Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
mungu akuzidishie kipaji cha kutoa ujumbe kwa picha kwa kweli hiyo ndio hali halisi ya tanzania yetu hongera ndugu KP
ReplyDeleteYou never been wrong, Thats tells all !
ReplyDeleteNo Comment.
By Mchangiaji
Usitie wasi. JK aliahidi kulitatu hili suala!!!!
ReplyDeleteHayo maghorofa mengi makubwa mazuri ya Bara na Unguja yamejengwa na wafanyabiashara waliofanikiwa wa Wapemba walioikimbia Pemba na kwenda zao kuiendeleza Unguja na Tanzania Bara.
ReplyDeleteHivi ni nini kinachowafanya wapemba walalamike kila siku kuwa Pemba iko nyuma wakati wao ndio wanaendeleza Unguja na Tanzania bara kwa biashara zao na ujenzi wa maghorofa mengi makubwa wakati kwao wameacha minazi tu?
Hivi kuna mtaalamu wa historia ya Pemba atusaidie ni kwa nini hawa Wapemba wenye pesa nyingi na biashara kubwa hawawekezi Pemba na kuipenda Pemba kama ambavyo wachaga wanakupenda kwao Moshi na kukuendeleza?
Ni kwa nini wanapenda zaidi Unguja na Tanzania Bara na kukuendeleza zaidi huko kwa vitega uchumi na maghorofa na kudharau kwao Pemba?
Kwelim mimi sielewi na sijafanya utafiti naomba anayejua atusaidie kulikoni wapemba waliofanikiwa kutopenda Pemba kuiendeleza kibiashara na kimaghorofa.
koloboi@yahoo.com
Kutesa kwa zamu. Tatizo lenu wapemba ni kwamba mlishiriki kuwachapa viboko waunguja ndiyo maana nao watesa ati
ReplyDeleteWandugu, Pemba napalinganisha na Kilimanjaro!!!
ReplyDeleteMiaka ya nyuma Kilimanjaro ilikuwa kichumi/kimapato iko kwenye tano(5) bora kitaifa sasa hivi Kilimanjaro iko kwenye ... 14-17; hii ina maana gani kwamba wanakilimanjaro wanafanya uwekezaji mikoa mingine zaidi kuliko nyumbani kwao... yaani wako Dar, Morogoro, Mbeya na Kila sehemu yenye neema.
Vivyo hivyo Wapemba, wapo sehemu nyingine na wamewaacha wasioweza kutoka kule ndio maana kuko vile...
Ushauri wangu... Serikali kuu ipeleke vyuo vikuu au taasisi kubwa kule ili na penyewe kuchangamke...
Nphembha bwanaaa! hata akienda phembha haagi kuwa anaenda huko, na siku ya kurudi haagi kuwa sasa nnaondoka zangu. Waphembha kutwa kunjenga maghorofa makubwa makubwa kariakoo na kukodisha kwa watu, lanini ntu huko nymbani kwao hata kibanda hanaa. Kwaninii atii? Kwanini nyie wapemba han-jengi kwenu ati, mbona hizo tabia za kutishana wenyewe kwa wenyewe hanziachi atii? Nani atawajengea kwenu, sikatai jengeni maghorofa kariakoo ka vitega uchumi lakini nkienda kwenu basi mfikie japo kwenye nyumba nzuri, nchangishane njenge kwenu, nyie mumatajiri bwanaa, acheni hizo!
ReplyDeletemie ntani wenu kutoka bwejuu!
Alah! Sasa weye anoni wa 2:09am kwani huoni maalim alipotoka phembha darala llivunjika? Atarudije lihali!
ReplyDeleteNtalalahaun intalufilin, umkhum salauriq. Yaani, hata daraja liunganishalo Unjuga na bara nalo li hatiani. Tizama vizuri, halafu npe jawabu!
Seve
katuni ina kitu cha ziada; utunzaji wa mazingira, bara miti vipi?
