Kaka Michuzi,
Habari za leo, na hongera sana kwa blog yako ambayo imekuwa msaada mkubwa sana kwa watu mbalimbali. Mimi ninaomba unipatie e-mail ya yule dada ambaye anaishi Italy na mume wake ni muathirika,lakini anamlazimisha waendelee kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kinga.
Kwa nini ninaomba e-mail yake wakati yeye amekuomba uiweke kapuni?: Mimi Bwana Michuzi mwaka 2006 niliwahi kuwa na uhusiano na msichana ambaye baada ya kwenda kupima alikuwa ameathirika,halafu pia nina ndugu yangu(Mwanaume) ameathirika lakini mkewe na watoto wanne hawajaathirika,hivyo basi nafikiri nitakuwa msaada mkubwa sana kwa huyo dada.
Kwa kuwa yeye amekuomba e-mail yake uiweke kapuni,basi si vibaya umtumie e-mail ya kumuomba kama unaweza kunipa e-mail yake ili nimpe ushauri lakini kwanza ukimueleza experience niliyonayo kuhusiana na gonjwa hili.
Nimeona haitakuwa vizuri sana nikimshauri kupitia blog yako kwa sababu watu wengi wanasoma hii blog na haya mambo ni ya ndani,si ya ndani kwa sababu nataka kufichwa ukweli kuhusu janga la UKIMWI kama ambavyo watu wengine wanavyokufa na ukimwi halafu ndugu zao wanasema amekufa na malari!! La asha,ni kwa sababu yeye dada ni mke na wa mtu,nafikiri ndio sababu hata yeye hakutaka jina lake na e-mail yake uiweke kwenye blog.
Pia naomba e-mail yangu hii husiweke katika blog yako.
Nategemea nitapata jibu 'positive' katika kumsaidia huyo dada.
MUNGU AKUBARIKI,
Mdau Majaliwa.


Mithupu watch out..asije kuwa jamaa mwenyewe ndo anataka kuhakikisha kama ni mke wake katuma huo ujmbe kusudi amfanyizie..please watch out.
ReplyDeleteKila lakheri,
Kaka Issa pamoja ya yule dada aliyetaka msaada nawashauri msitoe e-mail kwa huyu jamaa kwani inaonyesha huyu huenda ndiye mume wa huyu dada na kama akipata hiyo mél inaonekana anaweza kufanya kitu mbaya. kwa maelezo yake kwamba kaka yake ameathitika na mkewe na watoto wanne hawajaathirka inaonekana huyu ndiye mwenyewe. Michuzi WATCH IN na siyo OUT
ReplyDeletemdau majaliwa mimi ningeomba uweke huo ushauri wako hapo na sisi tuweze kufaidika nao kwani huu ugonjwa si wa kwake peke yake ni wa jamii kama leo umemkuta yeye kesho utaweza kunikuta mimi hivyo ni vizuri tukawa tunafahamu ni njia zipi tuzichukue
ReplyDeletenitashukuru kwa hilo nawasilisha
mh! kaaazi kwelkwel!
ReplyDeleteNafikiri anon 4:22 umeona mbali.
Japokuwa huyu jamaa ameandika kwa busara, pia uwezekano wa mtego pia upo; maana internet kwa kweli inachanganya sana watu.
Mimi nashauri kuwa huyu jamaa (Bwana Majaliwa-mtoa ushauri) aandike huo ushauri binafsi kwa kirefu kwa Michuzi (ila usiwekwe kwenye blog).
Baada ya hapo ni jukumu la Michuzi kutuma hiyo email kwa huyo dada. Hapa Michuzi tunamtumia kama mficha siri.
Hapo Michuzi ataficha email ya huyo dada, ila awe makini naye asije-forward hiyo email tena katika kuendeleza mawasiliano; maana address itaonekana.
Nikufanya copy & paste text only (no addresses)
Poleni sana!
Mdau namba moja inawezekana kabisa,ushauri mzuri, au anaweza akawa anamtumia mtu mwingine,au email tofauti, MICHUZI,MWAMBIE AKUPE NAMBA YA SIMU,HALAFU DADA AMPIGIE yaani MPE DADA SIMU YA MTAKA KUTOA USHAURI,ni kwa NIA nzuri tu ya kutaka KUMLINDA dada yetu.Na kama ni si hivyo BASI MDAU/MSHAURI,sina nia mbaya nakupongeza kwa moyo wako wa kutaka kusaidia.
ReplyDeleteUsa.
Chonde chonde michuzi! huyu jamaa asijifanye anajua kushauri kwa siri. Dada ameomba ushauri hadharani sasa yeye anajifanya anataka kumshauri kwa email hapo sas ni wapi. Asije kuwa ndo bwana ake. Michuzi usithubutu kumpa email ya huyo dada kwani hili linaonekana tapeli kubwa.
ReplyDeleteDuh hapa Michuzi chunga sana, huyu ni yuleyule mwanaume mhusika anasaka hiyo email ya huyo dada kwa "mlango wa nyuma" ili athibitishe mambo yake apate ushahidi wa kwenda kumfanyizia. USITOE EMAIL YA MTU. Kama ni mtu mwingine kweli anataka kutoa ushauri atoe hapahapa huyo dada atausoma na wengine watafaidika pia.
ReplyDeletethis is a smoke screen... michuzi lakini jamaa kakwambia usiweke huo ujembe hadharani. duh
ReplyDeletepeople people people! acheni unafiki.jamaa wa watu wants to offer help.if you dont know,then shut up please
ReplyDeletewe unaetaka kutoa ushauri kwa siri acha ubinafsi. unajua fika kuwa janga la ukimwi ni la taifa. Sasa kwa nini usimwage ushauri hapa ili wenye matatizo kama hayo wanufaike? We mwaga ushauri hadharani ili watu wenye matatizo wajue nini cha kufanya.
ReplyDeletekaka Nina mambo yafuatayo:
ReplyDeleteInawezeka wewe ni msaada mkubwa kwa huyo dada na wala tusikufikirie kuwa una nia mbaya ila:
Huyo dada ana tatizo kubwa sana tu ila aelewe kuwa kuna wapo wengine wana matatizo kama hayo au yanaweza fanana na hayo au makubwa kuliko hayo wengine humu humu bloguni.
Sasa Twajua wewe wataka kumsaidia huyu dada ila. Tunakuomba mpe msaada humu humu ili wengine wenye matatizo wapate faida.
Sababu Tunaangalia unaweza ukawa msaada au matatizo zaidi. watu wengi ma anony humu ndani hatujuani tunamwaga radhi tu
So our dear br. mpe msaada dada yetu hamna siri humu kila mtu amekua humu ndani hamna mtoto akiwepo atajiju, tupe mambo aelimike na tuelimike Pls.
Tunakuomba
mdau
Anna
Nina uhakika kwa asilimia 98 ya kila anayeandika au kusoma comment au hata kupitia tu blog hii ame-experience kwa namna moja au nyingine na hili gonjwa yaweza kuwa mdau mwenyewe, mtoto, mke/ mume, mama/baba, dada/kaka, wifi/shemeji, baba mkwe/mama mkwe, ndugu yeyote, rafiki au bosi wake kazini au mtu yeyote yule aliyepata kumfahamu na ubaya wa tatizo hili haliishi linaendelea kutukumba tu mpaka wa mwisho wa maisha yetu. Kifupi mdau naomba uweke ushauri wako humu kwa kuwa utakuwa umetusaidie wengi, Mungu akubariki na akupe roho ya ukarimu ya kuweza kusaidia wengine ambao hatukujaaliwa "guts" za kuomba msaada humu
ReplyDelete