JK akipokea zawadi ya albamu mpya ya mwanamuziki mpiga kinanda wa kulipwa na mwandishi wa vitabu Lister Elia anayeishi na kufanya shughuli zake jijini Tokyo, Japan. Hii ilikuwa wakati JK alipokuwa katika ziara nchini Japan mwaka uliopita. Kwa watakaopenda kumjua zaidi kijana huyu,tembeleeni tovuti yake www.listerelia.com
Home
Unlabelled
lister elia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Lister, nimependa nyimbo 'Mama Happy' na 'Utamaduni' maana vyombo vimerekodiwa kwa kiwango cha kuridhisha.
ReplyDeleteWasifu(profile/webusaiti) wako/yako inaonyesha una vipaji vya mambo mengi hivyo nina matumaini kwa kutumia uzoefu wa nyaja mbalimbali, ukifanya kazi kwa bidii ktk miaka ijayo mitano utakuwa mmojawapo wa wanamuziki bora Afrika.
Kumbuka wanamuziki waliokuwa mahiri walikuwa na 'nafsi' nyingi mfano James Brown(King of Soul) au Elvis Presley walikuwa na nafsi nyingi(wanawaloga watazamaji ukumbini, uanasiasa, nafsi ya mfano wa padre/ushehe, kutawala steji, wafuatiliaji wa current affairs n.k)
Tanzania tunaye mwanamuziki mwenye 'nafsi nyingi' Fresh Jumbe Mkuu na kwa bahati upo naye huko Tokyo, Ujapani hivyo muwe mnakutana kubadilishana mawazo na kukuza vipaji vyenu.
SeniorJunior
London
Kinanda analipiga barabara maana hata mie nimesoma kukipiga nimemnyanulia mkono ila sauti inabidi aingezee bidii, sauti yake ni kavu si ya mwimbaji mkongwe na vile vile kiingereza chake katika kuimba inabidi akifanyie mazoezi ya matamshi
ReplyDeleteNakuvulia kofia kaka,upigaji na aina yako ya miziki ni ya kisasa na hailingani na ya wababaishaji wengine.Ni miziki ya msomi na ajuaye kukitumia chombo chake.Sauti yako ni laini tamu na inaendana na aina yako ya miziki.Nyimbo kama "music of the people" na "i wanna make you mine" zinadhihirisha upeo na uwezo mkubwa alionao Lister na ni mfano wa kuigwa na wanamuziki chipukizi kwamba nyimbo katika lugha mbalimbali zinazaidia pia international audience kuitambua miziki ya wabongo.Kaka Lister kaza buti.
ReplyDeleteHaya ni Maendeleo makubwa, kumbuka 'like a father like a son'; bado unapaswa kuitangaza Injili kama Mzee Rev. Elia Nhukuwala kupitia jukwaa hili hili la uimbaji. Usikubali kuacha asili yako....usiishie UVUKE tu na akina Helmasy, Noel na Hudson....bado nakumbuka upulizaji wako wa Tarumbeta kwenye nyimbo kama 'Mtumaini Bwana' na 'Mungu aliupenda Ulimwengu'. Hongera sana Mungu akupe nguvu ya kutukuza yeye katika maisha yako yote!
ReplyDeletePamoja na musicians kuwa na nafsi nyingi, nakushauri imarisha sana nafsi ya Kumtukuza Mungu...nafsi zingine zitasimama kwenye mstari kupitia nafsi hivyo.