ReplyDeleteJamani, kilio cha wapemba kina hoja ya msingi. naomba tutenganishe mambo mawili 1. suala la maendeleo binafsi yanayoletwa na wananchi weneyewe. na 2. suala la kisera na mipango ya serikali kupeleka maendeleo mahala fulani. pemba ina wilaya mikoa miwili na kila mkoa wilaya mbili. vijiji-mji muhimu pemba ni Chakechake, Wete, Micheweni na Mkoani. Kinacholalamikiwa na wapemba kina msingi wa kisheria. Kinahoji mkataba wa kijamii [social contract] kati ya wananchi na serikali yao. Ni suala zima la legitimacy ya serikali yao, ubaguzi wa wapemba kwa upendeleo wa waunguja ndani ya SMZ hali inayosababisha tamaa ya wapemba kujitawala wenyewe [self determination] kama ilivyokuwa Kosovo, wakati serikali ya Serbia inawanyanyasa Wakosovo [maana wengi wana asili ya albania] ndivyo ilivyo SMZ kwa watu wenye asili ya Pemba katika masuala yote yanayohusu ajira ndani ya SMZ, fursa za elimu, vyeo n.k. mfano hai ni kuwa haijawahi kutokea Rais wa SMZ akatoka katika kisiwa cha pemba. Hili halifanyiki kwa nasibu/bahati mbaya la hasha. hili lafanywa kwa lengo maalum na pili katika uendelezaji wenye nia mbaya [mala fides] wa historia. nasema wenye nia mbaya kwa sababu pamoja na kuwa chama cha Hizbo kilichokuwa kikipinnga mapinduzi ngome yake ilikuwa Pemba, bado haimaanishi kuwa wapemba woooote ni wafuasi wa Hizbo! kama mawaziri viongozi wameweza kupatikana toka pemba, tatizo ni nini? kwa nini huo mwiko kuwa rais wa SMZ hawezi toka pemba usivunjwe katika zama hzi za demokrasia? Hoja ya pili ni kuhusu masuala ya Uchumi, Karafuu ndo zao kuu la biashara Pemba, lakini wakulima wanamiliki, mashamba na miti ya mikarafuu, karafuu ikishavunwa [strictly speaking] ni mali ya serikali. Nilishuhudia msako wa karafuu majumbani mwa watu ukifanywa na KMKM mwaka 2004 kule pemba kwa kuwa wananchi walipovuna karafuu waliamua kuihifadhi majumbani kutokana na bei iliyotolewa na SMZ kuwa kiduchu il-hali katika soko la dunnia karafuu iliuzwa kwa bei zaidi ya mara tatu ya bei iliyootolewa na sserikali, Habu niambieni hayo ya unyanganyi wa mali za watu yanafanyika mkoa upi mwingine? sasa madai ya pemba kujitawala yako katika kada mbili. Kada ya kwanza ni ikiwa pemba inataka kujitenga na Dola. Hakuna haki ya moja kwa moja kwa watu kujitenga na dola, Ila madai ya wapemba yanaweza kupata uhalali katika sheria za kimataifa ikiwa wataweza kuthibitisha kuwa dola imeshindwa kuheshimu mkataba wa kijamii. Hata hivyo suala la kijitenga na dola ya Tanzania katika siasa za ndani ya nchi huchukuliwa kama uhaini kwa hiyo wapemba inabidi wawe makini sana, kufanikiwa kwao kujitenga ndo kutakakowaondoa katika hatari ya kushtakiwa kwa uhaini [Maana kila dola ina wivu na maeneo yake, inapofikia hatua ya jamii fulani kutaka kujitenga, dola inakuwa katika hatari ya kusambaratika ndo maana dola huchukulia suala la kujitenga kama uhaini]. Kwa kada ya Pili ni pemba kujitenga na SMZ kama vile ambavyo Rorya walidai wilaya, Sikonge wakadai wilaya, mvomero wakadai wilaya n.k yaani ili kurahisisha utendaji wa serikali na kuifanya serikali iwe karibu zaidi na wanachi pemgine Pemba isingeomba kujiondoa kwenye Dola ya Tanzania bali iombe kujiondoa katika taasisi ya SMZ.[maana SMZ siyo dola kwa mujibu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, mada ambayo nafikiri inahitaji tahadhari kubwa katika kuijadili]Nadhani ili kuondoa mvutano uliopo inawezekana kufanywa mambo matatu:
ReplyDelete1. Kukubali kuweka uwiano wa makusudi kati ya wapemba na waunguja katika SMZ[kwa kuwa wapemba wengi ni CUF hapa serikali ya mseto ya SMZ haiepukiki]; au
2. Ikiwa hilo halikubaliki, basi ni kuifanya SMZ kuhudumia Unguja kisha kuanzisha mamlaka nyingine [semi autonomous] itakayokuwa na jukumu la kusimamia Pemba; au
3 Kuondoa kabisa semiautonomous administrations na kuifanya Tanzania kuwa muungano kamili ambapo Unguja na Pemba hazitakuwa na serikali zao bali visiwa hivi sehemu ya Tanzania kama ilivyo mikoa mingine, kusiwe na rais wa zanzibar, kusiwe na baraza la wawakilishi, kusiwe na SMZ kama ilivyo mafia ni wilaya, hakuna rais wa mafia then tutakuwa tumepunguza matatizo yooote. maana haya tunayoyashuhudia ni ile dhambi ya Ubaguzi aliyosema Hayati JK Nyerere, kuwa mkishaanza kubaguana mjue mmekwisha,
naomba kuwasiilisha
Heri Mchau
huyu mdau wa mwisho sijui umezaliwa lini, unguja na pemba zilikuwa nchi tofauti na bara kabla ya 1964, usilinganishe visiwa hivi na mafia. kama unadhani nyerere ana akili basi kwanini asirudishe rwanda na burundi yawe majimbo ya bongo kama vile zamani german east africa. bara tunashindwa kuendeleza kwetu tunang'aninia visiwani wasijitenge, bara tumebakia uhasidi tuu, wapemba wamejenga bara kwa sababu wametuzidi akili na bidii.
