baada ya mwenge kuondoka ilifanyika hafla ya kuwapongeza wakimbiza mwenge ikiwa ni pamoja na profesa anna tibaijuka, sha baraka, lady jd na mh. muhammad seif khatib
baada ya mwenge kuondoka ilifanyika hafla ya kuwapongeza wakimbiza mwenge ikiwa ni pamoja na profesa anna tibaijuka, sha baraka, lady jd na mh. muhammad seif khatib

Hey dada Asha, mbona umechukia ni kitu gani kimekusibu? au unatatizo gani na huyo dada Judith Wambura!!! aisee atakuitia afande Mwita Malanya!!hahahah
ReplyDeleteMwache ajifunze kuongea mbele ya wanaume/watu...au umechukia kaptula yake inayoonyesha migagi yake eti ni miguu na unataka umshauri awe anavaa kama wewe!! ebo!.
Sorry!!! hahahaha
JD mbona hizo adabu msoma hazikuwepo!!! naona unampigia magoti Mziray hapo juu....au kakupa adhabu, ushilie hilo tochi ukiwa umepiga magoti?
ReplyDeleteKunarafiki yangu ananichekesha..eti hapo mlikuwa mumesimama...nikasema, kama kweli mlikuwa mmesimama na Mziray...basi umejaliwa urefu wa kwenda chini...lakini mimi naamini umepiga magoti kwa mbwembwe...si unajua wasanii kilasiku hamchoki na urembo wa sanaa!!
Lakini kama ni kimo chako hicho...nooma nikishenzi.
Michuzi hiyo picha ya supercoach Mziray na binti machozi JD imeniacha hoi kabisa, naomba ufafanuzi, je:
ReplyDelete1. Mziray kasimama juu ya stuli au
2. JD kasimama kwenye kashimo au
3. JD ni mfupi sana basi (namfahamu Mziray).
Suala la umbo,kimo, haiba na kiwango cha akili ni zawadi kutoka kwa manani ambaye hakuna mtu anayeingia naye mkataba ili amuumbwe vipi. Ni kitu cha kustajabisha kumkebehi mtu kwa kimo chake kama vile yeye ndiye alitaka aumbwe hivyo! any way hizo ni dalili za kufilisika au kuchakaa kwa ubongo. Tutoe michango lakini siyo vema kudhalilishana.
ReplyDeleteMdau Kimanzichana
We need to hear about the tanzanian diaspora in UK. Tahts all forget about this other petty shit
ReplyDeleteJamani nimesikitishwa sana nilitegemea kuona mwenge unakimbizwa na wacheza mfano wanariadha kama nchi zingine zilivyofanywa sasa hawa watu wanahusiana nini na Olypic torch?TOC mko wapi?
ReplyDeleteMwanadamu hujafa hujaumbika, kila siku uamkayo shukuru Mungu uko hai na uko na viungo kamili. Mungu si Athumani wa kumchezea na kumtania kwa maumbile ya watu, aweza kukupa kibiongo na urefu unaoringia ukapotea, au ukapata maradhi, na hata ajali. Mshukuru Mungu ulivyo na usikashifu maumbile ya wengine.
ReplyDelete2. Kuhusu mwenge wa Olimpiki anayetaka ukimbizwe na watu wa kamati ya olimpiki tu Tanzania, kumbuka hata hao kamati ya olimpiki inahitaji sapoti ya watu wengine kufikia malengo yake, na kidole kimoja hakivunji chawa.
Mwisho mwenzetu unayesema unataka uwekewe mambo ya Tanzania diaspora in UK na hutaki hizi petty shit, kumbuka wanaweb site yao hao wa UK kwanini huendi uko ukatuachia sie tunaotaka kujua nyumbani kunaendelea nini. Au wapigie simu nafikiri contact zao zipo huko. Acheni tabia za kudharau vya kwenu, kwani hiyo Tanzania diaspora ya UK ina mambo gani makubwa ya kustua au watu kuacha kusoma na kuangalia mambo mengine?
Hao wanaokimbiza mwenge waone AIBU. Wenzetu nchi zote duniani mwenge unakimbizwa na wanamichezo kuliko korokoro sasa waimbaji, mameneja wa muziki n.k wapi na wapi?? Hii ilikuwa nafasi ya pekee kuwapa changamoto vijana wetu chipukizi kwenye fani ya michezo.
ReplyDeleteSafi sana anony wa April 14, 11:26pm, yaani umeongea maneno ya busara sana mi nakuunga mkono, waambie wapuuzi hao wanaoandika kuhusu maumbile ya watu, mkandye mtu kwa tabia yake chafu na si kwa maumbile yake pungufu, Waunde au waumbe watu wao warefu tuwaone, Bata Bukini wakubwa/Kuku wa kienyeji hao. Baelezee.
