katika kufuatilia tukio la huyu kijana pichani kukutwa na kichwa cha msichana leo asubuhi kule muhimbili, globu yenu imethibitishiwa kwamba jana usiku msichana mdogo alipotea nyumbani kwao tabata.
inasemekana leo asubuhi ndugu wa marehemu walikuta kiwiliwili kitupu cha msichana huyo karibu na nyumbani kwao na wakaita polisi ambao wakaupeleka hospitali ya taifa ya muhimbili kwa uchunguzi. huko ndiko kichwa kinachosadikiwa kuwa cha kwake kikakutwa na huyu kijana kwenye geti la chuo kikuu cha tiba cha muhimbili ambapo mlinzi alimkamata.
afande charles mkumbo, mkuu wa upelelezi kanda ya ilala, amethibitisha yote hayo usiku huu na kwamba kichwa hicho ni cha mtoto salome yohana mwenye umri wa miaka kati ya miaka 3 na 4 na kijana huyu ametambulwa kama ramadhani mussa na anashikiliwa na polisi yeye na mama yake kwa kutuma za kukutwa na kichwa cha mtu kwa kile kilichosemwa kuwa ni mambo ya kishirikina.
kijana mussa mwenye umri wa miaka 12 inasemekana pia amewahi kukumbwa na mikasa mingine, ikiwa ni pamoja na kuanguka toka paa la kanisa la assemblie of God la msasaani analoongoza mh. getrude rwakatare. inasemekana baada ya mkasa huo ambapo alikuwa na mwenzie wa umri kama yeye walipelekekwa kupimwa akili muhimbili na kuachiwa baada ya kuonekana wana akili timamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. du, kweli muhimbili hawakumpima akili vizuri huyu mtoto.

    ReplyDelete
  2. Duh hii kali naona hata camera zenu mkichukua picha zinatoka blur...Nisiiangalie sana isije ikaniharibia screen yangu....lol

    Huyu mtoto ndio yule yule kweli alianguka kwenye like kanisa watu wakasema kanisa linatafuta publicity....Leo yuko na kichwa cha mtoto ...I hope ni cha doll..manake kama ni mtu kweli mwee asije akaachiwa tena {Hao wameua kwa kukusudia kabisa} na siajabu wameua wengi...kwanza anaenda shule huyu kweli?

    ....miaka yetu ya 90's camera zilikua hazipo ...kwa hiyo tulikua tunasikia tu vitu hivi na kwa vile wengine ni Tomaso basi tunafikiria kama ni urbun legends...Sasa hivi tunaona picha kabisa haya makubwa

    lakini huyo mtoto kijeba kama ni miaka 12 tu basi anafanyizwa kazi sana labda usiku hakilali hiki kitoto...Anaonekana kama yupo 16 and up vile....

    Halafu huyu mtoto hiyo kazi naona haiwezi...mara ana anguka na ungo wenzake wanaendelea...sasa leo yupo na kichwa waliogawana share wao wameserebuka na viungo vingine bila kukamatwa yeye anampelekea shangazi yake!!!

    Bongo hiyoooooo

    ReplyDelete
  3. This is unbelievable, toka utoto tukisikia hizi habari kua zinatokea lakini uhakika hatuna kama kweli wapo binadamu kama hawa, leo tunaona in pictures. Natumai nao watanyongwa kwa unyama wao.Wangekua ulaya kisingizio kingekua wendawazimu maana ni ngumu mtu kuamini mtu timamu anafanya mambo kama haya, lakini huko nyumbani watashikishwa adabu na shirki zao.