ReplyDeleteNdugu Zitto, nashukuru kwa maoni yako, suala la mimi kuzaliwa lini halina mantiki hapa, hoja ni hoja umri si ndwele. Nashukuru kuwa umenielewa at least kwa sehemu. Hata hivyo mimi sijasema kuwa Unguja na Pemba ni sawa na mafia, ninafahamu fika kuwa hivi visiwa vilikuwa dola tangu awali tena chini ya utawala wa Sultani, lakini tarehe 26 April 1964 dola hii ya Unguja na Pemba ikaungana na Tanganyika. nafikiri huu ndo ulikuwa uamuzi pia wa mahaka ya rufani tarehe 21-11-2000 naomba ni nukuu swali lilikuwa "is Zanzibar a sovereign state in international law?"Mahakama ikajibu "After the above exposition, we have no difficulty at all to answer that question in the negative. The International Persons called Tanganyika and Zanzibar ceased to exist as from 26th April, 1964 because of the Articles of Union. The two states merged to form a new international person called the United Republic of Tanzania."
ReplyDeleteNdugu, Zito katika hoja yangu nilitoa mapendekezo matatu na pendekezo langu la tatu ni naomba nijinukuu "Kuondoa kabisa semiautonomous administrations na kuifanya Tanzania kuwa muungano kamili ambapo Unguja na Pemba hazitakuwa na serikali zao bali visiwa hivi sehemu ya Tanzania kama ilivyo mikoa mingine, kusiwe na rais wa zanzibar, kusiwe na baraza la wawakilishi, kusiwe na SMZ kama ilivyo mafia ni wilaya, hakuna rais wa mafia"
Hili ni pendekezo kuwa ikibidi kupunguza migogoro basi visiwa hivi viwe sehemu kamili ya Muungano wa Jamhuri na kufuta mamlaka nusu [semi autonomous authority] ya iliyokuwa dola ya Zanzibar [maana Mahakama ya rufani ilishatoa tamko kuwa Zanzibar siyo dola tena na hukumu hii hajawahi kubatilishwa hata kama Mahakama ya rufani ilikosea] Mimi pia ninafahamu akilini kwangu kuwa kama ilivyo Tanganyika ndivyo ilivyo Zanzibar kuwa zote ni dola zenye hadhi sawa sawa katika sheria za kimataifa. hata hivyo dola hizi mbili zilifanya mapatano ya kuungana na kuwa dola moja. kimsingi mapatano huweza kusitishwa, ikiwa hatua hii itafikiwa basi hisi dola mbili zitarejea tena kutambuliwa kama dola mbili tofauti. Nadhani ninapoongelea dola unanielewa kuwa naongelea nini. Labda kwa faida ya wengine dola kwa lugha ya kiingereza huitwa state. Na kawaida dola huwa na sifa kuu nne kwa Mujibu wa sheria za kimataifa [Convention on Rights and Duties of States, 1933 al maaruf kama Montevideo Convention] sifa hizo ni1. Wakaazi wa kudumu 2. Eneo la kijiografia linalotambulika 3. Serikali 4. Uwezo wa kimataifa wa kuingia mikataba na mataifa mengine. labda tafsiri yangu ya kiswahili si nzuri ila kwa kiingereza Ibara ya 1 ya huo mkataba wa montevideo unasema "the state as a persona of international law should possess the following qualifications a)permanent population b) a defined territory c) government and d) capacity to enter into relations with other states.
