kamanda wa mkoa maalumu wa polisi kanda ya kinondoni afande jamal rwambow akiwa na mmoja wa ffu waliojehiwa katika vurugu na wanafunzi wa chuo kikuu cha udsm leo
baadhi ya wanafunzi 39 waliotiwa mbaroni kutokana na vurugu zilizotokea udsm leo wakiingizwa kwenye karandinga ili kupelekwa selo leo jioni.


jumla ya wanafunzi 39 leo jioni wametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea udsm ambapo inasemekana wanafunzi kwa mwaka wa kwanza na wa pili wamegoma kuingia madarasani kusoma ili kushinikiza utawala wa chuo hicho kusikiliza malalamiko yao
kwa mujibu wa afande jamal rwambow, ambaye ni kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi ya mkoa wa kinondoni, ffu wawili walijeruhiwa katika purukushani hizo ambapo wanafunzi walioingia madarasani walijikuta wakilazimishwa kutoka humo na wanafunzi waliokuwa kwenye mgomo kudai haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na kutokubali kuingiliwa na uongozi wa chuo kwenye siasa zao (wanafunzi) katika wakati huu ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kumbe na wao(FFU) wanaumia!!! safi sana... mana wamezidi hawa jamaa...wakiingia sehemu hawana mswalie mtume..ni kipigo kama wanapiga wanyama.

    ReplyDelete
  2. Hivi ni mara ngapi matatizo haya ya UDSM yatakwisha, Hivi hakuna njia sahihi ya kutatua haya matatizo mpaka kutokea fujo na mpaka FFU kuja kutuliza ghasia hizo.

    Hii inaonyesha ni jinsi gani Viongozi wetu sio wabunifu wakutatua matatizo ya Watanzania sio UDSM tu ni matatizo ya Viongozi wetu karibu Tanzania.Sina maana hakuna Viongozi wabunifu wapo lakini Serikali yetu nadhani wamekuwa vipofu kuyachukua mawazo yao na hatima yake ni machafuku ya mara kwa mara.

    Hii sio njia nzuri ya kutatua matatizo kwa kupeleka FFU bali ni uchafuzi wa Amani.
    Kama watu wanaandamana waache waandamane na wapeni ulinzi mpaka wafikishe dukuduku lao na sio kuwapiga au kuwatawanya.Majuzi tu tumeona machafuko ya Kenya na mado tumesahau jinsi gani ya kutunza Amani.

    Amani haizuiwi kwa Mtu wa Bunduki au Virungu,kwani namba ya polisi wote na wanajeshi wote Tanzania haifiki hata Laki moja sasa kama asilimia 30 ya Watanzania wakiandamana na kufanya fujo je hao askari wataweza kuwazuia kweli au ndio itakuwa yale ya Kenya kuua raia wote na kubakia na Viongozi wachache ambao hawataki kuzikiliza Wananchi.

    Nchi yangu Tanzania,ni wapi tunakwenda na wapi tunaelekea..............

    POPO

    ReplyDelete
  3. Michuzi fanya mpango upate majina ya hao wanafunzi walioshikiliwa. Tuna ndugu zetu hapo na tunajaribu kuwapigia hawapatikani. Tusaidie kwa hilo Michu please!!!! @Rose

    ReplyDelete
  4. Tatizo hatujui namna ya kugoma kwa amani. FFU wakija nyie mnajikusanya mnaendelea kunyosa mabango yenu na kuimba kwa sauti msitembee tena, ujumbe utafika na utapokelewa sasa mnaenda kama mpo vitani wacha mkamatwe sawasawa. pole FFU nasikia walikupiga chupa. aliyekupiga hana akili!! Atajutia maishani mwake

    ReplyDelete
  5. I love vijana wa bongo, kwenye vitu kama hivyo wanawaacha dada zao mbali, jana kwenye tv naona wanaume tu wanawake hampo safi kumbe mnawajali mama zenu. tukiisha hakuna uzazi

