Mheshimiwa mkuu wa Wilaya,
Pole na hongera kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya ya kutujuvya kila linalotokea nyumbani na ulimwenguni kwa ujumla.Naomba kuandika mistari michache juu ya mada uliyoitundika leo yenye kichwa "Asilimia 13".
Nakubaliana na wewe kwamba Watanzania wengi hawapendi kujiandikisha katika balozi zao au jumuiya zao za kitanzania, au za Kizanzibari wawapo ughaibuni. Hilo nimeliona mm pia kwa mda mchache niliopata kutembelea nchi chache za hapa Ulaya.
Sababu kubwa nizionazo mimi ni mbili, mojawapo ni ya kiufundi na nyingine ya kibinafsi.Sababu ya kiufundi ni kuwa wengi wa Watanzania huingia ughaibuni kwa njia wanazozijua wenyewe (funika kombe mwanaharamu apite). Kwa maana hiyo, wengi huhisi kwamba kujipeleka balozini ni kujisogeza minazi mirefu kitu ambacho hawako tayari kujaribu, hasa ukizingatia ukweli kwamba hata gharama za nauli walizozitumia hazijalipa bado.
Sambamba na hilo ni kuwa wengi wa watanzania huja ughaibuni kwa sababu za kiuchumi. Hivyo mtu huona bora kushughulikia lile lililomleta na kupata mradi wake, kuliko kujitia joto la roho ambalo haoni faida za haraka, aghalabu huishia na malalamiko ya kuliwa pesa.
Zaidi ya hayo ni kuwa Watanzania hatuna utamaduni wa kupendana na kusaidiana tuwapo nyumbani sembuse tuwapo ughaibuni, hili linaweza kupingwa na wadau, lakini ni uhalisia.Tukiachilia mbali michango ya mtu kwa mtu yanapotokezea ya lazima kama kuumwa na kufiwa ambayo alhamdulillah imesaidia sana, balozi zetu hazina wasaa wa kusaidia wananchi wao hasa kama huna mwega balozini hapo, yaani kama zilivyo ofisi za nyumbani. Kuna tafauti kubwa kati ya balozi zetu na za wenzetu.
Wenzetu balozi zao hufanya kila wawezalo kuwasaidia wananchi wao ilhali zetu sisi haziko hivyo. Mathalan, binafsi yangu nimetuma maombi kadhaa ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika balozi takriban kumi za hapa Ulaya, Asia na Amerika. nikiwa najua kwamba kwenye kuomba kuna kukubaliwa na kukataliwa lakini pia kuna kujibiwa kwa lolote kati ya mawili hayo, mimi sijalipata hata moja, kuanzia November mwaka jana hadi sasa bado nasubiri jawabu, ambayo kama itakuja, natarajia sana kuwa hasi.
Hii kama si dharau kwa wananchi ni nini? Vipi utamtarajia Mtanzania kujipendekeza asipopendwa? Mwanafunzi mwenzangu Mjerumani, amepeleka ombi moja katika moja ya balozi zao, na ndani ya wiki akapata jawabu chanya.
Hakuna ugonjwa usio na dawa. Labda mambo mawili makubwa yafanyike ili kuweza kuitibu ndwele hii. Kwanza ni kwa wananchi kuelimishwa umuhimu wa kujiandikisha katika balozi zetu na kutolewa khofu juu ya khatma ya maisha yao, hata kwa wale walio Wasonjo, na hilo limaanishwe lisisemwe tu.
Labda tunaweza kutumia njia ya makongamano kama lile la diaspora lililopita London. Hilo ni moja. Lakini la pili ni balozi zetu kubadilika na kuwa marafiki na wasaidizi kwa raia zao. Hili linaweza kuchukua mda, lakini kama watafanya angalau yale yaliyoandikwa kwenye mikataba yao ya kazi tu basi tunaweza kupiga hatua angalau kufika asilimia 26.
Hayo ni mawazo yangu binafsi yatokanayo na uzoefu wangu binafsi. Natumai sijachafua hali ya hewa, na natumai wadau watakuwa na mawazo mengine, kama yangu au tafauti na yangu.
Tafadhali tujuvyane!
Mdau HaMad
Scandinavia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Enhee nkweli! Bahamad kuntongowa ndivyo, hweacha nukta! Manenoyo swadakta, kama n'dawa basi mujarab!
    Enhee kama m'pele impata nkunaji!

