Habari yako Michuzi, Naomba uwawekee wadau wenzangu fumbo hili la hesabu ambalo mwalimu wetu wa hesabu darasa la tano mwaka 1979 ktk shule ya msingi Igoma - Uwemba alitupa.
Watu watatu walikwenda motel:
Receptionist akawaeleza kuwa chumba ni shilingi 30, hivyo kila mtu alitoa shilingi 10.
Watu watatu walikwenda motel:
Receptionist akawaeleza kuwa chumba ni shilingi 30, hivyo kila mtu alitoa shilingi 10.
Kisha wote watatu wakaenda chumbani.
Baada ya muda kidogo receptionist akagundua kuwa bei ya chumba ni shilingi 25. Akachukua shilingi 5 akamtuma mhudumu ili akawarudishie wale jamaa. Lakini mhudumu hakujua jinsi ya kugawanya zile shilingi 5 katika sehemu tatu zilizo sawa, hivyo kila mtu akamrudishia shingi 1 tu na shilingi 2 akajibakizia…..
Hivyo inamaanisha kuwa kila mtu mwishoni amelipa shilingi 9… si hivyo jamani??
Kwahiyo jumla ni shilingi 27…. si hivyo jamani??
Mhudumu kabakiwa mfukoni na shilingi 2.... si hivyo jamani??
Hivyo jumla ni shilingi 29 .... si hivyo jamani??
Sasa ipo wapi hiyo SHILINGI moja??????
Sasa embu ichanganue hiyo kisha tupeane jibu....
Wasaalam
Revd. EVM,
Prague


Simple, Inamaana jamaa walilipa sh27(9*3) badala ya 25!! sh 2 ndo wameliwa na msaidizi wa receptionist!!
ReplyDeleteAlipogundua kuwa chumba ni shillingi 25 na huku alikuwa kapokea sh.30 alichofanya ni kurudisha shiling 5 na hivyo kabakiwa na sh. 25..na huyo mhudumu alicho fanya aliwarudishai sh. 3 ambazo ni sehemu ya ile sh.30 na hivyo kuwa 30-3(alizowagawia kwa ajili ya umbumbu wake wa hesabu)=27, na 27-2(alizochukua kwa ajili ya umbumbu wake wa hesabu na ufisadi kwa pamoja)=25, hivyo sioni hiyo shilingi moja inatafutwa wapi tena...labda nawewe uwembumbu wa namba. Lakini mahesabu yamekamilika....solve hesabu kama vile unakataa maji ya ngano(mbia), maana maji hayo yanakatwa kwa kusonga mbele na hesabu usiianzie chini anzanayo kule juu...yaani anzia kule sh.30 iliko ndipo utapata muafaka wake vizuri.
ReplyDeleteHesabu hazifanywi kama Makamba anavyosolve issue ya Muafaka Zanzibar..kwa kutumia mbinu alizojifunza Kigoma miaka ya 70 akiwa mwalimu wa shule ya Msingi...
Hisabu siyo uzoefu ni commonsense.
Cheers.
Okay, hii kitu ni ya zamani na jibu nimesahau....ila
ReplyDeleteShilingi 30, Ukitoa zile tatu alizorudisha zinabaki 27. Toa mbili alizonazo zina baki 25. sasa sijui hizi hesabu mnajifunzia wapi.
30/= - 3/=(jamaa watatu) = 27/=
and
27/= - 2/=(kachikichia) = 25/= (walizolipa)
Kama hapo mahali palikuwa na kimwana Basi Mhudumu alihonga.
-BooSt3D.
MDAU SH 1 IMEENDA KWENYE SH 25 YA CHUMBA KWANI walirudishiwa sh 5 ambayo kila mtu kapewa sh 1 na hesabu ikakupa kwamba kila mtu katoa jumla sh 9 inamaanisha mwanzo kila mtu alikuwa katoa sh 8 ambayo mara 3 inakupa sh 24 kwahio sh 1 imeongezewa kutimiza sh 25 ya chumba.
