Mpira umekwisha na taifa staa imetoka sare ya 1-1 na mauritius kwenye kutafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia kwenye wanja jipya la neshno. michuano hii inaendeshwa kwa mtindo wa ligi na staaz imepangiwa pia na cape verde na cameroun.
Home
Unlabelled
taifa staa yatoka droo na mauritius
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BORA YA AFADHALI KULIKO POTELEA MBALI.....
ReplyDeletemdau MOSCOW
kichwa cha wandaazimu sie siku tunacheka siku tunanuna, leo tumenuna "AIBU" kushambulia hatujui midfield za tanzania mbovu sana pale ndio panatakiwa tujue kuzuia mtu kutokupita. Midfield ikiweza kuzuia basi mabeki inakuwa kazi rahisi kwao, Taifa Stars tunasindikiza. Nyumbani Point muhimu mwisho tutakuja kubanana na mtu kwa point alafu wanatizama head to head home tunachemsha.
ReplyDeleteTry again jumamosi na cape verde
ReplyDeletekweli man, in the mildfield is where games are won or lost.Halafu draw siyo nzuri, zinaweza kuja kuigharimu timu mbeleni hasa pale itakapokuwa inahitaji points muhimu ili iweze kuvuka na kwenda hatua nyingine.
ReplyDeleteYani hadi hapo tushatolewa! Kama tumeshindwa kuifunga Morishaz nyumbani, hao Cameroun nini kitatupata?
ReplyDeleteWatanzania aibu tupu! Tutatokaje droo na timu kama Mauritius, timu isiyo na jina la soka ulimwenguni. Minadhani wakati wa kutathmini kiwango cha Maximo umefika. Kwanza amekazania wachezaji wake wabovu wlioshindwa hata kucheza ligi ya Umangani. Mi nadhani wakati wa kuwapa Tanzanite Fc chance ya kutuwakilisha, mimi kama mdau hapa US nimewaona hawa jamaa si haba bwana wanakanyaga ndinga.
ReplyDeletePili mi naomnba timu irudishwe kwa kocha mzuri zaidi ya Maximo kama muda amepewa two years??!! Fedha kedkede sasa anachotaka nini?? Kama hamuwezi kuajiri kocha Bora ni bora apewe mzawa kama Charles Boniface Mkwasa, lakini tatizo mkiwapa wazawa mnataka afanye kazi ya kanisa hata shuka za wacgezaji atoe nyumbani kwake. Mpeni timu ahalafu mmwage fedha kama manvyofanya leo hii muone mambo.
Mwisho, tunaomba mtuletee Tanzanite Fc hapa nyumbani sio kutuletea wachezaji walioshindwa majaribio Umangani. Pumba tupu!!
Shabiki Tanzanite FC Bongo!!
Wadau kwa upande mmoja au mwingine mechi zilizobakia kwa taifa stairs kwa zote zimekaa vibaya maana zimu walizopangwa nazo zote ni balaa sasa hapo kwa kufahamu kwangu wanaweza kufungwa mechi zote mbili ila kinachotakiwa kocha wa timu ya taifa ya tanzania apange kikosi ambacho ni wazoefu na hizo mechi sio apange tu kwa vile ni mchezaji mzuri ila inabidi apange kikosi ambacho wazoefu na mechi za kimataifa.....
ReplyDeleteUJUE WATANZANIA KU NA KITU KIMOJA TUNACHO; TUNACHONGA SANA, NA SIYO WATU WAKUCHAMBUA MAMBO KWA KINA.TUNAPENDA MAMBO MAZURI KWA HARAKA NA NI WAVIVU WAKUVUMILIA NA KUFANYA KAZI.KUJIFANYA KUJUA SANA KUMBE HAKUNA LOLOTE. TIMU YA TAIFA IMECHEZA VIZURI NI KWAMBWA KUNA MATATIZO MADOGO YA KIUFUNDI NA MAKOCHA WANAPASWA KUYASHUGHULIKIA. NI LAZIMA KUTAMBUA TIMU YA TAIFA SIYO SEHEMU YA KUWAFUNDISHIA WACHEZA PINU ZA MSINGI ZA KIMPIRA, MCHEZAJI HANAPASWA KUWA AMESHAFUNDISHWA HAYA KWENYE TIMU YAKE AU KATIKA MAFUNZO YA AWALI. KITI KINACHO MKUMBA MAXIMO NI KWAMBA ANABIDI KUFUNDISHA WACHEZAJI MAMBO YA AWALI ILI KESHA ASONGE MBELE KUFUNDISHA UFUNDI WA ZIADA. NA HAWA WACHEZI WAKIWA KATIKA KAMBI YA TAIFA WANAIVA KIUCHEZAJI LAKINI WA KIRUDI KATIKA TIMU ZAO WANASHINDWA KUBAKIA KATIKA KIWANGO WALICHOKUWA NACHO KATIKA KAMBI.KWAHIYO WAKIKUTANA TENA INABIDI KUANZA MOJA TENA.MAXIMO ANAJITAIDI SANA, HILA SISI WATANZANIA MDOMO SANA.
