Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. masoud hivi usalama wako huuogopei? Au una bima mwenzetu na immunity?
    ila katuni inajielezea swaafi. gudwork

    ReplyDelete
  2. IKO SIKU ATAPATIKANA TU !!! KWANI HAO WALIOUMBUKA HIVI KARIBUNI KWA UFISADI NA UZANDIKI NANI ALIEKUWA ANAJUA KUWA YANGEWAKUTA ???? HUYU CHE NKA... NA MWENZIE ATOKAYE UPARENI WASIDHANI WATAKA HIVYO NA UJANJA WA KIZAMANI MPAKA MWISHO WAO BALI WAKAE WAKIJUA KUWA MAMBO YATAWATOKEA PUANI SIKU MOJA !!!!!! ALUTA CONTINUA WATANZANIA WANYONGE WASIO NA KITU NA MAPAMBANO MBELEEEEEE MPAKA KIELEWEKE !!!! UJANJA WA MTU KWA MTU HUWA NA MWISHO AMBAO HUWA SIO MZURI !!! SALA ZETU KWA MOLA AJUAYE WAJA WAKE WANAVYOTESEKA NA KUWAWEKEA MIKONO !!!!!

    ReplyDelete
  3. endeleeni kumchokonoa labda itafika mahali ataona sasa inatosha na hivyo ataamua kusema. Big Up KP!

    ReplyDelete
  4. Ujumbe ni mzuri lakini hii caricature ya BM as an overgrown cat siyo nzuri hata kidogo.

    ReplyDelete
  5. yaani hapo kaka michu akikosekana wa kumfunga hapo ndipo tutaingia msituni kiosama osama maana hii siyo serikali ya viongozi bora tena bali serikali ya mafisadi tena wakupindukia,kaka michu natabiri siku za usoni kutatokea machafuko tena makubwa zaidi ya yale yaliyotokea kenya. hivyo naishauri serikali iliyopo madarakani isilifumbie macho suala hili na waache kuogopana na suruhisho lisiwe kujiuzuru na ihakikishe anayejiuzuru inadili naye sawia bila woga wala kuoneana aibu.

    ReplyDelete
  6. Kama mwenye Nyumba bwana Jah-Kaya hawezi hiyo kazi, basi wa kumfunga kengele huyo miauu aitwae che- ni wabunge kama Aloyce Kimaro, Anne Kilango Malecela, Dk slaa, Dk Mwakyembe, selelii, Wananchi, Magazeti, Mahakama n.k

    ReplyDelete
  7. Yaani kipanya ww ni hatari sana huyo simba wa nyika ila ipo siku tu atapatikana kwa kummudu EPA oyeee

    Katochi)

    ReplyDelete
  8. Wewe kipanya subiri tindikali hapo clouds fm. endelee tuu kumchokonoa our beloved former President BM.

    ReplyDelete
  9. INAWEZEKANA HAKUNA WA KUNFUNGA KENGELE KWANI HATA HUYO TUNAYETEGEMEA AWACHUKULIE HATUA TUNAJUAJE KAMA NI MSAFI????

    HADI KUFIKA HAPO ALIPO NI TEAM WORK SASA KAMA ALIOKUWA NAO TIMU MOJA NDIO HAO MAFISADI KUANZIA ALIYEKUWA CAPTAIN WAO HADI RESERVE HAKUNA KITAKACHOELEWEKA.

    HAPO MPAKA WA-TZ WAAMUKE KUWA NA NGUVU YA KUISHINIKIZA SERIKALI KUFANYA MAAMUZI KWA SASA HAKUNA TOFAUTI NA ZIMBABWE. NA ZIMBABWE WAKIBADILISHA UONGOZI TU UCHUMI WAO UTARUDI KAMA ULIVYOKUWA SI MUDA MREFU KWANI WAZUNGU KILA SIKU WANAMWOMBEA MUGABE MABAYA.

    LABDA NA SISI TUANZA KUWAOMBEA MABAYA VIONGOZI WETU MAANA KUINGIA MITAANI KUNA HITAJI SACRIFICE YA MAISHA.
    Mkulima

    ReplyDelete
  10. Atake asitake atanyakwa tu, tutaenda Nachingwea tukamtafutie dawa, kuna mabingwa wanao shughulikia simba wala watu. Atazingirwa huyo asijue pakutokea. Nchi imesambaratika kumbe kila kigogo alijimegea kakipande ka keki. Mzee wa vijisenti alijifanya kukomaa eti piga ua hajiuzulu mtu, yuko wapi??!! Kilio cha wengi...

