Yah: MAJINA YA WENYE PASI.
Mhe,
Hadi leo kuna baadhi ya wenzetu ambao bado hawajapata pasi zao
ambazo zimeshawasili hapo ubalozini tangu kitambo. Tunaambatanisha
majina yao kama yafuatavyo
;
1. ABDALLAH SALIM ABDALLAH
2. JUMA SALEH KIMOHO
3. WILIAM DAVID CHINYAMA
4. ELYAM SOLOMON SWALLOH
5. ABDULRAHMAN ABDULLAH
6. THABIT KITWANA ABDALLAH
7. WARITH SALIM MOHAMED
8. FAKUR GULAM HUSSEIN
9. MOHAMED MAGAMBE MWADINI
10.RAMADHANI RAMADHANI
Mhe,
Hadi leo kuna baadhi ya wenzetu ambao bado hawajapata pasi zao
ambazo zimeshawasili hapo ubalozini tangu kitambo. Tunaambatanisha
majina yao kama yafuatavyo
;
1. ABDALLAH SALIM ABDALLAH
2. JUMA SALEH KIMOHO
3. WILIAM DAVID CHINYAMA
4. ELYAM SOLOMON SWALLOH
5. ABDULRAHMAN ABDULLAH
6. THABIT KITWANA ABDALLAH
7. WARITH SALIM MOHAMED
8. FAKUR GULAM HUSSEIN
9. MOHAMED MAGAMBE MWADINI
10.RAMADHANI RAMADHANI
Tunaomba ubalozi utafute njia za kuzifikisha pasi hizo kwa ndugu hao tuliowataja hapo juu.
Ahsanteni
Suleiman Nassib Suleiman
Mwenyekiti
------------------------------------------------------------------------------------------------
Baada ya mazungumzo yako na bw. Kasa Musa, khs matatizo ya watanzania tunaoishi ugiriki, tunakutumia taarifa ifuatayo inayokusanya sehemu kuu tatu:
1. historia fupi ya watanzania tunaoishi hapa.
2. matatizo makuu yanayotukabili.
3. ombi letu.
2. matatizo makuu yanayotukabili.
3. ombi letu.
HISTORIA FUPI
Watanzania wengi waliokuwa wakiishi nchi hii katika miaka ya nyuma walikuwa ni mabaharia.walikuwa ni watu wa kupita, hawakuwa na lengo la kuendelea kuishi hapa. Hali hiyo hivi sasa imebadilika.
Watanzania wengi waliokuwa wakiishi nchi hii katika miaka ya nyuma walikuwa ni mabaharia.walikuwa ni watu wa kupita, hawakuwa na lengo la kuendelea kuishi hapa. Hali hiyo hivi sasa imebadilika.
Hapa nitapenda kukugusia mabadiliko yafuatayo:
a) Hivi sasa watanzania wanaoishi hapa wanakaribia 350 na katika hao, mabaharia hawazidi ishirini!!
b)Watoto wanaozaliwa hapa kuanzia 1990,na wanaoletwa na wazazi wao toka nyumbani, idadi yao inazidi kuongezeka.
c) Hivi sasa watanzania tuna jumuiya iliyosajiliwa rasmi tangu 2002 katika mahakama ya mwanzo (5246/2002) yenye lengo la kutafuta njia za utatuzi wa matatizo yanayotukabili
2) MATATIZO YETU
Matatizo yetu yanagawanyika katika sehemu mbili kuu zifuatazo:
a) Matatizo ya ndani. ( uhusiano wetu na idara za hapa )
b) Matatizo ya nje. ( uhusiano na ubalozi wetu uliopo Italy )
Khs matatizo ya ndani, yanahusiana haswa na beaurocrasy iliyopo katika legalization.Aidha ugumu wa upatikanaji wa ajira hali ambayo inawahusu wageni wote wanaoishi hapa.
Ama kuhusu uhusiano na ubalozi wetu , hili ni tatizo sugu ambalo hutuzidishia ugumu zaidi katika matatizo yetu tuliyonayo.Na hili ndiyo tatizo kuu tunalolilalamikia kila siku tupatapo wasaa.kama huu.