ReplyDeleteMdau wa darasa la pili.
hakuna fumbo lolote zaidi ya muuliza swali kufanya hesabu zisizo sahihi. Kwani baada ya kurudishiwa Tsh1 kila mmoja, jumla ilikuwa wamechanga Tsh 27. Kati ya hizo Tsh 25 ni za chumba, Tsh 2 mhudumu katia ndani
ReplyDeletebwana eeh kama chumba sh. 25 akarudisha sh. 3 zinakuwa 28 then mbili kasunda mwenyewe
ReplyDeleteHakuna kilichopotea, shilingi 25 wamelipia chumba, shilingi 3 wanazo wao, na shilingi 2 kabaki nazo mhudumu, jumla ni 30. Hiyo 27 unayosema (9 x 3) inahusisha pia hiyo shilingi 2 aliyobaki nayo mhudumu, kwa hiyo ukiiongeza tena hapo unakuwa umeihesabu hiyo sh 2 kwa mara ya pili. Hiyo 27 inapaswa ijumlishwe na zile sh 3 walizorudishiwa, utapata 30.
ReplyDeletewewe amna hella iliyobaki in short, cause kama wewe uliwarudishia tsh 3 plus 25 ni 28 na hella aliyobaki nayo mhudumu ni mbili so its 30tsh.
ReplyDeletehuyo mhudumu ni mwizi. kama wangelipa 8 mara 3 ingekuwa 24 wangedaiwa moja. hiyo moja ndo inawekwa kwenye hizo walizopewa na kufikisha 28. kwa hiyo 9 mara tatu jumlisha moja na hizo mbili za mwizi ni 30
ReplyDeletehuyo muhudumu mwizi na wala tusimtetee.
ReplyDeleteMbona simpo, hizo 2 za mhudumu usiziweke kwenye mahesabu kwanza. Jamaa watatu wametoa 10 kila mmoja. Wamerudishiwa 1 kila mmoja, hawajui kuwa mhudumu kabaki na 2, kwa maana hiyo basi wao wanajua wamelipia chumba kila mmoja shs9, jumla: 9 x 3 = 27. na zile walizorudishwa 1 x 3 = 3. Na 3 + 27 = 30. Hivyo kwao mahesabu yamekaa vizuri.
ReplyDeleteMtego wenyewe unaanzia na mhudumu kutowaeleza ukweli kuwa chumba ni 25 badala ya 30 maana amewarudishia kila mmoja 1 bila kuwaeleza bei halisi ya chumba si ajabu wangeidai hiyo 2 aliyotia ndani.
Ngoja nikokotoe jibu hapa, mimi nilikua kipanga wa hesabu:-
ReplyDelete1.Malipo waliyofanya = 25 Fedha halali na shillingi 2 alizobaki nazo mhudumu= jumla 27
2.Shillingi 3 ni zile walizorudishiwa na mhudumu ambazo kila mtu alipewa shillingi 1
Ukijumlisha 1 na 2 hapo juu= 30!!!
hakuna shillingi iliyoliwa na FISADI zaidi ya maskini mhudumu alizochukua.
wametoa 10 x 3 = 30
ReplyDeleterudishiwa 1 x 3= -3
jumla imelipwa -27
bei ya chumba -25
inabaki 2 ambayo ni TIP ya mhudumu
1. 30 - 5 = 25
ReplyDelete25 + 3 (walizorudishiwa) = 28 + 2 (alizochikichia)
2. 25 (malipo) + 2 (alizochikichia) + 3 (alizowarudishia) = 30
Naona ndugu zangu wengi humu hawajajibu swali la huyu jamaa bali wanajichanganya nitakujibu kwa ufasaha kwani hesabu ni Formula kwanza unakumbuka BODMAS (Magazijuto) katika hesabu unatakiwa uanze kugawanya kwanza halafu unazidisha halafu unajumlisha na mwisho unatoa.