ReplyDeleteNI HAYO TU;
MIMI SALVA
Ushauri wa bure tu kwa MBM soma alama za nyakati.
ReplyDeleteWachezaji walishindwa kabisa kucheza kitimu,badala yake walijisahau na kuingia kwenye mtego wa kujaa kati,mbinu ambayo iliwanufaisha sana wageni.Wageni walikua na flat four ambayo ilijaa watu warefu,lakini bado mipira ilikuwa ikiletwa juu,huku kukiwa na Danny Mrwanda kati ambaye akisimama na beki zao anaishia kifuani.Nilitegemea angewaasa vijana wake watumie sana mawinga ambao wangekua wanaombea mipira pembezoni mwa uwanja kisha kuingia ndani kwa kasi huku wakipiga square passes,kama aliyopiga Uli kipindi cha kwanza,ambayo ilifungua ukuta wa Mauritius,badala yake timu ilitaka sana kupita kati,hata walipoamua kufungua pembeni walitumia saana upande mmoja wa kushoto,kiasi kwamba jamaa waliongeza sana marking upande wao wa kulia.
Kifupi pindi timu inaposhindwa kuleta matunda bora kutoka kwa mafunzo ya kocha,basi kocha anawajibika moja kwa moja.Hasa kama timu inashindwa kutendeneza nafasi za kufunga,au kutumia vizuri nafasi kama za dead balls
Kwa Cape Verde kazi ipo,maana jamaa wale ni sawa na wapo Ureno(wanatumia Escudo(pesa) ya Kireno,na Euro)mpira wanajua japo wamefungwa na Cameroon 2-0 tena goli la pili limefungwa na Eto'o kwa tuta na wapo nafasi ya 107(Tanzania 102) kazi ipo huko Praia
gEoRGe
Bahati mbaya mdau sikujionea mtanange kwa kuwa ughaibuni ila shughuli imekuwa nzito mapema mno. Uzoefu unaonyesha pointi 12 zinatosha kwenda walau Angola kama sio Sauzi. Tusipoangalia, badala ya kumaliza ngwe ya kwanza na pointi walau tano tunaweza kumaliza na pointi tatu tu baada ya kutema hizi mbili. Kuwapiga Cameroon kwenye uwanja mpya katika wiki mbili tatu tukaze buti kweli kweli na kushinda huko Cape Verde wiki ijayo bila kupachika mpira wavuni nayo itakuwa kasheshe.
ReplyDeleteWadau nilioongea nao wanasema eti tulishambulia sana lakini washambuliaji wetu walikuwa wanazionea aibu nyavu, tulikosa penati moja na nafasi moja ya tap in ambayo mshambuliaji alifyatua mnazi akiwa amebaki na lango. Pia tulipata kona lukuki. Ni kweli yote haya nirejeshe matumaini yangu?
Tinoco unaiona changamoto hiyo? Tuandalie washambuliaji wasioona haya kupachika mpira wavuni.
FIFA nao wametutengenezea uwanja wa zamani wa taifa na kutukataza kuutumia. Isingekuwa hivyo tungeng'ang'ania kutumia advantage ya uwanja mbovu kuwafunga wanaokuja. Maji yashamwagika.
Kila la heri wiki ijayo Stars, tutafika tu.
Cameroon take Group 1 lead
ReplyDeleteCameroon striker Samuel Eto'o
Samuel Eto'o was on target for Cameroon against Cape Verde
Cameroon took an early lead in Group 1 of the 2010 World Cup and Africa Cup of Nations qualifiers on Saturday with a 2-0 win at home over Cape Verde.
