Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hahahha hiyo inaitwa 'UTAJIJU' kaka issa!
ReplyDeleteKweli amejuta kuongea, sasa atapewa maswali kibao na atalazimika kuyajibu
ReplyDeleteMjadala wa Mkapa moto
ReplyDelete2008-05-29 11:31:14
Na Dunstan Bahai na Simon Mhina
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kwa sasa hakiwezi kuzungumzia kauli ya Mwenyekiti wa Taifa Mstaafu wa chama hicho, Benjamin Mkapa kwamba si tajiri kama watu wanavyodhani na kwamba anaishi kwa kutegemea pensheni ya Urais.
Kauli hiyo ya chama ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Bw. John Chiligati, wakati akizungumza na gazeti hili jana.
``Sina maoni yoyote kwa sasa,`` alisema kwa sauti ya upole.
Naye Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Bi. Anne Kilango Malecela, alisema Rais huyo mstaafu wa awamu ya tatu, hajajibu hoja zinazotakiwa na wananchi.
``Wananchi wanataka kujua mali zake amezipataje na si suala la kuishi kwa pensheni, hiyo si hoja inayosubiriwa,`` alisema.
Moja ya utajiri ambao Mama Malecela alisema hakupashwa kuwa nao tena akiwa kiongozi wa ngazi ya juu serikalini ni umiliki wa mgodi wa Kiwira.
Alisema mgodi huo ni mkubwa sana na haupashwi kumilikiwa na watu watatu, tena viongozi wa serikali na kwamba kitendo hicho ni ukiukwaji wa maadili ya uongozi.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, hicho ndicho wananchi wanachokisubiria kwa hamu kubwa.
Bw. Mkapa juzi alikaririwa na vyombo vya habari akikana tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba alipokuwa Rais alikiuka maadili ya utumishi.
Rais huyo mstaafu ambaye alikuwa akisubiriwa na umma wa Watanzania kwa hamu kubwa sana kujitokeza hadharani kuzungumzia tuhuma hizo, alivunja ukimya huo wakati akiwahutubia wananchi wa kijiji alikozaliwa cha Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara kwamba wanaomtuhumu wana chuki binafsi dhidi yake kwa kile alichodai kutokana na kutowapa upendeleo wakati akiwa madarakani.
Bw. Mkapa alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kwa kituo cha afya kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki kijijini hapo.
Hata hivyo, kauli za kupinga majibu hayo ya Mkapa zilitolewa jana na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wa CCM na wale wa upinzani na hata wasomi.
Kubwa walidai kuwa Mkapa anatakiwa kujibu hoja, moja baada ya nyingine badala ya kujibu majibu mepesi, tena ya jumla.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amesema anashukuru Mungu kwa vile hatua ya Rais wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa kujibu tuhuma zinazomkabili kwa mtindo wa kulipua amejiingiza kwenye kitanzi.
Alisema hoja za kujitetea alizotoa Bw. Mkapa zimezidi kumsogeza gizani.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti huyo alisema Bw. Mkapa hatoweza kujinasua kwenye mtego aliojiingiza mpaka aseme ukweli wote.
``Mungu ni mkubwa, amekuwa na kiburi siku zote kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili, lakini hatimaye amejibu.
Hata hivyo, majibu aliyotoa yamezidi kumsogeza gizani kuliko nuruni,`` alisema Bw. Mbowe.
Mwanasiasa huyo alisema Bw. Mkapa hakujibu tuhuma dhidi yake badala yake amejiongezea zingine, pale aliposema wanaomsakama ni wale ambao aligoma kuwapendelea alipokuwa madarakani.
``Sawa tunaomba atueleze kina nani hao waliotaka awapendelee,`` alisema.
Bw. Mbowe alisema ameshangazwa na hatua ya Bw. Mkapa kwenda kujibu tuhuma dhidi yake kijijini na kwa nia ya kuficha siri ambapo hata alibagua vyombo vya habari.
Alisema kiongozi huyo mstaafu hakuwa na nia ya kujibu, badala yake alikuwa anawalaghai na kuwakebehi wananchi wa kijiji cha Lupaso, ambao pengine aliona uelewa wao ni mdogo.
``Tuhuma zake zilikuwa wazi kwenye vyombo vya habari, zimesemwa kwenye mikutano ya hadhara hadi Bungeni.
Kama alitaka kuzijibu ili Watanzania wajue ukweli kwa nini hakutumia njia za uwazi, badala yake anakwenda kujibu hoja hizo kijijini?