ReplyDeleteZeddy
Reading
Wabongo nao kujifanya mna hekima...mpaka mnatisha.
ReplyDeleteHao waliocomment hapo juu, wanatania tu!! wala hawana nia mbaya na waliyoyasema na kama ni urefu Mziray tunamjua na JD tunamjua na JD siyo kama anaufupi wa ajabu...ila ni picha tu...hao wote hapo juu wanatania tu.
Huwezi kujua!! tanzania nchi ya watani bwana..pengine aliye comment mara ya kwanza na ya pili anatoka Kigoma kwa hiyo anamtania mtani wake wa msoma..!! mimi binafsi sioni tusi hapo na hata JD atakuwa anacheka tu na sidhani kuwa atakuwa na sababu ya kujifanya anabusara za kuanza kufikilia katika mrengo hasi...
Pole sana kwa kujifanya unajari sana na naomba hizo msg zichukuliwe kama utani.
Kama kweli busara zako zingekuwa na maana basi wenye katuni wangefungiwa.
I believe, they didn't write as well as they would have, obviously if they worded things in a way that made people offended, they deeply regret that and i join them to help them by saying that even on my side i didn't take it in negative way as the above anony of 8.43 and 11.26.
HUKU NI KUTOELEWA AU KUPEANA UMAARUFU PASIPO HUSIKA? UWANJANI WALIKUWEPO WATU MAARUFU SANA KWENYE MICHEZO AMBAO DUNIA NZIMA INGEPENDA KUWASIKIA NA SI KUNDI HILO LINALOPEWA UJIKO.AKINA BAYI, KEINO, NYAMBUI NA WENGINEO WANAMICHEZO NDIO WALIOSTAHILI KUANDIKWA NA SI HAWA.
ReplyDeleteNinamasikitiko kuona bado kidogo tuko nyuma bado.Olympic torch ilibidi mwenge huo ukimbizwe na wanamichezo kama vile wanariadha,vilema yaani wana michezo.sasa hawa watu wa mabendi waimbaji,mameneja wanahusiana nini na hiki mwenge jamani hebu tuamke na kuacha kupeana sifa kwa watu wasiohusika.Nilitegemea kuona Mwinga Mwanjala,Juma Ikangaa,Bayi ,Morris okinda au Peter Mwita ,ma-footballer,basketball,Boxer sasa JD na hao wengineo wa music sielewi.Naomba tuende na wakati na tufanye inavyopaswa.
ReplyDeleteWewe anony wa 4.46 hakika unawajua watu wa Bongo. Watu wa Bongo ni watu wa raha katikati ya umasikini. Wanapenda utani sana. Bahati mbaya watu wengi hawaelewi. Namsifu sana Chibiriti yeye anawajua sana Wabongo na wala haogopi kutoa mawazo yake. Ukiogopa maneno na jeuri za kibongo hutaweza kwa mfano kuendesha gari DSM. Dereva mwenzako anakutukana kqyzyqq..yo halafu dakika chache baadaye anakuaomba nafasi kirafiki umpishe njia. Nawe unamrushia tusi unamwambia we ms...qqqseqq pita haraka. Hao ndio wabongo. Watu wa maraha na karaha ndani ya umasikini wao.
ReplyDeletewe hapo juu bora uwapashe hao wakina mwajuma wanaojifanya wanajua kuja juu kama moto wa kifuu hawajui hata utani..mnajifanya mnabusara eti hujafa hujaumbika mmh
ReplyDeleteMbona mnajitetea mnaogopa kuwa wafupi? Au mnaogopa hiyo metahli ya kiswahili ya 'hujafa hujaumbika' ian ukweli ndani yake na inatisha kweli. Lakini watu wengine wamezidi kuwananga wenzao kwa ajili ya maumbile yao kweli wanasahau kuwa hujafa hujaumbika. Au mnaogopa hilo neno kufa? Sasa mwataka kwenda mbiguni mbona mwaogopa kufa au mwataka mwenda kama Masiah bila kufa!
ReplyDeleteNyie mnaojinaya utani ni waongo wakubwa mmeogopa hiyo methali ya hujafa hujaumbika, ni kweli mwanadamu hujafa hujaumbika, leo unamcheka mwenzako miguu kama huyo anon wa kwanza, labda kwa kuwa wewe una miguu mizuri (na hii ni common watu kucheka maumbile ya watu) as if mtu aliamua kuwa awe na miguu ya aina fulani au urefu au ufupi. Hivyo ni vitu vya kupewa tu. Tena mara nyingi wa kuponda wanawake ni wanawake wenzao, vidudu mtu roho zao zimejaa kutu! Kakimbizeni basi na nyie mbona bado mwenge wa UHURU unaendelea kukimbizwa bongo kama huo wa Olimpiki umepita!
