Ushindi huu mkubwa wa Fc Kilimanjaro ni mafanikio ya ushirikiano mzuri kwa watanzania waishio Sweden.

Sherehe za kusheherekea ushindi huo zitafanyika hapo Ubalozini siku ya tarehe 14 june 2008 kwa nyama choma, munakaribishwa watanzania wote.


Jee...Fc Bongo ya Finland mumeshajitayarisha????
musisahau kuja na kapu lenu..!!!
www.kilimanjaroclub.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2008

    michuzi sherehe gani tena, huu ubalozi unatakiwa kushtakiwa umekiuka haki za binadamu ni wa kushtakiwa, michuzi unatoa taarifa za sweden, wana makosa ya jinai na inatakiwa kushughulikiwa haraka, nawakilisha usibane.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2008

    F.C.BONGO Chinjachinja tunanoa sasa hivi. Jumamosi ya tarehe 14 mwezi huu tunawakaribisha TAS ya Tampere. Baada ya Hapo Tuna mechi za kirafiki na Gambia na Siera leone kabla hatujaingia kwenye Tournament ya Prevention Cup mwezi wa saba. Mwezi wa nane tarehe mbili tutazuru Tampere na Tarehe 16.mwezi wa nane Tunawasili stockholm na Viking Line. Kilimanjaro kaeni mkao wa kuchinjwa teyari!. Khalifa nitakupigia hivi karibuni.


    Ezza.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2008

    We annon wa kwanza mbona hueleweki? embassy ya Tanzania imefanya nini? mbona sijasikia chochote kuhusu ubalozi wetu? Hebu toa details basi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2008

    Wewe anonymous wa kwanza hapo juu, unalalamika kwanini michuzi anaweka habari za sweden, kwanini usifungue blogu yako ikaiwekea sheria. Unalalamika kuwa ubalozi wana makosa ya jinai, unao uhakika huo kuwa washapatikana na hatia hiyo?. Uko teyari kujibu maswali haya ukihitajika?. Usiwe na wasiwasi tunakujua wewe ni nani ukihitajika kuyaeleza makosa haya ya jinai tutakufuata. Kuhusu hizo sherehe zinazofanyika hapo ubalozini, Ubalozi umefanya vizuri kuwapongeza vijana wetu wa Kitanzania.

    B.M.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2008

    aaaaaaah kilimanjaro fc kazi ipo kweli kweli,ila wachezaji waliotoa jasho mpaka kupata hilo kombe hawapo umeweka picha nyingine kabisa kama meddy,jameel,willy john,kablau,richard meddy was uppsala na hao sio waliokua kwenye kikosi cha kwanza

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2008

    Tunawapongeza sana watanzania wote wa huko Sweden pamoja na nchi nyinginezo za Scandinavia.Lakini msisahau kupitisha michango yenu huko muweze kuwasaidia ndugu zenu huku nyumbani katika nyanja mbalimbali vitabu mashuleni,makompyuta hata yaliyotumika yapelekwe mashuleni,ujenzi wa madawati na vyumba vya madarasa,walimu wa sayansi,visima virefu vya maji salama vijijini,mashine za viwanda vidogo,solar panels,windmills,karakana za vijijini,matrekta japo kuukuu kwa ajili ya kupanua mashamba vijijini etc the list is endless.Siyo lazima lakini kama mtaguswa na hali za ndugu zenu vijijini.Kutoa ni moyo.TUKIYAACHA HAYO YA KILA SIKU,nawapa pongezi zangu za dhati skwadi zima la Fc Kilimanjaro kwa ushindi wenu mnono na kazeni buti kila ktakaye pambana naye anywe bao nne kwenda mbele!Congratulations to you all and the entire Family.Sisi huku wazima mradi mkono uende kinywani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2008

    huyu jamaa aliyeshika kombe ni kama bw rashid vile. nimeanza kumuona akicheza mpira toka akiwa mtoto mdogo kule kigoma, halafu akasimama kwa muda mrefu. kama wewe ni rashid hebu tuwasiliane kupitia phillip_jr1973@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2008

    Congrats guys.Njooni basi mtusaidie kumwua Simba asitewalakika?(Indomitable Lions) tarehe 14-June,CAMEROON.Timu yetu ya Taifa inahitaji msaada wenu.Pliiz guys

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2008

    anon wa 1,what the hell are you on about?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2008

    Kessy Ngau nakutafuta sanaaaaa, please naweza pata contacts zako. Dada yako wa Tambaza.

    ReplyDelete
  11. Mtihani wa kwanza kwa FC Bongo ni siku watakapo onja chungu ya summer mwaka huu pale watakapo kutana na TAS mwishoni mwa wiki hii...

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 10, 2008

    Dada wa Tambaza pindipo ukitaka kuwasiliana na mdogo wako Kessy, tafadhali wasiliana nami kwa anuani hii: kilimanjaro@comhem.se

    ReplyDelete
  13. Dada Wa Tambaza nipontutafutane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...