Huyu bwana alikuwa hodari wa kuhutubia taifa kila mwezi na kuwaeleza Watanzania mambo mbalimbali yanayohusu nchi na utawala wake, sasa hivi anaogopa nini kufanya hivyo?\" Alihoji.
Bw. Mbowe alisema Bw. Mkapa alionekana msafi (Mr Clean) kwa kumhofu Mwalimu Nyerere na ndio maana alipokufa akaanza biashara Ikulu.
``Tunataka ajibu kwamba ni uongo kwamba hakugeuza Ikulu kuwa ofisi yake binafsi? Hajanunua mgodi wa Kiwira kwa bei sawa na bure? Hakuchukua mkopo usio na dhamana NBC,`` alisema.
Alisema Bw. Mkapa anatakiwa aelewe kwamba kauli zake alizotoa majuzi, zimetonesha kidonda kwa Watanzania.
Naye mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alidai kwamba Bw. Benjamin Mkapa, ndiye rais aliyefanya vibaya kuliko wastaafu wote kusini mwa Jangwa la Sahara.
Akizungumza na Nipashe jana, Mchungaji huyo alisema japokuwa marais wengi Barani Afrika wamefanya uharamia wa kuzipora nchi zao, lakini utetezi wao unafaa kusikiliza tofauti na maneno aliyosema Bw. Mkapa kijijini kwao Lupaso.
Alisema utetezi wa Mkapa hauwezi kufanywa hata na mtoto wa darasa la nne aliyekamatwa akiiba ndizi.
``Utetezi wa kusema tuhuma dhidi yake ni uongo, uongo, uongo! Maana yake nini?
Ni kwamba hana cha kujitetea, hana uwazi na ukweli kama alivyokuwa anajitapa,`` alisema.
Mwanasiasa huyo alisema inashangaza kwamba kwa muda wa miaka 10 watanzania waliongozwa na mtu asiye makini, ambaye hawezi hata kujibu tuhuma.
Alisema kiongozi huyo mstaafu alipaswa kufafanua huo anaouita uongo unaotungwa na watu aliogoma kuwapendelea enzi hizo akiwa madarakani.
Mchungaji huyo alisema kutokana na Bw. Mkapa kushindwa kujibu tuhuma dhidi yake anategemea kumburuza kortini hivi karibuni.
Alisema hatua ya Bw. Mkapa kujitosa hadharani hivi sasa inatokana na ukweli kwamba ameshajua kwamba Katiba haimlindi kama alifanya ufisadi akiwa madarakani.
``Na hapa naomba nimjibu mhariri wa Nipashe aliyeuliza kwa nini Mkapa amejibu wakati huu. Ni kwamba ameshaona hana pakushika.
Alitegemea katiba kwamba itamlinda kumbe alikuwa anajidanganya, sasa kaelezwa ukweli na wenye akili ndio anaanza kujiingiza kichwa kichwa.``
Lakini amechelewa, huyu tunaye. Tutampelekesha mpaka aikimbie nchi na hata akikimbia tutamfuata huko huko,`` alisema.
Alisisitiza kwamba Katiba inamlinda rais juu ya mambo aliyoyafanya kwa umma akitumia madaraka yake, akiwa na nia njema, lakini kwa bahati mbaya yakaleta hasara na kamwe si kutumia madaraka yake kwa ajili ya kufungua kampuni binafsi.
* SOURCE: Nipashe
Kipanya huyu Mzee utamtoa "LOHO" wallah Khaaaa!!!!!
ReplyDeletekweli baba huu mtaa sio wenyewe manake sasa imekuwa fungulia mbwa...ila hukukosea kusemea kijijini..tatizo hujasema kama ni uongo upi hawa jamaa wanaousema...ni ule wa Kiwira, Ilala, au ANBEN...au kuna uongo mwingine na huo ni ukweli?
ReplyDeletefanya usimame hapo mara moja useme japo sio veme tukuandame lakini tunahitaji majibu na ufafanuzi wako
nyaningedere
Mmmh Kipanya.No comments
ReplyDeleteMr> Clean au Mzee Ben hapo umejipalia makaa yako ya Kiwira moto. Sisi waswahili husema uile na kipofu ukamgusa mkono. Sasa umetugusa mikono inabidi utuambie ukweli kama hizo nyama zetu kweli hujazila wewe.