Tunapoomba barua ya “family status” ili tuweze kurenew permits zetu, barua hiyo haitufikii katika muda unaohitajika, (mara nyingine hatujibiwi kabisa) matokeo yake inatubidi tutumie njia nyingine ambazo hutugharimu pesa nyingi na upotezaji wa wakati.
Kwa wale wanaoomba pasi mpya, pasi zao hufika ubalozini (toka nyumbani) na hubakia hapo muda mrefu mno. Hivi sasa kuna pasi za watu kumi ambazo zimekwama ubalozini na kila tunapojaribu kuwasiliana nao hatupati majibu ya kukinaisha. Watu hawa wamefanya maombi tangu 20/1/2007(hujakosea ulivyosoma 20/1/2007na wala siyo 2008) Alikuja hapa afisa wa ubalozi bw. Kambona.
3) OMBI LETU.
Bila ya kuwa na ubalozi mdogo hapa Athens ,tutaendelea kusumbuka,
Tunaomba tupatiwe ubalozi mdogo kama walivyopatiwa wenzetu wanaoishi uturuki.Tulishapeleka ombi letu hili ubalozini ili walifikishe sehemu husika. tulimpendekeza mtanzania mgiriki NICHOLAOS CONSTANTINIDES.
Kayu ligopora Suleiman Nassib
(Katibu mkuu) ( Mwenyekiti )Mob.+306945347085 Mob.+306943068310
(Katibu mkuu) ( Mwenyekiti )Mob.+306945347085 Mob.+306943068310


wewe unashangaa huna pass mpaka sasa hivi...!!!!! Mimi nipo USA na nilifile yangu Summer 2006 na mpaka ninavyoandika sasa hivi sinayo mpya na hii ya zamani inaexpire soon.....
ReplyDeleteNi mambo meni yanahitajika sana kubadilika katika maubalozi yetu....Nikiandika hapa nitajaza hata kurasa nne.
Yaani wanavyofanya kazi zao utazania hawalipwi au sijui ni nini. God knows
Poleni sana ndugu zetu,ninaomba kutoa maoni yangu kuwa huko mliko hakuta badilika hali ya uchumi itazidi kuwa mbaya sana,mkipata pass zenu tafuteni namna ya kuhama
ReplyDeletemsibaki huko kama wa fungwa.
lakini ningependa kuwajulisha kuwa sio ubalozi wa kila nchi ndio wanaozembea hivyo, mie ni mdau wa helsinki na ubalozi wetu uko stockholm sweden, lakini ubalozi wetu wa sweden walifanikisha kumpatia kila mtanzania wa scandinavia pasi yake mpya bila ya kuchelewa hivyo, ofcourse pasi zingine zilichelewa kidogo lakini sio muda mrefu sana kama nyie mnaosumbuliwa huko ugiriki.
ReplyDeleteHao waliokuwa huko italy ubalozini wanaonyesha kuwa issue za wabongo wanaoishi nchi za huko hawana umuhimu nazo. Too bad wenzetu bado hawajali uwajibikaji wao.
Wahindi wanawapa hapo hapo,wengine hata kiswahili hawajuwi,ni shauri ya mshiko,njaa inauwa.
ReplyDeleteHilo tatizo liko kila balozi zetu nje. hapa US tena wanawazungikia wabongo state tofauti kana kwamba wana nia nzuri ya kuwabadilishia passport lakini wakishalipwa hakuna kinachoendelea. Balozi za Tanzania njaa kali na hiyo ni dili. Usishangae bora peleka info zako kwa ndugu yako bongo akupelekee uhamiaji na utoe kidogodogo utapata mkoba wako mapema.
ReplyDeleteWa2 kwa kulalamika we unategemea ufanyiwe kila ki2? rudini nyumbani mkalime!!
ReplyDeleteNami pia naungana na mdau hapo juu ni kweli msikalie kulalamika mkiwa nje ya nchi rudini kwenu mkajenge Taifa lenu mnakalia kuwa manamba wa wazungu oneni aibu.
