KUNRADHI WADAU,
KUTOKANA NA SABABU ZISIZOWEZA KUZUILIKA MAFUNDI MITAMBO HAWAKUWEZA KUCHEZESHA LILE SHINDANO LA KUMPATA MDAU WA MILIONI 4 MARA TU BAADA YA KUPATIKANA. NA KWA JINSI SPIDI YA WADAU KUTEMBELEA GLOBU HII YA JAMII KUWA KALI, ILE KUTAHAMAKI WAKAKUTA TAYARI NI MILIONI 4 NA USHEE.
HIVYO NIMEREJESHA HOJA HII KWA MDAMINI ILI AUNDE TUME YA KUAMUA NINI KIFANYIKE ILI ILE DOLA 500 ALIYOTOA IPATE PA KWENDA. NAOMBA TUFANYE SUBIRA NA HATIMA YA MKWANJA HUO ITATANGAZWA PUNDE TU....
- MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nanukuu maneno ya baba wa taifa "..ukishaanza kula nyama za watu, huwezi kuacha, hata siku moja utakula tu, utaendelea kula tu.." Mwisho wa kunukuu.
    Maneno hayo ni kweli 100%, na ndo maana ukishazoea ufisadi huwezi acha. Utafanya ufisadi hata pasipo stahili, Michuzi wewe ni fisadi, unadamu ya kifisdi, na huwezi kuacha abadani...! Yaani hata kwenye ishu kama hii wewe unataka ulete ufisadi?! Ona kauli zako zinavyogongana, mara ooh mafundi hawakuweza kuchezesha, mara walishtukia mdau kafika milion 4 na ushehe, mara sijui wadhamini wataamuwa dola 500 ziende kwa nani...hovyo tu, hakuna moja la maana, kauli za kifisadi fisadi!
    Wewe kama unawatu wako uliowapanga na bahati mbaya hawakuwa katika milion 4, wape tu! Mambo ya watu haya yanini kuyaiga, we endesha tu hii blog sisi wala hatuji hapa kwa ajili ya hizo zawadi, tutaendelea kuja bila kuweka ahadi hewa! Usitufanye watoto wa kuku bwana...! Unajidai kufa wakati kuzimia huwezi...!
    Ah ngoja ni sign off, nisichafue hali ya hewa.

    ReplyDelete
  2. Michuzi sema bwana kama hela umechikichia huko London,mie najua umefanyia shopping hizo hela..ppoa bwana tunasubiri mshindi..
    kyekue

    ReplyDelete
  3. Kwa kuwa hii ni blog ya jamii basi nashauri ili kuweka mambo sawa basi hizo Dola 500 zielekezwe kwenye shughuli ya kuisaidia jamii Mfano nashauri zitumike kuwasaidia watoto yatima na Bw. Michu utangaze kabisa kuwa unatoa msaada huo kwa niaba ya wadau wote wa blog hii.

    Naamini kabisa kuwa kwa kufanya hivyo pia utakuwa umemaliza kabisa lawama kuwa unapendelea washindi.

    Mbarikiwe.

    ReplyDelete
  4. michuzi bwana wewe sema tu umetukopa hiyo hela uongezee shoping ya huko majuu, sie tumekubali ila sio mbaya utafute ufumbuzi haraka wa jinsi ya kuturudishia hiyo hela yetu kabla hatujaamua kuandamana

    ReplyDelete
  5. Mimi naunga hoja ya mdau wa kwanza na wa tatu

    Kusema unaulizia wadhamini how to get the winner na wakati umeshakiri mitambo ilichemsha sio vizuri. Hii blog imeshapata sura ya kuwa blog ya jamii ni heri hizo hela zisaidie jamii. Tungeliomba hizo pesa kwa vile zimeshatoka mikononi mwa wadhamini basi zisaidie jamii. Tunataka zipelekewe watoto yatima au charity yeyote itakayosaidia jamii.

    Toa maelezo ya charity sisi hapa tupige kura kuchagua ziende kwa charity gani.

    Mambo ya kumpata mshindi sasa hivi na wewe umeshakiri kuwa mitambo ilikua mibovu inanukia UFISADI na hata kama mkimpata mtu mnayedhania ni wa kweli hamna mtu yeyote atakayeelewa.

    Wengi hatupo hapa kwa ajili ya zawadi na wala sikujua kuwa mshindi wa 4 millions ameshafika ila ninachokuomba ni kuwa ujue huku kwenye blog yako wako watu wa umri tofauti, elimu tofauti, career tofauti, uwezo tofauti, hata kabila na jinsia tofauti so please treat all with dignity. That is all I am going to tell you. ACHA KISWAHILI KIREFU

    ReplyDelete
  6. Hongera kwa kufikisha watu wote hawa million 4 ...Hongera sana...

    Mimi ninachokuomba ili kuondoa haya matatizo ya watu kuingia kwa mara moja kila mara inapokaribia hizi number ni muhimu ukanzisha kama bahati nasimu sasa. Uwaambie watu mshindi atachaguliwa kati ya watu walioingia kutoka labda 100 people before and 100 people after the hit. Mtu mwenye kutaka kushiriki acopy screen akae nayo na number ikitangazwa baada ya kuchezesha hizo number. Mtu mwenye screen copy ya number hiyo aseme yuko nchi gani...mkilinganita time na ip address kama zinamatch basi ndio awe mshindi bila hivyo utazidi kulaumiwa kila siku tu humu.

    Congratulations on another milestone! I have a feeling we will be congratulating you on your 10,000,000,000 very soon

    I am very impressed with the number of people you have able to reach.

    CONGRATULATION

    ReplyDelete
  7. HAHAHAHA KAMCHEZO HAKA!MHH vipi kapatikana mtu msiyemjua nini?si mbaya kwani mtu wa mil.4 si atakuwa ni mmoja tu?? why mambo ya droo tena? naamini kaunta itasoma milioni 4 moja tu na si nyingi mpaka iwekwe droo. Cha muhimu kama kuna alietuma mkakubaliana na vigezo vyake+uhalali basi apewe.Anyway hii ni blog yetu bado.

    Mdau

    ReplyDelete
  8. hizi ni njama za ki-chenge tu.

    ReplyDelete
  9. Heee! Babuali acha jazba! michuzi sio fisadi ndo wasamaria walobakibaki hao ktk kundi! Mtagaiwa tu kila mtu cent tano tano blog nzima! si zitatosha?
    Hujambo lakini?
    -> zilipendwa,(K-B-).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...