Captain Rigobert Song got the first goal for the Indomitable Lions after just nine minutes of the game.
Barcelona striker Samuel Eto'o was on target from the penalty spot for the second goal 11 minutes after half-time.
In the other Group 1 game Mauritius held hosts Tanzania to a 1-1 draw in Dar es Salaam.
The visitors took the lead in the 39th minute through Westley Marquette, who was then sent off in the 75th minute.
The Taifa Stars had to wait until the 70th minute before finding an equaliser from Danny Mrwanda.
Tanzania's next qualifier is away to Cape Verde while Mauritius play host to the Nations Cup runners-up Cameroon on the weekend of 7-8 June.
HAYA JK BOYS CAPE VERDE HAO,MTATOKA? AU TUJITOE MAPEMA TUJIANDAE NA CAN 2012?
Hi Bro Michuzi,
ReplyDeleteMaximo unalo hilo...Umelikoroga lazima ulinywe,Draw nyumbani...!!!!,Maana wewe ni kichwa ngumu hauambiliki kamwe.......!!!!!!
Mdau,
USA.
!!!!...Wapi Tanzania One,Juma Kaseja..???!!!,Wapi kiungo Mahiri Haruna wa Mosha..???!!!.Eti unaangalia Umbo la kujaa golini...!!!.
ReplyDeleteduh...tukiambiwa watanzania akili zetu ziko kwenye makalio tunakataa...sasa tungeshinda tungesema maximo kiboko...kadroo leo, maximo hafai.. get educated you people!!! acheni domodomo.. manake kungekuwa kuna domodomo cup basi tz tungeshinda!! badala ya kusapoti, nyie mnavunja moyo... mashabiki inabidi tuzisapoti timu zetu wakati mzuri na mbaya pia... timu inatuhitaji zaidi mashabiki kwenye nyakati mbaya kama hizi...
ReplyDeleteTunataka mabadiliko Maximo amefikia ukomo, tumpe mashindano haya kama michuano yake ya mwisho kisha aende zake . Mtu gani anawasikiliza Rais na Balozi tu. Kwa muelekeo ulivyo Taifa Stars itakua timu ya kwanza kutoka chini,Hata Uingereza walichoka na McLaren sababu ya kutovifunga vitim kama Macedonia
ReplyDeleteMichuzi,vijana walicheza vizuri lakini wadau wengine walivyochangia,nadhani tusiwe na haraka sana.Comments za kuponda sana timu kwa sasa si nzuri.Bado tuna tatizo la umaliziaji.Kocha hawezi kukufundisha jinsi ya kutumbukiza mpira wavuni.Kama mdau mmoja alivyochangia kundi letu ni gumu tofauti na wengine wanavyofikiria.Kinachotakiwa sasa hivi ni wachezaji wa mechi ngumu.Hii michuano ina michuano miwili ndani yake,wachezaji wetu lazima walijue hilo.(kuna angola na south africa2010),timu zimejiandaa haswa.Stars jitahidini kufunga magoli kadri muwezavyo otherwise hata best runners-up tutakosa nafasi,acheni show game,strike yuko na goli wazi anataka kufunga kwa 'lufundi'!
ReplyDeleteTFF:NDO KWANZA WEBSITE HAIFUNGUKI WAKATI HUU AMBAPO WADAU WANGEWEZA KUTOA MAPENDEKEZO YAO HUMO!MNATUKATISHA TAMAA.
MDAU WA UGHAIBUNI:DUNIA SIKU HIZI NI NDOGO,UNGEWEZA KUUNGALIA KWENYE CHANNEL ZETU ZA NYUMBANI ZILIZOKUWA ZINAURUSHA MOJA KWA MOJA TECHNOLOGY IKO JUU SANA,FANYA UTARATIBU MZEE WA KAZI AU ULIKOSA MUDA?.
CHANNEL ILIYORUSHA MPIRA WA JANA:MNUNUE CAMERA ZA KISASA(AUTOMATIC LIGHT REGULATOR),WAPIGA PICHA WALIKUWA WANAANGAIKA SANA MPIRA ULIPOKUWA UNAINGIA KWENYE KIVULI CHA PAA LA UWANJA,KUSABABISA POOR QUALITY YA PICHA.