    ReplyDelete
  6. Kiini cha matatizo yote haya ya wanafunzi ni udhaifu wa kiungozi alionao Profesa Rwekaza Mukandala,Vice Chancellor wa Chuo Kikuu cha DSM.Mimi nashauri mtu huyu abadilishwe na Mwingine bora zaidi ateuliwe kushika nafasi yake.Katika vyuo vikuu kama hivi tuanze kujenga mazoea ya kuwashirikisha wahadhiri wote cha chuo kikuu katika kupendekeza nani miongoni mwao atafaa kuwa Makamu Mkuu au Mkuu wa chuo na kisha washiriki katika kupiga kura ya kumchagua.Badala ya utaratibu wa sasa Mkuu huyo kuteuliwa na mamlaka nyingine nje ya chuo.Matatizo yote haya yatapungua kama siyo kumalizika.Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kauli za Rwekaza Mukandala kila lilipo zuka tatizo la wanafunzi ana udhaifu mkubwa katika kusuluhisha migogoro.Kwa kifupi hajui namna ya kuzungumza na wanafunzi without prejudicial biases.Amesahau kwamba ni wanafunzi haohao waliomfanya apate ajira pale chuo kikuu.Leo asubuhi nimemsikia akitamka kwamba kuna kundi la wanafunzi wapatao karibu 300 amabo wapo pale chuoni lakini hawajadahiliwa kwasababu hawajapata ufadhili(?),ndiyo amabao wamekuwa chanzo cha migogoro yote hiyo na kuwakosesha wanafunzi wenzao utulivu wa masomo.Yeye Rwekaza Mukandala alikuwa akitarajia nini kutoka kwa wanafunzi hao ambao wametimiza masharti yote lakini wamekuwa wakinyanyasika kwa kucheleweshwa ufadhili hapo chuoni kama vile wao siyo sawa na wenzao waliokwisha pata ufadhili.Huduma mbalimbali za wanafunzi chuoni hapo ni mbovu haziridhishi.Na hakuna mpango wowote wa wazi uliobainishwa kwa wanafunzi ili waelewe ni jitihada gani zinazofanywa na uongozi wa chuo katika kukabiliana na matatizo yao.Sasa huu ni udhaifu katika uongozi.Ukiona katika chuo chochote kile migogoro baina ya wanafunzi na wahadhiri au wanafunzi basi ujue kwamba uongozi uliopo haufai na umeshindwa kazi.Pengine wahadhiri wenzake Rwekaza wanashindwa kuyaweka mabmo haya wazi hadharani kwa sababu uteuzi wa Rwekaza kuwa Mkuu wa Chuo au Makamu Mkuu ulifanywa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.Rwekaza alipokuwa akiiongoza taasisi moja ya utafiti pale chuo kikuu alikuwa akiipigia sana debe CCM katika kutoa kura za maoni nyakati za pilikapilika za uchaguzi mkuu zilizo ipendelea zaidi CCM ionekane ndiyo inayo kubalika zaidi kwa watanzania kwa ujumla.Maoni ambayo yalikuwa yakizua msuguano mkubwa wa kimawazo katika jamii baina ya kambi mbili za upinzani wa kisiasa.ITOSHE TU KWA KUSEMA KWAMBA WAKATI SASA UMEFIKA KWA RWEKAZA MUKANDALA KUONDOLEWA KATIKA UONGOZI WA CHUO NA NAFASI HIYO APEWE MHADHIRI MWANDAMIZI MWINGINE.wapo wengi pale chuo kikuu.Na ikiwezekana nafasi hiyo apewe mwanamke safari hii tuone mambo yatakwendaje,fujo zaidi au utulivu na ustawi zaidi kwa wanafunzi na jumuia nzima ya chuo kikuu.Akivurunda na yeye abadilishwe mambo yaendelee mbele.Tumechoka na migogoro ya kila siku pale chuoni.Rais Kikwete achukue hatua za haraka kabla mambo hayaja haribika zaidi pale chuoni na kusambaa katika vyou vingine nchini kote.

