
Ni matokeo yasiowashangaza wengi wanaofuatilia maendeleo ya soka la Tanzania na mwalimu wa Taifa Maximo.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa nchi hii ya Cape Verde katika mashindano haya muhimu. Matokeo yanayoiweka Cape Verde katika nafasi ya pili kandika kundi hili lenye timu za Cameroon na Mauritius pia.
Matokeo haya yanaiweka Taifa Stars katika wakati mgumu, kwani baada ya kucheza michezo miwili wanashikilia mkia wakiwa na point 1!
Mchezaji wa akiba Babanco ndiye aliyekuwa mwiba kwa Tanzania pale alipofunga goli pekee katika mchezo huo katika dakika ya 73 ya mchezo huo, uliochezwa katika jiji la Praia.
Tanzania itakuwa na wakati mgumu sana, pale itakapo wakaribisha washindi wa pili wa kombe la mataifa ya Afrika, Cameroon katika mchezo utakaofanyika jijini Dar-es-Salaam ndani ya wiki mbili zijazo.
Kwa muda mrefu sasa mashabiki wa soka nchini Tanzania wamekuwa wakihoji uimara wa kocha Mkuu Maximo.
Hii inafuatia tabia yake ya kubadili wachezaji kila mara, na hivi karibuni kulaumu aina ya wachezaji alionao, kuwa eti hawafundishiki!
Anawalaumu kuwa hawafungi magoli pale wanapotakiwa kufunga, na kuwa sio kazi ya walimu wa Taifa kuifanya hiyo kazi, huku akiamini hiyo ni kazi ya walimu wa vilabu, ni kauli isiyokuwa na maana machoni mwa wapenzi wa soka.
Serikali imetumia mamilioni ya pesa na bado inatumia pesa nyingi kuendelea kuwa na Mbrazil huyu, kwa lengo la kukuza kiwango cha soka cha Tanzania, pia kuhakikisha Tanzania inafuzu katika mashindano muhimu katika Bara la Afrika, hii ikiwa ndio sababu ya kumtafuta kocha anayetoka Taifa la soka duniani, Brazil.
Binafsi sina tatizo na Maximo, kama binadamu! ila kama mwalimu, nina wasi wasi kama ana ufahamu mzuri wa aina ya soka la Afrika. Hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha mafanikio kwa walimu toka Brazil katika soka la Afrika.
Mafanikio makubwa katika soka kwa baadhi ya Nchi za Afrika kama Nigeria, Togo, Senegal, Mali,Ghana, Ivory Coast bila kusahau Cameroon, yameletwa na Walimu toka Ufaransa, huu ni ukweli ulio wazi, wafaransa wanaifahamu vizuri sana soka ya Afrika, na ndio sababu nchi kama ya ufaransa ina wachezaji wengi wenye asili ya afrika, na hivyo kuzisaidia nchi za Afrika kisoka.
Kazi inayofanywa na Maximo, ingeweza kufanywa vizuri zaidi na mwalimu mzalendo kwa kumpa msaada na heshima anayopewa Maximo, huku viongozi wa serikali wakimtetea kuwa anafanya kazi nzuri kuendeleza soka, na aendelee kupewa nafasi.
Mimi sidhani kama mafanikio aliyoyapata kwa kipindi chote alichokaa na Taifa stars, hayakuwahi kufikiwa na walimu wazalendo waliomtangulia, ila kwa kuwa ni MBRAZIL, basi chochote kidogo anachopata uwanjani kinakuzwa mara 100!
Kwa uelewa wangu kiongozi anapimwa kutokana na matokeo ya kazi yake, na ndio maana Vilabu na Nchi nyingine duniani haziishi kufanya mabadiliko katika uongozi wa soka, hasa pale matokeo yanapokuwa hayaendani na aina ya uongozi wa hizi taasisi za michezo, ambazo hugusa hisia za wananchi wake.
Kwa mtazamo wangu na ushauri wangu, ni vyema Mhe Rais Jakaya Kikwete, ampe Mhe Joel Bendera likizo fupi, ili awe mwalimu wa hii timu ya Taifa kwa kipindi kifupi kilichobakia kabla ya Tanzania kufufua matumaini yake ya kuwa moja kati ya Timu zitakazo fuzu kwenda Afrika kusini 2010.
Kwani tukumbuke Joel Bendera alikuwa ni Kocha mkuu wa Taifa Stars ya mwisho kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika kule Nigeria, mwaka 1980. Huyu ni mtaalamu wa soka aliyebobea, badala ya kufundisha timu za wabunge, apewe vipindi vya kuwa na wachezaji wa Taifa Stars.
Kama Mwalimu, Kocha, Mbunge na Naibu Waziri wa michezo, atasaidia kujua tatizo liko wapi na kutafuta dawa.
Hii itasaidia kurudisha imani miongoni mwa wananchi, kuwa pamoja na serikali kumlipa mshahara Maximo, lakini bado inajali matokeo ya Stars katika jamii, na jamii inaonyesha kuchoka na kusubiri.
Tanzania ni Nchi kubwa Duniani, ina historia kubwa na umaarufu mkubwa, wakati tunasifika kwa kuwa Taifa la Amani, kuwa na Kiswahili, Mlima Kilimanjaro, Mwalimu Nyerere, Mbuga za wanyama, Filbert Bayi, Juma Ikangaa na kutembelewa na viongozi wa mataifa makubwa, kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa, kuwa na Rais mpenda michezo na sifa kibao, bado hatustahili kutokuwa na mchezaji hata mmoja kwenye ligi za kubwa za dunia!
Wakati huo huo, TFF na Baraza la Michezo La Taifa, liangalie utaratibu mzuri wa kumpata Mwalimu wa Taifa, tumeona kule Mexico wiki iliyopita, kuwa walimu wa vilabu vya soka walipiga kura kura kumchagua Eric Goran-Erickson kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa, aina hii ya demokrasia na uwazi inasaidia kuweka hatima ya matokeo yeyote kwa mfumo wa kijamii kuliko taasisi moja.
Njia nyingine ni kutumia makampuni ya kimataifa ya mahusiano (PR) kutangaza na kusaili wale wote wanaotaka kuwa walimu wa Timu ya Taifa, katika hali ya utandawazi siku hizi, una nafasi nzuri ya kumpata Kocha mzuri wa Taifa kwa kuwatumia Ma-Agent wa kimataifa.