ReplyDeleteasante sana anonymous 11:39 ulietoa makala kutoka NIPASHE nimesoma na kuelewa, na kwakweli inasikitisha kwamba bwana huyu Ben Mkapa rais wetu wa zamani,na weza sema leo hii bila aibu ni he is the most hopeless husteler president in African history. ni fisadi mkubwa kuliko balali na mramba, ninachotaka kujua kwa sasa, NI LINI ATARUDISHA MGODI NA MALI ZOTE ALIZOIBA
ReplyDeletemichuzi pliz usiibanie hii comment - au nitajua you are one of them!
hapa patamu,moto unawaka sasa mi yangu macho.
ReplyDeleteMs Bennett
jamani, mzee labda alikua ameonja kidogo, na lile jua kali!!**!!@$!**! Tumsamehe....
ReplyDeleteMdau hapo juu ukila na kipofu kama ukitaka kula nyama nyingi kuliko yeye inabidi pale tu mnapoanza kula uzipungeze nyama kutoka wenye bakuli kwani mtakapoaanza kula yeye atazihesabu kwa staili ambayo wewe utafikiria huyu jamaa haoni na hiyo ni kawaida yake kumbe jamaa anakula hesabu na mwisho wa siku ukimpunja atajua kwamba hakutendewa haki. Hivyo Mkapa hapa alisahau wakati yeye akihangaika kutupa maneno ya kejeli sisi tunahebu ufisadi wake na mali zitu anazoiba na kwa kuwa sasa raisi habanii uhuru wa watu kutoa maoni yao basi sasa tunamwambia bwana hizo nyama wenzio tulizihesabu kabla hujazila. Umetudhulumu sisi walalahoi huku unatuita wavivu, wenye chuki binafsi na pia mlituambia tule nyasi au tufe ili upate raha (ndege ya raisi). Ukweli utapatikana tu na ni swala la muda. Si muombei mabaya huyu mzee wangu lakini asipoweka haya mambo sasa kwa sasa atajiharibi baadaye atakapoondoka duniani kwani familia yake haina kina ya kushitakiwa kama yake yeye na hivyo wananchi wataweza kwenda kuchukua mali zao kwa nguvu
ReplyDeleteMambo! Pooooa! Hehehehe,Mambo!Poooooa!
ReplyDeleteTatizo kuna tungo kibao zilishaimbwa na wasinii bongo,mfano hii ya wana njenje ya kinyau nyau "WAACHE WAACHE WASEME,WATASEMA MCHANA EEH,USIKU WATALALA"
KIFO cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Timoth Said Ballali (65) kinazidi kuibua mambo mengi, sasa waliokuwa karibu naye wanataka undani wa wosia aliouandika kwa mkono wake na maelezo aliyoandika alipohojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuondoka nchini kwenda Marekani, uanikwe.
ReplyDeleteWatu mbalimbali walio karibu na familia ya Ballali, wakiwamo wanasiasa na wanasheria, waliozungumza na Raia Mwema wiki hii, wamesema ni wakati mwafaka kwa sasa mambo yote aliyoyaacha gavana huyo wa zamani yawekwe wazi ili kuondoa utata kwamba kuna jambo linalofichwa.
Wakati hayo yakiendelea, habari zinasema kwamba kuna mkakati maalumu wa kuhakikisha kwamba siri ya waraka huo haitolewi hadharani na baadhi ya watu mashuhuri wamethubutu kusafiri hadi nchini Marekani kufanikisha mkakati huo bila kujua mengi zaidi yapo nyumbani Tanzania.
Akizungumza na Raia Mwema wiki hii, mwanasheria mmoja mashuhuri amesema anafahamu na ameuona waraka aliouandika Ballali kwa mkono wake akielezea mambo mengi ya msingi aliyotuhumiwa nayo ikiwamo lile sakata la fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) uliokuwa ukisimamiwa na BoT, ambako zaidi ya Sh. bilioni 133 zinadaiwa kupotea.
“Ballali aliandika kwa mkono bila kupigwa chapa mambo yote yaliyotokea ambayo anatuhumiwa kuyafanya kama mhalifu na amewataja watu wote kwa majina na muda bila kuacha katika waraka wake huo ambao ameweka saini na kuhitimisha kwa alama za vidole,” anasema mwanasheria huyo ambaye hajawahi kutajwa popote kuwa na mahusiano na Ballali wala BoT.
Maelezo ya mwanasheria huyo yameshabihiana karibu kwa kila kitu na Mbunge mmoja wa Upinzani ambaye pia ni mmoja wa viongozi muhimu katika kambi ya upinzani ambaye naye amekiri kuuona waraka. Mwanasiasa huyo hakukiri wala kukanusha kuwa na nakala ya waraka huo wa Ballali.
