
Wasichana watano bora katika shindano linalojulikana kama Face of Tanzania, ambao watakwenda nchini Afrika Kusini leo kesho kwa ajili ya kupata uzoefu mbalimbali katika fani hiyo ametajwa.
Kampuni ya Beautiful Tanzanie ya kina Irene Kiwia na Nancy Sumary inasema warembo hao ni Edna Makanzo,Emmy Malau,Irene Shirima,Neshino Laizer na Yvone Joseph ambao ni miongoni mwa warembo 16 walioanza shindano hilo kabla ya kuchujwa na kubakia warembo 10 na hatimaye 5 hivi sasa ambao ndio wanaelekea Afrika Kusini kwa uzoefu zaidi.
Warembo hao ndio wanaotarajiwa kushiriki katika fainali tarehe 26 Aprili katika ukumbi wa Ubungo Plaza.Wakiwa nchini Afrika Kusini, washiriki hao wanatarajiwa kutembelea makampuni kadhaa ya uwakala wa urembo kama vile O-Model Afrika na pia kufanya mazungumzo mbalimbali na warembo wa kitanzania wafanyao shughuli zao huko kama vile Happiness Magessa na wengineo ili kujua zaidi undani wa shughuli hizo.
Anko michuzi watoto wa kike watakupeeka kubaya rafiki yangu.Vipi safari yako ilikuwa shwari?
ReplyDeleteall the best sisters!
ReplyDeletemimi naomba ili neshino aonekane zaidi, mpeni zile nguo za kitanzania, mapozi yake ni ya kitanzania kabisa, atapendeza zaidi,
hongereni sana
I wish for you that your company will grow and grow and growwwww!!!
Duuuu!!! kasheshe kweli kweli.. yaani hata taifa laizer "neshino" naye ni mrembo!!! mbona hana mvuto!!!!! sidhani kama atafika mbali katika fani ya urembo. mimi napendekeza angejaribu marathon..
ReplyDeleteHongera sana. lakini hizo ndio pass za kusafiria ? au ni passport.
ReplyDeleteHONGERA SANA NESHINO. KEEP IT UP. WAPE CHANGAMOTO WAMASAI WOTE WA KIKE.
ReplyDeleteNaomba msaada kwenye tuta kaka Michuzi.
ReplyDeleteMimi ni msichana wa miaka 27 na boy friend wangu ana miaka 31. Katika muta wa kama miezi saba sasa boyfriend wangu amekutwa na matatizo ya ajabu. Baada ya kumaliza tendo la ndoa/ngono yeye siku hizi hupatwa na homa kali na hukosa nguvu za kufanya tendo hilo kwa muda usiopungua wiki tatu. Akipona tuu, na tukifanya tena basi anapata tena homa kali na kupoteza nguvu tena. Imefika mahali siku hizi hapendi tena kufanya mapenzi na hii mimi inanisikitisha kwa sababu nampenda sana huyu kaka. Sasa naomba kuuliza, jee hii ni kawaida kwa kina kaka wengine? au ni yeye tuu? Naomba wadau mnisaidie nifanye nini?
Tumepima maradhi yote na sote tupo safi.
Mdau Fausta Ndiboto,
Stockholm, Sweden
wau wamefanya kazi safi sana visura wote wazuri ni huo mkato wa nywele kwani wengine wahapendezi na nywele fupi lakini kwa ujumla wote wamependeza tunawapa hongera majaji wote kwa kutuchagulia visura mamodel wa tanzania good luck saudhiafrica kwenye kujifunza cat work.
ReplyDeletehongerani jamani mmetuchagulia watoto moto asanteni majaji vipi nancy mambo mzee hajambo umependeza mdogo wangu wasalimie nakaya jamani nawamiss kishenzi.
