu ya mwanamke!! ni kweli huyo dada nia yake ni nzuri sana ya kutaka mchumba lakini vigezo alivyotumia ndo vimeleta hizo bad responses.Na kama baba yako yuko serikalini nani anajali ?? kama yuko kwenye chama kwani ni kitu gani ??
ReplyDeleteSijui mara ndege, mara tuna nyumba nyingi mbezi... sasa weye huyo dada amekuambia kuwa anataka nyumba???
Be wise man do not talk nonsense.
Ooh nimesikia ni mtumishi NY City sasa weye inakuhusu nini?? Hayo si maisha yake..weye unasema ooooh tuna nyumba mbezi weye na nani ??
Kuwa mtu mzima weye,ni nyie ndo mlimtukuna dada wa watu kutokana na hayo mijimaneno yanu ya DHARAU.
Nyie wakina Washokera,Waitu,Bishanga mnamatatizo ya DHARAU.
I hope that you`re not offended with my strong language at the END.
CHILL OUT,STOPIT.
Kama umekasirika na umesema uko OHIO basi waweza nipigia simu 610-473-839.
Thanks.
Huyu msichana kajitakia mwenyewe haya yote. Haiwezekani kupata mchumba makini kwa mtindo alioutumia. Angejaribu pia kuwauliza waliofanikiwa kupata wachumba na waume wazuri, wangempa ushauri kuhusu jinsi walivyofanya, kuliko hii ya kujaribu kila kitu kwenye mtandao. Mtandao wa kompyuta ni kama zoleo lisilochagua, kila kitu kimo ndani kuanzia mahubiri mazuri ya kuwafundisha watu jinsi ya kuumfuata mwenyezi Mungu hadi yale maelekezeo ya kwenda jehannum! Kuna maandiko ya wasomi wa hali ya juu, na ya vichaa pia yamo humu. Ni virtual world! Ningemshauri huyu binti atafute mchumba kwenye real world, ajichanganye na watu halisi katika jumuia aliko, ashiriki shughuli zenye heshima kwa binadamu, kama vile ibada, kazi halali, harusi za wenzie, shughulu za hisani, misiba, sherehe, na mambo mengine ya kijamii, huko atakutana na binadamu halisi, miongoni mwao atakuwepo mchumba. Ndivyo sisi tuliyopata wachumba tukaoa na tuna furaha sana.Kutafuta mchumba kwenye internet (virtual world ambako huna nafasi ya kujua ukweli halisi wa wanaokuandikia) kunaashiria upungufu wa mhusika katika mawasiliano yake na jamii! Ndugu Michuzi hebu mshauri aangalie hili, uhusiano wake na jamii inayomzunguka ukoje? Anashiriki hayo niliyoyataja? Huku kwenyewe yalikoanza haya mambo ya internet dating watu wamekutana na vituko vingi, wapo waliopoteza zaidi ya mwaka kuwasiliana na "mchumba" waliyempata kwenye internet, wakaja kugundua ni katoto ka miaka 9 kalikuwa kanamsanifu! Na kalikuwa kanatuma picha za mtu mzima na kalikuwa na maongezi mazuri sana, tena romantic kwelikweli! Tusilemazwe na internet, tuishi maisha halisi kwenye jamii, na huko nina uhakika kutapatikana mtoshelezano wa kiasili, ambapo yote tunayoyahitaji yamo miongoni mwetu.
ReplyDeleteAsante ndg Michuzi.
Brian J.Y. Kithuku
Pole sana Dada yetu, napenda ujipe moyo kwani haupo mwenyewe.Wadada wengi hasa watanzania wanapitia hali kama yako.Ki-ukweli,unakosea formula na kanuni za suala hili.
ReplyDeleteki-sheria na ki-katiba ya Mungu ungepaswa kusubiri mpaka mwanamume akufuate wewe.Kumbuka EVA,mwanamke wa kwanza duniani aliumbwa kwa ajili ya mwanamume[Adamu} aliyekuwa tayari anamsubiri.Hata alipokwisha kuumbwa,tunaelezwa ya kuwa yeye[EVA]hakusema lolote bali mwanamume[Adamu] ndio aliweza kum-recognize yeye kwa kusema huyu ni nyama na mifupa ya mwili wangu...!!.