Na hii isiwe kwa soka tu, ila kwa michezo mingine yote, kwani Tanzania sio taifa la soka tu!Harambee Stars, imeanza kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, na hii ni baada ya kuwa na migogoro na kufungiwa na FIFA, CAF, kwa karibu miaka miwili hivi.
Wanafanya vizuri kwa kutumia walimu wa nyumbani na hapa tusikosee Kenya itafuzu hata Uganda pia, kwani wenzetu wanajua tofauti ya kucheza nyumbani na ugenini. Je Dr Msolla, Mziray, Kayuni hawana nafasi tena katika soka letu?
good article but ni ndefu mno. Next time try to be brief utaeleweka vizuri.
ReplyDeleteMdau
sasa nadhani tumechoka kuwa mdebwedo, jamani hata kaji siwa kadogo ka carpe verde kanatufunga?, nadhani wachezaji hawana uzalendo. Maximo sasa akapumzike rio de jenero. Marcelo Lipi bado anatafuta kazi ni kumpa nusu ya budget ya nchi yetu atatuletea lile kombe la dhahabu.
ReplyDeleteSawa Tunakubali kuwa Joel Bendera ni Coach mzuri na amesomea fani ya mpiara wa miguu lakini je, tujiulize alipokuwa Coach wa taifa alileta mafanikio gani? ama ndiyo machungu ya kufungwa ? hata kama ni machungu lakini tuwe na simile
ReplyDeleteMdau kibamba-Pwani
unategemea mtu asome article ndefu yote hii? umenoa basi. ujumbe bado hujafika
ReplyDeletewatanzania tumeisha anza majungu,kama maximo ana contract ya miaka mitano acha amalize,halafu mpewe timu yenu mnaweza kukaa nayo milele hakuna aliyesema mkamwite maximo,tuache majungu kwanza unapo pima uwezo wa maximo unaangalia nini?kushinda mechi tu mbona huangalii program zingine za kuandaa vijana,mpira wa tz unatakiwa miaka kama 5 hadi sita na tuwe na juhudi hizi hizi ndio angalau tutaona mafanikio ,sio ulale uamke ukute time ya taifa ipo inachukua kombe la dunia
ReplyDeleteHii nilisha sema hapo nyuma.Huyu kocha hatufai hata kidogo kwani hakuna alichoweza kuachieve mpaka hivi sasa.Kinacho hitajika sasa hivi ni KUMTIMUA tu!Tunahitaji kocha mwenye CV iliyoshiba(heavy cv) sio kocha wa kutafutwa kwenye GOOGLE.Kufanya vizuri hatuhitaji mpaka tuwe na professional players.hawa wa kwetu wana fundishika kabisa.Nasio suala la soccer la Africa.Hakuna kitu kama hicho.soccer ni tactics tu.Labda yawezekana pia hapati ushirikiano wa kutosha toka kwa makocha wazalendo kwani wanahusudu zengwe sana.
ReplyDeletePia chama cha Mpira nchini kina matatizo.HILI SWALA LINA HITAJI KUWAHUSISHA WANANCHI PIA.Wala hawatoi short list ili watu wapige kura za maoni.
kila kitu kina ukomo. mbrazili hana tena jipya.
ReplyDeletekuna mambo mengi yanayoathiri wachezaji na uchezaji. mwalimu mzalendo anayajua zaidi kuliko wageni. mpe mkwasa timu, mrizai, msola n.k na wape uhuru kama huyu. mabadiliko yatakuwa makubwa sana.
Tanzania na jadi yetu, wazuri wa kukosoa; ahsante kaka michuzi kwa uwanja wako huu ambao kila mtu anaongea yake! Hivi kweli Maximo afanye kazi ya kufundisha wachezaji kufunga magoli? au alete mbinu mbadala za kusaidia timu kushinda! Ingekuwa hivyo akina Dunga, Big Fili [Scholari] na makocha wengi wangekuwa wanawafundisha akina Rooney, Tevez, Henry, Kaka kufunga magoli! Lakini mara nyingi hasa wachezaji wa America kusini hukutwa hapa Europe kwa match nyingi tu za kirafiki, je National Manager kweli kapata muda gani kumfundisha Tevezi kufunga magoli kama sio toka klabuni kwake?? Hapo Tanzania labda aje Mtume au Jesus ndio tutaweza cheza soccer ya uhakika! Ningependa labda mtu/watu ajaribu kuangali wachezaji wa Taifa stars, je kuna wachezaji wangapi ambao kweli tunaweza kusema timu ina wachezaji? Pale Hawazidi wachezaji 2 au 3 basi; wengine basi wapo kulazimisha mambo! Wenye vipaji na uwezo hakuna, angalia maumbile tu! Watakuja akina Eto hapo speed 120, mapaja ya kufa mtu mtasema wanasukuma! Tuandae vipaji na vijana wenye uwezo na maumbile ya kutosha! Wapo kasulu, Mara, Rukwa Tunduru na sio hao vibaka wa Dar or Moro! Watu wakumbuke akina Boniphace, Homa ya jiji au Pondamali watu wameshiba! Sio hao vijana toka Mtaa wa Saba mpk 21!
ReplyDeleteAchaneni na kukosoa kocha wakati umefika sasa wachezaji binafsi kuwanyooshea vidole nawao.mijibaba hio hata kama kocha mbaya sio na wau ndio wawe butu kihasi wanachocheza.mijitu inacheza mpira kama wenda wazimu hata mpira wa watoto wadogo mchangani unavutia kwa vile wanatumia akili.mtabadirisha makocha wote hio mijamaa tumeilemaza wenyewe washabiki kutoka vilabuni.yanga wanachukua ubingwa kwa mpira mbovu tu ambao hata wakivuka mpaka wa nchi wowote hawawezi kushinda.taifa cup badala ya kuweka timu za vijana za mikoa tunaeenda kuikusanya hile hile mibutu yetu ya kwenye ligi kwenda kucheza tena kama sio upotevu wa hela na mda.wakati umefika kuwakosoa wachezaji sio manalalamika tu.wazomeeni mnapoona wanacheza mpira mbovu na muwaambia ukweli.makosa mangapi tunayaona yanafanywa na wachezaji wa timu ya taifa ambayo na uzembe wa mchezaji ndani ya uwanja? Je mnataka maximo haingie kiwanjani hawafundishe cha kufanya? Soka letu halitabadirika hata kidogo kama vilabu vyetu vitaendeshwa na viongozi walalahoi wanao jali maslahi yao binafsi kuliko mchezaji.
