leo nimepata heshima sio tu kutembelewa ofisini hapa dar na mzee wa busara, yusuf mahmoud a.k.a dj yusuf, bali pia kukabidhiwa kitabu cha picha kinachoelezea mambo yote ya tamasha la sauti za busara lifanyikalo kila mwezi februari ya kila mwaka kwa mwaka wa tano sasa. kitabu hiki ambacho kimeandikwa kistadi na kusheheni picha kibao za sauti za busara ni mkusanyiko wa matukio yote muhimu ya tamasha hilo ambalo limejipatia umaarufu mkubwa duniani kama 'the friendliest festival on earth'. asante sana dj yusuf na peter bennet kwa tunu hii.
kwa habari zaidi na picha za sauti za busara bofya hapa
Kabla sijasoma story yenyewe.. nikajua umetembelewa na mchawi!! Viswahili vingine bwn
ReplyDelete