wadau kiinglishi mie mwenzenu iz not richebo, lakini nimeona hii ya huyu stelingi nikaona nishee nanyi. sijui inasemaje....zaidi bofya hapa


Wesley Snipes was sentenced to three years in prison on tax charges Thursday, a victory for prosecutors who sought to make an example of the action star by aggressively pursuing the maximum penalty.


Snipes' lawyers had spent much of the day in court offering dozens of letters from family members, friends -- even fellow actors Woody Harrelson and Denzel Washington - attesting to the good character of the "Blade" star and asking for leniency.


argued he should get only probation because his three convictions were all misdemeanors and the actor had no previous criminal record.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Adhabu kubwa sana, lakini mjue bado kuna maamuzi ya kukandamizana, haijalishi ninchi gani, huyu jamaa kisheria kafanya kosa, lakini adhabu aliyopewani kubwa mno, ukizingatia hana rekodi yeyote ya makosa.Na kuna uwezekano angetozwa faini kubwa ili serikali ifaidi hizo hela.lakini hamna cha faini!!

    Pia ni fundishi kwa mafisadi wetu kuwa kila kitu kinawezekana ebu fikiria Mkapa anapelekwa jela kwa ufisadi patamu hapo!!!.

    hakimu ameamua kumfanyizia, kimakusudi, lakini mkumbuke wenzetu hawapigwi jerki, ameambiwa akiwa tayari ajipeleke mwenyewe gereza la karibu na mahali anakoishi!!!!!!! hii Tanzania haitatokea ikitokea basi tusha kuwa WADHUNGU.

    ReplyDelete
  2. HUYU MHESHIMIWA NINAMSHAURI AHAMIE TANZANIA, HUKU KWETU WLIPAKODI WAKUBWA NI WAAJIRIWA WA NGAZI ZA CHINI KWANI HAWA KODI YAO NI MUHIMU SANA KWA UJENZI WA TAIFA LINALODIDIMIA KIUCHUMI.

    ReplyDelete
  3. The guy didn't pay tax from his own earning, he get three years jail sentence.

    Hey, what about our own politicians not pay up taxes, but squirming our own tax. Wesley, he is called Tax defier, but our politician will be called ????, Some one can help me out on this ? and they are still out there enjoying an unprecedented royalty, for committing a more evil of the two.

    There is a need of keeping record of politicians earning, and what they hold in possession year in, year out, that should be leveled against all politicians. There is no such thing in our Country, which is badly needed now. Morals start from Top Down, the real change/push start from bottom up. The government is responsible to revitalize it, one of the recommendations make it public and keep it wired, then we can hold our politicians accountable, "if they cannot stand the heat, they should keep of kitchen."

    We will help out our lousy politicians, next you meet up in Parliament session, this is the issue to discuss, WE NEED AN ETHICAL BILL LIKE THIS ONE, to talk about, and see out its IMPLEMENTATION. because we are used with lot of talks - "kung fuh wah but less actions" - inspired by Kipanya Cartoon.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  4. Dah hii ni soo kwa mshakji.Alikuwa keshaanza kurudi katika soko.Braza Michu na wadau wengine me nna thwali..Hivi mbona watu huko mbele hawazeeki??Toka niko mdogo jamaa yupo ana-act hadi leo nna miaka 2* bado tuuu ndo kwanza anaoneka age mate wangu.

    Mdau wa Mayfair

    ReplyDelete
  5. WELL, TANZANIA SIO KUTOLIPA KODI TU, HATA UKIWEZA IBA KUANZIA BENKI KUU HADI HAZINA, KAMA WEWE NI WAZIRI IBA UMEME, IBA MAJI, IBA MADINI, IBA, IBA ,IBA NA KAMWE MKONO WA SHERIA HAUTAKUFIKIA.

    ReplyDelete
  6. we anon 11:53 we unakula kiporo cha ubwabwa kila siku tena ukoko.sasa unataka kushindana na huyu..utazeeka utamwacha

    ReplyDelete
  7. Mdau wa mayfair hiyo picha ni ya zamani. Picha za sasa hivi ukimuona sura, umri umepanda na mvi tele kichwani.