ReplyDeleteSasa walipotoa Tsh30 wkapunguziwa tsh 5 walibakiwa na shillingi Tsh25.tuanze mahesabu sasa 25/3 ni 8.33333333333 sawa. Sasa Mhudumu alipowarudishia Tsh 1 kila mmmoja maana yake 8.33333333333 + 1=9.3333333333.Sawa waheshimiwa na yeye Mhudumu akabakia na Tsh 2.Sasa tunakuja kwenye jibu 9.33333333333 *3=27.9999999999 ukijumlisha na Tsh 2. alizochukua Mhudumu jibu linakuwa
27.9999999999 + 2=29.9999999999. Kitakachobaki hapo ni senti moja na kwa wanaojua hesabu wataelewa kwa nini hiyo senti moja inabakia.
Senti moja inabakia kwa sababu Tsh 2 hawakugawana wao bali Mhudumu alikuwa nayo na alipoirudisha ikaongezwa kati ya jumla ya fedha walizogawana.
Hilo ndilo jibu na mwalimu wako alikuwa anakuchallenge ili ajue kama kweli unajua formula ya hesabu BODMAS au MAGAZIJUTO ambao ndio Msingi wa hesabu
Popo,Londoner........
Jamaa walianza kwa kuchanga sh. 10 kila mmoja kutimiza shilingi 30.
ReplyDeletePasipo wao kujua katika mchango wao wa awali, mhudumu alijipa takrima ya shilingi mbili kwa hiyo wakajikuta wamechangishana shilingi 28 kwa ajili ya chumba. Baada ya kurudishiwa shilingi moja moja kila mmoja (jumla shilingi tatu) basi ikawa kwamba kwa ujumla wao wamechangishana shilingi 25 kwa ajili ya chumba. Utaona kwamba Sh. 25 ndio gharama halisi ya chumba.
Swali kubwa hapa ni kuwa jamaa walipona vipi kufisadiwa dala kwenye chumba badala yake wakapigwa bao chuma bee tu.
YAANI KWELI NIMEAMINI WATU VICHWA VIGUMU... APART FROM AUGUSTN WENGINE WOOOTE MCHEMSHO
ReplyDeleteyaani kila mmoja kang'ang'ania kulipa shilingi 9..na kusahau kuwa whatever walichorudishiwa they can now calculate from there. in total watakuwa wamelipa hs 28 therefore... kila mmoja atakuwa amelipa 9.33333333 sasa ukijumlish hizo .3333333 ndio hukoo utakapoipata hiyo shs 1... au vipi bwana
3 people
ReplyDeleteprice 30 per 1 room
3 people pay=30
receptionist new price=25
reception hold 2
give 3 divide by 3=1
so 10 less 1=9
9 times 3=27
27+2recept.=29
?1
BODMASS APPLICABLE
1.DIVIDE
5DIVIDE3=8.333333333
8.33333333 ADD 1=9.3333
9.3333333
@3
27.99999999999
27.9 PLUS 2
29.99999999
1 CENT ITS DIDNT DIVIDE
Teteeeeee kwani risti ilikuwa imeandikwa shilingi ngapi? kama risti haikurekebishwa basi mambo bado ni magumu magazijuto wala majunguzo hayaleti majibu. Turudi kwenye risti kwanza
ReplyDeletePBawa
Muhudumu alikuwa na haki ya kuwafisadi hao jamaa koz mwaka1979 mitaa ya kuumeni(TMK)nyumba shing' salasini unapata;sa iweje wao wajishaue kulala hotelini kwa bei ya kununulia nyumba?
ReplyDeletewe anon wa Apr 14, 11:24pm ndio mbumbumbu wa kutupwa. Kwani unakuja kujifanya unajua halafu ndio unachemsha. Kila mtu katoa Sh.10, kisha akarudishiwa Sh. 1, unasemaje kuwe kila mtu katoa net Sh. 9.33333? Ingekuwa wamerusidhsiwa Sh.2 wagawane ndio ingekuwa sawa na kutoa Sh. 9.3333 kila mmoja. Lakini haikuwa hivyo, walirudishiwa Sh. 3 wagawane. So hela iiliyobakia kwa mhudumu ni Sh. 27, Sh. 25 ya chumba... sh 2. jamaa katia ndani
ReplyDeleteAugustine what you are arguing is essentially correct and is no different from what the rest of us said. Hesabu ina njia nyingi, na usifkirie njia 1 ikiwa sawa nyingine sio sawa.
