Meneja Mkuu wa hoteli ya Southern Sun Dar Adam Fuller akifungua shampeni kuashiria uzinduzi rasmi wa hoteli hiyo uliofanyika leo mchana. kufuatia uzinduzi huo jina la hoteli ya Holiday Inn iliyopo barabara/mtaa ya Garden limezikwa rasmi leo. pembeni ni baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo wakishuhudia uzinduzi huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. Swali ni moja tu! holiday inn ilikua ya mzawa au ya "muwekezaji" (mgeni)? kama haikua ya mzawa imeoperate kwa miaka mingapi? au ndi yaleyale ya changa la macho la "tax holiday"?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2008

    Mi sina tatizo na ''kifo'' cha Holiday Inn kama hawa wawekezaji wapya Southern Sunn wataendelea kulipa, kodi kama kawaida. Ila nitakuwa na tatizo kubwa na serikali kama hawa wawekezaji wapya nao watakapopewa tax holiday kwa kisingizio cha kwamba ni ''new comers'', na kama serikali imewapa tax holiday hawa jamaa nitajua ni mwendelezo uleule wa Tanzania a.k.a Bongoland a.k.a Fisadiland!

    Mdau,
    Gothenburg, Sweden.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2008

    SERIKALI IANGALIE UPYA MFUMO MZIMA, LAA KILASIKU TUTAKUA NA MAJINA MAPYA YA HOTEL KUKWEPA KULIPA KODI. WAMILIKI WALEWALE.

    ReplyDelete
  4. hapo hawajazika jina la holiday inn..ila wamezika kodi wanazodaiwa.

    kuanzia hapo sasa wanatumia jipya na taxi holiday.kweli bongo tambarare...

    ipo siku..

    Tutafika tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2008

    Wachangiaji hapo juu mnazungumzia jambo la msingi kabisa.

    Niliambiwa na mzungu mmoja mwenye wadhifa wa juu kwenye shirika la kusaidia Afrika Masharika (AMREF). Yeye alisema kuwa sio kwamba wawekezaji wageni hawataki kuendeleza uwekezaji wao. Bali tatizo ni kwamba mwisho wa kutakiwa kuanza kulipa kodi uwadiripo, vigogo wazawa wanawaomba "vijisenti" vyo! Na kiasi waombacho huwa ni juu sana hata kuzidi 10% za faida waliyoipata kutokana na uwekezaji wao.

    Kwahiyo, aidha wawekezaji wageni hao hufunga virago au mara nyingine hubadili jina la uwekezaji na kuwa wawekezaji wapya na kuendelea kufaidi vya kodi huria!

    Na tuliendelea na hayo ya hayo ya migodi, eti warudishe gharama za uwekezaji wao, tutajikuta tunamaliza miaka 20 hivi, kabla yao kuanza kulipa kodi. Na huenda wakafunga virago kwa kisingizio kuwa madini wakati huo hayapo!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2008

    Huku ni kuwapumbaza watanzania na kuwadanganya kwa kubadilisha majina kila baada ya muda fulani hivi "Grace stupidity period" Wanaopata hasara ni sisi wenyewe watanzania, na kuwaaneemesha vigogo wanaokula cha juu! Nchi haiwezi kuendelea kwa mfumo huu wa kifisadi.

    Lazima viweke vigezo muhimu kwa watu wanaofanya biashara kama hizi!
    I hate it!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2008

    hey! we go again, kapu la mjinga liko wazi tena.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 02, 2008

    Bila shaka kuna muda wa msamaha wa kodi umeisha, amekuja mwingine kupakua. Wajinga ndio waliwao?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 02, 2008