ReplyDeleteKuna watu duniani kazi yao kutetea maovu. Uliona wapi utani wa kumkosoa M'mungu kutokana na kazi yake? Sidhani JD alipewa choice ya either kuwa mrefu ama mfupi ni mola pekee aliamua kumpa kimo hicho kwa sababu zake anazozijua mwenyewe. Sasa ninyi wenzangu iweje leo mumkandye wakati hayo ndo majaaliwa yake. Ina maana mnamtania Muumba kuwa amekosea. Kwa mwenye imani ya dini hawezi kufanya utani huo wa kipumbavu kwani utani una mipaka yake. Ninaouleza ni ukweli wa mambo na wala si kuja juu kama moto wa kifuu. Najua mwenye hekma atafahamu na ambaye hakujaaliwa hekma hatofahamu maisha na ataendeleza ushindani uso kichwa wala miguu. Inshaallah M'mungu atawatieni nuru kwenye Mioyo yenu na Vifua vyenu na Macho yenu. Amin.
ReplyDeleteNawakilisha.
jd mfupi yeleeeeeuwiii kama
ReplyDeleteMimi ndo anon wa 3.46, bado naendelea kuwashangaa wabongo, nyie mnaishi wapi pasipo na utani?
ReplyDeleteHivi mbona wakiandika Tom Cruse kuwa nimfupi mpaka anaonekana kapiga magoti kwa mkewe mbona hamusemi, au kuwa sasa hivi anatumia high heels shoes..ili amkaribie mkewe mbona hizo kelele za kinafiki hatuzisikiii!!! Au wanapo msema rais wa Ufaransa Nicolous Sarkoz kuwa ni mfupi...na mambo mengi yanayoambatana na ufupi wake mbona kelele hizo za kinafiki hatuzisikii.....???
Kama mmezaliwa juzi muelewe Tanzania kuna utani mwingi sana..mpaka misibani. Mungepatikana watu mnaojifanya mnabusara za miaka ya 20's sijui tungekuwa wapi!!! Huo ni utani tu...ila tatizo la utani linaelement ya ukweli kidogo!! ndiyo maana naona mnang'ang'ana kuwa siyo utani.Hivyo ningeomba anayejua definition ya utani atusaidie kidogo.
Mtu hawezi kukutania mpaka awe na pa kuanzia.
Narudia tena, sidhani kama JD ni mfupi wa kiasi cha kuelezwa hivyo...pia na kwakuwa kakaa na Mziray ambaye ni mrefu zaidi ndiyo maana watu wakaweka kama utani...na hii kwa wale wanaomjua JD haiminishi kama ni mfupi wa kutisha...kwani kwa Tanzania kimo chake ni cha kawaida.
Pia, mimi sidhani kuwa usemi wa "hujafa hujaumbika" unanafasi kwa hizo kauli za utani zilizoelezwa humo...kwani hakuna ajali au ulemavu watu walioukebehi humo!! watu wamemtania dada wa watu na sidhani huo usemi kama unanafasi..maana naona watu wanadhani kuwa waliokoment wameogopa huo usemi...si kweli, kwani na uhakika aliye utoa, hakuwaelewa vizuri waliotania.
JD, lazima tukubalieni kuwa ni "public figure", anaikosoa jamii kwa mziki wake, na watu wanampenda..kama mtu wa jamii, hivyo wengine wanapenda tu kumtania..na narudia tena kuwa sidhani huyo JD hizo kauli zilimsumbua hata kidogo...JD ndo ukubwa huo.
Hivyo watanzania, nawaomba tujifunze kuwa na mtazamo chanya lasivyo tutajukuta tumestuck in the past
We anony wa 1:07 April 18 umeongea upupu mtupu, watu washakupeni pwiriri kwamba hakuna utani huo we basi ndo umekaa chini na kujifanya unabusara sana za kuwafafanulia Watz kuhusu utani, bado sana jidefend uwezavyo lakini ukweli utabaki pale pale hakuna utani wa kumuumbua mtu kutokana na maumbile yake. Anza mbele huna jipya. Katafute shule inayofunza busara kama utaipata, maana ni kitu NATURAL u don't need to go to school KIHIYO!!!!!!!
ReplyDeletewanalingana
ReplyDelete