Home
Unlabelled
jk na al bashir
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Picha safi!
ReplyDeleteJK anaonekana kumsikiliza jamaa kwa makini sijui anamwambia nini lakini nina uhakika sio mambo ya Darfur...inawezekana kabisa sio mahali pake lakini jamaa huyo kazidi ujeuri Darfur watu wanakuteketea yeye kapiga executive suits anapiga soga hapo. Pliz JK amweleze ukweli huyo. Darfur hakuna hayo masofa mama hapo ujep haina maana yeye kuwa Japan kuzungumzia maendeleo wakati hataki kuzungumzia suluhisho la watu wake wa Darfur au hajui...
chonde chonde watz kamwe tusishangilia misaada tunayopewa na japan kwa sababu zina masharti kama yafuatayo,
ReplyDeleteMagari lazima tununue kwao jiulize tumeishawaingizia japan kias gan toka tz ilipoanza kununua magari japan.
pia kuna mchanga unaenda japan kutokea bandarin ni makontena mengi lakin ndan ya uo mchanga kuna madin.najua awawez kuchukua mchanga mtupu washafanya utafit na kugundua kuna madin kwenye uo mchanga.hivo misaada tunayopewa ni changa la macho,mwaka jana japan ilitoa msamaha kwa tz wa billion 700.lakin ni kwamba tuliishalipa indirect,pia hayo masharti yake ni magumu sana kwa uchumi wetu,ntaeleza siku nyingine.
NAOMBA RAIS KIKWETE AFIKILIE TENA KUUSU OIC KWANI WALE JAMAA MIKOPO YAO HAINA RIBA HATA KIDOGO LAKINI HAWA JAMAA MIKOPO YAO INARIBA KUBWASANAA NDO MAANA KILASIKU TUNALIPA MADINI NA HAYATOKWISHA WEZETU UGANDA WANAKOPA OIC HAWARUDISHI KWA RIBA NA WANAZIDI KWENDA MBELE LAKINI SISI TUMEKAMATWA NA HAWA JAMAA NA TUMEKUWA WATU WA MADINI KILA KUKICHA JAMANII
ReplyDeleteOIC hawatoi mikopo bila riba kwa nchi za makafiri.
ReplyDeleteIli nchi ipewe mikopo bila riba lazima iwe ni ya kiislamu. Kama nchi ni ya kikafiri (Si ya kiislamu) Riba iko palepale.
Uganda waliitapeli OIC wakati wa Idd Amin.Idd Amin mtoto wa mjini alijua kuwa ili apate pesa zisizo na riba toka nchi za kiislamu za Uarabuni aitangaze Uganda kuwa Uganda ni nchi ya Kiislamu.Basi Waarabu wakalewa utapeli wa Idd Amin wakaiingiza OIC ikaanza kupata mipesa isiyo na riba pamoja na kuwa Uganda ni nchi ya kikafiri!
Na Tanzania tukitaka hela zisizo na riba tuwatume wasanii watoto wa kijiweni wavae kanzu na tasbihi mikononi waende OIC wakawatapeli wawaambie Tanzania ni nchi ya kiislamu tuvute mipesa yao isiyo na riba!
Hapo Generali Bashiri na Luteni Kanali Kikwete wanaongea. Inaelekea kweli JK alikuwa na nidhanmu jeshini si unaona anavyomsikiliza afande wake??? Duh tatizo hapo hawajavaa magwanda.
ReplyDeletewanajeshi wastaafu wanapokutana na kukumbushana kuwa mambo ya longo longo yakizidi lazima wavae uniform
ReplyDeleteza rangi ya chui chui
Wewe annon wa 30, 12:57 acha uwongo wako na kusambaza chuki zisizo na kichwa wala miguu, hebu ingia list ua nchi zilizojiunga na OIC uone kama zote ni za kiislam, halafu Uganda wanapata mikopo ya OIC sasa huyo Idd Amin bado yuko? Na hao wanachama wengine walipeleka nini kama hawana makanzu? Think with your head and grow up, na acha kubisha tu kwa sababu ya propaganda za islamophobia na kutoa taarifa za uwongo! Haya vaa basi na wewe kanzu halafu uende ukajiunge uone kama kanzu ndio kigezo. Usitake kuwafanya hao members wa OIC wote hawajui kuwa Uganda asilimia kubwa ni wakristo, ishu hapa ni membership na si udini wa serikali! Nyie ndio mtakufa na umaskini wenu wa woga wa kupandikizwa!
ReplyDeleteUzuri siku hizi si rahisi kumdanganya mtu maana taarifa nyingi ziko wazi.
ReplyDeleteMalengo ya OIC yako wazi kwenye website yao.Lengo la OIC kufuatana na website yao ambayo waweza soma hapa:
http://www.oic-oci.org/oicnew/page_detail.asp?p_id=52 ni
"The Organization is the collective voice of the Muslim world and ensuring to safeguard and project the interests of the Muslim world in the spirit of promoting international peace and harmony among various people of the world" Hayo ni machache tu ningekupa mengi zaidi.
