Ule mpambano wa soka wa kukata na shoka kama siomundu kati ya TANZANITE FC ya Atlanta Georgia na MASHADA FC ya Birmingham, Alabama, sasa umeshaiva!
Habari kutoka kwa wadhamini wa pambano hilo zimeshathibitisha venue ambayo mahasimu hao wawiliwatajitupa uwanjani kuonyeshana mpira.
Pambano hilo litafanyika katika Uwanja wa kimataifa wa Legion Field Birmingham, Alabama, wenye uwezo wa kuingiaza watazamaji 83,091.
Saa za mashariki ni 09:00 jioni. Hapo ndipo Nyumbani kwa University of Alabama Blazers(NCAA). Pia ni mara nyingi umekuwa ukitumika kwa mechi za Timu ya soka ya Marekani.
Address ni
LEGIONM cLENDON FIELD
400 Graymont Ave
W/Birmingham,
AL 35204.
Kwa niaba ya Tanzanite FC Organization tunawaomba watanzania wote waishio maeneo ya karibu hasa yaGeorgia, Alabama, Tennesee nk. kuudhuria uwanjani kuwapa moyo vijana wao ambao wameadhimisha kuifundishampira timu hiyo.
Kama utaweza please bring TanzaniaFlags, Vipeperusho na hata Jersey kama unazo. Hatujajua kama wenyeji wamepanga viingilio au ni free lakini kama kuna habari zaidi tutawajulisha.
Kwa habari zaidi pitia
Tunaomba picha za uwanja mjomba Michu!
ReplyDeletenyie washamba nini? mnatia aibu tu...yaani badala ya kuweka mikono yenu upande wa kushoto,kwenye moyo, nyie mnaweka kulia....mnachekesha kweli nyie...
ReplyDeleteBigUp,keep on keeping on,Boyz.We are proud of you all here down home,Bongo ie!
ReplyDeleteWAKUBWA WA ALABAMA NAMTAFUTA RAFIKI YANGU HUKO NILIKUWA NAE HOUSTON KIPINDI ANAITWA OMALI TUWANO...KAMA KUNAMTU ANAMJUA TAFADALI MPE MAIL YANGU...makude69@yahoo.com
ReplyDeleteYawezekana Hiyo syle ya kutumia mkono wa kushoto ni ya Kikenya . Si lazima iwe ni ushamba fulani .
ReplyDeleteHawa wabeba maboksi wa ATL si walisema watakwenda Bongo kwa ziara ya kimpira na wakadai watacheza gemu na Vigogo vya Dar(Yanga,Simba)safari imeishia wapi ama bills zimeongezeka?Nyie wachovu wa down south semeni kweli hamuwezi kulipa tiketi(zimepanda) za ndege na wengine hamna uwezo wa kurudi mana mna Record(1 in particular).Wachovu nyie njooni Up North tuwafundishe jinsi ya kutandaza bolli
ReplyDeleteWe Mbigiri hebu tuliza boli, mambo mazuri hayataki haraka! Bongo lazima tutashuka mwaka huu na tutakuja kuwaonyesha mpira hao wake wa Enyimba na Al Akhdar. Kuhusu kuja North sijui uko State gani lakini kama mko kamili tumeni maombi ili tuje kuwafunga. lakini sisi Chandimu hatutaki sisi tunacheza mpira na watu wanaojua mpira. Hii ni timu kuwa bwana!
ReplyDeleteInawezekana mpira ukatangazwa live kwa dk. 45 za kwanza. Kwa hiyo waliokuwa na mitandao wanaweza kusikiliza pitia internet radio @ www.bongoradio.com
ReplyDeleteSaa za kati 9 mchana na saa za Mashariki ni saa 10 jioni.Huu ni mwanzo tu!
Naomma nikufahamishe we anonymous unayejadili mkono sharti uwekwe upande wa kushoto! Kila nchi ina utaratibu wake na mila zake. Kwa Marekani kuweka mkono upande wa kulia ndo utamaduni wao. Hata wewe ukija huku inabidi ubadlilike. Kuna mambo kama kuvaa badge, sisi huko Tz tunavalia kushoto lakini huku wanavalia kulia na wanadai wanasoma kuelekea kulia hivyo na badge inapaswa kukaa kulia ili iwe rahisi kusoma. Ungekuwa na busara ya kuuliza mbona mikono imewekwa upande wa kulia ili ujibiwe na sio kuanza kukashifu!
ReplyDeleteKama huelewi kitu ni bora kuuliza kuliko kukurupuka tuu na kuanza kujieleza bila mpangilio.
Mambo ni tofauti kwenye nchi za watu na kama ni mambo mazuri sii vibaya kuyafuata, kujichanganya ni vizuri ili ukubalike na mambo yako yakunyookeee ukiwa mbali na nyumbani mradi usiige mambo mabaya tuu.
Kama huelewi uliza au uache kutoa maoni.