Maximo haambiliki, anamng'ang'ania Kipa Ivo Mapunda wakati Juma Kaseja yupo, goli gani lile la kufungwa. wakati beki alipobabaika na mpira kipa alitakiwa auwahi mpira kabla adui hajaipata na kumpiga chenga kipa. Kila mechi lazima Ivo Mapunda afungwa goli kizembe'hii ina-tucost sana. Pili, Maximo amemuacha Haruna Moshi kwa sababu ndogo tu, anamuacha mchezaji wa maana ambaye angefunga magoli na kuwaweka mabki mabutu. Ona Athumani Iddi alikuwa benci nje, hakika angecheza tungeweza kupata magoli mengi katika kona 19 tulizopata dhidi ya kona 1 ya Mauritius hakika tungewafunga hawa jamaa. Lakini ndio basi tumeshawakosa nyumbani, kwa sababu ya ignorance ya Maximo.
ReplyDeleteKocha asilaumiwe zaidi ya kuchelewa kumuondoa Emmanuel Gabriel Mwakyusa wakati wa mapumziko.
ReplyDeleteNilivyouona mpira ni kwamba Taifa Stars ilicheza vizuri sana na kushambulia huku wakijaribu kutoka mbali na hata ndani ya 18. Tulikosa nafasi nyingi sana kwani mawinga Mrwanda na Mwakingwe walitengeneza chances nyingi sana. Kona nyingi za Maftah ziliwapita walinzi na washambuliaji wote - nadhani jua lilichangia sana.
Mwakingwe alihangaika uwanja mzima, Mrwanda pia. Mwakyusa nimegundu kuwa ni mzito sana especially in reacting to opportunities. Ile penati naona kama wachezaji wake walimpa ili afute makosa especially baada ya wananchi kuanza kumpigia kelele na kumpigia kelele kocha Maximo amuondoe.
Nilivyo ona mimi ni kwamba Godfrey Bonny bado kidogo na Athumani Iddi Chuji angeanza nafasi yake - mara nyingi ilionekana Bonni kuwa indecisive and kinda slowing down the games movement. Canavaro, Mbuna na Suedi were solid although kosa la Suedi jamaa wakafunga goli - one mistake one goal, na mpaka goli lile linafungwa nadhani ilikuwa mara ya pili tu Ivo kaushika mpira, yaani kaushika mara ya pili akiuokota toka golini. Maftah kwa kiasi fulani mpira ulimkataa, vilevile Nizar hakuwa at his best.
We need a striker though, na wala msiniambie eti Machupa au Mgosi - Machupa alipewa chance yake and he didn't do jack shiit. Mgosi eti kwa vile alikuwa mfungaji bora wa Taifa cup where 5 goals from one game against a hapless and over matched Lindi team. So too for the call of Juma Kaseja - naye sio kwamba mzuri saaaana, la hasha, naye mbovu tu, kipa gani unafungwa magoli 17 na klabu moja tu?
My two cents.......
Wadau wanaomlalamikia Maximo wapo sahihi na mimi naona tusiwapuuze wale wote wanaotoa shutuma kwa Maximo, kwa sababu tukikaa kimya Maximo hataumia ataona hawa waTanzania wanaona poa tu hata tukifungwa hawalalamiki.
ReplyDeleteMaximo anapaswa kulaumiwa sana tena sana tu kwa mambo ambayo anayafanya yeye pamoja na benchi lake la ufundi.
Tuanze na game ya jana:-
Hivi kweli jamani Tanzania tunaweza tukabanwa na WAHINDI KOKO wale?? watu hata kukimbia vizuri hawawezi eti leo wanakuja kutukomalia nyumbani kwetu mbele ya mashabiki zaidi ya 20,000???
Hiiniingii akilini hata siku moja, kulikuwa na sababu gani za kumuacha Emanuel Gabriel aendelee kucheza ilhali mpira ulimkataa kabisa ukizingatia alikuwa majeruhi hakuna na mazoezi kwa wiki nzima leo unamuacha anacheza alafu hakuna anachokifanya uwanjani.
Kulikuwa na sababu gani za kumuweka Athumani Idd (Chuji) benchi while Nizar Khalfani mpira ulikuwa umemkataa??
Ubishi na ubabe wake wa kutaka kufanya mambo kivyake vyake bila kusikiliza maoni ya wadau na wapenda michezo hatutaifikisha popote nchi hii kwenye medani ya soka.