ReplyDeleteMdau msema kweli
Mdau Msema kweli nakuunga mkono.
ReplyDeleteWachezaji wetu mbumbumbu, ngoja ntie msisitizo...
WACHEZAJI WA NCHI YETU TANZANIA NI MBUMBUMBU. Si machungu ya kufungwa, ni ukweli. Hawa wachezaji bila nidhamu na juhudi binafsi, hata aje nani kufundisha....
Yale yale .kuna watu wamekaa wanasubiri matokeo mabaya ya stars waanze kumrukia kocha.mimi sio kwamba namtetea maximo sema toka aje maximo fifa rank ya tanzania imepanda kwahio kusema hajafanya chochote ni uongo mtupu.Soka la tanzania tatizo letu tunalijua liko wapi sema kwa vile sisi tunaendelea kuongozwa na vichwa vya wendazimu ndio maana TFF mpaka leo wanashindwa kuwa serious na kurekebisha mfumo mzima wa soka.shule ya kukuza vipaji ziongezwe tusitegemee vijana wote watatoka makongo.mitaani kuna watoto wadogo wanaotumia akili kucheza mpira wengi sana sema hakuna mfumo wakuwaendeleza.tatizo kubwa ni ligi mbovu inayotokana na klabu zinaongozwa na watu wenye njaa na mchezaji ni mtu wa mwisho kujaliwa katika vilabu.wachezaji wetu hawalipwi mishahara matokeo yake hawachezi kwa kujituma na wengine wanacheza mpira mbovu kutokana na matatizo ya kifamilia na njaa kali inayowakabili.huwezi kwenda kucheza mechi huku akilini kwako unawaza leo familia sijui itakula nini jioni.Tff inatakiwa hijaribu kushindikiza makampuni kununua hizi club na soka liendeshwe kibiashara.timu ziko miaka nenda rudi mpaka leo hazina hata uwanja wakufanyia mazoezi.halafu leo timu ya taifa inafanya vibaya unaenda kulaumu kocha.kama hile penati mchezaji wetu angefunga na mauritius wote mngemwaga misifa kwa maximo bila kujua ubovu au uzuri wa uchezaji wetu kwa ujumla.tunasahau kwamba mechi za kimataifa ni tunavuna tulichopanda kwenye vilabu vyetu vya nyumbani.na kitu kingine sijapenda jinsi wachezaji wa timu wa taifa wanavyopongezwa au kupewa ahadi.wakishinda mechi moja tu utaona viongozi wa serikalini wanawaalika chakula cha jioni na mazawadi kibao kiasi cha kwamba wanajisahau kwamba safari bado hijaisha.kwanini wasiwe wanapewa ahadi kuendana matokeo ya mechi zote za mzunguko fulani?,kama wakati huu wapeni ahadi kwamba mkiweza kumaliza nafasi flani kwenye kundi hili wote mtapata kiasi flani.hio itawasaidia kuwapa moyo zaidi kwani wameshindwa kujituma kuonesha vipaji vyao binafsi kwa faida yao wenyewe mpaka wapewe ahadi.
ReplyDeleteSerikali ina hela nyingi sana za kuweza kuekeza kwenye shule za watoto wenye vipaji na tukawatumia hao makocha wazalendo kukuza vipaji na pia makocha wetu wakapewa msasa kwa kumualika kocha mmoja tu mzuri wa nje ambae ana record nzuri.
Safari bado ndefu sana nchini kwetu kwenye kila kitu sio soka tu.
Mdau mzawa, jongo wa kisiju nasubiri majibu yako.
unajua nini mtoa mada? mpira wa Tanzania hautabadilika kwa kubadili kocha, na maximo kusema kwamba wachezaji wa Tanzania hafundishiki ni kweli na nakubaliana nae, kama unakumbuka kiswahili kinasema "samaki mkunje angali mbichi" je asili ya wachezaji wa tanzania wanatoka wapi? kuna shule inawajenga kisakologia kua tayari kucheza mpira kama njia yao ya ku earn a living? mpaka sasa mpira wa tanzania bado ni wa ridhaa yaani just to have fun? lakini mpira sasa hivi ni ajira na hilo lieleweke kwako.alafu kuhus bendera acha kuturudisha nyuma wewe bendera akae huko huko aliko na kama unataka coach mzalendo basi suggest tu recruit makocha wapya hao wote uliowataja walishafanya kazi taifa stars walifanya nini? hamna mambo ya kurudi nyuma, swala ni kwamba maximo ni mfunmbua tatizo kwa muda mfupi ila in long run lazima tufanye reforms kwenye soka la tanzania kwa kuwekeza kwa watoto, na hio sio kwenye soka tu hata katika fani zingineiwe elimu au michezo mingine hata kwenye udaktari pia,alafu tujifunze straight talk na ukweli,Bravo maximo nakubaliana na yeye kwamba hawafundishiki kabisa na siwalaumu wachezaji wa tanzania kwa hilo Its our system which is broken and needs to be fixed,we need to define our own path brother.we need to learn how to work and not politisizing every issues katika jamii yetu.joel bendera,mziray au yeyote kati ya hao wa zamani hakuna hata mmoja kati hao ataweza kubadili soccer la tanzania, kama unataka hao wafanye kazi basi kwanza wawe viongozi soccer chekechea.maoni yangu
ReplyDeleteMaximo anakaa na stikers wa Taifa staz kwa muda kidogo sana. sio kazi yake kuwafundisha kufunga, bali hiyo ni kazi ya makocha wa teams zao yanga, simba.....unafikiri makocha wa ivory coast au cameroon wanawafundiaha drogba na etoo kufunga magoli? inabidi strikers wajifunze mbinu na wapige mashuti 150 - 200 kila siku!
ReplyDeleteJamani watanzania, kwanini watu hawataki kukubali ukweli kuwa kuna tatizo la Kocha? Kwanza duniani kote timu ikiboronga anayechukua lawama ni kocha na mtu wa kwanza kufukuzwa ( Rijkaad, Mclareen, Ericson etc); Hivyo lazima tukubaliane nalo bila kuangalia kama forward inashindwa kufunga.
ReplyDeleteLa pili, kwa nini hatufungi magoal pia. Hakuna mchezaji alishawahi kuwa mfungaji bora ( Mzalendo) akaitwa na Maximo timu ya taifa (Kudra Omari). Athuman Machupa aliitwa timu ya Taifa lakini kabla hata hajapewa nafasi ya kucheza mechi hata moja akaondolewa; sijui tatizo lilikuwa nini?
