
uongozi wa mkoa wa mwanza unasemekana uko katika mchakato wa kuuvunjilia mbali uwanja wa michezo wa nyamagana na kujenga majengo mengine ambayo siyo ya michezo ila biashara.
shirikisho la soka nchini, kupitia kwa katibu wake mkuu frederick mwakalebela, leo limetoa tamko kali kulaani hatua hiyo inayotaka kuchuliwa dhidi ya uwanja huu na kuutaka uongozi wa mkoa kufikiria upya hatua hiyo, na kuiomba serikali iingilie kati kwa kuzingatia uhaba wa viwanja vya michezo na pia kumbukumbu ya uwanja wa nyamagana.
wadau hii imekaaje?


mi nafkiri wasiuvunje maana ulitumika kutambulia ndugu zetu wa
ReplyDeletemv Bukoba? wauache kwa ajili ya mechi ndogondogo maana wa kirumba ni kwa ajili ya mechi kubwa na za kimataifa
HII Hatari sasa, BWANA MICHUZI.NI HARUFUU YA RUSHWA TAYARI HAPO.NIMESAKATA KABUMBU HAPO MIAKA ILIOPITA KATIKA CLUB YA PUMA NA NIKE (SOYO LEAGUE) CHINI YA MUENDESHAJI MCHOPA. Huu uwanja una historia ndefu sana ktk mkoa na Taifa zima kwa ujumla.Magorofa wakajenge mtaa wa uhuru na Mbita au igogo mlimani.
ReplyDeleteNoma noma! Umenikumbusha mbali bro Michu. Hapo babu tulipiga boli sana enzi za kombe la yosso. Timu ya mchopa ndio ilikuwa tishio kila mwaka. Tukitoka skuli Nyanza tunachenji nguo tunaunganisha Nyamga, kama tulivyokuwa tukiuita uwanja huu enzi hizo.
ReplyDeleteNyamagana INA MAANA MAELFU-KWA-MAELFU,IKIMAANISHA JINSI MAELFU YA WATU WALIVOTEKEZWA KATIKA ENEO HILO NA MKOLONI(JERUMANI HUYU) NA BAADA YA HAPO TENA HISTORIA IKAJIRUDIA BAADA YA ENEO HILO KUTUMIWA KAMA MAHALI PA KUTAMBUA MIILI YA WATANZANIA WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MELI YA mv.bukoba.KAZI KWAKO MTANZANIA KAMA HUKO RADHI KUIFUTA HISTORIA HII AMBAYO INAITAJIKA KWA VIZAZI VIJAVYO
ReplyDeleteSIJUI NI KWANINI KIZAZI HIKI KINATAKA KUFILISI KABISA KIZAZI KIJACHO,TUNAMALIZA RASILIMALI ZOTE SASA HATA HISTORIA PIA TNATAKA KUIUA?!HAKIKA SIKU MOJA TUTAKUJA JIBU HATA KAMA TUKIWA HATUNA MIILI HII.
mtu wa mazoo(U.S)
uwanja huo unakumbukumbu nyingi sana hivyo itasikitisha sana ukibomolewa. Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kulinda vitu vyenye kumbukumbu
ReplyDeleteYAANI HAPO NASIKIA KI HARUFU CHA UFISADI TENA,YAANI BONGO IKO KAZI,HAYA WACHA TUONE MWISHO WAKE,HII NCHI INAHITAJI WEHU
ReplyDeleteKwa mpango huu basi nyanja ya michezo hususan soka katika nchi yetu tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu milele,kwani hata tukiagiza makocha kutoka mwezini sithani kama tutaweza kufanikiwa katika swala hili, cha muhimu ni kuboresha nyanja mbalimbali za michezo kama viwanja, vyuo vya michezo n.k , kama ni majengo ya biashara yamejazana nchi nzima, ni bora kuweka nguvu katika michezo ambayo ni faida kwa afya na pia ndo
ReplyDeleteinakusanya watu wa madaraja tofauti
yani maskini na matajiri na kuwapa furaha na kusahau uchungu wa maisha
na pia inatangaza nchi kwa uharaka zaidi
uwanja huo ubomolewe kwanza umechoka sana, pili uko mjini sana na hauzalishi kitu.its better wajenge mwingine waupe jina hilohilo kama ni kubaki na kumbukumbu.hii 21st century waungwana.
ReplyDeleteNgurubange
NDIO UWANJA UNA HISTORIA LAKINI HAUKIDHI MATAKWA YA WAKATI ULIOPO. KWANZA UMECHOKA SANA PILI UKO KATIKATI SANA YA MJI NA VILE VILE HAUNA MANUFAA YOYOTE KWA JAMII. KWA HIYO AMA UKARABATIWE AU UPISHE MAENDELEO.