Formula ni mwanamke kusubiri mwanamume amfuate,na sio kutafuta mwanamume especially kwa masharti kama uliyonayo.Kila mwanamume anaweza kufikia hayo hata kwa ku-fake tu ili akupate lakini kwake ni kama bei anayokununulia wewe na akisha kuoa basi ndio mwisho wako na itakuwa zamu yake kukupa wewe list ya sifa za mwanamke anayemtaka.Kama ndugu yako,ningekushauri tu utumie muda wako kumuomba mungu aliyeumba wanaume akupatie wa-kwako.Anao wengi wenye sifa zaidi ya hizo.
Kama huwezi kuomba,nenda kwa mchungaji yeyote aliyekaribu na wewe atakuombea na kukusaidia.
Roho nzuri ya mwanadamu hupimwa na nani kama si Mungu mwenyewe?.
Unaweza kutembea kwa mikono wakati unayo miguu na ukafika unakokwenda lakini mateso yake ni makubwa kuliko kufuata utaratibu wa Mungu wa kutumia miguu kutembelea.Nionavyo mimi unajaribu kutumia mikono kutembea angali unayo miguu.....!!.
Sijui wahenga walidanganya ya kuwa Kibaya chajitembeza na kizuri....!!
Nakupenda kwa upendo wa kristo YESU na ninakuombea uokoke na Yesu atakubadilisha maisha yako..!!.
UBARIKIWE..!Kwasiri@yahoo.com
Ee bwana ndioo! mshikaji kajikanyaga mpaka mwisho.
ReplyDeleteItabidi nae tumfuatilie inawezekana baba yake ni mmoja wa mafisadi.
Hili ni bonge la msala, yaani aibu kinoma kutongoza gani huko kwa kizamani namna hiyo.
UFISADI NDANI YA MAPENZI
ReplyDeleteWow, Wow. I suggest you keep them emails from Vingunge, I must say you have done a great job for walalahoi of all Tanzanians. These will creep bear of their ill intentions. I may Call it UFISADI NDANI YA MAPENZI- in short UNYAMA means Ufisadi Ndani YA MApenzi.
It is the purpose and aim of civil citizens of Tanzania to understand, these creepy vingunge in our government must be exposed, whenever it is necessary.
I would suggest don't ever DELETE THOSE MAILS, keep them in hand. Also I must add that you are doing a good job in SUDAN, and you will be doing a good job in Tanzania by exposing these vingunge-fanatics and you will receive protections doing just that, they are no difference to al-qaeda, Stealing our wealth, and leave the poor and vulnerable abandoned on the streets, and for those hard working folks people ripped off their tax, for the ill bad of these vingunge, some and a lot of them treated abroad and for their sons and daughters enrolled on private college and universities in the WEST.
Their time will come, THANK goodness INTERNET is here to stay.
May GOD bless Tanzania, we will get rid of UNYAMA, by any means necessary.
Note: Some people will be willing to help you out on these, seek a professional help, and I would iterate again don't ever delete those mails, for your own good. They can be used in court as evidence against wanyama, if they keep stalking you or do any harm, I am not scaring you but there are a lot of crazy people in these world.
By Mchangiaji
K'babake!!!
ReplyDeleteHuyu anayejiiya David msanii kwelikweli!!
Nimependa sana email yake!!!
Jovinata mie nasema hivi mdogo wangu!!usijali kwani wamekutoboa macho?au matusi tuu!!ingekuwa mugabe anajali matusi angegombea tena zimbabwe?usijali bwana wewe endeleza libeneke lako mpaka lieleweke,,tena kama unaweza weka picha nyingine bomba kichizii,mungu mkubwa utampata mwezi wako..wako dada kyekue
ReplyDeletempenzi dada yote yaliosemwa achana nayo kukusema ndio nini?wamesemwa akini michael jackson na bado wanadunda wee tulia german kula kuku wako mdogomdogo achana na maneno kwa ufupi nimekupenda sana tatizo moja umri wangu umeshakwenda sana na akijaeleweka.ila usikate tamaa mungu yupo na wewe. nitakuchek kwenye email yako.