Mchezaji alikuwa na red Card akaitwa timu ya Taifa wakati coach anajua kabisa hatacheza mechi inayofuatia na tukaona madhara yake siku ya mechi ya Msumbiji, wakati angeweza kuchukua mchezaji mwingine kwa ajili ya kucover nafasi yake( Nsajigwa).
Lazima tuseme ukweli nani anatakiwa kubeba lawama mara timu ya taifa inaposhindwa kufanya vizuri.
Watanzania mnalalamika eti Ilala walichezesha wazee taifa cup; kocha wa vijana ( TINOCO) anafanya nini; mbona anazunguka na Timu ya Taifa ya wakubwa. Amekaa anasubiri copa coca cola ndo afanye kazi yake; Nini jukumu lake?
Maximo si kocha inabidi akubali kurudi kwao Brazil maana hatuoni jipya zaidi ya hela za serengeti kuongeza morali ya wachezaji lakini si kocha. Bora tuendelee na kocha mzalendo.
HAPANA KUMGUSA MAXIMO,TUKOMAE NA TU NA KUKUZA VIPAJI VYA VIJANA.
ReplyDeleteBADO STARS INA NAFASI.TUKIKOSA TUNAJIPANGA KWA AJILI YA AFCAN 2012,WORLD CUP/AFCAN 2014.NO FUC**** SHORT CUT HERE
Botswana wametoka sare mechi ya kwanza na madagascar nyumbani wamemfukuza kocha mzungu wakampa mzalendo na timu juzi imeshinda away kwa kuifunga mozambique huko maputo. lakini tunajua TFF hawawezi maana kwanza huyu mwalimu hawakumleta wao. Mapendekezo yao ya walimu watatu yalikataliwa na serikali kwa kisingizio kuwa ni ghali. Na hao makocha niliambiwa na kiongozi nmmoja wa TFF kuwa wa juu sana sana alitaka dola 25,000 kwa mwezi. Kiongozi huyo wa TFF alinieleza kuwa cv ya Maximo ilikuwa nyepesi mno hata kumi bora hakuingia na aliendelea kusema kuwa Maximo hajawahi kuwa Head Coah hata siku moja, hata uarabuni alikuwa ni Assistant Kocha. Baya zaidi ni kuwa hata kocha wa vijan Tinoco anamzidi cv Maximo. Lakini kwa sababu Maximo kaletwa na serikali na Mh. Rais anamsupport basi hakuna kiongozi wa serikali wala TFF atakayesema kitu.
ReplyDeleteMdau,
DSM, Karume stadium
Watu mnajifanya wajanja hapa na kutoa maoni ya kukosoa wakti hata mkiulizwa mpira wa miguu una ukumbwa gani hamjui, Labda muulizwe kile kimpiraaa kingine mtajibu unajaa ndoo ya maji na haupasuki.
ReplyDeleteMwacheni mtaalamu afanye kazi yake. tuache hisia. kweli wachezaji wetu hawafundishiki na ndio maana hata kabla ya maximo mambo yalikuwa hivyo hivyo. Kati yenu nani kamnunulia hata kitenesi mtt wake ili angalau aanze kukua kimpira mpira. Wee unasubiri aje kuwa mtu mzima halafu eti mumpelekee Maximo amfundishe mpira? Watoto wetu wanafundishwa mpira wapi???????? Labda 'kipira' kwani huo hakuna utaaalamuuuuuuuuuu.
Sijui Itakaa Sawa Lini??? Jamaa Namuunga Mguu Alichoongea Ila Cha Kushangaza Waosha Vinywa Wengine Badala Ya Kutoa Maoni Yao Wanasema Ujumbe Ni Mrefu ..Mie Nazani hawa Hata Darasan Walikua Hawakai Kuona Somo Ni Refu. Kwa Kweli Jamaa Alichozungumzia Ni Cha Kukiangalia Jamani Watanzania. Huyu Maximo Ni Mfanyakazi Tumemuajiri Sasa Kama Hawezi Tufurahisha Au Fanikisha na Utendaji Kazi Wake Inatakiwa Ampuzishwe..Tusichukulie soccer Kama Siasa Ya Bongo Mtu Anavurunda Tunamuangalia Mpaka Anajiuzulu Mwenyewe.Hebu Fikiria Ni hela ngapi zinatumika Kwa Maximo +wapambe wake+cha juu cha waliomleta Hesabu Ikijawekwa Mezani Inaanza Mambo Ya Tume Tena.Natumaini Tukiliweza Hili Tu Tutaweza hata Kusafisha Uchafu Wa Viongozi Wa Nchi....Ni Mdau Mpenda Soccer Sio Nchi
ReplyDeleteJoel Bendera hajafundisha timu ya mpira yoyote kwa miaka mingi sasa uzoefu gani atakuwa nao kweli? Huyu alikuwa kocha mzuri miaka hiyo ya 1980s, kwa miaka hii mimi naona atafutwe mtu mwenye uzoefu wa mpira wa kisasa na awe anafundisha aidha klabu au nchi kwa sasa. Toeni CV za watu wanaostahili hapa tuzichambue!!
ReplyDeleteswala la kumtimua maximo na kukabidhi timu kwa kocha mzalendo kwangu mimi naona linaweza likawa 50-50% chance katika kuleta mafanikio kwenye timu, na hii ni kwa sababu ukiangalia hata baadhi ya nchi za west na hata zile za kaskazini kama morocco na tunisia zina makocha wa kigeni na bado zinafanya vizuri tu. Kwa hiyo tatizo siyo kuwa na kocha wa kigeni au mzalendo. Na kama tatizo ni kwamba timu haifundishiki,je ni hatua gani zilizochukuliwa ili kuweza kuhakikisha kwamba wachezaji wanaelewa vizuri kabisa mawazo na falsafa za mwalimu.Kama wachezaji hawafundishiki basi bila shaka tatizo linaweza likawa kwenye lugha.
ReplyDeleteWatanzania mtakalia majungu tu, hebu tujiulizeni, hivi hawa wakina mziray, msolla, bendera na wengineo hawajawahi kufundisha taifa stars, na kama walishawahi walifanya nini, jibu mnalo. Ni kwamba taifa stars kabla ya maximo ilikuwa haitoi hata draw hata kwa jirani zetu, lakini leo Kenya na Uganda wanatuogopa sababu tunawafunga, wakijitahidi draw. Toka maximo ameichukua timu tunafanya vizuri ingawaje si kwa kiwango cha juu sana. Tumetoa hata draw na timu iliyowahi kucheza kombe la dunia ikafika mpaka robo finali timu ambayo imejaa professional players wa ligi za ulaya , tumewafunga burkina faso ambayo ni timu nzuri na ina professional players, ambapo hata senegal mwenyewe alikula goli.