Kwa mantiki hii ndo maana nikasema japo Zanzibar ilikuwa dola kwa sasa siyo dola tena, ndo maana ni muhimu kuchagua kati ya kuwa na serikali ya mseto, serikali ya shirikisho au serikali moja. mimi ningependelea serikali moja ili kuondoa migogoro ambayo inaweza kujitokeza baadae. Nitaandika makala kuhusu Hukumu ya mahakama ya rufani katika kesi ya Machan Khamisi na Wenzie namba 8/2000. Lengu langu ni kujadili zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania kutokana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar, na athari za kuvunjika kwa Muungano. nakaribisha maoni, hoja, maswali, nk. kwa msaada zaidi tembelea www.kipimautu.wetpaint.com nitaweka hii hukumu ya Machano ikiwa ungependa uisome yote.ni mimi mdau mwenzio Heri Mchau,
habari zote hizi hazina kichwa wala miguu jamaa wa wapemba wanataka waindoe nchi yao kwenye zahma ya ccm , sisi bara hatuna demokrasia, hawa jamaa wamechoka na hii demokrasia yetu ya bandia wewe umebakia kutishia na kumlinganisha hawa jamaa na mohamed bacar, nadhani unasema bara watavamia kama vile mayote, kama hivyo basi watu wapemba lazima waipiganie nchi yao, ndugu zetu msiogope hawa manyang'au wa bara (heri) wakati wa nyerere kuvamia nchi za watu umepita i.e. seycheles,ngazija,uganda etc invading uganda to get rid of amin was ok but to bring back obote ilikuwa aibu tupu. pia heri pemba itajitenga kama vile eritrea,somaliland,bosnia,kosovo,ukraine,lithuania,estonia,belarus, to name a few and will not need recognition from nobody, pemba to be free of the mainland is their god given right!!! heri if you love united republic of tanzania please keep the name bcause tanganyika is such an ugly name bro!!!
ReplyDeleteNdugu Zitto umenigusa, nakushukuru sana kwa mtazamo wako kuhusu self determination ya Pemba. nafikiri hukuisoma hoja kuanzia mwanzo. baada ya kuona kuwa baadhi ya wadau wanapinga hoja ya wapemba niliingilia kati na kusemaa naomba nijinukuu "Jamani, kilio cha wapemba kina hoja ya msingi."
ReplyDeleteMimi hata siku moja sipingi uhuru wa mtu, nafikiri sikueleweka vizuri nilipotoa pendekezo la muungano kamili ambao kisheria unasababisha unitary sovereignity [umoja wa mamlaka ya kidola] tukumbuke kuwa muungano wa 1964 ulisababishwa na "surrender of sovereignity" Dola ya Zanzibar ili surrender kadhalika Tanganyika ili surrender. Wakati wa hiyo surrender, Pemba ilikuwa ni sehemu ya Sovereign ya Zanzibar. Japo hakuna mkataba wa muungano kati ya Pemba na Unguja [Hoja hii nafikiri tunapaswa kuijadili pia kwa kina]siyo kila dola huanzishwa kwa mkataba. Katika sheria za kimataifa kuna dhana tunaiita 'uti possidetis' ikimaanisha kuwa mipaka iliyokuwa ikitumika wakati wa ukoloni ndo itaendelea kuwa mipaka ya taifa baada ya kujipatia uhuru wake. unaweza kusoma paper yangu kuhusu Uti-posidetis katika blogu yangu ya www.kipimautu.wetpaint.com
Ndo maana leo Tanganyika haiwezi kudai majimbo yake mawili ya Urundi na Rwanda. Tukirudi katika hoja ya Wapemba kudai hati ya muungano na Unguja hii itawawia ngumu kupata mafanikio kwa kuwa dhana ya uti possidetis itawabana. tukumbuke kuwa kabla ya Mapinduzi ya 1964 Unguja na Pemba zilikuwa ni himaya ya Sultani kama Taifa moja, kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni lazima mipaka iliyokuwepo iheshimiwe na mataifa yote. Jambo pekee linaloweza kuwafaa wapemba hapa ikiwa watapenda kujitawala inabidi wafanye juu chini wafanikiwe kupiga kura ya maoni - referendum, na walio wengi wakisema kuwa wanataka kuwa taifa huru, nadhani pamoja na ubishi wa serikali ya jamhuri, au SMZ baraza la usalama la umoja wa mataifa itabili liwasaidie wajitawale