wabongo sita, wakiwemo mabondia wanne, inasemekana wametiwa mbaroni huko mauritius leo asubuhi kwa kile kilichoelezwa kukutwa na madawa ya kulevya.
kwa mujibu wa tovuti ya http://www.defimedia.info/ watuhumiwa hao walikamatwa na kikosi cha kuzuia mihadarati na kwamba watafikishwa mahakama ya Mahébourg mchana huu na kustakiwa kwa kukutwa na mihadarati.
huo unaweza kuwa ndio mwisho wa safari ya timu ya taifa ya ndondi ambayo iko huko kwa ajili ya kushiriki kwenye ubingwa wa afrika, kwani timu yote pamoja na kocha wao imehusishwa katika kashfa hiyo.
pichani juu shoto ni bondia emilia patrick ambaye ndiye bondia pekee wa bongo ambaye anatakiwa atuwakilishe kwenye michuano ya olympic huko beijing. wa chini yake ni kocha nassoro michael na kulia chini ni petro mtagwa. majina ya wengine hayakupatikana mara moja.
Kwa mujibu wa waandaji wa michuano hiyo wamesema tukio hilo halitoathiri mashindano hayo, ila tanzania ndio imeshajitoa yenyewe..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2008

    Ni kweli,nimelisoma hilo gazeti(la kifaransa).Box nne wamedakwa nazo leo asubuhi.Jamani jamani aibu gani tena hii nyie wanamichezo yetu na bendera yetu??Na mnafungwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2008

    Yana thamani ya Rs(?)millioni 40(Rand?)

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2008

    Poleni sana lakini kama ni kweli mmekutwa na hayo madawa ya kulevya mmefanya jambo baya ambalo pia limeibisha nchi pamoja na fani yenu. Nadhani tamaa zimewaponza kwa kutumiwa na watu ili mpate pesa lakini matokeo yake ndiyo hayo ni kuambulia mvua kadhaa jela. Huu ni uhalifu ambao hata tanzania haukubaliki kwani mnashiriki kuteteketeza hiki kizazi lakini pia kuongeza uhalifu na hili nadhani litakuwa funzo kwa wanamichezo wengine. Hapa nadhani mtaungana na timu ya Zombe na kasusura. Wizara inabidi ichunguze vipato vya wadhamini pamoja na mapromota hii michezo kwani wengi wao wanajificha kwa kivuli cha ufadhili

    ReplyDelete
  4. AMINA CHIFUPA UPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO. MAMBO YAKO SIO MCHEZO NIMEYAKUBALI. KEEP IT UP

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2008

    Naam,na kweli hao ndio wawakilishi halisi wa kibongo ughaibuni!!!au ndio wanachama wapya wa tawi la Livapuuu hapo kwetu!??

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2008

    Kama ni kweli basi ni aibu sana, ndugu zangu tutaacha lini tabia za kutaka kutajirika haraka haraka namna hii. watanzania wengi wako katika jela nying nchi za nje kwa makosa kama haya na bado hatujifunzi kutoka kwa wenzetu. Nawapa pole member wa familia zao. Jambo moja sasa basi wale jamaa wa kalamajuu wafanye fanye wachangishe pesa kuwapatia hawa ndugu zetu mawakili wazuri. kusema kweli hawa ni masikini zaidi ya yule mama alie huko.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2008

    Mh! hii aibu sasa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2008

    aibu kaka hiyo hebu fatilia kwa karibu hii habari utupatie up to date mara kwa mara ,.najiuliza hao mabondia waliondoka vp hapa bongo au ndio hatuna ulizi wa kutosha?? watu wa kitengo cha madawa vp walikuwa wamelala?? au ni zengwe wamefanyiwa?? MICHUZI TUAMBIE MZIGO SI KG NGAPI?? AU SAMANI YAKE??

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2008

    Ajali kazini

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2008

    AIBU KWA TANZANIA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2008

    braza michu,hii kali sana hawa jamaa tulidhani wanatuwakilisha watanzania kumbe wanatuaibisha!nimesoma link hiyo juu nimeshindwa kuelewa chenji 40m kulingana na dola kama ni kweli basi jamaa wanastahili kuwa huko.na kama wamechomekewa sina la kusema zaidi ya pole.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2008

    Hiiiii!!! hiyo hisiwe mbinu maana kisiwa chenyewe ni maarufu kwa fitina kumejaa wadosi hisiwe ni mbinu ya kututaka tuwanunue mabondia wetu kwa fedha nyingi kama kitega uchumi!???hapo kidogo tua mashaka Martius wakenya wengi na wabongo wapo jela kwa makosa yakusingiziwa

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2008

    Hivi hawa wana kichaaa!!nani aliwadanganya wabebe madawa ya kulevya?hata ukiona sura zao zimekakakaaa ki ninja ninja tuu..jamani kila mtu aende shule akasome hilo ndio langu jambo...wasekwe ndani hao,wametutia aibu sana taifa letu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 14, 2008

    Kaka Michu hii ni aiBU kubwa sana kwa Taifa letu. Yaani wawakilishi wa taifa wanakutwa na mihadarati tena wakiwa wamebeba bendera ya taifa!! Nadhani inanipa wasiwasi na kupata changamoto ya kufikiri kwamba inawezekana ndio ka machezo ketu haka,labda ndio arobaini imefikia kwa hawa jamaa. Labda hata timu zingine huwa wanabeba mihadarati na inawezekana kabisa ni biashara ya hawa wanaojiita wafadhili na ni lazima serikali itakuwa na taarifa kwa namna moja au nyingine. Afadhali imejulikana, shame on you timu ya ngumi na viongozi woote wa michezo hapa Tanzania!! Aibu sana!!