ReplyDeleteKwahiyo mnaweza kuona ni kwa jinsi gani kuna mafanikio, tatizo ni kwamba watu wanataka tupate mafanikio ya harakaharaka au tufunge kila match wakati hatujawaandaa wachezaji wetu kwa hilo.
Kwahiyo mimi nasema kwamba msipuuze mafanikio ya maximo, sasahivi tuko nafasi ya 102 katika FIFA Rankings na mwaka jana tulifika mpaka nafasi ya 92. Lakini kabla ya maximo tulikuwa tunashika mpaka nafsi ya 160, kwahiyo kama mnataka kuona kama kweli maximo hajaisaidia timu basi mfukuzeni muweke hao wazawa wenu, mtakuja kujuta.
Kwa kuhitimisha, wabongo tuwe na subira na tuwe na mikakati ya kukuza vipaji, siyo kutaka maendeleo ya haraka haraka. Hata hivyo namsifia maximo, ni mwanaume sana, kuikubali hii timu ya taifa, au sijui na yeye njaa kali. Ukimpa mtu kama Morinho hii timu hawezi kuikubali hata kama utamlipa shilingi ngapi, kwani yeye anataka aibu.
Big Sam
umeandika ujumbe mrefu ..sikunyingine jaribu kufupisha...msolla,mziray.bonifasi na wengine wazelendo wote walisha pewa na hakukuwa na mafanikio mimi nadhani nibora atafutwe mwalimu mwingine kutoka eu. by mdau
ReplyDeleteWatanzania lazima tuukubali ukweli kwa macho maangavu. Kwa mazingira ya sasa hata akija Furgerson, wenger nk hataweza kubadilisha timu ya taifa kwa muda mfupi: Tatizo: Hatuna mfumo mzuri wa soka tangu chini hadi taifa. Wakati wenzetu wanafundisha soka katika academy lukuki, wakati timu za daraja la kwanza kwa wenzetu zina timu za vijana na watoto, sisi timu zetu hususan simba na yanga hazina hata second eleven, na wanachokijua ni kukwapua wachezaji wanaoinukia na baadaye kuwamaliza kisoka kwa kutokuwa na mfumo mzuri wa kuwalea na kuwaendeleza.
ReplyDeleteKlabu za soka zisipokuwa na msingi imara wa kupika wachezaji hatuwezi kupata wachezaji wazuri wa taifa. Kwa hiyo ili kuondokana na tatizo hilo wadau wawekeze katika soka la vilabu ili liendeshwe ki-professional tofauti na sasa ambapo makomandoo na viongozi fisadi wanageuza kuwa ni mashamba ya bibi..wanayahujumu watakavyo. klabu ziendeshwe na makampuni yenye utawala uliowazi na usioingiliwa na watu wasiostahili, na ziwe na timu kuanzia kids, vijana, na second eleven, pamoja na kuwa na makocha waliosomea fani hiyo, siyo mafunzo ya ngumbaru.
maximo tumfukuze,tusimfukuze itakuwa haina maana kama hela za viingilio zinaliwa badala ya kuendeleza soka la watoto.
ReplyDeleteyeeee mi naona atafutwe kocha kutoka unguja,zanzibar au pemba yaheeeeeeee
ReplyDeleteaisee braza michuzi embu nisaidie swali langu hili, hivi ni lugha gani mr maximo anatumia kwenye mafunzo ili kuweza kuwasiliana na timu? kama anasema timu haifundishiki basi si ajabu kama nyamulongo alivyosema hapo juu tatizo likawa ni lugha, inawezekana kabisa wachezaji wakawa hawaelewi ideas na philosophy zake za mpira, nakumbuka hata wakati chelsea walivyotaka scolari aende kuifundisha, scolari aliwaambia kabisa mimi sizungumzi english, na akasema pia kwamba sharing the language of the players is important, and the coach must transimit his ideas and philosophy to the team in a simple and clear language that would help players to understand well. Kwa hiyo hapo naona tatizo linaweza kuwa ni kwenye mawasiliano kati ya mwalimu na wachezaji pamoja na lugha inayotumika.
ReplyDeleteWatu wengi wana mawazo mazuri naona na kweli kama mdau alivyosema juu kuhusu lugha inaweza kuwa tatizo kubwa sana kwa wachezaji wetu.hata kama wanamkalimani na sijui kama wanae haipendezi kazi ya kocha kutafsiriwa kila wakati.kocha anatakiwa hawe ana uwezo wa kufikisha ujumbe moja kwa moja kwa mchezaji hio inaweza hata kusaidiwa kocha kurekebisha makosa madogo madogo wakati mchezo unaendelea.
ReplyDeleteWadau mpendekeze makocha tuwasikie mimi binafsi nampendekeza JAMES SIANG'A hapewa kazi ya kukuza vipaji vya vijana na najua ana uwezo wapia kufundisha timu ya taifa ya wakubwa lakini tutakuwa tunapoteza mda kwani samaki mkunje angali mbichi.
JAMES SIANG'A hawe kocha wa vijana.
Huwezi kuanza kumlaumu Maximo kwa mapema yote hii...Ni si yeye kama alivyosema, ni wachezaji. Watu wale wamezeeka ndio wanaanza kufunzwa mpira, Mpira ni kutoka utoto mkuu. Inafaa zianzishwe soccer clubs za kutafuta vipaji, Na vipaji si wakubwa kama jamaa zetu walio stars NO. Bali ni watoto wa kuanzia miaka 15, Thats how soccer is.
ReplyDeleteNdio mana nchi zote zilizoendele ktk soccer zina Youth teams na youth leagues. Kwahy tusianze majungu mapema yote hii, mwachie maximo afanye kazi yake, wachezaji ndio butu, anajaribu kuwanoa. Tanzania tuache kujipa sifa za uongo ambazo ukweli wenyewe hatuna.
Matatizo yetu makubwa ni mawili, la kwanza ni kwamba wachezaji wetu wanavyo vipaji lakini ni wazito sana katika kufikiria. Uvivu huu wa kifikra unawafanya washindwe kutumia vipaji vyao vizuri ili wapate ushindi.