    mmmhh kazi kwelikweliii...Danganyika,the land 2b

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 02, 2008

    NASEMA KWA UCHUNGU MKUBWA TANZANIA TUTAKUWA KICHWA CHA MWANDAWEZIMU HADI LINI?HAWA INVESTORS NI MATEPELI NA WASHAGUNDUA KWAMBA TANZANIA NDIO MAHALA AMBAPO NI RAHISI KUFANYA MAMBO YA UTAPELI NA KUJIPATIA PESA ZA CHAPCHAP.HII ISSUE NI KWAMBA HAWA JAMAA WANAPOKUJA NA MAJINA MAKUBWA YA MAHOTELI KAMA HOLIDAY INN,SHARATON,N.K WANAKUWA WANAWEKEZA NA AINA HIYO YA INVESTMENT KWA KITAALAMU NI CAPITAL INVESTMENT NA WANKUWA INTITTLED KUPATA "TAX HOLIDAY" PUMZIKO LA TAX KUTOKANA NA KIASI CHA CAPITAL"MTAJI" WALIOTUMIA KUWEKA HIO INVESTMENT,SASA MATEGEMEO HUWA NI KWAMBA BAADA YA MIAKA MITANO(5) HAWA JAMAA WATAKUWA WAMESTABILIZE NA KUANZA KUILIPA SERIKALI KODI KUBWA,LAKINI IMEKUWA NI FASHENI KWAMBA MARA BAADA YA HIO TAX HOLIDAY HAWA JAMAA WANABADILISHA MAJINA YA HOTELI NI HIVYO KUPEWA 5 MORE YRS YA TAX HOLIDAY NA KUENDELEA KUKWEPA KODI.JE TANZANIA KWELI HATUNA WATU MAKINI KUWEZA KUINGILIA HUU UTAPELI?TUTAENDELEA KUWA MASIKINI HADI KIAMA.
    WADANGANYIKA AMKENI!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 02, 2008

    Watanzania tutaendelea kupigwa changa la macho mpaka hapo tutakapobadili hiyo sheria ya tax holiday.

    Long Live Capitalism!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 02, 2008

    Holiday Inn itafunguliwa tena palipo jangwani Breeze kama Holiday Inn Resort baada ya matengenezo na pia wahusika watafungua hotel mpya pale palipokuwa na Mawenzi Hotel kama Mawenzi Eclipse Hotel.source:http://www.eclipsehotels.co.uk/future_developments.html)

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 02, 2008

    Watanzani utahamka lini? TUNABALLALIWA kilakona.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 02, 2008

    wageni wanakwepa TAX,sisi wenyewe ndio usiseme,unavyo nyakua tukipata nafasi

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 02, 2008

    niyale yale ya kutoka sheraton hotel mpaka movenpick....na hao wameamua kutumia the same formula...tujihulize kama kodi inalipwa au ndio yale yale ya tax holiday!!!

    ReplyDelete
  16. HAMNA CHA KULIPA KODI WALA NINI NAKUMBUKA SWALI LA MUHESHIMIWA MBUNGE WAKATI HUO SEMINDU PAWA , ALIULIZA MBONA HOTEL YA SHERATON IMEBADULISHWA MAJINA MARA ROYAL PALM MWISHOWE ITA KUWA PAWA PALM NAONA GAME LINAENDELEA. TAX HOLIDAYS TO INFINITY

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2008

    Ujanja ni ule ule tumeishaujuwa...kumbuka ishu ya SHERATON..kisha ikaja...ROYAL PALM....sasa ni MOVEINPICK...Cha ajabu serikali yetu imejaa mawaziri maprofesa na ma-PhD graduate lkn up-stairs kwao ni 0....kwanini kila mara tufanywe wajinga na hao wawekezaji?
    PILI...yawezekana jamaa hawaku-meet standard za kubeba title ya Holiday Inn hivo wamenyanganywa....lkn sbb ya kwanza ndio most likely to be!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 02, 2008

    Yeah!What a Country???????ANOTHER TAX HOLIDAY.REMEMBER SHERATON? Uko wapi Mr.Luoga?Uko wapi Miss Shekidele?si nyie ndio maofisa wa juu wa TRA kuhusu hili?hivi kweli hamlioni au ni miongini mwa walewale sasa?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 02, 2008

    Yeees libeneke ni lile lile la tax holiday, Fikiria Sheraton to Royal Palm then Movenpik.Hivi ndugu hizi rafu marefa hawazioni tu? kwao wanaweza kufanya hayo? Je ni wawekezaji wapya au ni kanzu mpya shehe yule yule.je Friends Corner ya Kagera anaruhusiwa ligi kama hiyo?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 02, 2008

