Wawakilishi wetu katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Yanga, leo imekwaa kisiki na kushindwa kuwapa raha mashabiki wake kwa kutunguliwa bao 1-0 na Al Akhdar ya Libya katika mchezo wao wa marudiano uliochezwa leo neshno.
Goli la Al Akhdar lilifungwa dakika ya 83 na mchezaji Joseph Kanto kwa kichwa bada ya kuunganisha majalo ya Henry Kamala.
Yanga inabidi wajilaumu kwani dakika chake kabla ya mchezo kwisha walikosa penati baada ya mpigaji Hamisi Yusufu kumpa mpira kipa mkononi badala ya kupeleka nyavu ndogo. Hapo hatuzungumzii magoli ya wazi kibao waliyokosa.
Timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao wa kwanza uliochezwa, Tripoli Libya wiki mbili zilizopita.
Kesho hapo hapo neshno Simba itajimwaga na Enyimba ya Nigeria kwenye mchezo wao wa mguu wa pili kufuatia ule uliofanyika huko Aba ambapo wana-msimbazi walipigwa mabao 4-0 na Simba wanahitaji zaidi ya magoli matano washinde.
Walifikiri timu rahisi?Yanga nje,bado wenzao kesho!! teh teh teh.
ReplyDeleteInamaana goal limeengia na mpira kuisha au?
ReplyDeleteHongera Al Akdar!!!wa kwetu hawastahili kusonga mbele kwani hata penati kumlenga kipa...sasa mnamlaumu nani???bado boli uanasesere
ReplyDeleteYanga wametuzingua sana hata kufika golini walikuwa hawawezi kabisa sijui walikula ugali mtindi na Hamisi Yusuph katuzingua pia kukosa penalt.
ReplyDeleteKatochi
tehe tehe tehe, OO tuna kocha wa kimataifa, ooh tunacheza mpira wa kisasa, MUDOMO mrefu tu wakatio hawana lolote, sasa nyie tangu lini mkawatoa waarabu kwani mlikuwa hamlijui hilo. Nyie makimbe yenu ni hayo ya hapo Bongo. Hamna lolote hata muwe na Bill Gate
ReplyDeletekweli ng'ombe wa masikini hazai na kama akizaa anazaa dume.Yaani yanga waligangamala kutoa draw ugenini halafu wanakuja kufungwa nyumbani!!!!!!!!!!????kweli bado tuko nyuma halafu sidhani kama timu zetu za bongo huwa zinafanya mazoezi ya kupiga penalt wakati wa mazoezi yao ya kila siku ili kujenga kijiamini na kuwa na wachezaji mahiri kwa kupiga mikwaju ya penalt endapo itatokea maana hata ukiwaangalia wachezaji ya bongo wakienda kupiga penalt utaona kabisa wana hofu,wanaogopa na nakumbuka penalt ya Haroub Canavaro wa yanga alikosa,na yule wa mtibwa aliyekosa wataki wa michuano ya chalenji pale nesho,hata Abdi kassim akichezea Zenj kwny chalenji pia na leo huyu hamis yusuph!
ReplyDeleteKila la kheri kwa watani wa jadi )Mnyama)kesho ingawa kuwapiga Enyimba 5 bila sio rahisi ila wajitahidi tu kushinda nyumbani.