Hilo ni shirika la waislamu siyo makafiri .Uganda wapo wanaendelea sababu sababu ukishaingia hufukuzwi labda ujitoe mwenyewe. Uganda wanaona kuna hela za bure zinaendelea kuja hata mimi nisingejitoa mbele ya pesa nijitoe thubutu.Ila zikiisha najitoa nawaachia OIC yao.
EPA, Richmond kulitikisa Bunge
ReplyDelete2008-06-01 17:36:43
Na Mashaka Mgeta
Kashfa za ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) na mkataba mbovu wa uzalishaji umeme wa dharura wa kampuni ya Richmond, zitajadiliwa katika kikao cha Bunge baadaye mwezi huu.
Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, amesema atashangaa ikiwa Serikali itashindwa kuwasilisha taarifa za awali kuhusu hatua zilizofikiwa kushughulikia ufisadi huo.
Bw. Sitta, aliyasema hayo jana, wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.
Ufisadi katika EPA iliyo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ulibainika mapema mwaka huu, kufuatia taarifa iliyotolewa na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu ya Ernst and Young.
Aidha, vitendo vya ufisadi vilivyofanywa na kampuni ya Richmond, kupitia mkataba huo, viliibuliwa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyera, Dk. Harrison Mwakyembe.
Alisema Bunge lilitoa mapendekeo 23 kwa Serikali kuhusu kashfa ya Richmond, na kufanya subira ili kupisha kamati iliyotolewa kushughulikia kashfa ya EPA, ndani ya miezi sita, kukamilisha kazi yake.
``Tunasubiri taarifa ya maendeleo kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika kushughulikia EPA na Richmond, nitaishangaa sana (Serikali) kama hapatakuwa na taarifa hiyo,`` alisema.
Aidha, Bw. Sitta, alisema tamko kuhusu kauli iliyotolewa na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, kulihusisha Baraza la Mawaziri na mkataba wa kampuni ya TICS, atalitoa bungeni.
Alisema kwa vile suala hilo lilihusu mwongozo ndani ya kikao cha Bunge, haitakuwa sahihi kulizungumzia nje ya chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.
Kwa upande mwingine, Bw. Sitta, aliunga mkono hatua ya wanasiasa wanaokabiliwa na kashfa za ufisadi, kurejea kwenye maeneo yao ya asili ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Alisema suala hilo ni jambo la kawaida lililojengeka kwa watu wengi, katika ngazi tofauti za makuzi.
Wanasiasa waliorejea katika maeneo yao na kutoa na kukanusha tuhuma zinazowakabili ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Bw. Benjamin Mkapa, Mawaziri waliojiuzulu, Bw. Edward Lowassa (Waziri Mkuu) na Bw. Andrew Chenge (Miundombinu).
Bw. Mkapa alikwenda kijijini kwake, Lupaso mkoani Mtwara, wakati Bw. Lowassa alikwenda Monduli (Arusha) na Bw. Chenge, maarufu kama Bw. Vijisenti, alikwenda Bariadi (Shinyanga).
Hata hivyo, katika hali iliyotafsiriwa kama ni kejeli, Bw. Sitta, alisema hatua hiyo ilikuwa na maana kubwa, kutokana na uzito wa tuhuma zilizowakabili.
``Mtu akipata dhoruba, hakuna sehemu ya kupata faraja, wengine wanazomewa, sasa ni lazima watengeneze mazingira, na mazingira hayatokei hivi hivi, ndio maana mnaona wanapokelewa kama mashujaa,`` alisema.
Aidha, alisema vitendo vya hujuma za kisiasa, alivyowahi kuvitoa bungeni, kwamba vilifanywa na baadhi ya wanasiasa, Bw. Sitta, alisema hivi sasa vimepungua.
Alisema, kinachoendelea hivi sasa, ni kile alichokiita kuwa harakati chafu ambazo hata hivyo, hazina umuhimu katika maisha yake.
Kuhusu changamoto zinazolikabili Bunge, ikiwa utaratibu wa kuwa na wagombea binafsi utatekelezwa, Bw. Sitta, alisema mjadala wa suala hilo umechukua muda mrefu hivyo unapaswa kufikia ukomo wake.
Pia, Bw. Sitta, alizungumzia madai ya wabunge kutaka masurufu na mishahara minono, na kusema hayaeleweki vizuri kwa umma.
Alisema mishahara ya wabunge inaonekana kuwa mikubwa kutokana na kujumuishwa na mahitaji mengine kama vile mafuta kwa ajili ya magari na malipo kwa madereva.
Alisema hali hiyo ni tofauti kwa viongozi wa Serikali, kama Wakuu wa Wilaya, ambao tofauti na mishahara yao, wana fedha kwa ajili ya matumizi ya ziada.
SOURCE: Nipashe
kuhusu Tanzania kujiunga na OIC kwa sababu Ya pesa zao hayo ni mawazo ya kivivu.mi naamini watz tukiamua kukaza uzi wa kupambana na ufisadi,hicho kidogo tulichonacho kitajenga uwezo wetu wenyewe.
ReplyDelete