ReplyDeleteHihihi Kudadadadek Huyu KijanaMzuri au Kakapoa Wa DHW na JAMBO Analeta Tafrani Za Misifa Hadi Huku??? Kaaazi Kweli Kweli
ReplyDeletepole sana tena sana. ila dada jua kutongozwa ni kawaida. watongozaji huwa wana maneno mengi. ni kazi kwako kuchuja. unapotongozwa ni siri yako. unaweza kuleta ugonvi hata mauaji unapoweka bayana kila anayekutongoza.
ReplyDeletesipo katika mpambano huu ila usikate tamaa na kuchukia kila mtu.
mdau wa uholanzi
Huyo David hajui hata kufunga kamba. Naona e-mail yake imejaa contradictions. Kama anadai kwamba mambo ya mkwanja hayampi shida sasa anaogopa nini kurudi Tanzania. Kulingana na kauli yake ana dalili zote kwamba kajilipua na hivyo akitoa mguu US hawezi kurudi tena. Mtu gani mwenye mkwanja wa kueleweka anaweza kuamua kujilipua US na hivyo kujivurugia mambo yake ya baadaye? Hapo nimeona jamaa anapeleka usanii ndani ya jumba la sanaa.
ReplyDeletePia huyo dada mhusika anatakiwa kuwa makini, kuna watu kibao wanatumia majina ya watu wengine kwa ajili ya kukomba u-spoon. Nina mashaka hata huyo David anaweza kuwa katumia jina fake ili aweze ku-win nomination!
Yaani kweli kabisa David umenichefua kwa kujifagilia kusikokuwa na mpango wowote kwa sababu kujifagilia siyo vigezo alivyotaka Jov mara mna nyumba sita ataamua ipi ataishi atatuzwa na walinzi sasa kaolewa na walinzi au umeoa wewe? fikiri kabla ya kuandika Jov anataka mume mwenye utu na siyo vitu labda ulikuwa hujamwelewa, nyumba za Baba yako zinahusiana vp na luv baina yako na Jov?
ReplyDeleteKatochi)
Michuzi sasa funga huu mjadala, tuzungumze mambo mengine muhimu.
ReplyDeleteushauri wa bure kama kweli unataka mchumba kuna site nyingi sana za dating na kama utaki hizo ingia ktk social site una unapata marafiki kila siku then unapata mchumba humo humo,jiunge facebook,hi5,babe etc ukiwa na mtu unamjua toka mbali inakuwa rahisi kuwa mchumba kuliko kaka misupu akulekebishie hapa ndio maana unapata matusi pole sana na ktk hizo unaweza kuwazuiha watu na kuwatosa kama hawana picha so be makini na take it easy,kingine change mail address yako na hiyo funga kwa muda so majinga yagonge ukuta kwanza na matusi yao.kila la kheri na kupata mchumba
ReplyDeleteJovinata acha utoto, kubali criticism, waache watukane mchana usiku watalala! Wengine ni wagonjwa na wewe ukikasirika utfall kwenye mtego wao wa kukufanya na wewe mgonjwa wa akili. Matusi! Hayo matusi ni ya watu baki huwajui hawakujui, yachukulie kama phase ya maisha imepita. Badilisha email address yako, katika hioz email ulizokwisha pata chuja hapo utampata mtu ambaye unamtaka, zenye matusi delete.
ReplyDeleteSikia hiyo ndiyo dunia ndugu yangu, hao ni watu baki wamekutukana hesabu kuwa wamekufanya uwe strong kuweza kukabili challenge za maisha. Utakapoolewa hayo matusi ya watu baki hutayaona kitu watakapokuja mawifi na mama mkwe kukutukana bila sababu ya msingi.Au hawara ya mumeo atakapokupigia simu na kukutukana matusi ya nguoni (Temea mate chini Mungu apishie mbali balaa hilo). Hapo ndipo mdogo wangu utakapojua uvumulivu maana yake nini. Haya matusi ya watu usiowajua wala hujawahi kuwaona, delete wala usijisumbue kufikirisha kichwa chako. Subiri challenge za ndoa, sikutishi ila nakuhabarisha hali halisi ili ujue huko uendako kuna challenge na inabidi uwe very strong kuzikabili, hasa kutoka kwenye kabila la huyo kaka umayemzimia.
Mama aliyeolewa!
Anony 2:30 nakupa 5. yaani umeongea kweli tupu!!!