ReplyDeletePili, ni undekezaji wa ushirikina na imani chafu za uchawi. Huu upuuzi usipoachwa basi hatutaweza kupata ushindi kamwe. Tuache kuendekeza hizi kamati za "UFUNDI" ambazo ni njia ya kitapeli ya wazee wachache ya kujipatia mlo bila jasho.
Ni hayo tu.
Kama mdau KIPEPE alivyosema hapo juu, nafikiri wachezaji wetu wanatakiwa kufundishwa jinsi ya kuweza kufikiria kiufundi(creative thinking) na kiustadi wawapo uwanjani na hata ambapo hawapo uwanjani. Kwa mfano kama hawa washambuliaji wanaotupiwa lawama kwa kukosa magoli ovyo ovyo, kitu cha msingi cha kufanya ni kuanza kuwafikirisha tu kwa kuwauliza maswali madogo madogo, kwa mfano, what makes a good strikers?. Maswali kama haya yanaweza kuwamotivate na kuinspire them kutafuta majibu au solutions ambazo zitawasaidia kuelewa vitu ambavyo wanatakiwa kuwa navyo ili kuonekana tishio na kufanya mavituuz wawapo uwanjani.
ReplyDeleteKweli kabisa kama vilabu vitaendelea kuendekeza ushirikina soka halita kwenda popote .nendeni bagamoyo basi hili mshinde mechi zenu acha kumlaumu maximo.maximo kazungukwa na wachezaji waliozoea kushinda kwa kuroga sasa mchezaji kama huyo atafundishwa vipi?
ReplyDeletehatuna kocha, kamfukuza Haruna Moshi wiki mbili zilizopita kwa utovu wa nidhamu.baadae anasema amemasamehe lakini hadi aone kiwango chake.swali wiki mbili alipomwita timu ya Taifa alikuwa na kiwango gani?
ReplyDeleteMapunda alifungiwa miezi sita kwa utivu wa nidhamu, alipomaliza tu akamwita timu ya Taifa. bila kuona kiwango chake.
kocha ni mbishi na mjuaji kupita kiasi.
aondoke hana analofanya ni tapeli tu.
Acheni longolongo nyie mnaempinga Maximo! Kwanza kabisa ile trip ya kwenda Nigeria nilidhani kocha alikuwa mRumania au mCheckosolovakia na Bendera msaidizi wake? Anyway, Bendera hata vyeti atakuwa amesahau ameviweka wapi sembuse sasa hivi apewe timu eti afundishe? Please! Amepitwa na wakati! Hao wazalendo nao bomu tu na walishapewa nafasi yao na ni Mziray tu aliambulia Challenge mwaka fulani na timu bado ilikuwa ranged 160th in the world!!
ReplyDeleteVilevile, watu wanasahau kuwa pale uwanja wa Taifa alipowasili Maximo alisema yeye sio mchawi na tusitegemee mafanikio ya harakaharaka. Watu vilevile wanasahau kwamba alipotajwa atakuwa kocha alishatuma matakwa yake na mojawapo lilikuwa kuwepo na mashindano ya vijana na mikoa, and viola! copa kaka kola na taifa cup haya hapa. Aliomba pia kuwepo na timu za vijana na timu za risevu na wae na ligi yao pia - hili FAT ya sasa bado inasuasua.
Kuhusu "kubadilibadili" timu alishatoa kielelezo cha kina alichokuwa akifanya - naona sio tu wachezaji wa stars ambao "hawaelewi" bali hata wanachi hawaelewi vilevile!! A pity, really!!
Nachukua fursa hii kuwahamasisha wananchi kwamba hawa Kameruni tutawasimamisha hapa Dar na kufanya ile kitu kwa lugha ya kigeni wanaita UPSET!! Sijui ngapi ngapi itakuwa lakini tunawafunga hapa!! Sasa kuna lile kundi kutoka Temeke la wavulana wakubwa wameimba mwimbo fulani unasema 3 bila.........
pamoja na matatizo yoote haya yanayojitokeza katika timu, kuna swala mmoja tu ambalo nataka niulize. Hivi timu yetu ya taifa ina workout program(plan) yoyote au strength training programs for physical strength or fitness for the players. Kwa kweli ukiangalia picha ya timu ya taifa stars na ukilingalisha na picha za timu nyingine za taifa kama Ghana, Cameroon, senegal na hata ivory utaona tofauti kubwa sana hasa katika swala la fitness.Kwa kweli ili swala inabidi liangaliwe kwa undani, si ajabu tunapata shida ya kuwa na strikers na hata mildfielders wazuri maana unaweza kuta hawana nguvu za kutosha au stamina za kukabiliana na opponents wao na kuwa na endurance katika kumiliki mpira ipasavyo.Angalia strikers kama drogba,junior agogo, na eto, na mildfielders kama essien, papa diop, geremi, diof na wengineo, hii mijamaa ukiangalia physical strength, endurance na pace waliyonayo ni si ya kawaida na ndio maana mara nyingi huwa wanakuwa mwiba kwa opponents wao. Kwa hiyo mimi ningependa kuona swala la pyhsical strength linapewa kipaumbele pia.
ReplyDeleteMimi nadhani yote ni muhimu kuyapima kwa uwazi.Suala la wachezaji kuwa ni tatizo hilo nakubaliana nalo kabisa.Ni tatizo kwa sababu ambazo pengine ziko nje ya uwezo wao.Kwamba kiwango cha soka tunachokiona kwao ndio uwezo wao.Sasa hata ukamleta kocha gani,bado usitegemee mabadiliko makubwa.Mabadiliko ya soka la Tanzania yataletwa na chipukizi wenye miaka kati ya 14-20.Sio hawa wa sasa.Tutatoana macho bure wakati tatizo la msingi linaeleweka.Kwa hiyo kimsingi katika hilo siwezi kumlaumu kocha Maximo.
ReplyDeleteTatizo langu na Maximo liko kwenye mkataba wa kazi.Kama nakumbuka vizuri huyu bwana alipewa ajira yenye mkataba wa kuipeleka timu Ghana kwenye fainali za mataifa ya Afrika.Sasa hapa ndio kwenye ugomvi wangu,kwamba kwa sababu zozote zile pamoja na nilizozitaja hapo juu ni kwamba alishindwa kuipeleka timu Ghana.Kwahiyo,kwa maoni yangu hapo ndipo ajira yake ingeishia.Akaajiriwa kocha mwingine kwa masharti yake pengine kuipeleka timu Angola au Afrika ya Kusini.Muhimu ni kwa mwajiri wake kuona je Maximo ametimiza masharti ya mkataba wa ajira yake?Kama aliajiriwa kwa lengo la kukuza soka la Tanzania,basi ni mapema tena mapema mno.Anatahitaji hata miaka 10.
