
JK ameondoka nchini leo mchana kwenda India, kuanza ziara itakayompeleka katika nchi mbili za Bara la Asia na mbili za Ulaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ilotolewa leo asubuhi, katika hatua ya kwanza ya ziara hiyo, Jk, katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), ataliwakilisha Bara la Afrika katika mkutano wa kwanza kati ya Wakuu wa Nchi za Afrika na India.
Mkutano huo wa siku mbili utafanyika katika mji mkuu wa India wa New Delhi 8 April, 08 na 9 April, 08 wiki ijayo.
Mbali na Jk , viongozi wengine wa Afrika watakaoshiriki katika mkutano huo ni mwenyekiti wa AU aliyemaliza muda wake, Rais John Kuffour wa Ghana na mwenyekiti wa umoja wa New Partnership for Africa¢s Development (NEPAD), Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, pamoja na viongozi wa nchi waanzilishi wa NEPAD.
Viongozi hao ni Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria, Rais Umaru Yar¢Adua wa Nigeria, Rais Abdoulaye Wade wa Senegal, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Rais Hosni Mubarak wa Misri.
Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni wawakilishi wa jumuia nane za uchumi za bara la Afrika zinazotambuliwa na AU.
Jumuia hizo ni Umoja wa Uchumi wa Nchi za Kiarabu za Maghreb (AMU), Jumuia ya Uchumi ya Nchi za Sahel-Sahara (CEN-SAD) na Jumuia ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Nyingine ni Jumuia ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS), Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuia ya Soko la Pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuia ya Intergovernmental Authority and Development (IGAD).
Baada ya mkutano huo wa India, Jk atakwenda China kwa Ziara ya Kiserikali ya siku nne nchini humo kwa mwaliko wa Rais Hu Jintao. Huko atawasili tarehe 11 April, 08 , ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya Kiserikali nchini humo kufanywa na Jk tokea kuwa Rais wa Tanzania Desemba 21, 2005.
Hata hivyo, ikumbukwe kwamba Jk alipata kufanya ziara ya kikazi nchini China, ambako alihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ushirikiano wa China na Afrika uliofanyika Novemba 2006.
Wakati wa ziara yake katika China, Jk atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Hu Jintao katika mji wa Sanya, jimbo la Hainan. Rais pia atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa China, Wen Jiabao.
Baada ya ziara ya China, Jk atakwenda Copenhagen, Denmark, kwa siku mbili, ambako atashiriki katika mkutano wa kwanza wa Tume ya Kuendeleza Ushirikiano na Afrika. Rais Kikwete ameombwa na kukubali kuwa mjumbe wa Tume hiyo.
Tume hiyo iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Anders Fogh Rasmussen, itaelekeza nguvu zake katika kutatua matatizo ya Afrika katika maeneo ya vijana na ajira. Tume hiyo itafanya mikutano mitatu kabla ya kutoa ripoti na mapendekezo yake.
Jk ataondoka Denmark Aprili 16 kwenda London, Uingereza, ambako anatarajiwa kuzindua Mtandao wa Watanzania Waishio Uingereza (Tanzania Diaspora) kabla ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown.
Jk anatarajia kuondoka Uingereza tarehe 19 April, 08 kurejea nyumbani.


Namtakia safari njema na mafanikio mema katika mikutano yake. Mungu azidi kumbariki na kumpa nguvu.
ReplyDeleteAsante Michuzi
Rais wetu handsome jamani, duh!? Mpaka basi yaani...
ReplyDeleteDogo nae kwa kukata mitaa utadhani kala miguu ya kuku jamani duu we acha tu!!!!!!!!! Rais tumepata ila mtembezi nae tumepata.
ReplyDeleteKila la kheri,katika safari yake ndefu naamini itajibu tu kwani jitihada zake zinaonekana.
ReplyDeleteAcheni Rais wetu atembee exposure nayo muhimu! but at the end of the day tunataka outputs. Atuambie baada ya U 'Vasco da Gama' kaleta nini kwa wa TZ? Hilo ndilo jambo kuu!Akirejea tunataka hotuba na outputs!
ReplyDeleteTunamkaribisha tena na kumngoja kwa hamu sana CPH Rais wetu.
ReplyDelete