lugha ya mwili inajionesha kwenye hii picha ambayo mdau emmanuel mwandosya katuchomolea toka kwenye maktaba yake inayoonesha mwalimu akiwa na idi amini dadah na pembeni yake ni mzee john malecela wakati huo waziri wa mambo ya nje katika mkutano wa oau miaka hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. YANI HICHO KICHEKO CHA THE LATE JK KINANIKUMBUSHA ULE MSEMO WA WAHENGA WETU.....CHEKA NAO JAPO SI WEMA KWAKO.!!!!!!!!!!!!mdau alosto in UK

    ReplyDelete
  2. ha ha ha Yaani nawaza,nadhani Nyerere anacheka kwa kumsanifu tu Iddi. Maana in reality, hawa vichwa vyao ni tofauti kabisa.sasa Nyerere kalivyokuwa kembamba na Iddi baunsa.

    Nadhani hapo nyerere anasema "Huyu iddi kweli ana kichwa cha mwendawazimu"

    RIP Julius and Iddi

    dada T

    ReplyDelete
  3. Baada ya hapo "miaka 18" ya kujifunga mkanda. Ilianzia "kilo moja ya sukari lazima uchukue na spea ya jembe la kukokotwa na ng'ombe" hata kama huna matumizi nalo,

    Halafu, Chai ilyoungwa pipi zilizosagwa badala ya sukari. Sabuni za vipande nazo kwa foleni, na sabuni hiyo-hiyo unasugua mswaki juu yake ili iache povu kidogo usukutulie/ ng'arishie meno. Hiyo ndo "colgate" Mwe! tumetoka mbali! lakini sasa na ufisadi huu....! sijui kupi kwema.

    Samahani, Bwana Michu naona nimekukumbusha mbali...

    ReplyDelete
  4. Nyerere anacheka kinafiki.

    ReplyDelete
  5. MICHUZI
    HAO WANAOSEMA KUWA NYERERE ALIKUWA ANACHEKA KINAFIKIAU IDD NA NYERERE WALIKUWA HAWAIVI INAONEKANA HAWAJUI WASEMALO. NAPENDA KUWAAMBIA KUWA NYERERE NA IDD WALIKUWA MASWAHIB WAKUBWA HUKO NYUMA NA WALIKUWA WAKISHIRIKIANA,WAKITEMBELEANA NA KUSAIDIANA. NDIO MAANA KULIKUWA NA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI.

    UGOMVI NA UHASAMA WA IDD NA NYERERE ULIKUJA MWISHONI MWA MIAKA YA SABINI NA KUIFANYA TZ KUINGIA VITANI. HUKO NYUMA WALIKUWA WAKIELEWANA SANA. HIVYO PICHA HIYO NA YENGINE ZILIZOLETWA NA MWANDOSYA KIPINDI HICHO WALIKUWA MARAFIKI KABLA YA KUINGIA VITANI.

    KWA HIYO VICHEKO HIVYO NI HALALI NA VYA KAWAIDA SI UNAFIKI WALA UPINZANI KWA KUWA WAKATI WA PICHA HIZO UGOMVI ULIKUWA HAUJAANZA. IELEWEKE KUWA BAADA YA UGOMVI VITA ILIMTOA IDD MADARAKANI NA HAKUWA TENA KIONGOZI WA UGANDA WALA KUHUDHURIA VIKAO VYA OAU.

    WAKATI WA VIKAO HIVYO IDD ALIKUWA KIONGOZI WA UGANDA NA RAIS HALALI KABLA YA KUNG'OLEWA NA JWTZ

    ReplyDelete
  6. Hapa the late Nyerere kwa kweli anaonyesha kama hataki salamu ya the late Idd Amin .... anaonekana kama Nyerere hataki kushikana mkono na Idd Amin

    ReplyDelete
  7. Wote hawa hwakuwa wametulia. Wote walikuwa madikteta. Pia tusisahau Iddi alifanikiwa kuwatimua magabachori kule UG. Huyu alikuwa na wazimu uliotulia kwelikweli

    ReplyDelete
  8. naona kama vile Julius anagoma kumshika mkono Idd,au...? Halafu aliyesimama pembeni mwa Idd anatimiza kile kilichoandikwa katika misaafu,kwamba waheri wapatanishi maana ni wana wa Mungu

    ReplyDelete
  9. Julius ehe ! acha uhuni bwana, hata kusimama kidogo ?
    Unasalimiana na mkubwa mwenzako huyo !
    Na hiyo lugha ya mwili ni nini ?body language !
    Someone is having a laugh mate !
    JK

    ReplyDelete
  10. kusema ukweli hapo nyerere ndani anacheka unafiki na uoga. japo iddi amini alikuwa mtu mbaya. iddi amini hapo lazima kamuona nyerere akasema ngoja nikamfuate nimpe mkono. Iddi Amini alikuwa mtu mbaya ila sivyo wanavyosema Waaengereza na USA mpaka wakatengeneza Movie. Iddi Amini waengereza walimtumia nyerere sababu Iddi Amini alikataa Wayahudi kuishi Uganda akatishia wakija nitawafanya kama Hitler, na Pia alivyowafukuza Wahindi wakaenda UK. waengereza wakachukia UK na USA ni nchi zinazotaka watu wao wasifanyiwe baya. wanasema Africa waache rushwa ndio watasaidia kwani nani anaazisha rushwa si wao wanauza silaha na kuchukua madini bila izini. Baba wa Taifa tunamuheshimu ila mengine kakosea.