Akiendelea kuwasikiliza hao akina Mwakalebela na kina Tenga pekee ilihali kwa sababu wao ndo wenye kushika uongozi wa soka hapa nchini ipo siku tutawachapa bakora hapo hapo uwanjani maana haiyuingii akilini kuona tunalipishwa kiingilio kikubwa kuja kuiangalia timu ya Taifa ilihali mnapata udhamini wa hali ya juu kutoka Serengeti breweries na NMB alafu matokeo yanakuwa ya kutuumiza kila siku alafu nyie mnanenepeana mashavu kw akukamua kitimoto daily.......
Ipo siku hamtatoka uwanjani mnawajua fika watanzania walivyo walevi wa mpira sasa endeleeni hivyo hivyo... mifano mmeiona vizuri si mara moja au mara mbili timu zinapata misuko suko hapo uwanjani sasa mnapaswa kuzingatia ule usemi wa wahenga kuwa KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
ANGALIZO:-
RAGE ARUDISHWE HARAKA IWEZEKANAVYO HAPO TFF, YEYE ANAJUA MBINU NYINGI NA ANAKUWA KARIBU NA WACHEZAJI MOST OF THE TIME AKIRUDI HAPO KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WENGINE HAKIKA TUTAPIGA HATUA.
LAKINI MKIBAKIA KUMBANIA KWA KUHOFIA ATAKUJA KUFUMUA MAOVU YA UFISADI WENU BASI MKAE MKIJUA MTAENDELEA KUPATA MATOKEA MABAYA NA WATANZANIA TUTACHOKA.
Mdau uliyetoa maoni Tarehe June 01, 2008 10:25 AM, Mtoa Maoni: Anonymous, naomba utufahamishe wadau tulio ughaibuni chombo gani kilionyesha mechi hiyo ili tuweze kujitega wikendi ijayo. Toka jumptv watutose mambo yamekuwa si mambo.
ReplyDeleteKuuliza si ujinga, nimesoma magazeti ya bongo yaliyopo mtandaoni, sijaona hata moja likitumia JK Boys kufuatia matokeo ya mechi ya jana. Ina maana timu isiposhinda ndio inakuwa ya kwetu, sio?
Jamani mwacheni maximo. Tanzania hakuna vipaji kabisa hao mnaowasifia hamna kitu.Hata akipewa Ferguson hii timu bado kabisa wameshazeeka na hakuna kitu. kwanza wengi wao ni BANGE tu hata stamina hawana. mtu anatuliza mpira na ugoko... baaado sana. Maximo anajitahidi kufundisha lkn ndo hivyo jamaa washazeeka hawawezi kujifunza kitu.
ReplyDeleteTusidanganyane Angola haendi mtu wala South Africa. safari ni ndefu na wala hakuna shortcut.
Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hizi taarifa zinazosema kuwa wachezaji wa klabu mojawapo wameleta fitina na hujuma za utani wa jadi katika suala hili la kitaifa?
ReplyDeleteSio mseme kwamba wa tz wanapenda sana kuchonga mdomo hapa tunaeleweshana kila mtu afahamu kuna mdau kasema kwamba etii MAXIMO timu anainoa vizuri wakienda kwenye clab zao wakirudi wanakuwa wamesahau mpira ambao wamefundishwa sasa hao wachezaji wa aina gani unafundishwa kitu alafu unasahau basi maximo achukue wachezaji ambao ataweza kuwafundisha mpira na wakaelewa kwa ujumla tuseme kwamba tanzania mpira hatuna ila hapa inabidi tuwatengeneze wachezaji wazuri ambao watacheza mpira na wataweza kuelewa nini wanaambiwa ila tukisema tuwalaumu wachezaji na KOCHA kwa nini hawakumpanga huyu akampanga yule mimi naona kwamba hamna sababu ya kuongea hivyo kwasababu hamna kocha hapa na kocha wetu anaakili ndio maana akampanga yule na akamuacha ATHUMANI IDDI na anajua nini anafanya na alishafatilia mchezo wa mauritus na kawajua wale wachezaji wapo vipi na inabidi apange vipi wachezaji wake ili waweze kukabiliana nao.....Na pia labda nitoe mfano hai kwa nini nimesema hivyo tuangalie kwanza mechi ya Chelsea na Manchester United final champion Moscow Fargeson si mnaona jinsi alivyopanga kikosi chake kwasababu ronaldo ilibidi acheze na A.cole lakini angalia fargeson alivyobadilisha mchezo Ronaldo akaja kumpanga na Essien maana alijua kwamba nikimpanga na A.cole Ronaldo atapata tabu sana na hataweza kufanya kitu sasa hapo ndio tuone maximo kwa nini alimpanga ule mchezaji akamuacha benchi ATHUMANI IDDI mchezaji ambaye mnalaumu kwa nini alimpanga kwa hiyo mimi kwa mtazamo wangu ni vizuri sana tuangalie na tuujue mpira sio tunaongea bora tumeandika comment kwa michuzi na yule ndio maana akaitwa kocha anambinu nyingi sana za kuweza kupanga wachezaji wake na kuweza kufanya vizuri katika michuano ila sisi tusiojua tunaona kama kafanya makosa mimi sioni makosa aliyofanya ila cha kufanya hapa inabidi wachezaji wetu wajitahidi sana katika mechi zilizobaki maana ni ngumu sana kwetu...
