akiwa kacharuka kuendeleza libeneke kwa kutuchambulia mapicha ya muziki na wanamuziki wa enzi hizo, mdau john kitime safari hii katuletea mcharaaza gitaa wa vijana jazz hassan dalali wakati huo bendi hiyo ikienda kwa mtindo wa coca coca. pamoja na muziki dalali alikuwa mpenzi mkubwa wa soka hususan klabu ya simba na si ajabu kwamba hivi sasa yeye ndiye mwenyekiti wa wana msimbazi. asante jfk kwa picha hizi. najua uko mbioni kuanzisha wavuti ya muziki. kaza buti mkuu, tuko pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mze Kitime tuko nawe katika kuwaenzi wanamuziki wetu wa zamani. Wapi Jaerry nashon, marijani, hamisi Juma wa sikinde, Wema abdallah, michael enock, mze shem karenga, general nguza viking, juma ubao na wengineo wengi tu. Tuna-wamiss saaaana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...