    ReplyDelete
  7. Tatizo in kwamba wasomi wetu ni wapambe wa wanasiasa.Profesa Mkandala ni kiongozi wa kinadharia na si vitendo.Ndiyo maana anatumia mabavu na vitisho katika kuongoza chuo.Nashauri asome saikolojia kwani itamsaidia kulea vijana.Nasikia ameikimbia nyumba aliyokuwa akiisha chuoni.Bado kidogo atakimbia ofisi!

    ReplyDelete
  8. Kaka Misupu
    Niliposikia kuwa Proff Mkandala, bingwa wa masuala ya Democrasia na utwala shirikishi amekuwa makamu mkuu wa chuo nilifurahi kwani nilitegemea wanachuo wangepata nafasi ya kushirikishwa na kusikilizwa....kumbe hamna lolote, jamaa na maandishi na utafiti wake wooote anaishia kuwachanganya zaidi wanafunzi.....kumbe yooote ni upuuzi mtup......kuna tatizo gani wakijichagulia viongozi wao?Je huu ni mfano gani tunaoweka mbele ya wasomi wetu na viongozi wa taifa la kesho?

    Nyaningedere

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli hao wanafunzi wa chuo kikuu sio watoto wadogo, inahitajika hekima ili waweze kutatuliwa matatizo yao. mambo wanayoyahitaji ni ya muhimu sana, Jambo moja moja ambalo nimelisikia kutoka kwa wanafunzi hao ni kuhusu uchaguzi wa chuo ambao unawahusu wanafunzu tu. taarifa zilizopo ni kwamba mwanafunzi wanyemuhitaji ni kuwa rahisi wao uongozi wa chuo haumtaki, hivyo wamemuwekea mizengwe hadi kumsimamisha kwa madai kwamba kuwepo kwake hapo chuoni sio halali. huyo mwanafunzi ni raia wa Uganda na ni chaguo la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Profesa Mkandala anamtaka mtu wa CCM awe rais, sasa huo si uccm ndani ya chuo? mkandala ni kada wa CCm, asipoacha ukada wake migomo haitaisha Hapo chuoni, From Michael Laiser - Dar

    ReplyDelete
  10. Kama walivyosema mtoa maoni hapo juu kwamba Vice Chancellor Rwekaza Mukandara anachoche kwa namna fulani migogoro hapo chuoni kweli kabisa. Napenda kusema kwamba hata Chancellor Fulgence Kazaura pia ni sehemu ya tatizo ya matatizo ya UDSM.
    Naomba niulize swali au kuwakumbusha wanachuo wenzangu, je tangu Chacellor Kazaura ateuliwe kuwa Chancellor wa UDSM amekutana mara ngapi na(wanajumuiya ya UDSM) wahadhiri, watafiti, wafanyakazi, na wanafunzi?
    Je Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Mheshimiwa Nimrod Mkono amewahi kukutana na wanajumuiya ya chuo kikuu cha Dar es Salaam? Au ana namna yoyote ambayo bodi yake inaweza kuyapokea maoni ya wanajumuiya ya UDSM juu ya masuala ya mikopo?
    Kusema ukweli uhusiano na imani ya wanajumuiya ya UDSM kwa Chancellor Fulgence Kazaura, Vice Chancellor Rwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo Mheshimiwa Nimrod Mkono ni ndogo sana au hamna kabisa.

    Mwanajumuiya ya UDSM (Mtafiti).

    PS/ Hapo chini ni maoni ya Mhariri wa gazeti la Nipashe, 17.09.2006


    Migomo vyuo vikuu mpaka lini?

    2006-09-17 08:48:11
    Na Mhariri

    Vyombo vya habari, jana viliripoti tukio la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, kuungana na wale wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu wa Majengo (UCLAS), kugoma kuingia madarasani na kuzuia magari barabarani ili kuishinikiza serikali kuwapa mikopo ya pesa ambayo itawawezesha kuendesha maisha yao chuoni.