ReplyDeleteHII TIMU YENU HATA ICHEZE NETBALL,CHAPADUNDA,GOLOLI SIJUI BAO ITAFUNGWA TUUU!!!!!BANGE NDO SABABU!WACHEZAJI WANAONA MIPIRA DOUBLE DOUBLE HALAFU THEY PICK THE WRONG ONES!MTASHINDA KWELI? HATA MCHEZE NA KINA AUNT NANIIII....!!
ReplyDeleteHALAFU HUYU ANAYEFANANISHA MECHI YA CHELSEA NA MAN U NAYE BANGE TU!!!
MAXIMO NI KOCHA WA TIMU ZA DARAJA LA PILI HIVYO UWEZO WAKE HAPO UPO KIKOMO, HUYU BWANA NI MJANJA SANA KWANI UKIMUULIZA HUJIFANYA HAIWEZI KUJIELEZA VIZURI KWA KIINGEREZA LAKINI HIZO NI MBINU TU ZAKUTUPIGA MABAO AENDELEE KUKAA BONGO.
ReplyDeleteWACHEZAJI STARS:Kombe la dunia/Africa siyo mchezo,inabidi mkomae hasa siyo uzembe na show game kama mliofanya juzi uwanjani,inatakiwa bidii sana.Na Tanzania tuna bahati michezo yote iliyochezwa weekend hakuna timu iliyopoteza mchezo.
ReplyDeleteMchezo wa mwisho jana usiku kati ya Egypt na DRC ulifanana kabisa na wa kwetu.Hadi halftime DRC ilikuwa inaongoza 1-0(Cairo).Kipindi cha pili Misri walibadilika mbele ya mashabiki wao.Wakarudisha goli na kuongeza jingine.Nawatakieni safari njema ya Cape Verde,hatujakata tamaa.
JUNI 1 5:16PM TIMU YA TAIFA INA JINA MOJA TU, HAYO MENGINE SI UNAJUA BONGO TUNAVYOPENDA KUJIKOMBAKOMBA NDIYO MAANA IKISHINDA UTASIKIA WATANGAZAJI NA WAANDISHI WA HABARI ILI WAKUMBUKWE NA MHESIMIWA BASI HUMKOSHA KWA KUIITA TIMU JK BOYS, HUO NI USANII TU WA BONGO, HAIJATOKEA HATA SIKU MOJA IKASHINDWA WAKAIITA JK BOYS.
ReplyDeleteBahati mbaya soka ni mchezo ambao hauna demokrasia ya kweli. Haiwezekani penati akose John Terry halafu awajibike A. Grant au penati akose Gabriel halafu muanze kumsema Maximo. Ni kweli kocha wetu wa timu ya Taifa ana tatizo kubwa la kuusoma mchezo ila kuna haja pia ya kukubali kwamba mpira wetu bado upo chini na uwezo wa wachezaji wetu kufanya yale wanayofundishwa uwanjani ni mdogo sana. Kuna baadhi ya indicators zinazoonyesha, mfano ligi kuu ya Bara iliyokwisha hivi majuzi mfungaji bora ni Mganda somebody Katende akifuatiwa na Mkenya anayechezea Yanga, pia nakumbuka mara ya kwanza kabisa alipowasili Maximo alipenda sana uchezaji wa Edwin Mukenya ila akaambiwa kwamba sio Mtanzania. Nadhani mambo yanayomkuta Maximo ni kama ya Capello, nakumbuka baada ya Premier Leagues kwisha Capello alidai amevutiwa sana na Cesc, Cristiano na Torres ila anasikitika sio waingereza! Tuandae wachezaji wetu wakiwa watoto vinginevyo hata akija bingwa wa vipaji A. Wenger hakuna kitu. Tujiulize kwanini wazazi wetu walitupeleka shule tukiwa wadogo halafu TFF inasubiri kijeba kitoke huko Nangurukuru kinaitwa timu ya Taifa hakina basics za football. Tutabakia Aaaah, aaaah. ayaaa mpaka mpira unakwisha!
