Bro Michu,
Nawatafuta marafiki zangu Joseph Umila and Lord Lugano ambao nimepoteana nao miaka kibao iliyopita. Huyu Joseph nilikuwa nae shule Mlimani Primary last seen 1987 and for Lord last seen him was 1999 pale IFM then akaenda London.
Never seen him ever since I know he is in London but I dunno where, Jamani tuwasiliane thru
____________________________________________________________________
Kaka michuzi,
hongera kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuunganisha watanzania ulimwenguni kote.
Naomba sana unitafutie rafiki zangu popote pale walipo kwa kutumia blog hii inayosoma na watanzania wengi nimepoteana nao long time. Nao ni Adelina/Angelina Mulokozi mara ya mwisho tulikua wote Msimbazi mseto 1992 wengine ni Dorca Charles Nyantahe, cecilia Hamis, Nadra Omary, Blandina Haule hawa tulimaliza wote Kisutu Girls Sec 1996
Naomba tuwasiliane through
-------------------------------------------------------------------------------------------
Msaada kwenye Tutaaz
Kaka michuzi,
Kwanza kabisa nashukuru sana kwa kutupa habari za nyumbani Tanzania. Unautweka katika dunia kwa kiwango cha juu sana, hapa Dallas wenzangu wengi wanapenda sana kuangalia blog yako kupata habari za Uhakika.
Kazi nzuri sana na nakutakia kila la heri katika kujenga Umoja wa watanzania walioko nje ya nchi na walio nyumbani.
Naomba unitafutie marafiki zangu tuliopotezana kwa muda mrefu, Delly mchaga, Aron Mtui , Freddy Washokera , Dennis Mmanga, Bernard Washokera na Erick Mkondya. Hawa nilisoma nao shule ya msingi pale Mbuyuni (Oyster bay, kasha wengine walienda Mzizima Secondary school, Azania sec, na pia Tambaza wakati mimi nilikuwa Popatlal sec Tanga, timu yote hii tulikuwa tunakaa wote mitaa ya Kinondoni,enzi hizo kumekucha sana soko la ma Expatriate, muda mrefu sasa sijawasiliana nao, niliambiwa kuwa wako Uingereza ila sijafanikiwa kuungana nao.
Naomba anayefahamu contact zao au wao kama watasoma hii wawasiliane nami kwenye
Frank Mujuni
--------------------------------------------------------------------------
Salaam sana Bw. Michuzi.
Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuhabarisha mambo mbalimbali yanayojiri katika sehemu mbalimbali.
Mimi ni mpenzi sana wa blog yako.
Bw. Michuzi mimi ninamtafuta rafiki yangu anaitwa Roselinda Maro. Nilisoma nae Zanaki Secondary na tulimaliza mwaka 1995. Mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa siku tuliyofanya mtihani wa mwisho wa kidato cha 4 mwaka 1995. Nimemkumbuka sana. Sijui yuko wapi.
Ningependa kusikia kutoka kwake baada ya miaka mingi. Roselinda Maro, mimi ni Salma Ally tuliyekuwa wote Zanaki mwaka 1995.
Kama utapenda naomba tuwasiliane kwa
Ahsante Bw. Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2008

    wewe unaemtafuta joseph umila wa mlimani primary school pale chuo kikuu karibu na darajani,nipo hapa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2008

    We Joseph hewa. fuata maelekezo vizuri kama hujaelewa uliza. wewe umeoneshwa email address badala uwasiliane nae huko eti unasema "Joseph blabla mimi hapa...."wacha mambo ya ajabu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...