kama ilivyokuwa kwa kosovo, Timor ya mashariki. Itakuwa ngumu kwao kufanya kama Eritrea maana kisiwa cha Pemba hakiwezi kuwa na uwezo wa kijeshi kupambana kama Eritrea ilivyopigana na Ethiopia, matokeo yake itakuwa kama ulivyosema kuwa wembe uliompitia Anzouan ndo utakaopita Pemba. Ndo maana nikasema kuwa wapemba wasahau kabisa kudai uhuru wa taifa lao kwa kupigana vita [it would not work] Mimi siwashauri hata siku moja wasijaribu. Nimeona mataifa mengi yana wivu sana na himaya zao au na himaya wanazozikalia mfano suala la Ireland ya kaskazini, sulala la Bask, Pueto Rico, Falkland, Tibet,Sahara magharibi n.k
Ndo manaa ndugu yangu Zitto utakumbuka kuwa Mataifa mengi yahapendelei hata kidogo kusikia kuwa sehemu fulani ya taifa inataka kujitawala. Waandishi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa 1945waliacha kwa makusudi kuitambua haki ya kujitawala self determination kama haki ya msingi ya umma. Badala yake jamaa walisisitiza dhana za sovereign equality, territorial intergrity na self defence.
Pamoja na kuwa nimependekeza Pemba na Unguja kuwa sehemu kamili ya Muungano, sina nia yoyote mbaya ya kukatisha uhuru wao,bali nimenagalia chanzo na sababu za malalamiko yao ya sasa na kufikiri kuwa kujitenga na jamhuri hakutawafaa sana, maana tatizo lao la kimsingi halitokani na Muungano bali linatokana na SMZ. Mimi nimewatambua kama watanzania wenzangu, lakini wakiamua kujitawala hiyo ni haki yao ya kimsingi, mimi nina ubavu gani wa kuwakatalia? inabidi tuwasaidie waweze kufikia malengo yao hayo kwa amani na watambue kuwa kujitenga pekee siyo suluhisho. ndo maana wahenga wakasema kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. kwa mantiki hii ya umoja ndo tuna SADC, EAC nk. Hata mataifa matajiri yanasisitiza umoja zaidi ya utengano mfano ni EU na sasa Marekani, Canada na Mexico zinataka kuunganisha nguvu za kiuchumi. Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa kila jambo lina faida na hasara zake ni vema tukashauriana kama ndugu maana muingiliano wa kijamii uliokwisha kujengeka kati ya wapemba na wananchi wa sehemu nyingine za jamhuri ya muungano ni mkubwa. Ni imani yangu kuwa umenielewa.
Ombi, kwa kuwa kwa sasa siko Tanzania, naomba ikiwa kuna mdau anayeweza kunipatia nakala ya malalamiko ya Wapemba waliyowasilisha UN anitumie kwa anwani hii almondprinters@yahoo.com
ni mimi mdau mwenzenu Heri.
Wewe Zitto Kiaratu kashfa hazidii, nakushangaa unavyomtukana huyo Heri, Jibu hoja acha kuosha kinywa kwa jazba. Habari gani haina kichwa wala miguu, nafikiri hii yako ndo pumba, unashindwa kuelewa hoja za msingi sijui umesoma wapi wewe taahira. Inabidi ututake radhi "eti Bara hakuna demokrasia" nani kakuambia, pili umetuita sisi watu wa bara "manyangáu" nyang'au wa kike akiwemo mama yako.
ReplyDeletekwa kweli kuna watu mambumbumbu,
ReplyDeleteMisupu huyu jamaa anaitwa Zitto Kiatu umemuokota wapi? ni bonge la lofa. Nani kamwambia kuwa Tanganyika ni Ugly name? stupid, ndo maana unaitwa kiatu kazi kukanyaga vinyesi vya wenzio
Michuzi,
ReplyDeletemimi namuunga mkono huyu Heri, achana na muosha kinywa huyo najiita Zitto ili tumuogope. Kuna wadau mambumbumbu wasiopenda kujenga hoja bali wamekalia ubishi tu. Tutake radhi kwa kutuita sisi wabara manyangáu. Inamaana hata mtaalam wetu michuzi ambaye ni mbara naye ni nyang'au? tutake radhi la sivyo michuzi muondoshe huyu kwenye blog yako
Bwana Michuzi, Tafaadhali niruhusu niingilie hii mada, Nimjibu Zitto kama ifuatavyo:
ReplyDelete1. habari zote hizi hazina kichwa wala miguu
Jibu: huyu Zitto Kiaratu si mtu makini, ameshindwa kuona hoja za msingi? au hakusima hii habari.