    ReplyDelete
  4. kwa kweli shetani anafanya jukumu lake!lakini MUNGU yupo!tusipomshika MUNGU katika hii dunia maisha ni hatari sana!Shetani ana nguvu kuliko sisi ila shetani hana nguvu kumzidi MUNGU!hivyo basi ili tuweze kumshinda shetani ni lazima tuwe na NGUVU YA MUNGU!na bado wachawi wataendelea kuumbuliwa!MUNGU tuonyeshe zaidi na zaidi ili jina lako LITUKUZWE!hawa watu mimi naona waombewe tu maana huko polisi wanaweza enedeleza uchawi wako!bila YESU ni bure!

    ReplyDelete
  5. YAANI SIAMINI KAMA HIZI HABARI NI ZA KWELI NIMERUDI KUIANGALIA PICHA YA HUYO KIJANA, I ACTUALLY FEEL SICK TO MY STOMACH JUST THE THOUGHT OF WHATS DRIBBLING ON HIS LEFT CHEEK,FLUID FROM HUMAN FLESH.

    ReplyDelete
  6. Jamani zile sheria za kunyonga zipo ama? Bado tunazihitaji !!

    ReplyDelete
  7. Pole sana kwa wafiwa and please Get this demon and his crew out of misery ASAP
    i dont care if you shoot him, beat him to death, hang or chop him in peaces just get him off our community ASAP PLEASE
    roho inaniuma sana, ningekuwa hapo labda na mi ningeenda jela nisingemwacha huyu muuaji

    ReplyDelete
  8. uwiiiiii, mungu wangu weeee!!, yaani ndiyo imefikia hatua hiyo sasa bongo jamani?!!!.mbona inatisha!! hivi kweli huko kwa kuja na mtoto jamani?!! si unaweza ukaenda na watoto watatu ukarudi na mmoja au zero!! watu wakakufanyia wanao kitoeo!! jamani mkimbilieni mungu hayo mambo ya kishirikina hayana mpango mnauwa watoto wa watu buree!! yesu na maria. michuzi baadaye kaka, nashukuru kwa ufahamisho huu japo inahuzunisha sanaaaa, ohooh!

    ReplyDelete
  9. Yaani blog ya Chemi ilitoa vivid kichwa cha yule mtoto kilivyokatwa!Asante Michuzi hukufanya hivyo. Not very sure kuwa majority wameona sawa au vipi kuwa picha zionyeshwe kama zatisha namna hii.

    ReplyDelete
  10. Hivi haya mambo bado yapo huko Bongo jamani au ndo hali ngumu ya maisha? kwanini wasitumie kuendeleza nchi au kuwaondoa mafisadi wa nchi

    ReplyDelete
  11. Hellow hii ni kali sana kwa maana kijana mdogo kama huyu anafanya mambo makubwa namna hiyo. Nikiwa nchini Finland kimasomo nimeshituka sana kuona kitu kama hicho, nilikuwa naomba sana serikali yetu ifanye uchunguzi wa kina sana kwa huyo kijana shetani ili kitendo kama hicho kisitokee tena katika dunia hii ya ustaarabu. Nawapa pole sana wazazi wa marehemu, Mungu ailanza mahari pema peponi amini.

    ReplyDelete
  12. Sasa wao wakati hule watu walikataa huyo mtoto kudondoka kanisa wakasema wazushi .mchawi akapelekwa muhimbili sasa angalia matokeo yake leo.swala linatisha sana hili eh mwenyezi Mungu tuepushe na mabalaha haya.

    ReplyDelete
  13. Wachawi wengine wamo humu jwenye blog reh teh teh teh. Ati nikiwa Finland kimasomo. Ndio iweje? Ungekua bongo wasingekua hawa?

    ReplyDelete
  14. Sasa mbona watu mnashangaa kamandiyo kwanza kusikia haya mambo!! au mlikuwa hamjaona picha za viungo vinavonyofolewa na watu wenye imani za kichawi? Hivi leo watu wakianza kupost miguu, sehemu za siri, ngozi za kisogoni n.k za maalbino wanaouwawa kila siku ili watu wapate utajiri mtasemaje? Jana tu iliandikwa gazetini huko shinyanga kuna jamaa kamchinja mdogo wake kwa panga ili apate utajiri. Kwa kweli hali inatisha na nguvu za ziada zinahitajika ili kuitokomeza hali hii. Hili wimbi la ushirikina linaonyesha ni jinsi gani jamii yetu haijaelimika na inatakiwa nguvu ya zaida kuwapatia watu elimu japo ya msingi ili watu wawe na ufahamu mzuri zaidi kuhusu maisha yao.