    HILI NI BAO JINGINE LA KODI AU WAWEKEZAJI NI WALEWALE?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 02, 2008

    Hawa watu wahuni tuu,wanaogopa kulipa kodi,wanajifanya kubadili majina kama ilivyo Sheratoni mpaka ikawa movenpick,,hao ndio mafisadi wenyewe wanajifanya kubadili jina kumbe tajiri ni walewale..mdau Norway

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 02, 2008

    Michuzi Bro asante kwa taarifa hizo ,kuna kitu kinatokea pale kuhusu BEI ZA HUDUMA !!!
    Pamoja na kwamba upangaji wa bei sasa ni soko huria lakini kuna tatizo kubwa sana la kupandisha bei kihilela kila kikicha
    Beer Local = 3,500/=
    Beer Imported 6,500/=
    Glass ya wine 6,000/=

    AC hazifanyi kazi ,vyoo vibovu
    NATUMAINI NI WAKATI WA KULIANGALIA SANA HILO WATU WA VIWANGO WAINGILIE...

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 02, 2008

    Mimi kwa upande wangu sina Tatizo na "tax holiday" kama wengine walivyosema...maana hata hizo kodi zilizokusanywa zimeishia mifukoni mwa wachache.

    Chamsingi mimi naomba vyama vya wafanyakazi visisitize suala la kutopunguza wafanyakazi..maana hii ndiyo mbaya zaidi...naiomba serikari iangalie kwa marefu na mapana suala la wafanyakazi.

    Mdau wa KMNL

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 02, 2008

    mhhhh!!!!!!!yale yale ya kumdandanya mtoto na peremende,washatufanya watanzania hatujasoma,hiyo inaitwa TAX AVOIDANCE WADAU Au nayie mnaamini nikifo cha kawaida(natural death of holiday inn) au kukwepa kodi?????????

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 02, 2008

    Lakini kwanini hakuna sheria ya kukabili mambo haya ya ukwepaji kodi? mambo haya yanafanyika ndani ya nchi tena waziwazi namna hiyo...why?!! kwanini yasikabiliwe!! we seem to be stupid.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 02, 2008

    Hivi hawa watu pale hazina wamepata kazi vipi ? au kwa sababu au ndi shughuli hamna hivi ni nani aliyehusika na kukipitisha hiki kipengele cha five years tax holiday kwani inabidi aturudishie tu mshahara wetu nina hakika alichofanya ni kwa maslahi yake
    Hata kama watamlinda lakini sio kwa mipango ya mungu

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 02, 2008

    Mimi naona ni wale wale Holiday Inn ..wamebadilisha tu jina. Hawa watu wajanja sana!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 02, 2008

    Almost certainly we gonna see a new name at the end of the "tax holiday". What a shame to those who do it and those who encourage it. Think of the poor mother suffering due to poor health services at Mwananyamala hospital, think of a peasant in sukumaland who has given up on the test of sugar, think of the poor Zanzibaris enduring the experience of the yester years and think of all "vijisenti" flowing down the drain of corruption and selfishness.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 02, 2008

    Mimi ni mtanzania naangaikia maisha ya wanangu na nina uchungu sana na haya mambo. Ukweli i had enough siku moja tutakuja pigana tu hata iwaje cause sasa hii inakua mbaya.
    We have to think jamani , i swear one day yes.
    N a ni soon.

    ReplyDelete
  30. I HATE THIS!! Huu ni ukwepaji kodi tu hakuna kitu kingine. Jamaa wanasema wanabadilisha jina lakini ukisoma tangazo lao kwenye magazeti ambalo limeandikwa kwa viherufi vidoogo, utaona wannajikanganya wenyewe kwa kusema hoteli hiyo sasa iko chini ya Sourthen Sun ambao....WANA UZOEFU WA MIAKA 40 KATIKA BIASHARA YA HOTELI!!! kwa hiyo swala si kubadilisha jina, ndugu zanguni. Swala ni kwamba mtu ameishamaliza miaka yake mitano ya nafuu ya kodi anamuita na mwenzake shambani kwa bibi naye ajitwalie miaka yake mitano ya nafuu ya kodi kisha 2013 utasikia imekuwa NORTHEN SUN!!! hivi sisi tuna viongozi kweli????

