Hi Kaka Michuzi,

Pole na uchovu wa safari na karibu nyumbani.

Mimi ni mdau katika hii blog yako, na ninafahamu kuwa katika kipindi tofauti blog hii imekuwa ikidhaminiwa na taasisi za fedha, kwa maana ya mabenki.

Michuzi huwezi amini huku wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi ina tawi moja tu la benki ya NMB na tawi ilo linahudumia wilaya hiyo ya Nachingwea na wilaya mpya ya Ruangwa. Nasema hivi kinachotokea katika tawi ilo ni hatari kwa wenye fedha zao na wale wanaohitaji huduma za kibenki.
Unapotaka kuchuka ama kuweka pesa basi inakubidi umtume mtoto alfajiri aende kuweka foleni ya kupata huduma hizo kwani idadi ya wateja imezidi hata muda wa benki kutoa huduma kwa wateja wake. Watu ni wengi kwa maana ya wafanyakazi, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida toka wilaya mbili husika hutegemea tawi ilo moja kwa huduma za kibenki.

Ninachojaribu kusema ni kuwa wilaya hizo mbili zina wahitaji wa huduma za kibenki wa kutosha, ikumbukwe kuwa hizi ni wilaya zinazolima korosho na mazao mengine ya biashara kama vile ufuta. Wananchi wa wilaya hizi wanafedha zao ambazo sidhani kama wanastaili kupata mateso ya huduma ya kuzitunza kama yanavyotokea kwa sasa.

Nilikuwa natoa rai kwa mabenki yaliyopo hapa nchini kuangalia uwezekano wa kufungua matawi katika wilaya hizi ili watu wapate huduma stahiki na siyo bora huduma yenye kero ya foleni.
Naomba kuwasilisha.

Mdau Nachingwea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Amani, Heshima na Upendo kwako Kaka na wadau.
    Alilosema mdau wa Nachingwea ni kweli kabisa maana nami nilibahatika kuishi wilayani pale miaka kadhaa iliyopita na hali ya kimaendeleo inakuwa inafika kule kwa joto la kibatari. Ni kweli kuwa pamoja na mabenki kujitangaza saaana kuwa yanatoa huduma kote Tanzania, bado hayawafikii walengwa na hata wenye kupanga sera za huduma za kibenki hawawafikirii wananchi wa wilayani angalau kwa kuweka masharti ya mabenki kuwa na asilimia ngapi ya matawi wilayani. Hakuna uwiano kabisa katika utoaji wa huduma muhimu kati ya mijini na vijijini na hii inasikitisha saaana. Na yote hii ni kutokana na wakuu wa nchi kutotembelea vijijibaada ya uchaguzi kujionea hali halisi. Wanapofanikiwa kwenda huko wakakutana na mambo yalivyo wao wenyewe wanastaajabu na kuanza kusimamisha watu kazi kwa uzembe lakini bado hawaendi na kwa tafsiri yangu ni kuwa hawawajali wananchi ambao wanaishi vijijini na ambao ndio wengi zaidi. Ni kama walivyosema Morgan Heritage ktk wimbo wao wa Nothing To Smile About, ni kuwa pamoja na matabasamu na sura za furaha walizonazo viongozi wetu wanapokutana nao ofisini kwako ama wanapowaandalia wageni hao dhifa za kitaifa, bado kuna wengi wasiojua raha ya maisha nchini tena katika huduma nyingi muhimu. now look at the life in the villages and tell me if you see anything to smile about.
    Blessings to ya'll.
    Ras Twin

    ReplyDelete
  2. Kwa ushauri tuu. Hiyo ni hali nzuri ya kuwahamasisha wananchi wenyewe wa Nachingwea kufungua Credit Union Bank. maelezo yako mdau ni ushaidi tosha wa kutayarisha feasibility study/ business plan. Sometimes ni vizuri wananchi kujihamasisha na kujiletea maendeleo wenyewe. Jaribu kuongea na wataalam wa kifedha, financial advisers, kwa ushauri yakinifu.
    Chukulia hali hiyo kama mtaji wa maendeleo badala ya kuliona kama tatizo lisilotatulika.
    Kuna baadhi ya wilaya kwa sasa Tanzania zimeanzisha benki za wananchi. Jaribu kuongea nao watakueleza mchakato mzima uliotumika katika uanzishaji wake.

    ReplyDelete
  3. Jamani acheni tuu,nchi hii ina mambo,yani huko Nachingwea ni balaa tupu,Maana ukashamaliza mambo ya Bank,angalia jirani zao hapo posta,yaleyale simu za kukoroga unaomba posta.Sijui kama yameisha lakini wilaya hiyo kwa kweli Mungu atusaidie.Mifisadi tuu imejaa huko.Maendeleo ya aina yoyote hamna shule,hospitali shida,barabara nguja tupu.Yaani siwezi sema zaidi uchungu.

    ReplyDelete
  4. Someone should have told you folks !Kufungua tawi la benki sio swala la kisiasa ama upendo na urafiki
    NI BIASHARA !
    Hii ni sawa na kumuuliza mhindi kwa nini hajafungua duka Ikwiriri !
    KAIMA

    ReplyDelete
  5. Naomba viongozi wetu wawe wanazunguka wilayani, vijijini ili waweze kujionea wenyewe kuliko kujinadi kipindi cha uchaguzi baada yakupata uongozi wanawasahau waliowawezesha wakafika pale

    ni kweli kabisa kwani hata hapa kwetu manyoni mkoa wa singida tatizo ndio hilo hilo tunayo bank hio hio moja na kunakipindi inafikia uende kupanga foleni asubuhi mpaka jioni ndio unatoka, viongozi muwe mnazunguka ili mtutatulie problems zetu.

    ReplyDelete
  6. kwa kifupi huko kusini kuko nyuma sana kimaendeleo sio suala la ma bank tu.Umeme,maji,barabara shida tupu ndio maana hata vijana wakipangiwa kazi huko wana hiari kuacha kwenda watafute kwenginepo.
    Sawa suala ni biashara lakini sasa imeshaonyesha kuna mahitaji makubwa huko,wafanyabiashara na watupie macho huko.

    ReplyDelete
  7. we kwani hauna friji? tunza hela zako kwenye friji au chini ya mto sio unatusumbua sumbua hapa

    ReplyDelete
  8. Unajua nini bank ni biashara na ni waizi tu....Chukua plastik weka hela yako chimbia chini ya ardhi weka vijiti ili ukumbuke mahali zilipo ..lakini weka kwa mafungu mafungu. Kila ukichacha unajichimbia shimo moja unaendelea na life yako...You save yourself from the hussles, your spare your time and you save on iterest...

    But psssss don't tell anybody

    ReplyDelete
  9. Mimi naitwa H.T. Komba nipo hapa Nachingwea, nyie leteni hela zenu kwangu mimi nitawaifadhia nyumbani kwangu na wala sitawatoza ushuru kwa kuwa nyie ni watanzania wenzangu, napatikana kila siku ya jumatatu hadi ijumaa pembeni ya duka la vipodozi karibia na bank ya NMB, karibuni nyote!

    ReplyDelete
  10. Michuzi , naomba uitoe hiyo ya MATATIZO YA USAFIRI WA GONGOLAMBOTO, nimeituma kwa kupitia e-mail yako. Tunaomba uiweke hadharani ili `wahusika' waione, au nimekosea?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...