Wote wawili wanasema kwamba waraka huo unaweza ama uko mikononi mwa watu zaidi ya watano wakiwamo wanasheria, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa sasa na wa zamani, wanasiasa wawili wa kambi ya upinzani na baadhi ya wanafamilia na hivyo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kuubadili ama kuuficha “milele”..
Kwa mujibu wa habari hizo, sehemu ya waraka huo inaelezwa kuelezea kwa kina kuhusu nini hasa kilichofanyika hadi BoT ikaidhinisha kutolewa kwa kiasi cha Sh bilioni 133/- na Ballali anaeleza kwa uwazi wahusika wote wakuu wakiwamo viongozi wa juu wa Serikali na wanasiasa walioshinikiza na waliochukua sehemu kubwa ya fedha za EPA pamoja na watendaji wa BoT walioshiriki katika zoezi hilo.
Waraka huo ambao kwa sasa unatafutwa kwa udi na uvumba unadhihirisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Serikali kutokana na baadhi ya wahusika muhimu wanaotajwa na Ballali kutozungumzwa popote linapozungumzwa suala la EPA na hata katika vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa waliouona waraka huo wa wosia, Ballali, kwa mfano, anaeleza jinsi alivyosita kuidhinisha malipo ya Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ambayo pekee ilikabidhiwa kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh. bilioni 40/-) kwa kutumia nyaraka za kughushi.
“Ballali ameeleza katika waraka ule kwamba alikataa kuidhinisha malipo hayo akielezea jinsi isivyo sahihi kutumia nyaraka za kughushi lakini aliitwa na mwanasiasa mmoja akiwa na mwanasiasa mwingine mkongwe mwenye ushawishi hadi sasa ambako aliamrishwa kuidhinisha malipo hayo mara moja.
“Unajua alivyoitwa aliwaeleza athari za kutumia nyaraka za kughushi wakamlazimisha na baada ya kuona wanamlazimisha akawaambia kama BoT itaidhinisha basi mtu anayatakiwa kukabidhiwa fedha hizo hastahili kwa kuwa kuna fedha nyingine zaidi ya Dola za milioni 60 alizotakiwa kurejesha kwanza kabla ya kukabidhiwa fedha zozote, lakini akalazimishwa kumlipa huyo huyo,” anasema mwanasheria aliyezungumza na Raia Mwema.
Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara huyo ambaye ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania alikuwa akiwasiliana na wanasiasa waliomshinikiza Ballali amlipe kiasi cha kumpigia simu Ballali kabla hata ya kuondoka viwanja vya majengo alikokutana nao.
“Unajua inatisha kwani Ballali anasema katika waraka wake huo kwamba alipotoka tu kuzungumza na wazee wale kabla hata ya kuondoka akapigiwa simu na mfanyabiashara huyo akimuuliza kama alikwisha kupata maelekezo na yeye kumtaka aende ofisini ambako atakutana na msaidizi wake ambaye ndiye anayeshughulikia fedha za EPA,” anasema.
Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara aliyekabidhiwa fedha hizo ana uhusiano wa karibu sana kibiashara na kijamii na ofisa wa BoT aliyehusika pia na sehemu ya mchakato wa EPA, jambo ambalo limeelezwa kwamba linazidi kuibua utata baada ya wote wawili kutotajwa popote katika sakata hilo.
“Sijasikia popote huyo ofisa wa BoT akitajwa maana hata nafasi ya ugavana alikuwa akitajwa kuwa anaweza kupewa lakini bahati ndiyo akateuliwa Profesa Benno Ndulu, maana angeteuliwa (anamtaja jina) mambo yangeendelea kuwa mabaya zaidi na siri nyingi zingefichwa lakini sasa najua mambo yatajulikana tu,” anasema.
Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inatajwa kuchota zaidi ya Sh. bilioni 40/- hadi sasa haijulikani ilipo pamoja na kuwapo madai kwamba ilikabidhiwa kwa mfanyabiashara mmoja mwenye kashfa nyingi nchini ili ionekane kuwa ni ya kwake lakini hadi sasa haijaelezwa bayana hasa ni mali ya nani.
Kampuni hiyo kwa kumbukumbu za Msajili wa Makampuni (BRELA) inaonyeshwa kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina kampuni tofauti jirani lakini namba hiyo haionekani na kinachoonekana ni viwanja kuanzia Plot 77 na hata Plot 86 na Plot 88 katika eneo hilo maarufu la viwanda lakini plot ilipo Kagoda haionekani popote.