ReplyDeleteKaka angu Michuzi,
ReplyDeleteNazani utakubaliana na mimi kua nywele fupi zina wenyewe. Ningemshauri huyo dada aliekaa mwenye gauni la braun aweke dawa za kukuza nywele arudie u-feminine wake. Anaonekana kama anataka kumng'ata photographer. Duh!!
Jamani kuwa mrembo wa Afrika mpaka mnyoe nywele?
ReplyDeleteAnon 9:48Pm si unajuwa wabongo tunaiga sana.Hakuna mtu anayefikiria kuja na staili yake ni mpaka aige sehemu ama toka kwa mtu mwingine.Usishangae kuona hawa wasichana wakinyoa nywele.Jamani mnaonaje mkianza kuweka majina(nicks),bonyeza name/url unaweza kuweka jina.
ReplyDeleteMdogo wangu Fausta ungemtumia ujumbe Michuzi kwenye email yake ambayo ni issamichuzi@gmail.com,halafu wadau wangechangia kukupa maoni yao. Hapa nafikiri watu wataku overlook,hii ni sehemu ya hao warembo ambao hawana hayo matatizo yako.Although I must say tatizo lako pevu,linataka kafara.tehetehe!
ReplyDeletehongereni visura kwani mnavutia sana. majaji mnajitahidi hongereni kwahilo. haya we unaeomba ushauri eti kuwa huyo jamaa anapata homa akimaliza kunanii pole kama mmepima na hakuna kitu mgeukieni Mungu wenu kwani yeye ni muweza wa vyote.
ReplyDeletesweet
Arusha.
We Fausta wadau wanazungumzia warembo Wewe unaanzisha mambo ya ngono na Boy friend wako au unamuonea wivu Taifa "Neshino".Nafikili hilo jambo lako muuliza Utamu atakuwa na majibu.
ReplyDeleteyani so nice so good, furaha yangu imetimia kumwona neshino katika list ya 5 bora kweli mmeonyesha kuwa hamna ubaguzi kama bongo star search majaji wao, nafurahi kuwa neshino atapata kitu cha kuielimisha jamii yake ya kimasai kwa kweli big up IRENE NA NANCY, huo ndio uhalisi wa mtanzania, sio kuweka manywele ya kizungu mawigi halafu unasema ni face of afrika upuuzi mtupu tumezoea kuiga sana, nimefurahi sana kwa neshino kwa kweli na nyie waandaaji msimtenge najua hapo kiingereza itakuwa ngumu kidogo hasa huko anakoenda lakini si mbaya maana sisi ni watanzania na lugha yetu ni swahili mbona wachina wanaongea kikwao kila mahali so big up NANCY NA IRINE BIG UP warembo wa 5 bora. asante.
ReplyDeletesalo.
Hongereni visura/vipusa kwa bidii mloionesha. Pia hongereni watayarishaji wa vipusa hao, hasa Kiwia mumejitahidi sana kuwatia moyo na kuwaandaa mpaka wamebadilika m.f Neshino/Nashon kumtoa kwenye viatu vya chini mpaka kwenye mchuchumio, na anatembelea vizuri si kazi ndogo ni ya ziada. Maalumu pongezi zikufikie dada kiwia kwa lugha ya upendo uliyokiitumia wakati ya kuwaandaa, ukweli inaonyesha kiasi gani familia uliyokilelewa walifanikiwa kukulea katika utaratibu wa maongezi safi na mawasiliano ya upendo hata kama unaongea kitu cha kuumiza unakiwakilisha kwa upole bila dharau au kumuathiri unaemfundisha.
ReplyDeletejamani hivi neshno ni kisura kweli wa Tanzania au mnauza tu sura? haya nae ni kisura wa kimasai anajitambua!!!
ReplyDelete2ladies!!!