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 02, 2008

    Adam Fuller si muwekezaji mpya wala nini ni mjanja tu anakula na wakubwa ,huyu bwana kwa ufahamu wangu alianza na STEAS FAST FOOD sijui ndiyo inavyoandikwa maana kimombo not reachable, hivi sasa atakuwa anacontrol miradi kibao, ni hiyo SOUTHERN SUN ndiyo ametoka live lakini the darkside of him only JAH knows.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 02, 2008

    Mimi nafikiri ipo haja ya kujielimisha kuhusu sheria za kodi, tax holiday ilishafutwa zamani. kinachotokea ni kwamba mwenye jengo yupo lakini mgt hukodi jengo ili kuendesha hoteli kwa jina lake. Inapotokea kubadili mgt na jina linabadilika. Kodi inabaki pale pale. fikiria una kibanda cha salon unakodisha, je akipanga mwenye salon si ataweka jina la salon analolitaka yeye? akihama siatakuja mwingine ambaye si lazima atumie jina la awali lakini kodi yako utamsamehe? Pengine ni vema tupate ufafanuzi wa wataalam wa kodi kwani nadhani hatuko sahihi.

    ReplyDelete
  33. jamaani wahenga walisema"maneno matupu.....?" saasa hapa watu mnatoa maoni memngi tu na yanaonekana ya msingi kabisa je swali ni NINI KIFANYIKE? na mimi na wewe kama WaTanzania wa kawaida tufanyeje? tuweke siasa pembeni na tuangalie maslahi ya taifa letu! hivi mnajua kuwa Mmbunge ni mfanyakazi wa wananchi? tunawatumiaje? je wapinzani kazi zao ni kuwania ruzuku na kungojea magazeti ya ibue skendo ndio na wao watafutie umaarufu hapo hapo? tuweke itikadi pembeni (michuzi na jua unakakadi kako ka jembe na nyundo mfukoni)na tuangalie maslahi ya taifa hili! nini manana ya nchi kuwa na wasomi ambao ni mabubu jamani! mimi nawazo, kwanini tusianzishe kitu ambacho kitapigania hayo mambo? mimi najitolea na nitashughulikia mambo yote ya kisheria ya kukiandikisha hicho kiorganization(not a political organization) ambao wapo interested wajitokeze!!! "ukikaa juu ya misumari na kukaa kimya bila kuonyesha kuwa unaumia watu watajua umezoea". mungu ibariki Tanzania!
    ni hayo tu!

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 02, 2008

    mie nimeisha fanya nao kazi hao holiday inn ni kwamba waga wanatumia jina la hotel kuwa ni holiday inn ila wakikuliza cheque yoyote inaandikwa southernsun mbona tangu siku nyingi tuuu tena ni karibia hotel zote za dar zina tumia mtindo huo.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 02, 2008

    Mimi nadhani wahusika wazungumze ili tujue ni kwa vipi hilo jina limebadilika na pia kama hao wamiliki wapya watapata TAX holiday. Nionavyo mimi kama hawa jamaa kama watapata hiyo TAX holiday, basi Tanzania itakuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na watu wajinga katika maswala ya kodi na uwekezaji. Pia kama itakuwa hivyo, serikali itabidi iache kuchangisha michango kutoka kwa watu masikini kwani yenyewewe inaongoza kwa uzembe kwa kuwaachia wachache wafaidike