Aliyesimamia na kufuatilia BoT na hatimaye chukua fedha za kampuni hiyo katika Benki ya CRDB Limited tawi la Azikiwe anajulikana waziwazi na wafanyakazi wa maeneo hayo, lakini kumbukumbu zake zinaelezwa kupotea ama kufichwa na wahusika kwa nia ya kuwasaidia watuhumiwa ama kwa sababu za kichunguzi.
Hata hivyo, inaelezwa kwamba wapelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwisha kuchukua nyaraka zote muhimu ikiwa ni pamoja na kadi ya benki iliyotumika kufungulia akaunti tawi la Azikiwe, ikiwa na picha na saini za wahusika wote muhimu kwa uhakika zaidi.
Sakata la BoT na zaidi akaunti ya EPA lilichukua sura mpya baada ya kuelezwa kwamba sasa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha fedha zote kiasi cha Sh. bilioni 133 zinarejeshwa kabla ya kuchukuliwa hatua kwa wale waliofanya makosa ya kijinai katika kupata fedha hizo.
Imeelezwa katika hali ya kutatanisha tayari hata fedha kutoka kwa wamiliki wa Kagoda nazo zimekwishakuanza kurejeshwa japo kwa awamu, jambo linalodhihirisha kwamba Serikali inawafahamu kwa hakika kabisa wamiliki wa Kagoda na inawaficha ama inataka kuwalinda kwa sababu za kisiasa zaidi.
Katika uchunguzi wa awali wa mkaguzi wa nje, Samuel Sithole wa kampuni ya kimataifa ya Deloitte & Touche tawi la Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo “nyeti” ya kiusalama.
Hata hivyo, siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na Gavana Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo ambaye sasa ameachwa nje ya Baraza la Mawaziri.
Baada ya kifo cha Ballali sasa inaelezwa kwamba uchunguzi unaoendelea dhidi ya wanaotajwa kuchukua fedha za EPA unaweza kufungwa kwa kuwa shahidi muhimu atakuwa hawezi kutoa maelezo yake mahakamani jambo ambalo linaelezwa kuweza kuichafua zaidi serikali.
Ballali ambaye amefariki dunia akiwa nchini Marekani na kuzikwa huko huko anaelezwa kuondoka na siri nzito ikiwa ni pamoja na mazingira ya kuondoka kwake, kuugua na hata kifo kumkuta huku serikali ikiendelea ‘kuweweseka’ na ‘kutapatapa’ kutokana mkanganyiko mkubwa wa yaliyomsibu gavana huyo wa zamani.
Hata mahali na siku aliyofariki Ballali ni mambo yaliyoelezwa kuwa na utata hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba alifia Boston, huku wengine wakisema alifia nyumbani kwake Washington DC Ijumaa ya Mei 16, 2008 na baadaye taarifa zake kutangazwa Jumanne usiku ikiwa ni siku tano baadaye, huku baadhi wakianza kudai kwamba alifariki Jumapili ya Mei 18, 2008. Hata mazishi yake yalifanywa kuwa siri na ni wanafamilia wachache tu waliobahatika kuuona mwili wake Jumanne Mei 20, 2008.
KANISA la Mt. Stephen Shahidi
Mwili wa marehemu Ballali ulihifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko Washington DC, kabla ya ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC. Kanisa hilo lipo 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037 na baadaye kuzikwa kwa faragha katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, Maryland.
Pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali, hasa magazeti na kutangazwa majukwaani, Ballali hakuwahi kushtakiwa rasmi pamoja na kuwapo taarifa kwamba aliwahi kuhojiwa na TAKUKURU.
Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.
“Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti,” alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.
Aliongeza Warioba: “Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.
“Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.
“Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.
“Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.
“ Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika.”
Ballali ambaye ameacha mke na familia, amekuwa akitamka wazi kwamba hajawahi kuiba hata senti moja ya umma katika kipindi chote akiwa BoT na kuwashutumu watu ‘aliowakwamisha’ kuwa chanzo cha kuandamwa kwake na tuhuma mbalimbali kabla ya kukataliwa kujiuzulu na hatimaye uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Marehemu Ballali alijiunga na Benki kama Gavana Julai 14, 1998 hadi Januari 8, 2008.
Ballali alikwenda ghafla nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana akiwa na nia ya kurejea nchini, alikwama huko baada ya kubainika na matatizo makubwa tumboni kabla ya kulazwa hospitali na kufanyiwa upasuaji mkubwa.