    ReplyDelete
  11. Sio mchezo paka shume lenyewe kali kama nini halitaki kuguswa wala nini ukimgusa tuuu unaliwa vibaya mno si unausikia hata mngurumo wake.Chakufanya sasa hakuna cha nini wala nini ni kulikamata na kulihoji ama lipigwe risasi tu life kwa yeye ni nani?hakuna aliyejuu ya sheria ni kweli umeiba wajibika na ikiwezekana unasweka tu lupango AU MNATAKA TUINGIE MTAANI TUIVURUGE HII AMANI KWA KUDAI HAKI ZETU MAANA MMETUONA MNAOTUONGOZA NI WAPUMBAVU SASA KIKOMO KIMEFIKA MWISHO,BIG-UP KIPANYA KWA KATUNI YAKO HUYO NI BENJAMIN MKAPA.

    ReplyDelete
  12. Mimi mboni sijaelewa, kwani huyo ndi nani?

    ReplyDelete
  13. Anon. April 24, 12:39 acha kutia watu majaribuni, mwenye macho haambiwi tazama hupwesa atakapo. We kwani ulipokuwa mdogo hukusoma hadithi ya Paka nunda mla panya mpaka panya wakafanya kikao ili kujinusuru wakaamua watafute kengele ili paka afungwe kengele, kengele ikapatikana sasa naaaaaani? atamfunga huyo paka ili kuwanusuru wenzakeeee!!!!. Mh! mi simo ,shaurilo watakucheka wenzakoooo...

    ReplyDelete
  14. Nawe anony hapo juu you are daft, au wewe Tomaso mpaka uguse ndio ujue. huelewi nini na picha inajieleza waziwazi. ndio nyie mnaponza moto mpaka unaenea nyumba nzima ndio unashtuka, alaa! kumbe kuna moto, too late.

    ReplyDelete
  15. Jamani KP ni mtundu and talented. God bless you, God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  16. Kiongozi mkubwa wa awamu ya tatu

    katochi

    ReplyDelete
  17. we anon Apr 24,12:39 Ndo kusema hapo umetoka KAPA? mwenye macho haambiwi tazama hujizungushia macho kwa raha zake.

    ReplyDelete
  18. Akifungwa Kengele tutajua aliyeichoma Ikulu na kwa nini. Alikuwa anaficha nini? Hizi ni zama ukweli na uwazi kama mwenyewe alivyotaka ingawa hakuwa muwazi achilia mbali mkweli.

    ReplyDelete
  19. Se bm of the year doooooooooooo!!!! Hatari sana hii.

    ReplyDelete
  20. kweli jamaa ni sawa na paka-shume maana kwa kawaida paka shume huiba nyumbani kwa mmiliki wake, si mnajua vicent vya BM au nanyie mnataka 'kubweteka na wivu wa kike'? KP big up kunasiku tutamkamata tu maana za mwizi siku hizi nadhani hata 40 hazifiki, tutampatia kipigo chaa paka mwizi.

    ReplyDelete
  21. Alikuwa waziri wa kwanza kuukana ujamaa wazi wazi: Ujamaa unatupeleka wapi! (Kasikikika kwenye uwanja wa ndege Nairobi (Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mzima)!

    Hao ndio wanafunzi wa ujamaa wa Mwalimu Nyerere ambao hawakuhitimu!

    ReplyDelete
  22. Hili ndo tatizo la siasa zetu saidia nikusaidie,inabidi mfumo mzima ubadilike ili hata wale wanaokuwa madarakani awe huru kufanya maamuzi bila la kuangaliana usoni.

    ReplyDelete
  23. Duu yani kipanya kachora mpaka balls pale nyuma karibu na mkia. KP anajiamini kinoma unajua ni zaidi ya MTANGA ZAJI. unatisha mzee

    ReplyDelete
  24. kp kp michu michu mimi nafikiri tumnge wenyewe kengelele kwani tunashidwa nini sisi wananchi??


    jose morinyo

    ReplyDelete
  25. Uchunguzi tuhuma dhidi ya Mkapa utafanyika

    2008-04-25 09:53:59
    Na Joseph Mwendapole, Dodoma


    Serikali inafanya uchunguzi juu ya tuhuma za Rais mstaafu Benjamin Mkapa kufanya biashara akiwa Ikulu ili kujua iwapo alifanya makosa ya jinai au ya kiutendaji.

    Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge jana wakati akijibu swali la papo kwa hapo kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed (CUF Wawi).

    Alisema iwapo kosa hilo litakuwa la jinai hatua za kisheria zitachukuliwa nakama litakuwa la kisiasa litashughulikiwa kisiasa.

    Katika swali lake, Bw. Hamad alisema Rais wa Awamu ya Tatu alitumia Ikulu kufanya biashara kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hivyo akataka kujua kwa nini serikali inapata kigugumizi cha kumfikisha mahakamani kwa kosa hilo.