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 02, 2008

    Jamani enhee, waacheni wanaojua kodi waongee kodi. Hapa hamna kodi yoyote iliyokwepwa. Michuzi usiibane hii acha niwaelimishe waosha vinywa. Wenye hoteli yaani walioijenga ni Southern Suns lakini wakawakodisha holiday inn waiendeshe. Holiday inn dunia nzima biashara yao ni kukodisha mahoteli ya watu wengine na kuyaendesha. Kwa Tanzania wote southern sun na holiday inn wamekuwa wakilipa kodi. Southern sun wanapata kodi ya pango kutoka kwa holiday inn wanalipa kodi ya serikali. Holiday inn wanafanya biashara na wnapata faida na wanalipa kodi ya serikali kwa faida yao. Sasa kodi ya pango imepanda holiday inn hawawezi kulipa wameamua kwenda kupanga kwingine (Janwani Sea breeze na hotel mpya inayojengwa ilipokuwa Mawenzi hotel zamani zote zitakodishwa na holiday inn na zitaitwa holiday inn). Sasa southern sun wameamua kuendesha hoteli yao wenyewe badala ya kuipangisha. Sasa kelele za nini? Au watu mmebeba sana mabox na hamuelewi kufanya research kabla ya kuongea?

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 02, 2008

    grace period ifutwe,ask me why!!!

    miss keys

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 02, 2008

    anon 5:43 UMETUMWA WEWE!TOKA ZAKO

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 02, 2008

    wewe miss keys anon 5:45 why should we ask you,and that has already been said and answered in other comments.au unataka attention?

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 02, 2008

    WENYEWE VIONGOZI WANACHUMA PESA KWA MITINDO HII, UJINGA TUNACCHEKWA WATANZANIA WOTE.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 02, 2008

    weye annon wa 5;43,mbona huku ughaibuni hawa Holiday Inn hawapangi kihivyo???Au hakuna kupanga??Au majina hawayabadilishi kihivyo???JIULIZE KWANZA!!!Hapo kwa watani wa jadi tuu hakuna mchezo huo au nao hawawapi kupangisha??MNAIBIWA MNABAKI KUDANGANYIKA,kweli nchi ya wadanganyika ina wajinga wengi. Na always WAJINGA NDO WALIWAO.
    God bless UFISADILAND aka BONGOLAND.
    Mdau- Helmand Province-Afghanistan

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 03, 2008

    holiday inn ni franchise kama ilivyokuwa sheraton dar unajenga hotel yako kwa standard zao halafu unatumia jina lao na pengine management>mitandao ya franchise sio ukwepaji wa kodi nadhani wachangiaji wengi hapa hatuelewi mifumo ya biashara kwani hata kwa wenzetu ulaya na marekani hotel za holiday inn ni franchise tu.Amkeni jamani muielewe sekta binafsi kabla hamjaropoka
    nzehe

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 03, 2008

    Anonymous wa June 02, 2008 5:43 PM

    what is your problem? Wanakupa nini hao kukujaza ujinga huo? Are you among Adam Fuller's little pay ladies or? Au ni miongoni mwa wale dada zetu walioolewa na Wazungu na huyo FOOLER ndio anaona wa maana? Unamtetea a man who is in your country to fool you? Oh sometimes huwa natamani huu ujinga wetu waTanzania tungeutua......... they are all FOOLERS...Michu nina hasira sana na hii kitu na tafadhali usiibanie, manake nilikuwa nasoma postings zote hizo then huyu the mos FOOLED person akaja na hizo zake akanitibua kabisa... lakini sometimes ni udhalili wake ndio umemfanya aandike yote hayo Oh God Have Mercy on her/him,whoever he/she is

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 03, 2008

    Wandugu, mimi ni mtaalamu wa kodi na napenda kukubaliana na anon wa 5.43 kwamba yuko sahihi pamoja na huyo aliyetoa mfano wa Saloon kwa sababu huo ndio ukweli uliopo hapa. Kwa wake wanaofuatilia bunge letu Tax Holiday ilishafutwa siku nyingi sana kwenye sheria za kodi za Tanzania tangu wakati ule Sheraton ilipobadilisha jina mara ya kwanza kuwa Royal Palm. Watu walishtukia loophole na ilishazibwa. Nafikiri tufanye upembuzi yakinifu kabla hatujaanza kuongea. Mwalimu wangu wa sheria chuo kikuu nilichosoma Masters in Taxation hakuacha kusisitiza kila siku kusema "No research, no right to speak". Naomba iwe hivyo huku kwenye blog ya jamii.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 03, 2008

