Na Mwandishi Wetu, Dar

Ikiwa ni wiki moja tangu jopo la majaji lianze kazi ya kuzipitia filamu zilizowasilishwa na watayarishaji wa filamu nchini ili kuwania tuzo za filamu za Vinara (Vinara Film Award), imeelezwa kuwa kumekuwa na mchuano mkali miongoni mwa filamu hizo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mratibu wa tuzo hizo zinazotolewa na One Game Promotion, Khadija Khalili, imetanabaisha kwamba mchuano huo umetokana na sehemu kubwa ya filamu hizo kuwa na kiwango cha juu cha ubora.

"Kazi ya kupitia filamu zilizowasilishwa inaendelea vizuri, hivyo tuna imani kuwa kazi itamalizika kwa wakati uliopangwa... Isitoshe, mchuano umekuwa mkali sana tofauti na tulivyodhani, filamu na wasanii vinakabana koo kwa viwango vya ubora," akasema.

Akaeleza, jopo hilo lilimtumia taarifa ya maendeleo ya kazi hiyo iliyoonesha mchuano kuwa mkali miongoni mwa filamu zilizowasilishwa kuwania tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, huku kazi hiyo ikiendelea vizuri.

Aidha, majaji hao wanatarajiwa kumaliza kazi hiyo Mei 17 mwaka huu na kutoa fursa ya kutangazwa majina matano kwa tuzo zipatazo kumi na tisa zitakazowaniwa huku tuzo ya heshima ikipangwa kutolewa kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa katika sanaa hiyo.

Onesho la utolewaji wa tuzo hizo litakalofanyika Mei 30 mwaka huu, limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt ikishirikiana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Global Publishers.

Wiki chache zilizopita, mratibu huyo alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini za Kitanzania zimewasilishwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo hizo kwa mwaka wa 2007/08.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2008

    Wewe Khadija Toka lini unajua filamu !!!hizo ni (Local Drama ) au michezo tu ya kuigiza kama ile tuliyokuwa tunaiona miaka ya nyuma , kwenye maigizo ila imekuwa advance kidogo .. kutiwa katika motion pictures .. na vikorombwezo.. unaposema Filamu lazima kuwe na realistic , kama mtu anachinjwa unaona anachinjwa ukweli .. au jiji linawaka moto basi ni moto wa ukweli .. hakuna facilities zozote za kuzita hizo ni filamu .. hata hizo za Nigeria ambazo Waafrika wengi tunazitukuza bado sio filamu.
    Kwa mantiki hito hata vile vichekesho vya kina MARTIN , WILLY SMITH , JAIME FOX , nazo ni filamu ?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...