JK jana jioni kafanya badiliko dogo la baraza la mawaziri ambapo kamteua dk. shukuru kawambwa (pichani) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na mh. andrew chenge ya wizara ya miundombinu na naibu wake sasa atakuwa mh. hezekiel chibulunje.



wizara ya mawasiliano alikotoka dk. kawamba imechukuliwa na profesa peter msola ambaye wizara aliyokuwa akiongoza ya kilimo waziri wake sasa ni mzee stephen wasira ambaye alikuwa tawala za mikoa na serikali za mitaa, wizara ambayo sasa itaongozwa na mama celina kombani.



NB: wadau kunradhi kwa kuwaletea habari hii ya toka jana usiku muda huu kwani mtandao ulikuwa noti richebo kwa muda. vinginevyo libeneke linaendelea....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2008

    ...du! Utaratibu huu wa kutokujali 'Taaluma' ya Mawaziri unanichanganya sana. Mimi naamini kama Waziri angepewa Wizara kutokana na taaluma yake ingepunguza udanganyifu kuliko ilivyo sasa kwamba Waziri yeye anategemea 'taarifa' kutoka kwa wataalamu wa Wizara husika. Na kudanganyana kunaanzia hapa! Hivi ni kweli TAALUMA haina nafasi Tanzania???? Kwa kweli sielewi kama tuna lengo madhubuti la kuendeleza nchi yetu!
    Kwa nini lakini hatutaki kubadilika???????????? Why?????

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2008

    Pole sana mzee kwa mtandao kuwa down kwa muda....

    Lakini hii sijuwi ni 4-4-2 au 4-5-1 au 4-6-0??

    Nchi zetu hizi bwana..kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2008

    hongera waziri mpya wa miundo mbinu, labda kuja kwako wewe kunaweza kuharakisha kivuko kipya cha kigamboni kikaanza kaazi kama tunavyohadithiwa kitakua tayari may 2008.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2008

    This guy is among the few guys who can be trusted in JK's cabinet at the moment.

    He's down to earth and hardworking guy!

    For those who have known him would agree with this!

    Congratulations Dr!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2008

    Wazaramo wana msemo usemao"Ukitaka kujua nani fundi ujenzi na nani ni kibarua wa fundi ujenzi wakija kuomba kazi kwako unachotakiwa kufanya ni kuwapa kazi".

    Wape jengo la kujenga kila mtu mpe upande wake wa ukuta wa kujenga halafu waambie jengeni.Kisha angalia kazi zao mwisho wa siku utajua nani fundi ujenzi na nani ni kibarua.

    Kawambwa Wizara hiyo ya ujenzi wa miundombinu umepewa.Tunasubiri mwisho wa siku tuone kama wewe ni fundi ujenzi au la.Kazi kwako na kwa huyo aliyekuteua.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2008

    Bwana Michuzi, mbona wengine tukutuma comments zetu huzitoi, Mambo ya mpira yameisha jitahidi mwakani na kwa sasa mutuache tufurahi na Mwanaume Wewe "MAN U"

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2008

    Nakubaliana na anonymous wa May 11, 10:55 PM. Huyu jamaa ni mchapakazi, asiyependa makuu, anayejaji watu wote bila kuangalia hali ya mtu. Anaweza kukaa na watu wakawaida ("wadogo") na akajisikia yupo nyumbani kabisa. Ukikaa naye karibu hata dakika tano tu utaona haraka sana jinsi alivyo mtu muungwana!

    Hongera sana Dr. Kawambwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2008

    Nikiwaambia JK mchemkaji mtasemaa oooh majungu...ndani ya miaka 2 Kawambwa ameamishwa wizara 4...sasa ndio tija gani hiyo kama si uzushi. JK anapenda misara ya kujiongezea posho badala ya kukaa ofisi akatafakari vitu muhim kama ivyo...Agray baada ya kutolewa katibu muenezi wa ccm kapewa shavu jingine du kweli kazi ipo....mara kesho Bw. Mithupu waziri wa habari na mikonooozzz

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2008

    Mimi napatwa na wasiwasi na huyu jamaa maana ni kama Wizara ya 4 au ya 5 sasa katika kipindi cha miaka 2 na nusu ya utawala wa JK.

    Haya na embu tuone.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2008

    Nakumbuka ile picha ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Profesa Juma Kapuya, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Mheshimiwa Andrew Chenge na wale wawekezaji wa Kihindi wa TRL wakiwa wamekaa meza kuu, wafanyakazi wa TRL wakiwa upande wa pili, na Polisi waliokuwa waliokuwa wametanda kulinda usalama wakati wafanyakazi wazawa wa TRL waliposhinikiza kuongezewa mshahara toka shilingi elfu themanini kwenda shilingi laki moja na sitini elfu kwa mwezi(Shilingi 80,000 kwa mwezi kwenda shilingi 160,000 kwa mwezi).

    Picha ile inaamsha fikira.

    Si siku nyingi zilizopita tulisikia na kusoma kwenye vyombo vya habari Mheshimiwa Juma kapuya alivyoibiwa zana zake za kuvunia madini ya rubi huko Morogoro. Na Siku chache zilizopita tukasikia tafarani la mabilioni ya vijisenti vya Mheshimiwa Andrew Chenge. Hawa wawili walikuwa ndiyo wawakilishi na walinzi wa masilahi ya wafanyakazi Watanzania wa TRL. Ninachowaza kutokana na habari juu ya Waheshimiwa kutokana na habari zao na picha ile ni nini hawa Waheshimiwa Mawaziri walichokuwa wanafikiri walipokuwa pale kikaoni?

    Siku hizi Watanzania tunapongezana kwa kila hali. Ukiingizwa unapongezwa na ukitolewa unapongezwa. Ukiumbwa, ukiumbuliwa, au ukijiumbua unapongezwa. Kwa hiyo pongezi za Kitanzania zitamfikia yoyote kwa lolote. Hizo ndizo pongezi za Kitanzania za siku hizi. Sijui ni pongezi za kirafiki au kinafiki?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 12, 2008

    Hii yote ni Mazganyanza..... Kwanini isifike mahala Broza JK akawapa shuhuli wasomi wengi waliopo humu njini.... Ni kitu gani kinamfanya kuzunguka mbuyu?? Pls mwenye jibu atusaidie hapa labda pia itamsaidia pia Mh JK.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2008

    JK hapa kalenga sana huyu jamaaa ni katika mawaziri wachche au pekee makini kwenye baraza.

    wizara hii inaendana na taaluma yake amefundisha sana university of Dsm na alikuwa best student katika rekodi za injinia hapo UDSM.

    kuwa mtu wa watu nadhani ni utaratibu wa watu wa pwani.

    Hongera kaka Kawambwa usituangushe tuna kuamini na kukutegemea.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2008

    waarabu wa pemba hao..wanajuana

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2008

    MUUNGWANA NCHI IMEMSHINDA..ATUACHIE NCHI YETU MAPEMAAA TUCHAGUE MWINGINE,MAANA NAONA BISHOO HUYU ATACHEKA CHEKA TU NA KUONEA MAFISADI AIBU WHILE HE SHOULD BE DOING HIS JOB.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...