    ReplyDelete
  8. naungana na wadau wote....kwetu hapa tanzania kodi ni stahili yetu watu wa kawaida.....wafanyabiashara na viongozi wengi kwao kulipa kodi kituo cha polisi...lakini ndio wanaokula sehemu kubwa ya hiyo kodi tunayokatwa sisi....tanzania haiitaji pesa nyingi kuweka mambo kwenye mstari......ni kurekebisha mifumo iliopo.....kuanzia kwenye mitaa tunayoishi.....kila mtu ajue haki yake na haki ya mwingine...sheria zilizopo zifuatwe....mwenyekiti wa mtaa,katibu tarafa,diwani,kila mtu ajue na kutekeleza wajibu wake.....atakayeenda kinyume na sheria achukuliwe hatua muafaka....kila mtu awe na sense of ownership...aone kuwa sehemu aishiyo au atumiayo kupatia kipato chake halali na yeye anahusika nayo....kwa kuanzia hapo hata uchafu mitaa kwetu kutakuwa hakuna,ujenzi wa hovyo kutakuwa hakuna,serikali za mitaa ziwe ni sehemu ya wananchi,hata uhuni na ujambazi utapungua kwa kuwa ulinzi shirikishi utakuwa na nguvu.....kisha tunapanda hadi kufikia kule juu kabisa....kiongozi akileta uhuni wa kutofuata sheria ya wesley yanamkuta........serikali lazima iwekeze kwenye elimu ya haya mambo kupitia media...na imani baada ya muda nchi inabadilika...tupate kiongozi mwenye `udikteta wa maendeleo` wakati wa kuendeleza siasa ulishapita...wenzetu walioendelea sio werevu kutuzidi sisi watu weusi...wamefanikiwa sababu ya kuwa madikteta wa maendeleo.....kujenga miji ambayo iko urbanized hata sisi tunaweza....biashara ya kubembelezana kuwekeza kwenye masuala ya maendeleo umepitwa na wakati.....tunaweza kuanza kuendeleza nchi yetu kwa projects.....inaanza sehemu moja hadi nyingine....hata huko manhattan au harlem ambako leo ndio indicators za uchumi imara wa dunia ya kwanza hazikushuka kama manna...ni moyo wa kizalendo wa wenzetu.....hatujachelewa..tuanze leo

    ReplyDelete
  9. Ni kweli yawezekana Wesley Snipes hakuwasilisha malipo ya kodi ya Mapato yake kwa wakati uliotakiwa!Lakini Mapato yake hayakuwa siri,yalijulikana.Wasiwasi nilionao ni kwamba Ma Supa Staa wengi wenye asili ya Afrika-Marekani Weusi ( Afro American Super Stars ) wamekuwa wakisakamwa sana na kufuatiliwa kwa karibu sana,ili kuwachokonoa makosa yoyote watakayo husika nayo hata yawe madogo kiasi gani, ishara ya wivu wa mafanikio yao na bidii kubwa ya kujituma kazini,kwa lengo moja tu la kuwakatisha tamaa na kuwafanya waonekane wahalifu katika jamii hususan ya Wamarekani Weupe ili kuwaharibia sifa yao wapoteze mikataba na ajira na warejee katika ufukara wa kuomba omba petty deals iwe katika sinema ,muziki au ridhaa.Kwa ujumla ni mchezo mchafu unao endeshwa nadhani na syndicate moja ya majambazi waliodhamiria kushusha hadhi ya Wamarekani Weusi.This is purely my personal feeling.Maana nimefuatilia kwa karibu yaliyowasibu kina Michael Jackson,Foxy Brown,OJ Simpson,James Brown,mwanadada mmoja wa riadha jina limenitoka,kina Tyson,kina Tupac na wengine wengi.Mtu aliyechipukia na kupata mafanikio ya haraka makubwa sana basi atasakamwa mpaka apoteze mwelekeo hadi ahusishwe na uhalifu,sometimes 'cooked up'brother!Hawa jamaa washenzi sana.But the Truth shall always prevail!Snipes anaheshimika sana Hollywood hata miongoni mwa Matajiri Weupe.Najua hawezi kutumiia hata nusu ya kifungo chake ataachiliwa huru.This is how life esp showbizz is in the States if you choose to go up there and try your luck in the showbiz.Fuck or get fucked as simple as that motherf*&%#!

