magwiji wa muziki nchini waziri ally wa kilimanjaro band 'wana njenje' (shoto) na hassan rehani bitchuka wa orchestra ddc mlimani park 'wana sikinde' wakibadilishana mawazo wakati wa semina ya hakimiliki leo kwenye ukumbi wa baraza la sanaa la taifa, ilala shariff shamba, dar. mengi yamezungumzwa ikiwa ni pamoja na kupiga vita uharamia wa kazi za sanaa unaofanywa na watu wachache wanaofaidi matunda ya wasanii wengi. hata hivyo hii si semina ya kwanza na wala hakuna kilichoendelea huko nyuma, sijui sasa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Michuzi hapo hakuna staili ya kujadili wala kutafakari. Inaonekana huyo mwenye kikofia chekundu anampiga mzinga waziri.
    Angalia alivyokunja sura.

    ReplyDelete
  2. Naona Bitchuka umri umekwenda. Nadhani anajiandaa kustaafu.

    ReplyDelete
  3. Duh!! kweli wazee wamechoka na wana haki ya kulilia haki miliki ili wafaidi vipaji vyao. Hivi mambo ya haki miliki yameishia wapi au wasanii nao wenyewe wamekuwa kama wanasiasa kwa kuendesha makongamano bila mafanikio yeyote? Naona wahindi siku hizi mmewashau kabisa au wameanza kuwalipa vizuri? tehee!! teheee!!! teheeee!!!!

    ReplyDelete
  4. Bitchuka afanye collection ya nyimbo zake zote za huko nyuma katika DVD umaskini wote utamtoka!Kama hana pesa atafute ushauri haraka iwezekanavyo wapo watakao kubali kumsaidia,ikibidi hata makampuni ya nje!Wapo Wabongo Majuu hivi sasa biashara ya muziki wanaijua.Wakati ukuta ndugu yangu Bitchuka,anza kula matunda ya jasho lako sasa!Yasije yakakukuta ya wenzako waliokutangulia.Muziki wako ni mzuri sana na unauzika asikudanganye mtu!Ukisubiri hao jamaa wa Cosota sijui ujue utakufa masikini.Wewe siyo masikini.Utajiri wako unawanufaisha watu wengine!Bitchuka amua sasa!DVD zitalipa zaidi kuliko CDs kwa umri wak hivi sasa!

    ReplyDelete
  5. Hawa ni wakongwe ambao kazi zao tumeziona na tumezikubali. Nasikitika kwamba kazi zao hazijapata warithi. Wanamuziki wa leo kazi yao ni kuiga wakongo. Wamewaiga mipigo, sauti na mpaka mwisho wameamua kuwaleta wazima wazima katika bendi zao. Ukija kwa hao wanaojiita kizazi kipya ndio usiseme. Wazungu si wazungu wabongo si wabongo. Wanaiga mambo yasiyo na maana imefikia wasichana wanaimba nusu uchi na wavulana chupi nje na kujishika nyeti. Hakuna ubunifu wa utunzi wala melody. Hakika TZ inaangamia kimuziki. Hongereni akina Bitchuka, Waziri etc.

    ReplyDelete
  6. Hapo ndipo nilipowaambia ..mnawapo mahela kibao watoto wanoimba nyimbo za copy Bongo star Search .
    na kuwasahau wazee wenyewe walioimba nyimbo hizo.....

    ReplyDelete
  7. HAPO KILICHO KOSEKANA NI COLGATE MAANA HIYO HALUFU WANAJUA WENYEWE DAMN NASIKIA KICHEFUCHEFU....

    ReplyDelete
  8. Bongo star search, tusker project fame na pop idols zinatatrtibu zinafanana lakini ya pili kwa vile imefanywa na wabongo waswahili wanatafuta maneno, acheni hizo.Na kwa taarifa Bongo star search peke yake ndio imelipia performing rights kwa copyright society of tanzania kwa hiyo waliotumiwa nyimbo zao watapata kifuta jasho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...