    JINA (MOVENPICK) NI KEJERI DHIDI YA UDHAIFU WA MTANZANIA, UKIWA NA MAANA (INGIA/NENDA NA CHUKUA) HII INATOKANA NA MSAMAHA WA KODI HIVYO UNACHOTAKIWA NI KUWEKZA (INGIA NCHINI) MIAKA MITANO YA BILA KULIPA KODI IKIISHA (FAIDA) ONDOKA (PICK) SASA JAMANI HII SI NCHI TAMU KAMA ASALI.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 03, 2008

    Mimi ni anon wa 5.43 na ninaandika kutokea Wellington New Zealand. Mbele tu ya hiki chuo ninachosoma (Victoria University) kuna Holiday Inn hotel ambayo imeanzishwa 2006. Before that it was Hotel Continental for the past 15 years. Continental wamejenga yao wamehama na Holiday Inn kama ilivyo biashara yao wamekodisha wanaendesha. Hii vile vile ni sector yangu na siropoki. Anayesema huku majuu hoteli hazibadilishi majina ni majuu gani anakoongelea? UK,US,Australia,Germany (ambapo Mungu amenijalia kupita) kote hii biashara inafanywa hivi hivi. Na hiyo anayeniita FOOLER I feel sorry for him for he does not understand where the world is going - umebaki nyuma sana. Kama suala lingekuwa Kodi our revenue authority (TRA) would be shouting by now - they are not fools!

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 03, 2008

    Same Wine in New Bottle,

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 03, 2008

    anon june 2 9:13 una nini na mimi wewe,kama hukutaka kuuliza si ungenyamaza,sasa unamshushua nani?

    miss keys

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 03, 2008

    anon 5:43 pole sana kwa kutukanwa na kushushuliwa,ila ndio ujue,usiongee pumba or u shall be condemned as a fooler

    babygyal-09

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 03, 2008

    Weye annon 5:43 pumba tuu huna lolote hio fani gani ulosomea??mbona tunaona sheraton Nairobi,Hilton Kensington,Sheraton Addis Ababa hazibadilishwi??Na kuna maHoliday Inn kibao sijaona yamebadilishwa?hivi weye ni mtoto wa MAFISADI NINI??Haya kawadanganye wajinga wenzako, hapa hupati kitu.Na ukweli ni kwamba BONGO NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU KILA MTU ANAJIFUNZIA KUNYOA.period.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 04, 2008

    Anon wa 5.43 usiongee tena kwani level yako ya uelewa iko juu kuliko ya hawa wengine wanaopiga kelele bila research. Just know you are right - Mtaalamu wa kodi Tanzania

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 04, 2008

    Mimi ni mzawa damu.... Nimikasirika sana natamani nilie kwa sauti kubwa.... Nwauliza wenzangu... TUFANYEJE??????????

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 04, 2008

    wewe mtaalamu wa kodi Tanzania aka anon june 4 8:42,i have doubts,naomba uanike vyeti vyako na qualifications hapa!!maana i see no proof of knowledge!


    babygal-09 aka mtaalamu wa research Tanzania and the whole world

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 09, 2008

    I have worked for the then known Holiday Inn Dar es salaam(Hidar) for three years.
    Adam Fuller is only an employee of Southern Sun Africa which is in South Africa. He is based in Dar to manage a Hotel which is operated by Southern Sun Hotel(T) Ltd which by then it had a frachised name Holiday Inn from Six Continets hotels (Pty)Ltd based in America. southern sun (t) Ltd was paying royalty to Six Continets Hotels for the use of the name Holiday Inn. Now that the Southern Sun has come to a time they need to use their own name in business and that is not only in Tanzania but also in East, Midle East and Africa (EMEA) region where it as hotels in franchised names. Na mimi ni mtanzania tu ila sijui kama katika hilo swala la kodi linaendaje ila jina wamerudisha na hawataki tena kutumia majina ya kukodisha. Majina mengine ambayo walikua wakikodisha ni Pamoja na Holiday Inn RoyalCrown, Intercontinental(ambayo ni highest standard), Formula 1(hii ni lowest standard in SA), and may others. Angalia www.southernsun.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...