KULIKONI??? JAMANI MICHUZI, MBONA NANCY SUMARI, ANAONEKANA KACHAKAA (naombeni radhi, kwa hili swali)MAANA DADA HUYU ALIKUWA ANAVUTIA SANA, AU ZILIKUWA FAKE HAIR,? SASA AMEAMUA KUWA NATURAL, ndio tunaona utofauti? ila bado tu anaendelea na MKOROGO, kama wakina LEILA AHMED MSANGI aka LILY MZIRAY. Lakini poa Nancy maana natural kuwa natural ndio hasa wanaume wa kibongo TUNAPENDA. na umeanza na nywele zako kwanza. Nakupongeza kwa hilo.
ReplyDeleteMdau Fausta Ndiboto, wa Stockholm, Sweden, pole sana. Lakini naona wewe upo huko kwa wenzetu ambapo vipimo, wataalamu na madawa ni bwelele.
ReplyDeleteNingekushauri tatizo hilo mlifikishe kwa wataalamu, sio tatizo la kawaida. Huenda ana presha, au mataizo yanayofungamana na hayo.
Sio kweli kuwa wanaume wote wapo hivyo. Nahisi jamaa yako ana tatizo la kiafya, kamuone dakitari.
M3
Mimi ningependa kuuliza, ina maana wasichana wafupi sio warembo? au wanene sio warembo? je ina maana nguo au fasheni ya nguo sio kwa watu wafupi na warefu?
ReplyDeletem3
hi, naomba kukumbushwa...hivi Irene Kiwia alisha wahi kuwa miss? ni wa kitongoji au sehemu gani?.. anapendeza!
ReplyDeletePole Fau tatizo la boyfriend wako mwambie arudi bongo amuelezee babaake au mjombaake anaweza akamshauri vizuri kuwaona wataalam zaidi.
ReplyDeleteJAMANI, JINA LA VISURA NI LA WASICHANA WOTE, HAWA SIO VISURA KWA MASHINDANO, HAWA NI MODELS, INABIDI MJUE TOFAUTI, MODELS KUNA WENGINE WA AJABU ZAIDI, YANI HUYO NESHINO NI MREMBO KWA MODELS WENGINE WA KIMATAIFA.
ReplyDeleteIRENE NA NANCY JAMANI HONGERENI KWA VILE HAMKUWA KAMA BONGO STAR SEARCH, WATU TULIOWAPIGIA KURA NDIYO WALIOINGIA 5 BORA KWELI, YANI SAFI SANA.
KWA NESHINO, ONGEZA BIDII MPENZI, MPAKA HAPO ULIPO UMEJITAHIDI SANA, KWANZA KUPATA NGUVU YA KUVAA VIMINI TU UNASTAHILI HONGERA, WEWE ULIYESEMA AVAE MAVAZI YA KIMASAI UNACHEMSHA, INABIDI AVAE NGUO ZOOOTE MANA NI MWANAMITINDO HUYO, HACHAGUI NGUO!!
ILA JAMANI NAMPENDA SANA EMMY, YANI NI MODEL KWA KWELI!!!
NAWAKILISHA
Their all beautiful ladies but neither of them could be models. Maybe they could if their people would teach few things and that thing is how to POSE. Dang what kinda model take these kinda poses? Somebody needs to call Ms.Jay on em girls. Seriously i ain't hating but we gotta do better on our models. They'r really beautiful but lack of talent with who ever is directing this ish.
ReplyDeleteTanzania inakuwa sasa kama Nancy na Irene wanakampuni yao basi safi watu wachangamke kuanzisha vitu vitakavyowaletea maendeleo si kushabikia siasa na kupoteza muda na wakati tu. Hongera sana NANCY NA IRENE.
ReplyDeleteMimi,
edward alex mkwelele.
Nancy mdogo wangu hongera kwa kazi nzuri.We ni mrembo unayejulikana..Nimekuwa nakuona kwenye vyombo vya habari siku za karibuni ukitafuta visura na umekuwa ukishindwa kuyatendea haki macho yangu na ya wadau wengi nadhani.let me make it clear to you..Your current hairstyle is BORING..Please do something.
ReplyDelete