ReplyDeletePoleni sana ndugu zetu wa Ugiriki. Ila mnayoyaona huko Ugiriki ni sawa na Uturuki, ubalozi wmdogo wa hapa Uturuki unapeleka maombi ya watanzania wote huko Rome, hadithi ni hiyo hiyo. Wapo watu wameomba kabla yenu nyie, mpaka leo hii hawajapata. Mimi naona kama hawa mabolozi hawawezi kufanya kazi zao wawajibishwe, au kama Watanzania walio sehemu fulani hawachukuli kama raia,bora waseme. Nchi inaenda pabaya, wanafunzi wanapata taabu kwenda na kurudi shule, hawaoni? Vipi tulio mbali na Tanzania? Mungu tubariki!
ReplyDeletewe anonymous hapo wewe shamba unalo?au walima kwa wadosi au bakhressa? na hao viongozi inabidi wajiuzulu kazi zao kwani kumdhuru mtanzania mwenzio ni usaliti ndio maana wageni waja hapo wachukua na kumiachaa na njaa zenu,hivi lini mtaamka?mcheza kwao hutunzwa hebu wapeni passport zao angalau wakitaka kuwaona wazazi wao wanaweza jamani.tusijifikirie sisi tu na pass za ki diplomat sabu tuko serikalini,jamaa wakirudi bongo hela ya nje yaingia so inainua nchi yetu kwani ataziacha hapo bongo ndio nyumbani lakini mdosi na wengineo watazipeleka siss au canada.
ReplyDeleteby Mlalahoi
Poleni sana ndugu zangu wazalendo,mkanda wa miezi 18 tutaendelea kuubeba mpaka vitukuu vyetu.hebu wahusika wapatie pass zao i wish wewe ungekuwa kwenye jahazi lao,ningeomba serikali iangalie jambo hili kwani mzalendo anapokuwa nje ya nchi kitambulsho kikubwa ni passport.tafadhali wazalendo wasaidieni haki zao kwani pass ni hiki ya mtanzania yoyote bara na visiwani.
ReplyDeleteby mlalahoi
Balozi zetu nyingi njaa kali. Mie niliomba passport mpya 2006, baada ya kuona imechelewa sana nikaanza fatilia huko London. Mara ubalozi ukanambia eti haukupata passport yangu toka Tanzania kwani baadhi zimepotea hivyo nijaze fomu upya na kulipia tena. Jamani si balaa hilo. Kwa nini wasingeniambia kuwa passport imepotea na badala yake kukaa kimya hadi naenda ndio wananiambia eti imepotea nijaze tena fomu. Kitu kilichoniudhi badala ya kutumia busara, wanatumia ubabe. Yaelekea balozi ni mtendaji kazi mzuri isipokuwa hao wanaosimamia vitengo hivyo sio wafuatiliaji na pia njaa kali inawasumbua
ReplyDeleteNdio maana wabongo wengi waliooa na kuolewa wanaamua kubadili uraia wao wa Tanzania. Iwapo ofisi za ubalozi hazitatui matatizo yao ipasavyo, watu hao wanaamua kuchukua uraia wa wake au waume zao.
ReplyDeleteAnonymous wa April15,6:23.Hivi unaelewa nini kinazungumziwa hapa au?Ndugu zetu huko Ugiriki na wengine sehemu kadhaa za USA wanalalamika kuwa haki zao za kuwa na pasi hazitimizwi na balozi zetu huko waliko hawaongelei KILIMO hapa!!Wana kila haki ya kutoa malalamiko hayo na hasa ukizingatia kuwa kweli kuna waasia wasiojua hata kile kiswahili cha kuomba maji eti na wanapassport ya kiTanzania!!
ReplyDeletenjooni huku rudini mpambane na foleni mnalalamika nini?
ReplyDeleteutatuzi siyo kuwataka hawa ndugu warudi nyumbani.WATARUDI VIPI NA HATA HIZO PASI HAWANA?utatuzi ni hizi balozi zetu ziwache ubinafsi na wakuu wa wizara ya mambo ya nje wawe wakali kidogo.
ReplyDelete