ReplyDeleteUlichofanya wewe umechukua
3*(8.3333333 + 1)
Lakini ukifungua mabano kwa kufanya hiyo bodmas uliyoitaja utaona kuwa unapata
25 + 3 ambapo 25 ni ya chumba na 3 ni chenji waliyoridishiwa. Plus the Sh 2 alizokula jamaa unapata 30.
Which is exactly what everyone else before you said
MICHUZI NAFURAHI SANA KUONA WATU WANADIGEST ISSUES HIVI MUNGU AKUBARIKI NA KUKUZIDISHIA MICHUZI UTUPE VITU KAMA HIVI WATU TUCHEKE NA UZEE USITUTEMBELEE KWA HARAKA MAANA MAJUKUMU YA UZEENI YANAZIDI SEHEMU KAMA HIZI ZINATUFAA ANGALAU KUCHANGAMSHA BRAIN KWA SAA HIVI SAFI SANA MJADALA HUU UMENICHEKESHA SANA HASA YULE ANONY WA PALE JUU ALIPOSEMA MHUDUMU MBUMBUMBU NA UFISADI JUU YAANI NIMECHEKA SANA KWELI WATU WANAVITUKO.
ReplyDeleteHaya sasa vile vichwa vyetu vibovu ndio tunaviona hapa hapa bila hata kwenda mbali ndio maana kumbe watu wanakuwa wagumu kuelewa na kuponda sana kumbe kichwa empty daa kweli leo nimeamini sasa maana 90% ya waliojibu ni ziro kabisa.
ReplyDeleteKweli kumbe kina balali hawajaanza siku hizi!!!
ReplyDeleteboo.. tu shilingi tuwili jamaa kakitia mfukoni.
halafu inaonesha kuwa huyu ticha ndio katiwa ndani shilingi 2 zake akajidai fumbo ili akapate kudai. tehetehe.
mdau wa risiti hapo kaongea la maana, inaonesha hawa jamaa hata VAT hawajalipa.
Mhudumu nae njaa tu inamsumbua.
Wadau jibu sahihi, ni kwamba shilingi moja walinunuliwa mishikaki ila jamaa hajaeleza hapo juu vizuri!
bila shaka hiyo guest ni ya bwana Balali.
ReplyDeletehilo halina ubishi.
Hesabu rahisi sana hiyo kama walikuwa watatu wakatoa shilling 30 wakarudishiwa 5 sasa chukua 30-5=25 chukua 25 jumlisha 3 walizogawana =28 baada ya hapo chukua 28 gawanya kwa idadi yao ambayo ni 3 ujue kila mmoja alitoa shillingi ngapi maana yake 28/3=9.33333333 *3=27.9999999 jumla ya waliyotoa ukijumlisha na shillingi 2 alizobakia nazo unapata jibu alafu kuna kuaproximate kwenye hesabu point ikiwa tano na kuendelea basi inakuwa kamili wadau mpo???
ReplyDeleteFumbo mfumbie mjinga, Mwerevu ......,
ReplyDeleteKwanza kabla ya kujibu naomba kupata ufafanuzi kiodgo kutoka kwa muuliza swali, hao jamaa watatu walikua wa jinsia gani???,
Waliingia wote watatu chumba kimoja kufanya nini??
Walikaa muda gani huko chumbani??
Na mwisho walipotoka walikua katika katika hali gani, ya uchivu au uchangamfu??
Baada ya mwaswali hayo jibu ni kwamba hakuna cha Magazijuto wala nini, hapo ni Uliotumika ni U-richmond uliobalaliwa na Epalism,
Yule mhudumu awarudishie Tsh 2 yao wao watajua jinsi ya kugawana,
Au lah awanunulie mvinyo ndipo awagawanyishie kwenye glass,
Ikishindikana zaidi ndipo majibu ya yale maswali pale juu yanapokua na nafasi,
Kama waliingia kunanihii, basi mhudumu kwa kujali maisha ya wateja wake anaweza kutumia hiyo Tsh 2 kuwanunulia "Ruff Ryder" maana hatujui waliingia kufanyaje wote,
Huenda Pengine .........