Kwa mujibu wa habari za awali, Ballali aliieleza familia yake kwamba alikuwa akihofia kula kitu chenye madhara makubwa hasa baada ya madaktari wa Marekani kumfanyia uchunguzi mara tu alipowasili nchini humo, madhara ambayo alionyesha kuhisi kuyapata alipokuwa nyumbani hasa kati ya miji ya Dar es Salaan na Dodoma.
Wakati akiendelea na matibabu, Ballali aliandika barua kuelezea nia yake ya kuomba kujiuzulu kutokana na kuendelea kuzorota kwa afya yake huku akiwa bado na majukumu mazito ya kusimamia uchumi wa Taifa.
Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za upande wa Serikali kuthibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Ballali siku kadhaa kabla ya serikali kutangaza matokeo ya ukaguzi wa kampuni ya nje iliyopewa kazi ya kukagua hesabu za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kupitia ripoti ya wakaguzi hao, ndipo alipotamka kumfuta kazi Ballali bila kuzungumzia lolote kuhusu kujiuzulu kwake.
MICHUU NIMEITOA KWENYE GAZETI LA RAIA MWEMA WAPE WADAU WANOE VINYWA
MKEREKETWA
Mkereketwa tupe jina la Hospitali aliyokua anatibiwa Ballali huko Marekani.
ReplyDeleteWOU! WOU! WOU! KAMAATAA HUYOOO!! KAMATAAA HUYOO!! WOU! WOU!....BAHATI YAKO!! NA TUSIKUONE UKIPITA MTAA HUU TENA!!! LIONE KWANZAA!!!...................
ReplyDeletekp mi ningependa kurudi kwenye katuni ya juzi kati,ambayo ulionyesha polisi huko sauzi wanavyowaambia wenyeji kua wawafanyie fujo wageni,na kusema ndio sababu ya wao kukosa kazi,na ukauliza kwa bongo itakua vipi,kwa bongo itakua kwamba viongozi wa upinzani watawaambia wananchi ya kua mafisadi ndio wanaosababisha wao kukosa kazi, na watawaua then baadae viongozi wa upinzani watapinga kwa nguvu zote ila ni gumashi tu.
ReplyDeleteHuyu jamaa muda wake wa kumshughulikia umefika kwani aliiba sana kupindukia. kila mara najalibu kufikilia iweje ujilimbikizie mihela ambayo hata idadi yake haujui. Kipara vumilia ulikuwa mrafi unakula kwa mikono miwili bila kunawa!
ReplyDeleteKwa mwendo mkali huo, ni lazima mbwa wamkamate tu. Ngoja tusubiri
ReplyDeleteANON WA TAREHE 29 MAY SAA 4:33PM UMENIACHA HOOI NA MAMBO POOOOA MAMBO POOOA , SASA SI MAMBO POOA NI MAMBO BOOOORE BOOOOOOOOOOOOOORE NA UKUMBUKE WANA NJENJE WALIIMBA
ReplyDeleteBOKO WALA WENZIOOOOOO BOKO WALA WENZIOOOOO BOKO ANAE ATALIWA BOKO NAE ANALIWA MMMK
"CHOMO KWANI N'KAPA KOCHOMOKA HAPO ? KAJI KWELI KWELI , KWANI WALE KUCHEMA NINI? BAAA KUKUCHINGIZIA CHEEEEEEEEE! MI KUFIKIRI UKWELI KUWA UMEKWIBA CHIWIRA MMMM
Ipo katuni moja kipanya alikuwa anapakua vitu kwenye boks huku akisema "utasema tu"
ReplyDeleteNadhni hiyo ni muafaka kuliko hizi ulizozitundika. turejeshee
KP Nakuaminia siku nyingi sana kwa kuweza kufikisha ujumbe wa uhakika kwa njia hii ya katuni - keep it up and God bless you kwani hiki ni kipaji cha kuzaliwa.
ReplyDeletedaa!!!!ulipokanyanga mzee siko,manake walivyokondeana kwa ukame lazima wakuingize kaburini
ReplyDeleteWAHENGA HUSEMA ALIYE JUU MGOJE CHINI,ULITHANI UTAKUWAJUA MILELE??SASA UTANITAMBUA,SIJUI UTANIELEZA NINI NIKUELEWE,UMETUWEKA JUU YA MAWE TOKA 2005,SASA KUTESA KWA ZAMU MZEE
ReplyDelete