    Huu ni mfululizo wa matukio ya mara kwa mara ya wanafunzi wa vyuo vyetu vikuu kuandamana kama njia ya kudai haki ambazo wanaamini serikali inazembea ama haitaki kuwapa kwa makusudi.

    Migomo, licha ya kuwapotezea wanafunzi muda wa kusoma, imekuwa pia ikiandamana na tafrani mbalimbali ambazo zinahatarisha maisha yao, maisha ya watu wengine na mali zao.

    Kwa mfano, mgomo wa juzi ulisababisha kero kwa watumiaji wengine wa barabara inayopitia katika Chuo Kikuu na kile Kishiriki (UCLAS) baada ya wanafunzi kuziba barabara. Mgomo huo pia ulisababisha FFU kuwavamia wanafunzi na kuwatawanya. Bila shaka kuna walioumia kwa kukimbia.

    Kuna wakati ambapo migomo ya wanafunzi wetu wa vyuo vikuu huwa inaacha maswali mengi kwani unakuta kwamba katika kile wanachoomba, tayari kinashughulikiwa ama kingeweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

    Lakini katika mgomo wa juzi, unaweza kuona kwamba wanafunzi walikuwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa ya uvumilivu. Kuna msemo kwamba mtu mwenye njaaa, hana uvumilivu, aibu wala soni.

    Madai ya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanatokea mikoani ni kwamba kwa takriban wiki nne toka chuo kifunguliwe kwa ajili ya masomo ya mhula mwingine, hawajapewa mikopo ambayo ndio inawasaidia kujikimu wakiwa chuoni hapo.

    Kwa msingi huo, wanafunzi hao ambao idadi yao ni zaidi ya 6,000, wamekuwa wakiishi kwa shida, ikiwemo kubahatisha kupata chakula, huku wale wanaokaa katika hosteli ya Mabibo wakilazimika kutembea kwa miguu hadi chuoni kwa kukosa nauli ya kupandia daladala.

    Kuna maelezo yametolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo, Nimrod Mkono, kwamba matatizo ya sasa yalisababishwa na mchakato mzima wa kuchambua fomu za waombaji ili kuona kama wametekeleza masharti na hasa kwa vile zingine hazikufika katika bodi kwa wakati.

    Mkono alisema kwamba tatizo jingine linatokana na maagizo ya serikakali, baada ya kuamua kuwapa ufadhili wanafunzi wote wanaosomea ualimu.

    Pamoja na maelezo hayo ya Bodi, tunadhani kwamba kuna tatizo katika utendaji wao. Tarehe za vyuo kufungwa na kufunguliwa zinajulikana.

    Inakuwaje uwaweke wanafunzi bila nauli wala pesa ya kujinunulia chakula kwa wiki nne au zaidi eti kwa vile bado unachambua fomu? Watakula nini hawa?

    Kama kuna agizo jipya la serikali kuhusu kuwalipia wanafunzi wa Ualimu, kwa nini Bodi isishughulikie kwanza tatizo la wanafunzi ambao tayari walishaanza masomo kwa mtindo wa kukopeshwa na tayari kalenda inaonyesha kwamba wako chuoni, halafu ndipo bodi ishughulikie jambo jipya?

    Je, katika hali ya kutokopeshwa pesa ya kujikimu, tunawaweka wapi mabinti zetu wanaosoma katika vyuo hivi. Haiwezi kuwa sababu ya kujiingiza katika vitendo vya kuuza miili yao ili wapate pesa ya kubabaishia mlo?

    Vyuo vyetu vikuu vimekuwa na matatizo mengi, yakiwemo ya uhaba wa vitanda, usafiri wa wanafunzi na hata waalimu ambao wamekuwa wakikimbilia kwenye fani nyingine zenye mishahara minono.

    Tunadhani kwamba huu ni wakati wa serikali yetu kukuna kichwa kwa ajili ya kuboresha zaidi elimu kwa kujenga mazingira mazuri zaidi kwa wanafunzi badala ya kufanya mambo ambayo yanaathiri taaluma kama hili la kuchelewesha mkopo kwa wiki nne.