    ``Suala hili limeibuka kwa nguvu sana katika siku za hivi karibuni na sisi tunajaribu kuliangalia likoje na tutakapofikia uamuzi tutawajulisha,`` alijibu Waziri Mkuu Pinda.

    Kuhusu kumfikisha mahakamani, Bw. Pinda alisema, ``unampeleka mtu mahakamani pale unapokuwa na ushahidi wa kutosha Ni lazima ifike mahali tujiridhishe iwapo suala hilo ni la jinai au la kimaadili,`` alisema.

    Awali Bw. Hamad alisema taarifa za Rais mstaafu Mkapa zinaweza kupatikana katika Kampuni ya Kusajili Mashirika (BRELA).

    Kwa upande wake, Mbunge wa Kahama (CCM), Bw. James Lembeli aliuliza hatua ambazo zinachukuliwa na serikali kutatua mgogoro wa wakazi wa kata ya Mwendakulima ambao wamekuwa wakilalamikia fidia mbalimbali kwa kampuni ya Barrick Gold Tanzania kufuatia madai ya mradi wa Buzwagi kuwapunja fidia wananchi.

    Pia mbunge huyo alitaka kujua hatma ya wakazi 14 waliokamatwa na polisi hivi karibui kwa madai ya kufanya vurugu katika eneo la mradi wa Buzwagi na kunyimwa dhamana.

    Akitoa maelezo kuhusu maswali hayo, Bw. Pinda alisema wananchi wale wote walilipwa tena zaidi ya kuliko makadirio yaliyofanywa na serikali.

    Alisema dalili zinazojionyesha kwa sasa ni kwamba baadhi yao hawaridhiki na fidia hiyo, na wengine wanataka kurudi tena katika maeneo hayo.

    Hata hivyo, aliwaagiza Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja pamoja naibu wake, Bw. Adam Malima wakutane jijini Dar es Salaam kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

    ``Kwa sasa nimemwagiza Naibu Kamishna wa Madini kwenda huko Buzwagi kupata taarifa za kina kuhusu mgogoro huo,`` alisema.

    Aidha Waziri Mkuu Pinda alitoa wito kwa wakazi hao
    kuepuka matumizi ya nguvu kwa kuwa haitawasaidia.

    Kuhusu wananchi 14 waliokamatwa, Bw. Pinda alisema ataagiza watuhumiwa hao waachiwe kwa dhamana na akamtaka mbunge huyo naye kuwaomba wananchi wake waache kutumia nguvu kiasi hicho.

    Mbunge wa Chambani (CUF), Bw. Salim Hemed Khamis alitaka kujua hatua ambazo serikali imechukua dhidi ya taarifa za tuhuma za baadhi ya vyombo vya habari zinazochafua ofisi ya Spika wa Bunge.

    Waziri Mkuu Pinda alisema, tuhuma hizo sio jambo zuri lakini zilitolewa ufafanuzi na Spika mwenyewe mwanzonimwa mkutano huu wa Bunge.

    Alisema Spika alikuwa jasiri sana na aliahidi kutoa taarifa za tuhuma hizo zitakapokamilika bungeni.

    Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Bw. Omar Kwaangw`, alimwuliza Waziri Mkuu kuhusu kupanda kwa bei ya bidhaa mara kwa mara hususan mbolea na hatua ambazoserikali inafanya kudhibiti hali hiyo.

    Katika majibu yake, Bw. Pinda alisema kazi kubwa ya serikali kwa sasa ni kujaribu kupunguza kasi hiyo, kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vinavyosimamia bei.

    Lakini alisema kupanda kwa bidhaa mbalimbali kikiwemo chakula kunatokana kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kwamba azma ya serikali ni kuwafanya wananchi wake wazalishe kwa wingi zaidi.

    Alisema baadhi ya mawakala wanaosambaza mbolea wamekuwa sio waaminifu na hao ndio wanaopandisha bei ya mbolea.

    Alisema kwa sasa serikali inaangalia uwezekano wa kutumia zaidi vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) vya wananchi badala ya kuwatumia watu binafsi ambao wameonekana kuwa ni tatizo kubwa.

    Waziri Mkuu alijibu maswali ya wabunge tisa kwa muda wa nusu saa yakiwemo maswali ya nyongeza kutoka kwa wabunge wanane .

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  26. Huyu hakika ni simba, na sio danger man mwana wa mkaa hapa!

    Breaking news: Anamalizia bonge la HOTELI huko Entebe Uganda.

    Sevedo

    ReplyDelete
  27. These people are untouchable, tutapigwa politiki mpaka basi tena. Hamna cha balali, mkapa,ngoyai-marialle, chenge, chenji wala nini. Itaisha tu tutasahau, watabaki na vijisenti na ngurdoto zao. Prosecution my butt?! Go after petty thieves!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...