Home
Unlabelled
maandamano kulilia nyamagana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nasikitika kusema kwamba uwanja huo utabomolewa tu maana Serikali tuliyo nayo inajali maslahi ya matajiri wachache wenye pesa.
ReplyDeleteNatanguliza pole zangu kwa wakazi wa Rocky City na vizazi vyao vitakavyofuata maana wataambulia kusimuliwa tu....'hapo zamani za kale hapa palikuwagepo na uwanja ambao watu walikuwa wanachezeamo futiboli..!
Viongozi wa Tanzania nikazi kushawishiwa kama wanaelimu,
ReplyDeleteDu..Rest in peace my dear Nyamagana.
ReplyDeleteNakukumbuka sana enzi zile za kombe Lottery,yosso na matukio mbali mbali ya kitaifa.
Ukiwauliza Yanga na Simba wanakumbuka bado mechi yao ya kihistoria waliyoipigia hapo.
Nyamagana...nailaumu nafsi yangu kwanini sikupanda kwenye jengo la ilipokuwa TRA au pale Tivol bar na kukupiga picha ya mwisho kabla ya kuondoka.Nahofia nikirudi itakuwa ni historia kama "uliwahi kuwepo."
Wachezaji wakongwe kibao wamepitia hapo kuanzia wazee wa kawekamo..pamba ya mwanza wakina George magere masatu n.k
Ila naamini hata kama watakuondoa kwenye uso wa mwanza ..maandamano na vilio vya wanamwanza vitakuwa nawe popote.
Tutafita tu.
Ufa huo Mwalimu aliuona zamani sana,Ukuta unazidi kupasuka.Anayefanya huuutumbo si anajulikana Serikali iko wapi si ipige stop hii kitu?
ReplyDeleteBro michu,kweli natamani kulia,kwani nakumbuka wakati ule ninachezea timu ya mchopa OAU NA EKWADO,hawa viongozi nathani awakucheza mpira ndio maana awaoni uchungu!!wenyewe wamekaria vijisenti tu?kwani sisi watoto wa rock city ndio mahara petu pa kujidaia hapo??si bola hata wagepauza bugalika???
ReplyDeleteNyi watu wa Mwanza hebu acheni utoto. Mji wenu unajengwa nyie mnang'ang'ania magofu. Kama uwanja si tayari kuna CCM kirumba?
ReplyDeleteHebu acheni wawekezaji waje kushusha majengo ya nguvu hapo. Au hamjaona MLIMANI CITY ilivyobadilisha mandhari ya pale Survey? Zamani landmark pale ilikuwa Kanisa la Kakobe lakini suiku hizi keshafunikwa bovu.
Uwanja wa Nyamagana ukibomolewa tu basi Madiwani wotewa Jiji la Mwanza wajue wamejifukuzisha kazi.Watambue kwamba hao kina Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji ni watumishi wa kuja tu.Leo wapo kesho hawana kazi wamefukuzwa watatuachia umaskini wetu Mwanza lakini wao wamesha kwenda mbele kwa mbele.Lazima wakazi wote wa Mwanza tushikamane kidete ili Uwanja wa Nyamagana usipewe mwekezaji binafsi na kamwe matumizi yake yasibadilishwe na kutumika kwa ajili ya biashara zingine tofauti na mpira na michezo mingine.HIVI NIULIZE,MWANZA MAENEO YALIYO WAZI NA TUPU KWA UJENZI WA SHUGHULI ZA KIBIASHARA YAMEKWISHA AU BADO YAPO?Kwa nini Mkurugenzi wa Jiji ang'ang'anie kulitwaa eneo hilo kwa matumizi mengine tofauti na uwanja wa michezo?Au kuna Rushwa ndani yake tuelezwe?Nashauri uwanja huo sasa ukabidhiwe Chama cha Mpira cha Mkoa wa Mwanza ili kiweze kuingia ubia na taasisi za kifedha kwa ajili ya kuuendeleza uwanja huo uwe wa kisasa zaidi.Tofauti