    Ha ntu kunkuja ulayangwa kwa mitikas, hata hujachunguwa vyema, ndo kwanza wataka chuunza mijingwa, wende ubalozini?!Nako kujaa mahasidi viwembe,ukazinge rudishwa?! Ama leo Bahamad kunsema, loh ha bankubwa weye wekuwa waa?

    Ngoja ni sign off, nisije bonyeza kizenji tena!

    ReplyDelete
  2. BWANA INGENERAL TULIOPO ABROAD TUNAONA KAMA MAMBO HAYO NI KUPOTEZA MUDA TU KWANI HAKUNA FAIDA YOYOTE KWENDA KUJIANDIKISHA HUKO EMBASSY,KWA MFANO MIMI NIPO CALIFORNIA NA UBALOZI UPO WASHINGTON,ARE YOU TELLING ME THAT I SHOULD GO TO REGISTER OVER THERE,HELL NOT SINA MUDA HUO,JAMAA WENYEWE WA EMBASSY MIYEYUSHO,WAOGA NA HATA KAMA UNA SHIDA THEY WILL NOT HELP YOU,BORA NITAFUTE MAKARATASI NIWE RAIA WA US KULIKO HILO LA KUJIANDIKISHA.KWANZA UKISHAFIKA ABROAD HUO URAI WA TZ UNAUONA HAUFAI TENA NA HAUNA MAANA TENA,UKISHAKUWA US CITIZEN UNAENDA MANCHI KIBAO BILA KUWA NA VISA KWA HIYO MIMI BINAFSI SINA MPANGO NA HUO UBOLOZI WA TZ NATAKA KUWA US CITIZEN AND THATS IT!!!!!!

    ReplyDelete
  3. BA Hamad, hujui unachoongea zaidi ya kutapa tapa, on one said uko up for the idea, na wakati huo huo hauko na idea yako mwenyewe.

    Inabidi urudi darasani, kujifunza zaidi hizo hicho unachokisoma. Unachemsha, hakuna chochote cha msingi unchaoongea zaidi ya contradicting yourself.

    Sikiliza, bwamdogo kama ulaya umekuja juzi, unaonekana una mwaka tu kuishi huku kwa maongezi yako hayo yasiyo ya msingi, inabidi urudi kwenu unguja. NAULI HAZIJALIPA??Are you for real, au una shida sana kwenu kwa hiyo wafikiria kupata nauli yako uliyokwendea huko ? Hapa watu wote wanaongea humu, wanazidi zaidi ya miaka 3 kwenda juu, sasa kama wewe unafikiria maswala ya nauli, fikira zako ziko chini kabisa.

    ReplyDelete
  4. Ba Hamad, si wasonjo tu waliooko huku ulayaa, kuna watu wa pwani dar, kuna watu wa bara Musoma, Mwanza, na wengineyo kama nkule kwennu kengeja, wantapakaa hadi dar.

    ReplyDelete
  5. Mmmh! Kazi kwelikweli!! Poleni kumbe wanawasambu (wanawanyali) (wanawasusa) hivyo kweli mabalozi sio wazuri. Lakini kuna kitabia mtu akifanya kazi ubalozi anajiona kama vile ni msaidizi wa rais hata kama ni karani tu wakawaida wanapenda kunyanyua pua sana. Poleni jamani. Mkitaka kuwaweza na nyie anzisheni umoja wa walikwenda ughaibuni kwa "funika kombe mwanaharamu apite" ehehe kaka umeongea asante kwa mada ila kuwa watanzania hatupendani sijui... labda kwenu (mkoani)sisi huwa tukikutana kwetu wote ndugu tukirudi bongo kila mtu kwake

