Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteua majaji 11 wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa jana Ikulu, Dar es Salaam, na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Philemon Luhanjo inasema kuwa uteuzi huo umeanza Jumamosi iliyopita, Mei 24, 2008.
Kati ya majaji hao wapya, saba ni wanawake na wanne ni wanaume.
Wanawake walioteuliwa kuwa majaji ni Bibi Sophia Wambura, Bibi Crecencia William Makuru, Bibi Zainabu Goronya Muruke na Bibi Upendo Hillary Msuya.
Wengine ni Bibi Atuganile Florida Ngwala, Bibi Rose Aggrey Teemba na Bibi Rehema Kiwanga Mkuye.
Majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Bwana Kassim M. Nyangarika, Bwana Gabriel Kamugisa Rwakibarila, Bwana Ibrahim Sayida Mipawa na Bwana Lawrence Kisenge Nziajose Kaduri.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi ametangaza pia kuwa Rais Kikwete amemteua Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Bwana Wambali anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bibi Sophia Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Wambali alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani.

Kama kawaida(Nisieleweke vibaya).
ReplyDeletehongereni sana! fanyeni kazi kwa usawa na haki
ReplyDeletehongera ninyi mliochaguliwa,lakini kumbukeni vyeo ni dhamana.acheni rushwa,pia fanyeni huduma za haraka kurahisisha kesi zote kusikiliszwa kwa wakati na muda mfupi,bila kuwachelewesha wanaotaka kesi zao kutatuliwa,nyinyi msinunuliwe na wahindi na waarabu,wazungu,na mafisadi kwa kutoa hukumu za upendeleo.kuweni wazuri kwa kuiga mfano wa jaji augustine said.enzi ya nyerere..punguzeni maonevu kwa masikini,wasio na uwezo kwa kuwapendelea wahindi na waarabu na kununuliwa kwa chips na wageni,wasomali.nk..maana majaji wa bongo ni waongo na amtumii haki ya kazi zenu,kataeni rushwa kama pontius pilate.aliposema sioni sababu ya kumua jesus christ,alipokataa kushurutishwa kutoa hukumu ambayo makuhani wa kiyahudi walilazimisha..nanyi lazima muwe stable kutoa hukumu ya haki
ReplyDeletemdau mkereketwa.uk.
safi sana....!
ReplyDeleteHii ni safi...Hongereni Waheshimiwa
ReplyDeleteNaona JK anatambua thamani ya Mahakama kuwa na Majaji wa kutosha ili kesi zisikilizwe na kutolewa maamuzi kwa muda mfupi lakini kwa kuzingatia misingi ya haki. Wataalamu wa sheria wanasema "Justice delayed is justice denied". Sasa waheshimiwa mkumbuke hiyo ni dhamana kuwatendea watanzania haki sio tena tuone uwingi wenu bila mabadiliko ya kweli katika haya manun'guniko kwama kila siku kesi zinapigwa tarehe.Pliz...Waheshimiwa pia mzingatie uhuru wa mahakama "Independence of the Judiciary" hasa kuepuka kuingiliwa na waheshimiwa saana wanaopenda kupindisha sheria ili watimize matakwa yao...Tafadhali mtetee wanyonge na kusimamia haki kwa kila anayestahili sio haki iwe kwa wenye vijisenti...halafu sisi wenzangu na mie ambao pesa zetu sasa zimekosa tafsiri sahihi tukose haki.
Sawa jamani Hongera...
Napenda kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Mh.Rais Jakaya Kikwete kwa namna ambavyo anavyochukua hatua za maksudi kabisa za kulishughulikia suala la upungufu wa majaji wa mahakama kuu ya Tanzania.Kwa muda mrefu sana, kumekuwapo na madai kwamba moja ya sababu kubwa zinazopelekea uchelewashaji wa mashauri mengi yaliyoko ngazi ya mahakama kuu,ni pamoja na uhaba wa majaji wa mahakama hiyo.Katika kutatua tatizo hili,ni mara ya pili sasa Mh.JK anafanya uteuzi wa majaji wa mahakama kuu kwa idadi inayoridhisha na hivyo kuonesha kwa vitendo azma yake ya kuondoa kero hii ya ukosefu wa majaji wa kutosha katika mahakama kuu ya Tanzania.Kero iliyokuwa inakwamisha utoaji wa haki kwa muda muafaka.
ReplyDeleteZaidi ya kushughulikia uhaba wa majaji wa mahakama kuu,Mh.Rais pia ameonesha dhamira yake ya kweli ya kuzingatia usawa wa kijinsia ikiwa ni katika kutekeleza maazimio ya umoja wa Afrika(AU) juu ya umuhimu wa ushirikiswaji wa wanawake wenye sifa katika ngazi mbalimbali za maamuzi.Hilo nalo anastahili pongezi sana.Nina imani(japo sijafanya utafiti wa kutosha)kwamba Tanzania bila shaka ni moja ya nchi chache barani Afrika na Duniani kwa ujumla kuwa idadi kubwa ya majaji wanawake.Ni jambo la kujivinua sana !Hureee! kina mama mliokabidhiwa dhamana hiyo muhimu kuhakikisha kwamba mnatumia uwezo na uadilifu wenu wote katika kutekeleza majukumu hayo muhimu ya kutoa haki kwa raia.
NAOMBA UNIPATIE KANAFASI JAPO KIDUCHU
ReplyDeleteNafikiri hatua ya rais kuteua majaji wapya ni jambo la kupongezwa.
Lakini hata hivyo kuna masuala ya msingi tunapaswa kuyaangalia.
Tuanze na suala la mrundikano wa kesi mahakamani, na ucheleweshwaji wa kesi mahakamani. Suluhuhisho la tatizo hili si tu kuongeza idadi ya wafanyakazi wa mahakama kama Majaji na wengineo bali ni kuangalia mazingira wanayofanyia kazi na vitendea kazi.
Mahakama inatumia bado type writer tena ile ya kutumia nguvu ya binadamu afu tupo karne ya sayansi na teknolojia. Hata komputa hakuna.
Inchi nyingi zina tumia teknolojia ya mawasiliano katika mahakama na inapungiza mrundikano wa kesi mahakamani.
Na siku hizi imekuwa jambo la kawaida kukuta hakimu anaaihirisha kesi kwasababu hana karatasi au kalamu ya wino. Hivi mtu anaweza fikiri ni utani lakini ndo hali halisi.
Mi siongei sana naishia hapa.
Tuteue majaji lakini tuangalie na mazingira ya kazi na vitendea kazi za mahakama zetu.