ReplyDeleteAno. April 06, 2008 2:05 PM,
ReplyDeleteNani kakwambia face book ni dating site au ujinga face book, my space intelli...kama ujui tunawafuatilia kila sehemu na kujua kila kitu kuhusu...kuna dating sites achana na hizo zitakumiza. David wahangaza ndio mpango wa Cd's huo duh alafu si useme tu mi muhaya uhangaza ndio nini, hesabu bado alafu unarudha ndege sound phising buddy!!!
Central London
Girl acha kulalamika. Umepata ulichoomba, katika 6,200 huwezi kosa mume hapo, kaa cjhini acha uvivu, chambua, tumechoshwa na hii malalamishi kwa kuwa wewe ni msomi na ulipaswa kufahamu kuwa mabo haya yatatokea na zaidi uliona mfano kwa waliopita sasa usilalame sana. Sisi kama wadau tumesikia shida yako na tumejituma kujaribu kuitatua. Isipokuwa tu wengine midomo yetu mizito, hatujui kujieleza, tunaposema malaya tunamaanisha wewe ndo mama hasa utufaaye, kiburi tu tumejaaliwa.
ReplyDeleteTumia shule uliyonayo kaa chini pitia kila barua na utoke na jibu.
Mbona hao walokuandikia mambo safi hutuletei tujue walichosema?
Katika 6,200 ukishindwa kupata mume, wewe ndo matatizo.
Bye for now
wewe anon wa april 06,2008 10:49 pm,
ReplyDeleteSoma kwanza ndio ukosoe nilisema kuna dating site kibao na kama utaki hizo kuna social network kama facebook,hi5,bebo etc sasa ukiwaza na kusema kuwa unaingia kila siku kutizama wewe ndio maphidaphiles(wabakaji)kwa kisa cha kuchunguza life ya watu kisa unawataka??acha ujinga wewe,na box zako huko central london.unatakiwa kufagia train mida hii za ken mayor wenu wa london
nashangaaa dada analalamika nini. na hiyo email alitaka kuprove nini? naona sasa anakuwa stupid na anakuingiza na wewe michuzi kwenye ustupidity wake.
ReplyDeletemtu si anajipigia debe tu au? hiyo ndo kaiona imemtukana au?
dada hueleweki ....
utawaanika wapi? iwapo michuzi atakubali kuchukuwa emails zenye kuwaanika watu hapa wakati watu walifanya kitu privately kwako nitamjua hafai, na hana maana.....bora akuoe yeye. (maana itakuwa lazima ana macrush kwako au asingeweza kufanya upuuzi huo wa kuwaanika watu majina, kwa kuwa wamekutaka!)
ReplyDeletesasa Jovinata unalalamika nini? kwani ulitaka kusikia unachotaka tuuu,umeweka picha yako na unachotaka na hakuna mtu alikumbia uweke vipi message yako,sasa ukijibiwa unaanza kulia lia umetukanwa...just ignore what you dont like,na kwa nini umetoa email ya watu hapo huoni kama ni violation of privacy,na sioni kibaya jamaa alichofanya zaidi ya kukuambia anachoamini na jinsi alivyo,sasa naanza kuamini una matatizo wewe na usipoangalia hutapata mwanaume kabisa,ulitakiwa ushukuru kwa kujibiwa na kuanza kuwajibu waliokuandikia sio kuwaumbua watu na kutoa vitisho,kila la kheri na kutafuta kwako mume ila nina wasiwasi sana na judgement yako.
ReplyDeleteMdau Beverly hills!
Ano.April 07, 2008 1:52 PM
ReplyDeleteWe mchumba tu ndio unazojua hizo!! Punguza hasira kaka ukibahatika siku moja njoo uone, utajua sijui unapumulia wapi vumbi eh! In shortly ujui kitu so nyamaza alafu jitaidi ukusanye hela uende shule
Kaka Michu, hivi huyu Jovi.. anahitaji mabwana wangapi? Kama ninavyofahamu mimi anapaswa kuwa bwana mmoja. Kama hivyo ndivyo, katika mkusanyiko wa e-mail hizo 6200 na pengine zaidi sasa, hawezi kukosa mtu mwenye nia hasa ya kumuoa, mmoja tu. Naomba tumuombe aache lawama kwanza, akae chini na kuchambua barua alizopata. Lazima atatoka na shortlist ya watu kadhaa, pengine 100 hivi au 20 au 5 au pengine mmoja tu mwenye nia ya kumuoa. Hivyo basi ndo kusema kuwa shida yake imekwisha tatuliwa, labda kama alikuwa anahitaji kila mwanaume ampende na aonje wote hapo atalalamika kuwa katukanwa na kadhalika, ila kama nia ni kupata candidet mmoja tu, humo hakosi na akikosa yeye ni matatizo makubwa anahitaji msaada wa kisaikolojia.