    Tunadhani kwamba ni wakati mwafaka sasa wa serikali yetu kushughulikia matatizo kwa wakati na kuacha kusubiri kushughulikia mambo kwa shinikizo la migomo.

    * SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  11. huyu profesa mkandala yupo kama muhidin issa michuzi ..ni makada wa ccm

    ReplyDelete
  12. HAYO NDIYO MATATIZO YA KUZIDI ASILIMIA 13.
    KAMA WANGEKUWA ASILIMIA 13 KAMA TZUK DIASPORA, YOTE YASINGETOKEA. LAKINI UKITAKA ZAIDI YA ASILIMIA 13UTAKIONA KILIMCHOTOA KANGA MANYOA, AU UTAJUA KUWA KITUNGUU NACHO PIA NI MBOGA!

    ReplyDelete
  13. Sehemu kubwa ya matatizo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya kifedha, Posho na Chuo kuwa kama lending instution. Hii inatokana na posho za wanafunzi kupitia chuo au chuo kuwa wasimamizi wa hizo fedha. Unajua ukiritimba wa bongo ni baishara ya wachache.
    Cha muhimu ni kwa wahadhiri kubaki wahadhiri na chuo kutojihusisha na masuala ya posho za wanafunzi. Jambo hili ni kuundwa kwa education loan board an hoa ndio wawe na dhamana yote. Sio kama ilivyo sasa kuna bodi lakini posho za wanafunzi zinakaliwa na chuo.
    Nimesoma bongo chuo na migomo kila mwaka.
    Cha maana wahadhiri acheni njaa na wanafunzi wapewwe posho zao in timely manner kuliko kufanya migogoro mingi ya vyuo vya juu kuonekana kama ni ya kisiasa.

    ReplyDelete
  14. Chuo Kikuu sasa siyo chuo kikuu ni 'CHOO KIKUU" mijutu inavyuta bangi chuoni... poa waacheeni tuuu wapelekwe rumate... angalia sisi tunalipa visenti (kodi ) ili wao wasome wao hawataki wanafanya vurugu... mimi nauliza ,, vurugu za awali zilisababisha mwanafunzi mmoja kufa, munategemea sheria isitumike kuwa fikisha mahakamani watuhumiwa? sasa kwa nini munataka warudishwe chuoni wakati wanatuhumiwa kuua? acheni ufala wana chuo! someni

    ReplyDelete
  15. kaka michuzi u know what watu wa mtaani wanahisi sisi wadau wa UDSM ni wakorofi tunagoma bila misingi yoyote ile, lakini kabla mtu hujaongea wala kutoa comment yako yoyote ile kaa chini tafakari fikiria na changanua mambo jiulize leo hii mtu akurupuke tu nakuanza kugoma!! Is not easy kama wanavyojinadi kwenye vyombo vya habari nawashauri mnaotoa maono kaeni chini fikirieni kwa makini kisha njooni na maoni yenu na mtazamo positive without having locked with any itikadi ya chama chochote cha siasa especially CCM. Kwa taarifa fupi kiini cha mgomo ni UCHAGUZI tu!!! hakuna kingine wadau suala la bangi sijui kubaka na mengineyo ni mawazo finyu tu ya huyu kada wa CCM anayekiongoza chuo kwani hata mkimuona akiongea na vyombo vya habari ni mtu asiyejiamini anakurupuka tu!! Na kuamka na new idea kuhusu mgomo, hili suala was very easy to be solved but the pbm is limechanganyikana na suala la siasa ndani yake na kufangamana na ugombaniaji wa uongozi baina ya CCM na CHADEMa chuoni hapa, kwani uongo kila mtu analijua hili, ndiyo maana rwekaza anangangania sie wahuni unadhani kwa nn De Slaa alikataliwa kuchangia hoja hii bungeni ni kwa sababu ya uchama ndani yake Yaaaaap fuatilieni mambo kwa makini msichonge tu wadau ds is reality!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...