Filamu ya Copy, juzi usiku ilifanikiwa kunyakua tuzo ya kuwa filamu bora ya mwaka 2007-2008, katika shindano la tuzo za vinara wa filamu Tanzania liliandaliwana Kampuni ya One Game Promotion ya Jijini Dar es Salaam.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, filamu hiyo pia ilinyakua tuzo zingine tano kupitia kwa Khalfan Ahmed aliye nyakua tuzombili za Mtunzi bora na Muongozaji Bora, Rashid Mrutu aliyenyakuwa mbili pia za mpiga picha Bora na Mhariri Bora na Elizaberth Chijumba ambeye alinyakuwa tuzo ya kuwa Mwigizaji bora wa Kike.

Wengine walionyakuwa tuzo katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera ni Jacob Steven kutoka filamu ya The Stranger (Muigizaji Bora wa Kiume), Irine Uwoya filamu ya Diversion of Love (Mwigizaji bora Mwandamizi wa kike), Grace Michael wa filamu ya Malipo ya usaliti (mwigizaji bora Chipukizi wa kike).

Wengine ni Cleophance Ng’atingwa wa Kolelo (mnasa Sauti bora), Sebastian Mwanangulo wa Misukosuko II(Adui bora), Kulwa Kikumba wa Diversion Of Love (mwandishi bora), Emmanuel Muyamba wa Fake Pastors (muigizaji bora mwanadamizi wa kiume), Yussuf Mlela wa Diversion Of Love (Muigizaji bora chipukizi wa kiume) ambapo pia Filamu ya Kolelo ilitwaa tuzo ya kuwa na maleba na mapambo bora.

Awali katikahafla hiyo Naibu Waziri Bendera aliwapongeza wasanii wafani ya filamu hapa nchini kwa juhudi zao katika kukuza sana ahiyo ambapo pia aliwata kutengenezafilamu zinazolenga kulinda na kuhifadhi mila na desturi za Utamaduni wa Mtanzania.

"Filamu zilenge uhalisia wa Mtanzania, zilenge katika kuelimisha maadili mema na ziwe chachu katika kutanga utamaduni wan chi yetu, tusikimbilie mambo ya kuiga ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia katikammomonyokowa maadili," alisema Bendera.


Pia Waziri Bendera aliwataka wasanii kuongeza ubinifu katika utunzi na kwamba Tanzania ina utajiri mkubwa katika nyanja ya Utamaduni hivyo wasanii hawana sababu ya kuiba hadithi kutoka nje kwani hapa nchini katika makabila mbalimbali kuna hadithi nyingi na nzuri ambazo kama watazifanyia kazi vizuri zitachangia katika kuitangaza nchi yetu vyemakatika fani ya filamu.

Pichani: Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akimkabidhi Tuzo ya Filamu bora Mwongozaji na Mtunzi wa filamu ya Copy, Khalfan Ahmed maarufu kwa jina la kisanii la Kelvin kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za Virana iliyofanyika Ijumaa usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...