    ReplyDelete
  15. UJINGA, UJINGA, UJINGA! NCHI YETU BADO TUKO NYUMA KIASI CHA KUTISHA, NO WONDER HATUWEZI KUJITAWALA WENYEWE. SERIKALI NAYO IKO LIKIZO, PLS, ANZISHENI KAMPOENI YA KUELIMISHA UMA MAGAZETINI, RADIONI, TV, MASHULENI, KILA MAHALI KUHUSU UBAYA NA UPUUZI WA UCHAWI. PIA UMASKINI UNAZIDISHA UJINGA, PUNGUZENI UFISADI, LIPENI WAALIMU, JENGENI BARABARA, ZALISHENI UMEME WA KUTOSHA, MKIFANYA HIVYO, WANANCHI WATAJISAIDIA WENYEWE ZAIDI. NAULIZA: SERIKALI IMECHUKUA HATUA GANI BAADA YA ZERUZERU KUUWAWA?

    ReplyDelete
  16. WEWE UNAEMUITA HUYO WA FINLAND KIMASOMO ATI MCHAWI, UNA MATATIZO. WATU KAMA WEWE NI TATIZO KUBWA SANA NYUMBANI KWASABABU MNA UELEWA MDOGO SANA. FINLAND ALIPO HUWEZI KUSIKIA UJINGA HUO WA KUUWANA OVYO, KUUA MAALBINO.... WAKO KARNE YA 21, SISI BADO YA 18. FINLAND ALIKO JAMAA AMEONA JINSI WATOTO WA MIAKA 12 WALIVYOELIMIKA, WANASOMA HARRY PORTER, WANAANGALIA SCIENCE FICTION, SISI BONGO MTOTO KAKA HUYO ANAKATA KICHWA CHA MTOTO MDOGO....NDIO MAANA ANAFANYA COMPARISON.

    ReplyDelete
  17. Asante mkuu wa wilaya kwa mwendelezo huu.

    Ila sielewi kama kuna sheria za kimahakama zinazohusu hukumu juu ya mambo ya kishirikina. Kitakachofaa hapa ni washitakiwe kwa kosa la mauaji!

    ReplyDelete
  18. Kuna mdau kashikilia bango kwamba inahitajika nguvu ya ziada watu wapewe elimu angalau ya msingi. Nadhani hajuwi mambo yalivyo. ..

    Viongozi wengi kwenye ngazi mbali mbali za serikali na wanaamini katika ushirikina. Chaguzi zinapokaribia huwa wanaonekana kwenye vibanda vya makuti vya waganga wa kienyeji( wachawi) wakisaka dawa za ushindi. Sasa anaposema elimu angalau ya msingi, ina maana watu hao(viongozi) hawana angalau elimu ya msingi?

    Nguvu ya ziada inayotakiwa kutumika ni kuwafundisha watu wamjuwe Mungu wa kweli kwa kumwamini na kumpokea Yesu Kristo. Mtu kama hana Yesu moyoni ushirikina ni kitu cha kawaida, hata kwa hao wanaojiita wakristo huku wakikana kuishi kama kristo anavyoagiza!

    ReplyDelete
  19. Ni habari ya kusikitisha sana.

    Nawapa pole wafiwa.Na pia lazima hatua za madhubuti zichukuliwe ili kubaini nini chanzo cha haya yote.