ReplyDeleteKUNRADHI BRAZA MICHU NA WADAU,MIMI NDIYE NILIYEANDIKA JUNE02,2008 10:45AM.NILIKUWA NAMAANISHA HAKUNA TIMU ILIYOPOTEZA MCHEZO WA NYUMBANI KWA MICHEZO ILIYOCHEZWA.KUNRADHI NILIKUWA BADO NA KIZUNGUZUNGU CHA WEEKEND,SI UNAJUA MAMBO YA WEEKEND USTAADHI,ARUSHA VIPI?
ReplyDeleteTatizo sio maximo wala wachezaji, tatizo ni kwamba mfumo mzima wa football Tz ni mbovu. TFF hawafanyi lolote kujenga mazingira ya kukuza michezo zaidi ya majungu, upendeleo na kikubwa wanachoshabikia ni kutangaza viingilio vya mechi maana huko ndio kwenye ulaji.Mfano waliruhusu Yanga kumfungia ivo kwa majungu lakini wakakataa simba kumfungia chuji kwa utovu wa nidhamu. Tukitaka kuendelea kimpira lazima mpira uendelezwe mashuleni na pia TFF iwe makini kusimamia vilabu hasa vikubwa vya ligi kuu kuona kwamba vinaongozwa kitaalamu,pia viongozi wabovu wa michezo watimuliwe.TFF irekebishwe kusiwe na mlolongo wa kamati zinazotoa maamuzi tofauti juu ya jambo moja mfano mechi ya simba na coastal iliamuliwa zaidi ya mara tatu na kamati za tff. ule ni upuuzi. Maximo pia nina wasiwasi na ujuzi wake kwani kocha mzuri ni yule anaeweza kumbadilisha mchezaji hata kitabia sio kumuapia mchezaji kuwa hawezi kuitwa timu ya taifa akiwepo (haruna moshi) na kaseja. Nawasilisha
ReplyDeleteJ4 udsm
Tunisia 1-Burkina 2(Rades,Tunisia).Siyo ajabu hata kama tanzania ingepoteza mchezo huo nyumbani.That is football.Leave Maximo alone.Burkina ni timu pekee iliyoshinda ugenini tena kuishinda Tunisia kwao.Wakati Tanzania alimfunga Burkina home and away!!!Teeeh teeeh.Mpira wa miguu ni mkitu kibaya sana
ReplyDeleteNAWAPONGEZA WADAU WOTE WALIO CHANGIA MADA HII KWA WINGI INAONESHA UNAVYOTIA UCHUNGU,KWA NILIVYOUONA MPILA TIMU ILIONESHA KUCHEZA KAMA TIMU INAYOFUNDISHWA,MAANA ILIWEZA KUTENGENEZA MASHAMBULIZI KWA NJIA YA PEMBENI NA NJIA YA KATI HILI NI MUHIMU MAANMA TIMU NYINGI UTUMIA MFUMO MMOJA KTK KUSHAMBULIA ILA TATIZO NI KUTUMBUKIZA MPIRA KTK NYAVU JAMBO AMBALO MAXIMO LAZIMA AWAJIBIKE NALO MAANA FINAL SCORE ALIKUWA NI GABRIEL NA TUMESHUHUDIA ALIKUWA NJE YA KIWANGO ALITAKIWA KUPUMZISHWA TOKEA DK 35 YA MCHEZO SABABU BIASHARA HASUBUHI.HIVYO KWA KUWA BADO TUNA MUDA AWAHI MAREKEBISHO KABLA YA GHARIKA YA AKINA ETOO KUTUFIKIA
ReplyDelete