Haya,timu imefungwa juzi huko visiwani.Kesho ndio wanawasili kisha wapitilize kambini kwa ajili ya mechi na Cameroon hapo jumamosi.Sasa hivi wadau kweli tuko makini kweli?Sasa ni bora hata timu ingerudi na ushindi,tungejifariji kwamba kwa ushindi huo inatosha kuwapa wachezaji morali wa kuweza kuwakabili Cameroon.Sasa tunakutana na timu bora duniani tukiwa hatuna maandalizi yoyote ya kujipima nguvu kabla ya kuwavaa vigogo hao wa soka barani Afrika.Kinyume chake tunakumbana nao tukiwa bado tuna majeraha ya kufungwa.Na tukumbuke hawa jamaa wana hasira ya kukosa fainali zilizopita za kombe la Dunia.Kwa hiyo wanakuja na nguvu zote.Leo mtu anakuja na ndoto za mchana eti watafungwa 3 bila majibu.Tuache masihara katika masuala ya soka.
kwanza wachezaji wetu ni mbumbumbu wa soka wavivu wa kufikiria na wepesi wa kukata tamaa
ReplyDeletepili Maximo anatuchanganya kidogo au na yeye ana leta siasa juzi Haruna Moshi kaomba msamaha yeye amekubali lakini anasema kwanza akakuze kibaji chake katika club yake sasa sijuwi aende club gani na ligi imeisha bora ungekataa msimamo wake.
nimesema analeta siasa kwenye soka KWANI KWA KINA MAPUNDA NA NSAJILWA ALIPOWAITA KWENYE KIKOSI ALIWAONA KWENYE LIGI GANI NA HALI WALIKUWA KIFUNGONI MIEZI 6? kwahiyo kumkataa Haruna hakuna msingi
Tatizo kubwa na la msingi ni kuwa mfumo mzima wa uendeshaji mpira ni mbovu katika ngazi ya vilabu na TFF yenyewe.Vilabu vyetu vinaongozwa kibabaishaji mno na vimekaa katika mfuma wa vyama vya kijamii na sio vilabu vya kimashindano vya mpira.kila siku migogoro vilabuni. Ili soka likue inabidi tufanye yafuatayo:
ReplyDeleteVilabu viendeshwe kibiashara nawababaishaji wote waondolewe(makomandoo nk),TFF iendeshe mpira kitaalamu kama ulaya ,waziri wa michezo na serikali zisiwe na sauti juu ya mpira ibaki kuwa kazi ya TFF na kamati za rufani zisizo na maana ziondolewe,
Kwa kufanya hivyo tutakuwa na wachezaji wazuri wa kwenda taifa na tutafanya vizuri.
J4
.......ila sisi wabongo, tunaongea sana bila vitendo, hiyo ni kero moja wapo. pili tuna mambo ya kubembelezana bembelezana. zama hizo zimepita. watu mnamtetea maximo....oooh sijui apewe muda ....muda huyo nyinyi wa kusubiri kila wakati watanzania mnaupata wapi. dunia hii watu wanakimbizana na muda na sayansi ipo juu. practical then exactly results hiyo ndiyo sayansi.
ReplyDeleteMtoa mada na wewe ni wale wale watanzania fulani hivi.......Bendera sisi wanini???
ReplyDeleteKama alibahatisha mafanikio ya kwenda kufungwa huko Nigeria basi ndiyo imekuwa nongwa???
Tena mwaka 19880 leo ni mwaka gani??
Vipi wewe???
Akae hukohuko kwenye uongozi na hapo alipo anauwezo zaidi wa kuisaidia star kuliko kama mkimpa ukocha. Hafai kuwa kocha..
WATANZANIA HATUNA TOFAUTI YOYOTE NA WAINGEREZA..TUNAONGEA SANA NA TUNAJIDANGANYANA ETI NA SISI TUNA TIMU YA KIWANGO CHA JUU..WALIOTUTAWALA WAMEJIONGOPEA KWA MUDA MREFU TU LAKINI MWISHOWE WAMESHINDWA KWENDA EURO 2008..WAMEWAFAGILIA SANA MASTAA WAO LAKINI HAO HAO WAMESHINDWA KUWAFIKISHA POPOTE!!..TUNAZIFANYA SIMBA NA YANGA KAMA VILE NI TIMU KUUUBWA ..LAKINI MBONA HAO MASTAA WETU WANASHINDWA HATA KUCHEZA LIGI KUU ZA MAANA KAMA VILE SPAIN?..KUNA WANIGERIA WANGAPI WAKO EUROPE?..KUNA WAGHANA WANGAPI WAKO EUROPE?..SISI TUNAOWANGAPI?..STARS INAWEZA IKAFUNDISHWA NA KOCHA YOYOTE YULE LAKINI KWANZA TUTENGENEZE MISINGI IMARA..LA SIVYO KILA SIKU TUTAISHIA KUTAFUTA MCHAWI HUKU TUKIENDELEA KUJIONGOPEA KWA KUWAPA SIFA NYIIINGIII MASTAA WETU AMBAO KIPIMO CHA USTAA WAO NI MAFANIKIO MADOGO WAYAPATAYO KWENYE LIGI ZETU AMBAZO HAZINA KABISA UBORA.
ReplyDeleteTanzania imefika wakati tuanze kuwa wakweli!
ReplyDeleteImefika wakati tuanze kujipa sifa tulizonazo tuache kudanganyana.
To be honest, Kwa timu tuliyonato hii sasa hivi, Hata kama aje Rafael Benitez, Wenger, au Capello unafikiri tutafika mbali???
Kuna mtu hapo juu anaonekana hajui soccer kabisa kwa kusema kwamba Maximo kazi yake kubadilisha timu, Yeye haoni kwa wenzetu waliondelea ktk soccer kwamba mchezaji kiwango kikishuka lazma apigwe benchi? Ukiangalia Arsenal, Gilberto alichapwa benchi kwa ajili ya kiwango change, Liverpool Xavi alonso alichapwa benchi, England nao kuna wkt Beckham na jina lake akachapwa benchi...Siku hizi ndio mpira unaenda, ukitaka kuwa kwenye 1st eleven lazma upige soccer.