    RIP mtoto aliyeuwawa kikatili

    ReplyDelete
  20. Huu ni mwaka wa WACHAWI NA MAFISADI kuumbuka! kinachofuatia ni kuwaadhibu na sio kuwaacha tena wakarudi kwenye jamii na kuleta madhara kama haya! Nawapa pole wafiwa na Mungu ailaze roho ya mtoto(malaika) Salome Yohane, MAHALI PEMA PEPONI, AMEN.

    ReplyDelete
  21. JAMANI, KWA NINI MNAMLAUMU KIJANA MUSA WAKATI MADAKTARI WA MUHIMBILI WLIM-CLEAR KWAMBA HANA MATATIZO YA AKILI? MIMI NINAONA TUSIMLAUMU SANA KIJANA MUSA SABABU ANA MATATIZO YA AKILI, ILA TUWALAULU MADAKTARI WA MUHIMBILI. SABABAU WANGEFANYA KAZI YAO KAMA INAVYOTAKIWA, KIJANA MUSA ANGEPATIWA MATIBABU AU ANGEKUWA MIREMBE MENTAL HOSPITAL, NA HAYA YOTE YASINGETOKEA. POLENI SANA WAFIWA. KAMA INGETOKEA KWENYE NCHI ZILIZOENDELEA, HAO MADAKTARI WANGIPATA KASHESHE YAO. ANYWAY SIKU MOJA TUTAFIKA.

    ReplyDelete
  22. Huyu Mtoto sio mchawi wala mgonjwa wa akili, nina uhakika Muhimbili walijua kwa vipimo vyao kuwa hakuwa na ugonjwa wa akili.

    KIjana huyu ni tapeli anaye taka msaada wa jamii, na njia pekee ya kuweza kupata anachotaka ni publisity, na kwa vile umri wake mdogo ana shindwa kujua njia muafaka ya kuweza kufanya utapeli wake ufanisi zaidi.

    Ukiangalia njia zote walizo tumia, utagundua ni wajanja sana na wana akili zuri na wana jua wana cho kifanya.

    Walidai walianguka toka kwenye ungo ,juu ya paa la Kanisa la Mama Rwakatare, halafu baada ya muda wakagundulika huko Mbezi, walisha fanya utapeli ,tena kwa kujifanya walichukuliwa kiuchawi.

    Kwa kuwa walishindwa kupata kw autapeli wa kwanza walio ufanya,sasa walicho fanya ili waweze pata msaada , ina wezekana ndio wakaamua kuwa njia bora zaidi ni kuua mtoto na kudai wao ni wachawi ili waweze kuonyesha kuwa wanacho sema ni cha ukweli.

    Kama tunavyo sikia kuhusu wachawi, wote wana dai ni siri kubwa ambayo huwezi kuitoa hata kama ukiwa mtoto

    Sasa iweje huyu mtoto akutwe na hicho kichwa na adai kuwa eti ni kawaida uao kula nyama za watu na kwanini watu wana mshangaa, nilipo sikia hivyo tuu nilihisi huyu mtoto hana uchawi wala sio mgonjwa wa akili bali ni tapeli

    ReplyDelete
  23. hakuna cha kulaumiwa madaktari wala nini nani amekwambia wachawi wanaupungufu wa akili?wana akili sana ndo maana wanafanya mambo ya kishetani,kwa kweli tumrudie Mungu wajameni.

    ReplyDelete
  24. Mumeambiwa serikali haina dini! Hamna sheria ya mambo ya `uchawi'. Huyu kashikwa laivu anafanya hivi vitu, na ni `mtoto' itakuwaje?
    Hawa wanaofanya mambo haya wanajiamini kwasabu ya `kutokuwepo na sheria kama hizo!

    ReplyDelete
  25. michuzi umekosea,kanisa linaloongozwa na dr rwakatare halipo msasani,lipo mikocheni b,na linaitwa mikocheni b assemblies of God.