2.jamaa wa wapemba wanataka waindoe nchi yao kwenye zahma ya ccm , sisi bara hatuna demokrasia, hawa jamaa wamechoka na hii demokrasia yetu ya bandia
Jibu: Pemba siyo nchi, pili tatizo la wapemba halitokani na CCM pekee bali ni mjumuiko wa kadhia mbalimbali ikiwemo historia ya visiwa hivyo
3. wewe umebakia kutishia na kumlinganisha hawa jamaa na mohamed bacar, nadhani unasema bara watavamia kama vile mayote,
Jibu: kama nilivyosema huyu Zitto siyo mtu makini, ni mkurupukaji, nani kamwambia mayote ilivamiwa? na mbona sijasoma mahali huyo Heri alipoandika kuhusu Mohamed bacar? wewe Zito acha uzushi
4. kama hivyo basi watu wapemba lazima waipiganie nchi yao,
Jibu: nani kakuambia kuwa Pemba ni nchi? pili unapowashawisi wapiganie nchi yao unamaanisha nini? wapiganeje? wewe huwapendi wapemba unataka wajiue? [suicide]
5.ndugu zetu msiogope hawa manyang'au wa bara (heri) wakati wa nyerere kuvamia nchi za watu umepita i.e. seycheles,ngazija,uganda etc invading uganda to get rid of amin was ok but to bring back obote ilikuwa aibu tupu.
Jibu: Unaposema manyangáu unamaanisha nini? inamaana kila mtu wa bara ni nyangáu? nani alivamia ngazija? nimetangulia kusema kuwa huyu Zitto ni muosha kinywa mwenye jazba na povu mdomoni.
6. pia heri pemba itajitenga kama vile eritrea,somaliland,bosnia,kosovo,ukraine,lithuania,estonia,belarus, to name a few and will not need recognition from nobody, pemba to be free of the mainland is their god given right!!!
Jibu: unapaswa kubainisha tofauti za kimsingi, kihistoria na kiufundi za kujitenga kwa mataifa haya. Ukichukulia whole sale utakuwa unawashauri vibaya wapemba wenzio
7.heri if you love united republic of tanzania please keep the name bcause tanganyika is such an ugly name bro!!!
Jibu: Kwa mtizamo wako kiduchu ulionao unadhani tanganyika ni jina baya, ukitaka kuona wapemba wakitaabika basi ombea siku moja tanganyika irudi. mpo hapa Tanganyika kwa sababu ya Muungano, tukiunja muungano mtaula wa chuya kama wenzenu wa komoro, kudadadeki.
Watu duniani sijui lini tutakuwa tuna uchambuzi wa kitu katika upeo mmoja!nashangaa..
ReplyDeletehivi mchangiaji wa juu hapo ni nani aliyekwambia kuwa ili wapemba wakuwepo bara ni lazima kuwe na muungano???
hivi mbona kuna watanzania tele tu wanaishi nchi za nje na wanajiendeleza vizuri tu..je kuna muugano wa aina yoyote kati ya tanzania na nchi hizo???
mtu yoyote anaweza kuishi sehem yeyote dunia hii asikwambie mtu!alimradi havunji sheria za nchi husika tu...
kinachoonekana hapa ni kuwa ukweli usemwe kua wapemba wamechoka na madhila ya ccm..hata kama historia inachangia..kusema kuwa wanataka kujitenga sio kweli mimi ni mpemba na ninajua zaidi ya wewe kuhusu pemba ,kilichokuwepo ni kujaribu kuonyesha jinsi walivokata tamaa na utawala wa ccm wanataka just kuwashtua watu kama nyie mnao ona kuwa tanzania ni DAR ES SALAAM peke yake na ndipo panastahili kuwa na maendeleo(tena DAR ES SALAAM kwenye ni pale mjini tu posta,ukisogea kigogo tu na mwananyamala kwa mfuga mbwa hatari tupu)..kuna na sehem nyengine zinataka maendeleo pia..tizama uzuri katuni kipanya hiyo uone jinsi gani kaionyesha pemba..