ReplyDeleteLakini, ninataka kufahamu inakuwaje dada wa Kitanzania, alieishi na kusoma Bongo, ughaibuni na sasa yupo kazini na ni mzuri kama yeye akose mtu wa kumuoa? Mambo mengine braza Michu tutakuwa tunawalaumu wadu bila sababu, kwa kuwa wengi wao hawaelewi ni kisa gani hasa kwa dada kama huyu, umri huu, na exposure yote hiyo asiwe na mwanamume pembeni mwake.
Wote tunajua tunavyoishi Bongo na kiwanja, makazini na sehemu zote za mikusanyiko ya kijamii. Inakuwaje dada kama huyu asiwe na mtu? Haya ndo mambo wadau sisi hatuelewi na tukiambiwa tunaona tunazinguliwa kimtindo.
Tujaribu kuwauliza wadau humu wanaowagfahamu watu hawa, ambao wamekuwa nao na ni marafiki au mabwana zao waliopita pengine wanaweza kutupa ufumbuzi hawa ni kina dada wa namna gani, kitabia na interaction yao na wanajamii.
Braza Michu, kutokana na uzoefu wangu na mabo ninavyoyaona hapa duniani, watu hufahamiana mashuleni, katika mikusanyiko ya kijamii, kwenye madaladala, sokoni, msibani, mitaani wanamoishi, makazini, kwenye michezo, na kadhalika na kadhalika. Sasa hawa kina dada wao huko kote hawajaweza kupata watu kweli?
Sometimes, watu hupata wenza kupitia kwa wapenzi wa marafiki zao, yaani kama mimi nina demu sehemu na demu wangu ana rafiki yake, iwapo rafiki yangu hana ngozi, basi tunaongea tu na mamaa ana mhook na rafiki yake au ndugu yake au ndugu ya rafiki yake.
Sasa inapokuwa hawa kina dada wanakuja humu kutafuta wenza, inakuwa haikai vizuri akilini mwangu. Naanza kufikiri na kuchambua inakuwaje huyu akose mtu mpaka sasa iwapo ni mtu ambaye yote niliyoyaeleza hapo juu yanamgusa? Na nafahamu wadau wenzangu pia swali hilo linawakumba na ndo sababu wakiona hakuna uwiano huamua kuponda. Kwa sababu it doesn't make sense.
Jambo hili laweza kuwa kweli kwa mwanamume, kwa kuwa kikwetu yeye ni lazima atongoze mwanamke wa jinsi anayotaka yeye, na mara nyingi huwa kuwa ni mwanamke ambaye karibu kila mwanamume anamuona anamfaa, hivyo hujikuta katika mashindano ya kumpata bibie, hapo wanaume wenye roho ndogo hukaa pembeni wakisubiri wapigiwe pasi na dada zao au rafiki zao na wakikosa ndo hukaa singo mpaka wanakuwa watu wazima hawajawahi kuwa na ngozi, hii si utani, namjua rafiki yangu mmoja pale arusha, hawezi kabisa kuongea akiwa karibu na ngozi hasa kama ndo umemletea mzigo.
Hii ni tofauti kabisa na upande wa wanawake, hasa wazuri kama hawa kina Jovi, kwa kuwa wao kitendo cha kuvaa safi na kupendeza, wanapotoka tu nje ya kizingiti cha mlango wa nyumbani kwao, hapo hapo watu macho nje na huanza kuwafuatilia, na wanaume wote wanapenda wanawake wazuri na wenye uwevo wa kujitegemea waweze kuwasaidia katika maisha. Ina maana huyu Jovi na mwenzake Mamnka wao hawatongozwi? Braza Michu wanawake hasa wazuri hutongozwa kila siku.