ReplyDeleteHao wawekezaji wajenge kwanza uwanja mwingine ndio wanunue hapo.Fanya kama Dumila ukitaka ku invest sharti ushirikishe mzawa
ReplyDeleterushwa tupu hapo wakishavunja ndo utaskia ohhh......hatua kali zinachukuliwa kwa wahusika kumbe umbea mtupu
ReplyDeleteNilifikiri hili suala lilisha shughulikiwa na aliyekuwa waziri wa aridhi mh. John P. Maghufuli, ambapo alitoa amri yakutovunjwa uwanja huo muhimu. Watanzania lazima tuelewe sehemu kama hizi ni muhimu sana kwa burudani na maendeleo ya jamii kiujumla!
ReplyDeleteMdau wa Rock City
Jamani unatakiwa uujue uwanja wenyewe upo kwenye hali gani kabla ya kulalamika. Uwanja wenyewe ni kama umetelekezwa. Nitajaribu kuwatafutia picha ulivyo ilimuuone then muendelee au kustop kulalamika.Watumiaji wakuu wa uwanja wanatoka nje ya nyamagana, so kama vitajengwa viwanja vingine nje ya city centre itakuwa poa. Mdau MAK
ReplyDeleteMimi mdau wa hapa mwanza. naomba niseme kuwa watu wanasema tu uachwe kama ulivyo lakini hawajui hali ya uwanja huu kwa sasa.
ReplyDeleteImekuwa maficho ya vibaka na wavuta sigara kubwa. wauza ngono pia hawachezi mbali nyakati za usiku. na hata kukiwa na kitu kinafanyika hapo basi hakuna mtu anaetaka kwenda kwa sababu harufu ya haja ndogo imetapakaa kila kona na vinyesi kila sehemu. hauna uangalizi na kwenye vyoo (vilivyozeeka) masinki na mabomba yote yalishang'olewa na vibaka.
Kama wadau wanashauri usivunjwe basi ubinafsishwe kwa sababu serikali imeshindwa kuingia gharama za kuuendesha kama kulipa walinzi na watu wa usafi. ni hayo tu.
MAK DOGO UMEKUJA MWAKA JANA TU HAPA MWANZA UNGEULIZA WAZEE WA LONG KWANZA WAKUPE KHABARI NYEPESI NYEPESI ANGALAU KWANZAAAA.
ReplyDeleteTUNAJUA FIKA NINI KINAENDELEA WENGI HAWAAFIKI. UMETELEKEZWA ILI WAUFISIDISHE TU NA WAKUBALIWE KUWA HAUFAI WALIDIRIKI KUETA GREDER KIPINDI CHA NYUMA KUBOMOA BOMOA BAADHI YA SEHEMU MFANO MILANGO NA BAADHI YA SEHEMU. NA UNAPOSEMA WATUMIAJI NI WATU WA NJE UNAMAANISHA NINI MI NIJUAVYO WANATUMIA WATU WENGI HATA MAANDAMANO NA MAADHIMISHO MENGI YANAISHIA HAPO,
NA HAO WAHE... WANAPOSEMA ETI WAKIJA NA MAGARI YAO WATAPARK WAPI, KWANI SIKU ZOTE WANAPARK WAPI HATA LEO WAHOJI BUNGENI ETI WATAPAKI WAPI, HAPO NAHISI PANA MCHEZO UNACHEZWA NA VIONGOZI WA MANISPAA KWA UWANJA HUO, SASA WANAJARIBU KUTOA KASORO AMBAZO ZITAKUBALIKA ILI IONEKANE KWELI HAUFAI.KWA NINI WASIUKARABATI SIKU ZOTE HIZO JANJA YAO NA HUKU ACCOUNT ZINAENDELEA KUMWAGILIWA MAJI SIKU NYINGIIII.
UVUNJWE THATS IT.Kuna kumbukumbu gani zaidi ya mechi ya Simba na Yanga na Maafa yaMv.Bukoba.Uvunjwe upishe investments za muhimu hapo pia watu watapata ajira.
ReplyDeleteKwa michezo gani bongo!!!eti kudumisha.
Ngurubange
Nyie watu wa Mwanza vipi bwana? Mtabadilika lini? Vile vijumba vya babu zenu vingeendelea kuwepo hapo mjini leo mngeitwa jiji?Huwezi kuacha kitu cha hovyo kiwepo eti kisa history.Yani muache huo uozo hapo kisa eti Hussein Marsha alicheza hapo?Kama ni MV Bukoba mbona kuna mnara ulijengwa kwa ajili ya kumbukumbu hiyo au sio? Sehemu ya kutambua maiti nayo ni history? Nilidhani history nzuri zaidi ni ile ya sehemu meli ilipozama na maiti kuzikwa.
ReplyDeleteInawezekana hata mkiambiwa muwekewe reli mpya ya kisasa mtagoma na kutaka hii iwepo kisa hata wazee walitumia hii ya kizamani..
Nilikuwepo hapo last week na hamna kitu kinaendelea hapo zaidi ya mechi za mchangani ambapo vipo viwanja kibao vinaserve same purpose kama Nyamagana licha ya huo mtakaojengewa.Kama ufisadi, mzee wa visenti si ndo mjomba wenu nyie??
Siwakashifu ila badilikeni washkaji, Mwanza izidi kushine kwa structure mpya na kama mdau alivyosema,ajira ziatongezeka.