na hivyo Uongozi mzima wa Mkoa wa Mwanza utakuwa umejipalia makaa.Wenye mji wao wamekataa uwanja huo wa Nyamagana usitumike kwa matumizi mengine mbali na michezo.Uwanja huo pia hutumika kwa ajili ya mikutano ya hadhara ya kihistoria.Uwanja huo ulitolewa kwa wakazi wa Mwanza na Williamson Diamond ambaye ndiye aliye umiliki toka enzi hizo kama kumbukumbu ya upendo wake kwa wakazi wa Mwanza.Pia una historia ya kumbukumbu ya Bismarck,mtawala wa Ujerumani wakati huo Tanganyika ilipokuwa chini ya utawala wa Wajerumani.Kwa hiyo mtu tu wa kawaida kupewa uwanja huo akajenge jumba kwa ajili ya biashara yoyote ile hata lingekuwa Kanisa au Msikiti,siyo jambo la busara hata kidogo.Maeneo ya wazi Mwanza bado yapo mengi sana.Wenye uwezo kipesa wa kujenga maghorofa wapewe maeneo mengine ili jiji letu liweze kupanuka zaidi kuliko kuendelea kung'ang'ania katikati ya jiji tu kila kukicha.Huu ni ufinyu wa kufikiri.Tukiendekeza hii njaa ya matumbo tu itatufikisha pabaya.Tufikirie na vizazi vijavyo,tuwaachia kumbukumbu zipi za kihistoria?PIA NINGEPENDA NIMUULIZE MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA lile eneo lililopo katika makutano ya barabara iendayo Uwanja wa Ndege(Airport),na barabara iendayo Sokoni Kirumba hadi Polisi Kirumba,mkabala na Hospitali ya AIC Misheni,eneo hilo hivi sasa limezungushiwa uzio wa mabati,swali,PANATAKA PAJENGWE KITU GANI? Eneo hilo liliwahi kuzusha mgogoro mkubwa wa kisheria lilipo ruhusiwa kujengwa Kituo cha Mafuta cha Mfanya Biashara mmoja wa hapa Mwanza mwenye asili ya kiasia,kwa jina Mansoor,ambaye hivi sasa ni Mweka Hazina wa CCM MKOA WA MWANZA,kituo kile cha mafuta kikalazimika kibomolewe kwa sababu eneo hilo ni la wazi haparuhusiwi kujengwa jengo la aina yoyote na isitoshe pako karibu sana na Transformer ya Tanesco,kutokana na hujuma hiyo iliyo zingirwa na harufu ya rushwa Ofisa mmoja mwandamizi wa Manispaa ya Jiji la Mwanza alisimamishwa kazi au alihamishwa kituo kingine kama adhabu.Na inasemekana mwenye kituo hicho kilicho bomolewa alidai fidia ya mamilioni kutoka Manispaa ya Jiji kama fidia kwa kubomolewa jengo lake ambalo alidai kwamba alipewa vibali vyote vya ujenzi na Mamlaka ya Jiji la Mwanza.Sasa ule uzio wa Mabati uliowekwa hapo hivi karibuni unaashiria kwamba kuna jengo lingine tena lililoruhusiwa lijengwe pale licha ya gharama kubwa waliyo bebeshwa wakazi wa jiji la Mwanza kwa sababu ya uzembe wa wafanyakazi wachache wa jiji walijawa na ulafi wa kutajirika haraka haraka kwa njia za mkato? Namuomba hata Mheshiwa Waziri anayehusika na Tawala za Mitaa atusaidie sisi wakazi wa Mwanza kutatua mgogoro huo!Madhambi mengi hivi sasa yanafanyika kwa kisinngizio cha Ubinafsishaji na Uwekezaji.
ReplyDeletekumbukumbu ni kitu muhimu kwa kila jamii, kama huna kumbukukmbu basi tena kuna kitu kimebaki? sisi wengine hatutaki kiwanja cha ccm kirumba. Nyamagana july 10 1974 Simba VS Yanga mechi ya karne bongo, haitasahaulika hata mkibomoa!!!!
ReplyDelete