Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. 2010 kwa kweli lazima kieleweke.
    I wish tungepata watu strong kwenye vyama vyetu. CCM tumekuchoka kwa kweli. SIjui WaTz wenzangu, ingetokea uchaguzi leo mngemchagua nani? Nilimpenda sana JK, kumbe nilipenda sura. Mdaku kama nini, kumbe mtu wa Pwani ni wa Pwani tu. Anauza uzuri tu siku hizi. Huku wananchi tunaangamia na mambo madogo madogo tu. Mungu Ibariki Tanzania ipate kiongozi mzuri.
    KP big up sana.

    ReplyDelete
  2. jk bado ndo chaguo la wengi na 2010 kama unamuweka tena madarakani,wewe fisadi nini,maana jk ndo aloanza kuzipa uhuru vyombo vya habari,namafisadi wakaanza kutajana wenyewe,wewe unadhani angekuwa mkapa kungekuwa na kamati ya mwakembe,kwanza kuna watu kama kina vito kabwe usingewasikia,awamu ya nne imewapa uhuru wa watu kuzungumza,ubapari wa mwalimu nyerere umeanza kuondoka now,ndo maana mnaona mafisadi ni wengi,kumbe huko nyuma ndo kulikuwa na mafisadi zaidi,tena ulikuwa ukijaribu kuja juu kidogo wanakuondoa,viongozi kibao wanajulikana waliokuwa k utata sana,sasa hivi ccm watu wanauhuru ndani ya chama ya kusemeana madhambi yao,sema wale mafisadi ndo wanataka kuugeuza uhuru huu kuwa sehemu ya kuchafuana.

    ReplyDelete
  3. Asiyetaka kumchagua JK shauri yake lakini siye tunayoona kazi yake tutamchagua tena kwa raha zetu. Kama si JK nani angeyajua ya EPA na Richmond? Kwani Richmond inatofauti gani na IPTL na mikataba mingine iliyosainiwa enzi ya BM? JK amekuta kitu gani kimebaki zaidi ya Tanesco iliyo ICU? Jamani kweli viumbe wazito. Na kwa taarifa yenu hicho chama chenu cha kidikteta Chadema hatuiingii, naenda kutafuta tawi la CCM lililo karibu nijiunge namimi wiki hii hii. Kwanza nilitaka kujiunga Chadema lakini nilivyosoma habari ya wanavyomnyanyasa Wangwe kwa kuwa tu si mchaga basi nimechoka hoi, tena eti wabunge wa kuteuliwa kati ya sita watano wanatoka mkoa mmoja. Uongozi wa juu wote sijui directors (kwani kampuni ile) asilimia kubwa wanatoka mkoa mmoja. Wanapewa ruzuku na serikali karibu 66m Tshs lakini huoni hata matawi ya chama yakifunguliwa. Jamani ngoja nitafute tawi au shina lililo karibu yangu nikakate kadi.

    ReplyDelete
  4. Binafsi namuona JK kama mkombozi kwa watanzania kwa namna fulani. Najua kwamba kila kiongozi ana kasoro kama binadamu na pia kama kiongozi. Kitu kinachonifanya nimuamini JK ni ukweli wake, huruma kwa wananchi na pia namna alivyotuachia wananchi uhuru wa kujadili mambo yetu kwa njia mbalimbali bila kuingiliwa hovyo hovyo. Linapotokea tatizo JK huwa halifichi bali huliweka wazi ili lijadiwe na pia hujaribu kulitafutia ufumbuzi, mfano njaa zilizotokea wakati wake. Wakati wa BM watu waliwahi kufa kwa njaa, waandishi waliandika lakini serikali ilikataa kwamba hakuna mtu aliyekufa kwa njaa, mifano ni mingi. Wote mlishughudia CUF kilivyoitwa chama cha magaidi lakini tangu aingie, viongozi wa CUF wanaonekana ni bora na mchango wao unaheshimiwa. Lakini pia mchango wa wapinzani na wabunge wa CCM bungeni umekuwa mkubwa wakati huu kuliko wakati wote. Ni JK aliyoleta dhana ya kiongozi kumtumikia mwananchi na siyo kinyume chake kama ilivyokuwa kabla yake. Waliokuwa mafisadi enzi zile na ambao leo hawamo serikalini(siyo mawaziri) na wengine bado wamo hivi sasa ndiyo wapo mstari wa mbele kuuzungumzia ufisadi. Kama kweli wanayoyasema ndiyo wangeyanfanya leo hii tusingezungumzia umasikini wetu ktk hatua tuliyonayo. Polisi waliwawinda watu kama wanyama na unapoonekana na pesa nyingi polisi wanakuua na kukuunganisha na tukio la ujambazi, hapa wote mnafahamu. Tatizo lililopo sasa ni viongozi waliopo chini yake ambao wengi wao bado hawajabadilika na bado wanaendeleza mazoea na huenda ndiyo wa kwanza kulalamikia ufisadi wakati wao ndiyo wanaoufanya. Kuna mengi JK amefanya ambayo yanafanya nimuone kiongozi bora kuliko waliomtngulia hasa ukizingatia wakati tuliopo

    ReplyDelete
  5. VERY CREATIVE KP, KEEP IT UP!!!

    yaani bomba kishenzi!!

    ReplyDelete
  6. Moto wa gesi feki?CCM wamuulize Monsieur Mugabe kilichomkuta!Kanga kukosa Manyoya!2010 siyo mbali.Keep on Buying Time Fallas!Tupo hapa,sikio la kufa kamwe halisikii dawa.Watu wata waachieni tena masanduku ya kura yakalale kwa Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Jiji hadi asubuhi ndipo kura zihesabiwe!Watanzania si wana njaa sana,au?Kp ,keep on Panyalisiiiiig!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...