    ReplyDelete
  11. Namuunga mokono mdau wa 3:37am. Ile 'Miezi 18' iligeuka Miaka 18! Sabuni, mafuta ya kupikia, sukari adimu. Kadi za kaya! Yaani watu waliokuwa wnaafanya kazi RTC na National Milling walikuwa ni Miungu wadogo! Unakwenda dukani, hamna kitu cha kununua! Viatu matairi, wewe vijana wa siku hizi hawajui taabu ya wakati huu!

    Mwizi anavunja vyumba na kuiba Mchele au unga! Kama mnao ndani mnakaa kimya! Unga wa YANGA mnakumba na kuvaa magunia! Ukifua nguo unakaa nje na kuzilinda wakati zinakauka. Watu walikuwa wanaiba mpaka chupi!

    Japo Mwalimu anacheka hapo, alikuwa hampendi Idi Amin Dada. Mwalimu alimwaita, "Idiotic Buffoon!"

    ReplyDelete
  12. HAPO NAONA NYERERE ANAONESHA JEURI YA CHAMA ANACHEKA LAKINI HAMPI MKONO NDULI. KUDA DEDEKIIIIIII.

    ReplyDelete
  13. ANON WA APRIL 15 2008 4:14 ASANTE
    KWA UKWELI WAKO MAANA MZEE HUYU
    ALIKUWA NA SURA MBILI MOJA YA AJABU
    SANA.HAPAKUWA NA HAJA YA KUPIGANA
    NA IDD AMIN WAKATI TULIKUWA MASIKIN
    WA KUTUPA.TAMAA ZAKE ZA KUWEKA WATU
    WAKE KWENYE UKANDA WA MAZIWA MAKUU
    NDIO ZIKATULETEA ALIODAI NI WANAFUNZI WAKE.MARA WAKAJA KUWA
    MAFISADI NAMBARI WANI.ALOO MAISHA
    HAYA.WE ACHA TU.WOTE WAMETANGULIA
    MBELE YA HAKI SASA.HUKO HAKUNA UONGO WALA UPENDELEO.MUNGU AWALIPE
    KWA KILA WALILOTENDA HAPA DUNIANI

    ReplyDelete
  14. Namwona kwa nyuma aliyekuwa Body-guard mkuu wa baba wa taife mzee Peter Bwimbo akimtazama Iddi Amini kwa makini kabla hajatoe zile kipigo. Michuzi hapa umenikumbusha mbali sana.

    ReplyDelete
  15. Timu imekamilika baba wa taifa, mzee Malecela na Kamanda mkuu wa usalama wa Taifa zama hizo Peter Bwimbo. Hawa ndio mashujaa wa taifa letu.

    ReplyDelete
  16. Kipindi cha uongozi wao nch iliheshimika na upeo wao wa juu wa maongozi ulitambulika ulimenguni kote. Nyinyi mnaosema oo maisha yalikuwa magumu, mnajua gharama ya vita na kulikomboa taifa kutoka kwa nduli au mnacheza TU. Idi Amini angetawala Afrika nzima kama siyo Nyerere, Malecela na mzee Bwimbo.

    ReplyDelete
  17. Duu kaka michu hii historia kumbe mzee Peter Bwimbo na malecela wametoka mbali na nchi hii.Kumbe wazee hawa hatuwasikii vinywani ni moja ya wazee wa taifa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 13, 2008

    its not funny kwa miaka nane amin alipotawala uganda watu 600,000.00 waliuwawa, baada ya hapo nyerere akamweka rafiki mpenzi obote ambae nae kwa muda wa miaka minne aliuwa zaidi ya 800,000.00 wengi wao wapinzani wake wa baganda,bunyoro nadhani wasomi mnakumbuka genocide ya luwero triangle. as far as malecela is concerned alipokuwa waziri wa mambo ya nje alianza kuwa maarufu zaidi ya baba yetu mtukufu nyerere sasa ikabidi nyerere abadilishe kikao cha nyumbani (furniture) lakini malecela hodari kijijini kwake mvumi kuna umeme 24/7 pia hospitali ya mission (optomentry, school of nursing etc)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...