    ReplyDelete
  6. DUUUU! NINAUNGANA NA WADAO WALIOTANGULIZA MAONI YAO HAPO JUU KWAMBA BALOZI HAZINA MSAADA WOWOTE NA RAIA ZAO. UKIWA NA SHIDA YA AINA YOYOTE ILE NDO KWANZA ITAKUWA TOPIC OF THE DAY (GOSSIP!) UTAYEYUSHWA NA HATIMAYE KUKATA TAMAA. WENZETU WA MATAIFA MENGINE R' SO PROUD OF THEIR EMBASSY.....!, AAAAH NGOJA NISISEME MENGI, THEREFORE... KWA MPANGO HUO WALA SIONI SABABU YA KUJIANDIKISHA KWA KWELI.... JAPO MIMI BINAFSI NILIJIANDIKISHA NIKIWA NAJUA UMUHIMU WAKE (HEWA FOR TZ'S EMBASSY ABROAD!)

    ReplyDelete
  7. Kamichu naomba kuchangia kidogo tuu,Mi mwanafunzi huku Norway,sasa kipi cha kunipeleka sweden kujiandisha ubalozini,kwa nini wao wasitufwate maana most of the times wanakula happy tu ubalozini shughuli ya maana ipi zaidi ya umbea.
    Then kuhusu hivi vyama vya kitanzania,sioni umuhimu wake zaidi ya kutafutana undani na majungu ambayo hayana nyuma wala mbele na uzinzi tuuu.Mi sioni mana ya kujiregister ubaloni au kwenye chama cha wa TZ.mambo yangu kivyanguvyangu.

    ReplyDelete
  8. Watanzania hawana matatizo yeyote na wanajua umuhimu wa kujiandikisha na wengine wamekwishajiandikisha vilevile.

    Balo ndizo ambazo hazijui umuhimu huo.
    hivyo basi unaposema kuwa tuwaelimisha watanzania waliopo ughaibuni waone umuhimu wa kujiandikisha unakosea. Wanaopaswa kuelimishwa hapa ni Balozi zetu. Hili suala kwa balozi kuliongea ni kuonesha ni jinsi gani alivyo mzembe na hajui alifanyalo ukichukulia kuwa hivi karibuni tu watu walikwenda katika balozi zetu kubadilisha pasi zao. Hivyo ndo kusema kuwa wanazo taarifa zote za watanzania walokuwa ughaibuni katika kipindi hicho.

    Hii inamaanisha kuwa ni jinsi gani mabalozi wetu walivyo wazembe na wasojua kazi yao na zaidi wapo kwa kukandamiza watanzania na kuwalaumu tu kwa matatizo wasiyokuwa nayo.

    Hii pekee maana yake ni kuwa hatutakiwi huko ubalozini.

    ReplyDelete
  9. NIKIPIGA SIMU POLISI AU BANK HAPA NASIKILIZWA HARAKA, KWA MAKINI NA HESHIMA. NIKIPIGA UBALOZINI SIPOKELEWI, NA HATA NIKIPOKELEWA WAKO MIKUTANONI, NA NYODO NYINGI, WHY SHOULD I CARE? MIMI MBONGO LAKINI WABONGO HATUFAI.

    ReplyDelete
  10. MAKOFI NA VIGELEGELE KWA NGWENGWE

    ReplyDelete
  11. ahhha hivi kunakujiandisha ubarozini?nilikuwa sijui maana hao watu wa ubarozi wenyewe wazushi tu iweje mie naingia usa dc data zangu zote wanazo,sasa huko kujiandikisha kwa nini hao wafanyakazi wa ubarozi wanajidai mungu mtu hapa tunachapa kazi bwana mambo mengine mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  12. hiyo ni kweli hasa sisi wa huku japan sasa kuna matatizo makubwa sana na ubalozi uhusiano ni mbaya kabisa hasa huyu balozi wetu mbinafsi kupita kiasi anajali baishara zake za vinyago na maslahi yake binafsi watu wamegawanyika kwa kiasi kikubwa mno hana msaada hata kidogo ana kundi lake dogo analotumia kumjenga na kumsifia pale anapokuja kiongozi wa nchi ila sasa kuna mgawanyiko wa hali ya juu asilimia 90 ya watanzania wamejitoa na kuunda umoja wao binafsi kweli japan kwa watanzania sasa yamoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...