Bila shaka huyo receiptionist alikuwa mzuri sana na alifaa kimini ndio maana jamaa hawakushtuka kuwa wameliswa shilingi mbili zao.
ReplyDeleteAu na wewe umbumbu umekuzidi.
Kwa heriiiiiii!
Ngoja niwaambie, Chumba ni shilingi 25.
ReplyDeletesasa 25 gawanya kwa 3 inakuwa shilingi 8
Ina maana walilipa shiling 8 kila mmoja jumla inakuwa shilingi 24. Wakarudishiwa shsiling 3 na mhudumu akachukua shiling 2. Kwahiyo ile Shilingi moja ambayo haijulikani iko wapi IKO KWA RECEPTIONIST. MAANA CHUMBA NI SHILINGI 24 YEYE AKARUDISHA CHANGE YA SHILING 5
Mh! Hapo no comment maana naona kuna mdau NALITOLELA P S keshadadavua!!!!!!!huyu aminia kipanga wangu wa obay enzi zileeeeeeeeeee (ly 94)aaaa nimefurahi sana.I gues He is correct
ReplyDeletemdau XXXL
Unauliza shilingi ya EPA imekwenda wapi wakati hiyo motel ni BOT na huyo muhudumu ni Balali?
ReplyDeleteSSM, Tz
Hivi culculator yangu iko wapi vile, duuu,hesabu hii bila culculator haipandi. Samahani kidogo.
ReplyDeleteDuuuh hivi ufisadi umeanza siku nyingi eeh? Huyo muhudumu fisadi tuu aundiwe kamati tena nashauri mwenyekiti wa kamati awe Mwakyembe na siku nyingine wasirudie kulala hotelini hizo fedha mbona wangepanga nyumba nzima jiko bafu choo sebule vyote ndani na chenji ingebaki ya kuajiri beki tatu
ReplyDeletetatizo lenu wewe na mwalimu wako hamjuai umuhimu wa kutumia mabano katika hesabu...kama mkitumia mabano hakuna shilingi itakayozidi inayotafutwa.... wakati wa kipindi cha hesabu acheni kutoroka!
ReplyDeleteMwanafunzi dawati la mbele
Haya mimi huwa najibu maswali magumu tu kama hili kwani watu wanaingia chaka mchana kweupe.
ReplyDeleteWalitoa 30
wakarudishiwa 3
baki kwa muhudumu 27
aliyobana na mhudumu 2
malipo halali 25
Gharama @ 9
kubakiwa 1@
Hakuna balance c/d or b/f
Ndimi wa kujibu maswali magumu tu.
Wadau,
ReplyDeleteNaomba wadau walio Japan tuwasiliane kwa email rakeyescarl@yahoo.ie
Ahsante.
Said.
Jamaa amekosea kuuliza hili swali namuona yuko shalo sana hakufuatilia story mpaka mwisho. Inaendelea hivi walipotoka wakapewa risiti ya sh 25 ugomvi ukazuka mpaka sasa ugomvi unaendelea.Swali ni kua utaisha lini ili balali arudi nchini ndio issue iliyopo.
ReplyDeleteWadau naomba msaada ktk last koment yangu pale katika neno verification palitokea neno kama hili 'FSADI" sijui maana yake ndio ina uhusino na EPA
ReplyDeletehii ndo njia ya kujibu hili fumbo au (kumjibu huyo mwalimu wako mlevi)
ReplyDeletemwalimu, sh.2 alizoiba muhudumu sio mojawapo ya malipo ya chumba, chumba ni sh.25, kwa hiyo huwezi jumlisha sh.25 ya chumba na sh.2 ya muhudumu alafu uongeza tena sh.2ya muhudumu ((shs 25 + sh 2) + sh.2) hii si hesabu sahihi mwalimu labda umelewa... hesabu sahihi ni (sh.25 chumba + sh.2 muhudumu = sh.27 )+ sh.3 ambayo ni change = sh.30
Muka Msambaa