Nimerudi tena, mada imenigusa sana.
ReplyDeleteDada Jovi unamtaka Mashaka, OK, si tatizo. Kama hivyo ndivyo kwa nini usiombe email y ahuyu jamaa ukamuandikia kuhusu shida yako moja kwa moja na akakujibu huko, nasi tusijue kilichotokea? Badala yake wewe ukaja humu unafuta mchumba, halafu hapo hapo unamtaka Mashaka. Si ungesema kuwa unaomba wadau wakupigie debe kwa Mashaka? Pengine ingekuwa na positive response.
Sasa haueleweki, unamtaka Mashaka au unatafuta mchumba? Hata kama mimi ningelikuwa Mashaka nisingelikuandikia, kwa kuwa huna msimamo na unachokitaka, kama ni mimi mashaka unanitaka, ungelisema ninakuomba bwana Mashaka niwe mpenzi wako. Na si kuomba penzi kwa Mashaka na wakati huohuo unaalika wanajamii nao walete qualification zako.
Hili tu ni upungufu kuwa hujatulia na inaonesha kuwa huna msomamo na pengine ndo sababu hasa inakufanya hadi leo huna mwenza. Wanume tunataka wanawake wenye msimamo. tunataka wanawake wanaoseam kuwa, nakutaka wewe na wewe peke yako, si wewe lakini na wengine walete maombi yao nione kama wanafaa.
Kosa kubwa sana kwa mwanamke kuwa macho juu, kupata mume wa maana inakuwa ngumu, kwa sababu wanaume bora hupenda kuwa na wanawake wanaamini wataishi nao milele waweze kula familia pamoja. Akikuona macho juu, naye anaegesha akitafuta mke anayemfaa.
KUWA MWANGALIFU NA UNACHOOMBA.
Nyie wakina Washokera,Waitu,Bishanga mnamatatizo ya DHARAU.
ReplyDeleteI hope that you`re not offended with my strong language at the END.. We ndio unaleta ukabila comment za David zimesababisha wa2 wa Kgera kuwa na dharau?? Wazimu
nikisema jovinata una matatizo naona nitakuwa sijakosea. ....mtu kakuandikia mail privately kwa kumpa email yako mwenyewe kwa khari yako, kuja kuianika ni kuonyesha upeo wako mdogo katika kutafakari mambo.
ReplyDeleteisitoshe wewe mwenyewe sio humble kwa sababu sikuona sababu ya wewe kusema upo likizo ujerumani sasa hadi tarehe 9 ( coz haiwezi kusaidia kitu katika huu mjadala wako hapa unless ulikuwa unataka kujifagilia au unataka kumpa hints mashaka kama akufate ujerumani)
dada kama unataka kuwa humble acha kutoa information ambazo hazina msingi, la si hivyo thamani yako itashushwa igaregare kama ikiwa haijafika huko bado!
Wewe msichana grow up...wewe ulitegemea kila mtu atakujibu email according to your dreams????
ReplyDeleteNilikuona wa maana mwanzoni lakini baada ya kuona unapost email za watu huku nahisi wewe ndio una matatizo...
Si mambo ya private hayo....???kama hupendi alichosema delete...kwani hujui wabongo wanavyotongoza....Na wewe ulivyoeleza habari zako na familia yako ulitegemea wao wasikueleze habari zao?
Kwanza pressure za nini kutafuta mchumba na umri huo ...???? Kama vile hujaelimika au hujatoka nje ya nchi...????? Bongo ndio kuolewa muhimu ukiwa mdogo lakini kama unatembea nchi za nje I think you know...
kwa mapost yako haya I think you are not well matured....You know unaweza kukua umri , elimu but maturity growth can be a fugly process and that is unreachable to some.
Tulia tu utapata mume....
bibie...sasa kilichokutuma kuweka habari zako hapa Michuzi nini? umetendwa vilivyo sasa..usilalamike ..u cant always get what you want, kama mtu hapo juu alivyosema ..chambua izo email zako mama huwezi kosa aliye desperate like yourself..
ReplyDeletesiulitaka chai chai..sasa unalalamika unaungua....sikiliza hiyo nyimbo ya juma nature ya kkitambo kidogo
ReplyDelete