Na mwisho, huwezi kumkubali mchezaji mwenye utovu wa nizamu ktk team. Ktk kitu chochote respect ndio muhimu. Respect to the coach, team-mates and anybody around. Respect is the key to success. without respect everybody is an enemy.
Big up Mtoa Maoni: Mliakuvana Tarehe June 09, 2008 10:57 PM, mpira dakika tisini. Hakuna sababu kufungwa kabla ya kuingia uwanjani. Twende neshno tuishangilie Taifa Stars mpaka mwisho na tutaibuka kidedea.
ReplyDeleteJamani Bendera mara ya mwisho alipofundisha timu ni lini? Sasa hivi anaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwa timu kwa sababu anaelewa mpira na yuko serikalini lakini kumrudisha kuandaa vijana ni kumtafuta lawama. Hata hizo sifa za Lagos 1980 si zake peke yake. Tumewasahau kina Victor Stanslescu na Tambwe Leya? Ndio waliowaibua kina Pondamali toka miaka ya 1970.
Nikimnukuu aliyekuwa waziri kwa muda mrefu Joseph Mungai, ukioa mwanamke mwenye mimba unaweza kumwita mtoto kuwa wa kwako lakini kibaiolojia kuna mwingine aliyewezesha.
Ndugu yangu uliyemnukuu Mungai,ubarikiwe na bwana..umetoa point kali sana ila mwenye akili tu ndiye awezaye kuielewa
ReplyDeletekuna wabongo wanatumia mfano wa Misri eti wakisema kuwa mbona wao wameweza kutwaa ubingwa wa afrika kwa kuwatumia wachezaji ambao ni wa pale pale Misri!!
wanasahau kuwa karibu vilabu vyote vikubwa vya nchi ile vimeajiri makocha kutoka nje ya bara hili tena wanalipwa mshahara usiopungua dola 30,000 kwa mwezi
wabongo wanasahau kuwa timu za Al ahly na Zamalek kwa miaka mingi zimekuwa zikitwaa ubingwa wa afrika, kwa hiyo wachezaji wa timu zile tayari wana winning mentality na ni wachezaji waliokamilika kutokana na mafunzo waliyoyapata kutoka kwa wataalam wa nchi mbalimbali walioko kwenye vilabu vyao..ni kichekesho cha mwaka kumlinganisha mchezaji wa timu ya taifa ya Misri na mchezaji wa taifa stars!!.
Ujuaji wetu ndio unaotufanya tusiheshimu taaluma ya makocha wanaokuja kufanya kazi hapa bongo
Masupastaa wetu ndio hawa wanaoishia kucheza kwenye klabu za Oman hatuna mchezaji yoyote yule unayeweza kusema eti amefikia kiwango cha kimataifa halafu tunakuwa wa kwanza kuwakandia makocha kutoka nje!!kwa soka lipi linachozwa nchini mwetu!!
tunaweza tusifanikiwe kwenda Afrika ya kusini mwaka 2010 na pia tunaweza tusifanikiwe kwenda Angola mwaka 2010 kwenye african cup of nations lakini tukumbuke bado kuna kombe la dunia la 2014 na bado kuna african cup ya 2012..kwanini tusiendelee kujianda na mashindano hayo ya mbeleni na tunaanza mizozo isiyokuwa na kichwa wala miguu!!?.
Leo hii baadhi yetu wanajifanya wana uchungu sana na stars lakini mbona tulikuwa tunafungwa 5-0 na Kenya na mbona tulikuwa tunafungwa 5-0 na Rwanda..huo uchungu unaoonyeshwa sasa hivi mbona hatukuuonyesha wakati ule!!?..kama sio unafiki ni nini?
safari ya soka letu bado ni ndefu..na tutafika salama kama tutaendelea kuwa wavumilivu.
Hivi Mtu Kama Gabriel kaanza kucheza mpira lini mpaka leo Maximo amfundishe kufunga?Hao makocha uliowataja kina Mziray na wengine si wamemfundisha ktk club na timu ya taifa,mbona mpaka leo anashindwa kutumbukiza mpira wavuni ndani ya mita 6?unamlaumu Maximo wa nn?Tukubali ukweli,hatuna striker mwenye kipaji, na sisi hatufundishi watoto mpira.Germany kw a kujua hawana striker mkali waliwapa uraia kina Podolski at the age of 16.ona leo anavyowatoa!tukubali ukweli tutafute solution,sio kuleta majunggu ya kumlaumu kocha. Hao makocha wa CV nzuri unajua wanalipwa sh. ngapi? S.Africa wanamipa dola 200,000, sie Maximo tunampa dola 15,000. Tutaweza makocha wa CV nzuri?Tuendeleze vijana ndio solution ya kudumu
ReplyDeleteKuna wazo moja ninalolisikia sana mitaani..eti makocha wa kutoka Brazil hawana mafanikio wanapofundisha nje ya Brazil..ina maana Felipe Scolari ni mndengereko!! au ni mmakua!!.
ReplyDeleteKwa jinsi kiwango cha wachezaji wetu kilivyokuwa duni..sisi si watu wa kuchagua eti kocha mwenye Standard kubwa sana , kwa kiwango kipi kinachoonyeshwa na wachezaji wetu?
Nigeria,Tunisia, Cameroon na mataifa mengine yaliyopiga hatua kisoka ndiyo yana jeuri ya kuwaambia makocha kwamba wewe hujafikia kiwango tunachokitaka , kwa sababu wao wana lundo la wachezaji wakubwa ambao wanacheza kwenye vilabu vikubwa vyenye makocha wakubwa..sisi hatuna mchezaji yoyote kwa sasa anayekaribia kiwango cha Yakubu Aiyegbeni halafu eti tunaleta nyodo za kuchagua bora..Kondic wa yanga kasema wachezaji wetu wengi hawafundishiki..micho pia aliwahi kusema kauli kama hiyo siku za nyuma..sasa kama wachezaji wetu ndio hawa ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa na vyepesi kusahau ,huyo Mourinho aje hapa kufanya nini? , au huyo Ancelloti aje kufanya nini?.
Tunajidai eti tuna mpira wenye standard kubwa wakati ukweli ni kwamba hata timu dhaifu kama Al akhdar zinaifunga yanga tena hapa hapa bongo!!.
Tuamke kutoka usingizini na tuanze kuuchukulia mpira wa miguu kama taaluma inayohitaji kuheshimiwa..majungu ndio yanayozifanya Simba na Yanga zionekane kana kwamba ni timu za wahuni wa mitaani..