    ReplyDelete
  10. Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na vombo vyako vya dola , nikimaanisha Polisi , Mahakama na Ofisi za Mwanasheria Mkuu za serikali ...please take NOTE from this and DO SOMETHING ABOUT MAFISDI WA TANZANIA !!!! Tutapiga kelele mabloguni mpaka vidole vituume kwa kutype hawafanywi lolote si mnaujua ule usemi wa KESI YA KUNGURU UMPELEKEE MWEWE ??? Kwanza wezi wenyewe ndio hao hao. Hebu oneni hii ni aibu ya aina gani mtu hakulipa Tax tu tena kwa hela yake mwenyewe aliyoitolea jasho anafungwa miaka mitatu haya bongo mtu unaiba miaka nenda rudi yaani wewe tangu umeshika Uongozi ama nafasi yeyote nyeti unaiba na unaendelea kuiba mpaka mwisho ndio kwanza unakaa kwenye kiti cha Bunge kuwakilisha wananchi na unazidi kupewa nafasi katika Serikali yaani ni fedheha kubwa kwa sisi wananchi ama kweli WAJINGA NDIO WALIWAO !!! Its about time things have to change!

    ReplyDelete
  11. we anon wa April 25, 2008 11:58 AM acha uongo,

    iba wewe uone kama hutakamatwa,

    Wasiokamatwa ni wakubwa tu kama kina "Vicent" BM, former PM, n.k

    Lakin waizi wa kuku, bata, nguo wote kiberiti kinawahusu

    ReplyDelete
  12. jamani katika ufisadi huu wa tnzania kuna sababu gani ya kulipa kodi? ikiwa tunagharamia matibabu wenyewe, tunagharamia elimu wenyewe, kil kitu tunanunua, kisha zile kidogo kwenye mapato yetu kinaporwa na kupelekwa Jersey kikiitwa vijisenti, Kisha tukitaka umeme tunaongezewa adhabu ya kuilipa IPTL, na Kiwira ya Mkapa nayokula 146 Milion per day naye aliipata kwa milioni 70 tu, kisha tunauza shirika la reli kwa bei poa halafu tunalilipa pesa zetu za kodi ili liwalipe wafanyakazi mishahara, AAAAAAAHHHHHHHHHHHHHH #@./?....xyz zao
    Kwanini/ sote tusikatae kulipa kodi kama ulaji ni huu????? kwa nini tusile pesa zetu wenyewe hata kama ni visenti kwa nini tuwape majambawazi mafisadi?

    ReplyDelete
  13. Marehemu bondia Joe Louis, (Bingwa wa Dunia ndondi uzito wa juu, 1937-1949),ambaye ndio namba moja katika ma mabondia wa dunia uzito wa juu katika historia(Zaidi ya Mohd Ali) alikutwa na jambo kama hili. Hadithi inakwenda hivi: Alipostaafu ndondi, kikundi fulani cha watu wakamtaka arudi kupigana kwa manufaa yao, akakataa. Watu wa kodi wakamwandama kuwa alikuwa halipi kodi, hivyo wakamwambia alipe hiyo kodi, hivyo ikamlazimu kurudi kupigana, akapigwa na bado akawa anadaiwa kodi. Wakamfilisi, na tangu hapo akawa anaishi maisha ya kimaskini kweli hadi alipofariki mwaka 1981. Ukweli ukaja kujulikana kuwa si yeye binafsi aliyekuwa anahusika na ulipaji kodi, ila watu wake wa uchumi walikuwa hawalipi kwa nia zao.

    Sasa... hawa wasanii wengi si wao wanaoenda kulipa hizo kodi, wanakuwa na timu ya watu, ikiwemo watu wa masuala ya pesa. Hivyo kama hufuatilii kwa makini unaweza kukuta jamaa hawalipi sehemu ya kodi husika. Kwa kuwa wao ni wafanyakazi wako, we ndiye unayekuwa responsible na kosa.

    Kama alivyosema mmoja hapo juu, CHA AJABU, ni WASANII WEUSI TU ndio wanaoandamwa sana MAREKANI. (Kwani hivi majuzi Valentino Rossi kalipa mamilioni ya pesa za kodi baada ya kukutwa na hatia ya kutolipa huko nyuma. Rossi ni bingwa mara nyingi zaidi katika kuendesha pikipiki za motogp [around 500cc])

    Dani, London

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...