madai ya wapemba yana ukweli na ni just kuwafikiria musikae mukawalaumu kwa kuja na kauli ya kutaka kujitenga.(kama ni kweli wamesema hivo)
watu hamutaki kukubali ukweli kuwa hivi sasa kama si bara pemba ingekua mbali kimaendeleo..ccm kule haitakiwi kabisaaa lakini cha ajabu imekushikilia halafu haipeleki maendeleo ya aina yoyote..
ccm iachane na wapemba mbona haiwafahamu??
bara kuna matatizo kibao nako(ufisadi)
lakini ajabu ni kuwa viongozi ccm bara baada ya kujipunguzia mzigo wakaachana na wapemba wanazidi kuwafrustrate!
its such a shame!
I really dont understand what is it to be in this injustice world..
ndugu watanzania tusisahau hawa wapemba tumewaonea miaka mingi sana nawao bado wana uwezo si jui inakuaje sasa endapo tutawapa haki yao ya kisheria kama watanzania wengine sina wasi wasi wataweza kuijenga pemba naitakua bomba kuliko tusisahau . utawala umewabana vibaya mnno. lakini bado wanatutesa kwa matanuzi tusisahau ukweli haufichiki nauongo.
ReplyDeleteKoloboi umeuliza vema, kuhusu katuni ya kp,Mimi si mtaalamu wala si mpemba ila nimezaliwa Zanzibar nimeishi huko kwa miaka ishirini nikaondoka kwenda bara kufanya kazi bara, na ni kweli wapemba wamejenga sana zenjy na bara kutokana na hali ilivyo pemba ya kubaniwa baadhi ya mahitaji na haki, zaidi ya hilo ni swala la kisiasa ukionekana wewe unaufahamu zaidi na kuweza kuwafumbua na kutaka kuwakomboa wenzio juu ya hali ilivyo hutafutwa na kuwekwa kizuwizini na kuuziwa kesi kubwa kubwa zinazohusiana na serekali,ufupi ni kwamba wengi wako nje ya pemba kwa sababu za kisiasa hivyo huona nyumbani hakurudiki au hakukaliki ndipo huanzisha maskani pale ambapo anaona hatabugudhiwa wala kuwekewa vikwazo juu ya biashjara zake,
ReplyDeleteUkweli ni kwamba madhila ni mengi kuanzia elimu mahitaji ya muhimu mpaka burudani na starehe zote ziko zenjy sio pemba Bugudha bugdha za kuwakamata na kuwafunga ni kubwa linalowakimbiza fikiria wewe mzazi wako amapigwa anateswa mkongo'to mtaa mzima wewe utanyamaza lazima utachukia pia, ila wao wanaitwa wanavurugu ila ukweli hawajausema wanalazimisha mambo ambayo wao wanayaona hayana maslahi kwao. haki zao za msingi za kuishi kwa amani na uhuru haupo
nani mdau ametoka pemba au anayeiishi pemba? hadi sasa Taxi zimeongezeka? maana pemba nzima ilikuwa na Taxi moja ya mzee Jafari mwenyewe anajiita Jeff, taxi hiyo ilikuwa ikipaki Chake chake 2005. hicho ni kiachiria tu cha maendeleo duni katika kisiwa cha pemba. pamoja na madhila mengine meeengi kama ya kupokwa karafuu, n.k Ninachotaka kusema ni kuwa Watu wa Pemba wanabaguliwa na SMZ. wanahitaji kuungwa mkono katika madai ya haki zao. ni mimi mtanganyika
ReplyDeletesamahani!! jamaa wote wa bara sio manyang'au, wale wanaaotishia kwamba pemba ikijitenga itakuwa hatari ndio manyang'au, wale wanaofananisha hali mayotte na pemba ndio manyang'au, watu hawa ndio wanatakiwa kuelimishwa/kujielimisha.pemba kulilia haki zao haihitaji ufundi au maeleano ya kimataifa, last i read the paper gen nkunda was kicking kabila ass,kagame was kicking the whole of congo in the face, sasa sielewi kwanini itakuwa vigumu pemba kujiamulia mambo yao. waingereza wanasema the truth is center to everything, smz inatawala zanzibar na pemba lakini ni prince karume ni chama gani?
ReplyDelete