    Kaka Gee, Arusha.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2008

    bongo njaa kali

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2008

    wala sishangai, serikali haiwaangalii wao wanaangalia mpira wa miguu tu na mauritius soko zuri, kilo mpaka elfu 80 dollars kwanini wasijaribu, yote maisha, bahati haikuwa yenu tu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 14, 2008

    Since I dont have anything nice to say let me.........Okei

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 14, 2008

    Haaah!! Ama kweli Bongo hali ni mbaya ya kiuchumu, hii yote ni njaa maana mafisadi wamekula kila kitu kiasi kwamba hata wawakilishi wetu wanapopata fursa za michezo km hawa akilini wanafikiria dili tuu, na tena dili zenyewe za hatari, poleni sana, japo mmetuaibisha, lakini tunaelewa, sasa serikali ikawakamate wanaoleta uchumi mbovu na kuathiri ndugu zetu wengi, hao ni baadhi tu na wachache saana kati ya wengi wanaodumbukia katika misukosuko km hii japo hawatangazwi....Poleni saana, na tunaomba ubalozi wetu huko uwasimamie na kuwadhamini.
    Mungu ibariki Tanzania na walaani Mafisadi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 14, 2008

    Presumed innocent until proven guilty.
    Mauritius imeamua kuilia dipu Tanzania mwaka huu, undava undava tu!!! Hapo wengine walienda haja hovyo kwenye uwanja wetu mpya.
    Taifa Stars mtakapoenda huko inabidi mtoe kipondo cha mbwa mwizi, inaanza kuwa tabu sasa.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 14, 2008

    Huyo bondia ndio yule tulikuwa tunaombwa watanzania tumchangie aende kwenye olympic?Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 14, 2008

    Wenye udaga wako Bongo.Aibu tupu kwa taifa,vigogo, taifa stars,ndondi,scouts,wanariadha.Haya kazi ipo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 14, 2008

    haya yote ni matikeo ya matatizo ya kiuchumi yanayosababisha njaa na tamaa kwa wabongo wengi, ila wameliabisha sana Taifa letu na sekta ya michezo kiujumla.
    Lily - DSM

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 14, 2008

    Hi kaka Michuzi. Leo katika baadhi ya magazeti kuna habari ya Mbunge mmoja wa Bunge letu aliyekuwa anawanga Bungeni akimwaga uganga kwenye viti vya wenzie na kamera zikamkamata. Magazeti hayajasema ni nani laikini mimi kwa utafiti wangu nimegundua kwamba ni Bwana Vijisenti. Je habari hizi ni za kweli

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 14, 2008

    nimepokea kwa masikitiko makubwa sana hii habari kaka Michuzi,Tanzania inakwenda wapi hasa huyu kocha Nassoro Michael ni afisa mkubwa wa Jeshi kuingilia biashara ya ujinga kama hiyo kama ni kweli pia amliaibisha jeshi letu

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 14, 2008

    Hakuna cha njaa kali wala nini. Mshenzi ni mshenzi tu. Watu wanuza madawa marekani na ulaya na hawana njaa kali wala nini na wala hawatosheki kusema wataacha.

    Hawa ni watiwe jela for life. Wanatuharibia vijana wetu na madhar tunayapata wote. Kila kona ni mateja kwa kwenda mbele. Siwafagilii hata kidogo. Washenzi wakubwa.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 14, 2008

    Kama alivyo sema hapo mwenzangu, boiashara ya madawa ni tamaa ya pesa za haraka na nyingi.

    Tabia ya kubeba ma dawa kwa wana michezo haswa mabondia ni sio kitu kipya, nilisha wahi kutana na bondia aliye wahi kwenda Thailand kwenye shindano na aliniambia alibeba madawa so sidhani ni jambo jipya ni lipo na lina fanyika sana.

    Nadhani uanze kuwa sikitikia hawa jamaa pale ambapo mtu wa karibu yako au hata mtoto wako awe ana tumia madawa ,ndio utajua uzuri wa madawa na nadhani uta wasikitikia sana hawa jama kwa kufanya kazi nzuri ya kuingiza madawa , ingawa hatuna cha kusema sababu hatujui mazingira halisi na bado hawaja kutwa na hatia mahakamani.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 14, 2008

    Jamani huyu wa kwanza na wa mwisho mbona wana fanana ? hizo pua mashavu naona zina fanana sana ni ndugu? kama ni ndugu what a loss!!!! yani two brothers.....oh gosh

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 14, 2008

    Really saddening for many obvious reasons. In addition to that, I personally knew Nassor Michael having seeing him in the ring on several occassions in the mid and late eighties - twice or so he was up against mighty Cubans. I recall him winning one of those fierce encounters. Surely, this, if true, is an adverse addition to his otherwise brilliant CV...

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 15, 2008

    A Kenyan woman in Mauritius has been arrested along with two Tanzanian boxers and four officials after they were busted trying to smuggle heroin worth a reported USD $1.8 million into Mauritius.

    The woman, whose name has not yet been released, appeared to be the contact in Mauritius for the Tanzanians who had just arrived in the island for the African boxing championships with the heroin. They were arrested as they attempted to hand over the drugs to the Kenyan woman by placing them outside near their hotel.
    Source:http://breakingnewskenya. wordpress.com
    Mdau
    Port-Louis

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 16, 2008

    dont be ridiculous you whiney people

    first of all wewe TUMAINI sasa unasema marehemu amina chifupa amefanya mambo yake for what purpose?

    second mnaolia aibu aibu mnajua watu wangapi na raia wa wapi wanakamatwa na madawa kila siku.mnalia lia aibu ya nini.aibu kama ingekua baba yako.kila mtu anavuta mibangi siku izi,sijui mnabung'aa nini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...