    ReplyDelete
  26. MICHUZI. HUYO MTOTO NI KWELI NA SIO MARA YA KWANZA NA WATU WANAJUA WENGI WANATOA STORY YAKE AMBAO WALISHAKUMBANA NAE LIVE AKAWAPA SIRI ZOOOTE TENA KWA MAANDISHI NA PICHA JUU. TATIZO WAANDISHI WETU WANASUBIRI KUPELEKEWA HABARI MAOFISINI SASA TOENI NAFASI KWA NJIA YOYOTE ILE WANANCHI WAWAELEZE UKWELI NA WAPO ZAIDI YA MIA MOJA HAPA DAR. WATU WAKO TAYARI KUSEMA LAKINI WASEME KWA NANI POLISI NDIO HAO IMANI HAKUNA WANASEMA HATA WAKIWAAMBIA KAZI BURE WAWEZESHENI WANANCHI KUTOA HIYO HABARI HATA KWA SIMU YA BURE AU BARUA MUONE UKWELI. TAFADHALI WATAARIFU NA WANAHABARI WENGINE. TENA HAWA WATU WANATAFUTA SIMU YA MAMA RWAKATARE KAMA UNAYO ITOE NITAWAPA ILI WATOE HIYO HABARI.

    ReplyDelete
  27. MNAOTUMA MAONI JAMANI SOMENI HABARI YOTE KAMA ILIVYO KISHA TUMA MAONI, KWANI BAADHI YA MAONI YANAONESHA WATUMAJI HAWAJUI UMRI WA ALIYETENDA JAMBO LICHA YA KUANDIKWA. KWA UFUPI ALIYETENDA NI MTOTO ALIYE NA UMRI KATI YA 12 NA 17 LICHA YA KUANDIKWA 12. MTOTO HUYU HAHUSIANI NA UGUMU WA MAISHA AU KUTAFUTA UTAJIRI BALI ANAMATATIZO BINAFSI.

    ReplyDelete
  28. acheni Mungu aitwe Mungu mkubali mkatae atabakia kuwa Mungu tu!! walisema kuwa Mama Rwakatale anatafuta publicity lkn haikuwa hivyo sasa Mungu kajidhiirisha na kuwaonyesha kuwa Mama Rwakatale ni mtumishi wake, tusiwanenee watumishi wake maneno magumu tusije tukalaaniwa jamani tumrudie Mungu tu

    ReplyDelete
  29. Anon wa 28 7.30 am umenifungua macho hata mimi hayo unayosema yanawezekana ni kweli, kwanza sijasikia wachawi wanaua mtu laivu ili wale nyama yake. Wana mbinu zao na mambo yao hufanya kwa siri kabisa na hata ikibidi kula nyama basi husubiri mtu akishazikwa makaburini na kwenda kufukua huko ili kula nyama yake. Hako kasichana kangefanyiwa mazingaombwe, kakapotea au kakafa kwa uchawi lakini sio kuchinja live. Cha msingi alichokuwa anakitafuta sasa amekipata, hako kanyongelewe mbali nimesoma kwenye magazeti wanasema ana miaka 18, basi watuondolee huyo 'Vampire' kwenye jamii na si kwa kufungwa bali kunyongwa kwa kuua kwa makusudi. Hakuna haja ya kumpima akili wala nini angekuwa mwehu angetembea na hicho kichwa huku anakitafuna tangu huko alikotoka sio alipokamatwa sasa kutaka namna ya kusave ndio anajitai wendawazimu. Huyo aliona wakati mwili wa marehemu ukichukuliwa na kupelekwa Muhimbili, unajua damu ya mtu ni nzito hasa kimalaika hicho walichokiua Mungu amewaumbua hapa hapa, nafikiri lengo ilikuwa kukipeleka hicho kichwa mochwari!

    ReplyDelete
  30. anon,hapo juu inaonekana una experience kweli na wachawi wanavyomla mtu nyama...umeenda in detail kabisaaa..si mchezo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...