mwanamuzikio nyota Kelendria Trene Rowland almaarufu kama Kelly Rowland ambaye ni mmoja wa wadada watatuw a kundi la Destiny's Child sasa hivi tumetoka kutembea naye uwanja wa fisi sehemu za mburahati kwa mfuga mbwa ambako alitembelea maghetto ya kinadada wanaofanya biashara ya ukahaba mahali hapo na kuonega nao kwa lengo ya kutafuta njia ya kubadili tabia zao. pia alisikika kila mara akiwaomba wawe wanatumia kinga ya kondom kwenye shughuli zao, tatizo walimwambia sio kama hawataki kutumia kinga ila bei huwa chini ukilinganisha na mambo ya pekupeku ambapo jamaa analipa zaidi. huko manzese tandale aliongozana na msichana eliza joseph ambaye aliwahi kuishi na kushughulika hapo uwanja wa fisi na sasa ni mwanaharakati wa kutaka kukomboa wenzie, hasa baada ya kujigundua kwamba tayari ameshaathirika na ukimwi. jioni hii kelly anaongea na waandishi wa habari hoteli ya kempinski na kesho utakuwa mwisho wa ziara yake ya siku tatu akiwa balozi wa. habari zake zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...