Home
Unlabelled
kificho na lipumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
WABUNGE WETU WASIJE WAKAUZIWA MBUZI NDANI YA GUNIA KATIKA BAJETI YA 2008/2009!.Wabunge wetu wanayo haki ya kudai kuelimishwa ama kwa kupewa Semina fupi ya siku moja mbili au Kupata Rasharasha tu ya Mapitio kutoka kwa Mtaalamu au Msomi wetu mmoja wa masuala ya Uchumi nchini,kwa mfano kutoka kwa Dr.Ndullu,kuhusu 'Impact'ya Bajeti hiyo katika Maisha ya kila siku ya Mtanzania wa kawaida na katika kuchochea ukuaji wa uchumi.Serikali imetamka kwamba imepunguza sana Utegemezi kwa Wahisani wa Nje katika Bajeti hiyo.Kwa hiyo Bajeti itategemea zaidi Mapato yatakayo tokana na Vyanzo vya Ndani ya Nchi.Serikali pia imetamka kwamba haitakopa kutoka Mabenki ya hapa nchini.Kwa hiyo ni wazi kwamba Mapato hayo ya Ndani yatatokana zaidi na Kodi mbalimbali.Pia tunafahamu kwamba sekta ya Viwanda hapa nchini ni duni mno sawa na hakuna.Kwa hiyo kodi itakayo tokana na bidhaa za Viwandani ni kitendawili!Sawa na hakuna.Pia tunajua kwamba Sekta yetu ya Kilimo haifanyi vizuri na uzalishaji wake kwa mazao ya kuuzwa Nje ni duni vilevile.Lakini pia tunajua kwamba Mapato yatokanayo na Madini sehemu kubwa inakwenda Nje haiingii katika Mfuko wa Serikali kutokana na Mikataba Mibovu.Tumebakiwa na nini sasa?Labda Kodi ya Mapato kutoka kwa Wafanyakazi na kiasi fulani kutoka kwa Wafanya biashara.Siyo siri kwamba Uchumi wetu haufanyi vizuri kutokana na sababu mbalimbali.Uthibitisho wa hilo ni kwa yeyote aamue tu kuzunguka madukani na masokoni ili kujionea mwenyewe ni bidhaa zipi zinazo uzwa huko na zinatoka au kuzalishwa wapi!Ndipo atakapo baini kiwango cha utegemezi wetu na jinsi gani uzalishaji wa ndani ulivyo zorota.Kwa maana hiyo, ni wazi kwamba Tegemeo kubwa la Bajeti ijayo ni Mapato yatakayo tokana na Kodi kutoka katika Wigo Mwembamba sana wa Vyanzo vya Mapato.Kwa hiyo Watanzania watarajie katika mwaka ujao wa Fedha ongezeko kubwa sana la 'Beifumuko'- 'Inflation';kushuka kwa thamani ya mishahara na mapato yao mbalimbali;kuongezeka zaidi kwa umaskini miongoni mwa watanzania;kudumaa zaidi kwa uchumi;kuongezeka zaidi kwa nakisi ya bajeti;kuongezeka zaidi kwa utegemezi kutoka nje;kuongezeka kwa ukosefu wa ajira nchini hususan miongoni mwa vijana wetu;kuzidi kushuka kwa thamani ya shilingi yetu.Wabunge waibane serikali ibainishe wazi ni vyanzo vipi vya mapato vitakavyo toa kiasi hicho cha mapato ya serikali walicho kikadiria.Na pia wabunge waibane serikali ili iweke wazi na bayana ni wafadhili wepi waliothibitisha kutoa misaada na ni katika miradi ipi.Na miradi ipi ambayo ahadi zake bado hazija thibitishwa!Mengine Mtajaza Wenyewe!
ReplyDelete