Home
Unlabelled
manchester oyeee!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Manchester na Sinza wapi na wapi? Ningefurahika kama hawa wadau wangekuwa wanapanga mikakati ya kuifanya Taifa Stars nayo ifanye yaliyofanywa na Manchester United.
ReplyDeleteWatumwa wa kizalendo!!!mawazo bado ya kiutumwa!!!
ReplyDeleteMi nashindwa kuelewa watu wanaosema Mawazo ya kitumwa... ama kumshangaa Michuzi na wengineo kutaka kufungua tawi la Liverpool...
ReplyDeleteNashindwa kuelewa kwa sababu....
1. Mpira ni ushabiki na hisia.. na mara nyingi mtu anapenda kitu kilicho bora. Dunia sasa ni kama kijiji, kama Manchester United ama Liverpool ama timu yoyote ina mpira bora, na una uwezo wa kuona huo mpira, na wachezaji walioko ni kati ya wachezaji bora duniani.. sasa kuna tatizo gani kuwa na ushabiki... hayo mawazo ya kitumwa yanakuja vipi hapo...
we anon wa 11:04 acha uvivu wa kufikiri.
2. Ushabiki ni hiari
3. Kama we ni mpenzi wa mpira wa kikapu (Basketball), lazima wale wachezaji bora utawapenda, na kwa kuwa wachezaji wengi bora wako NBA Marekeni, lazima utaangalia na kushabikia timu moja wapo..
hapo mawazo ya kitumwa yanakujaje?
Utakuwa na mawazo ya kitumwa iwapo 'utashabikia' kichuguu kilichopoa UK ama USA na kuacha 'kushabikia ' mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania
Jifunze kuchanganua mambo.. tofautisha mawazo ya kitumwa na vitu vinavyohusiana na ubora.
na we anon wa 10:47...
Hamna uhusiano wa kuwa mshabiki wa timu ya nje na kushindwa kupanga mikakati ya timu za nyumbani...
huo uhusiano unakujaje? au wasema tu?
Jamani.. toeni hoja za msingi ili kutupunguzia sisi kazi kuanza kuwakosoa...
AU? :)
JK please! Watafutie kazi za kufanya hawa vijana.
ReplyDeleteWabongo acheni ushamba na kushabikia vitu vya nje wakati vitu vya ndani mnavidharau. Alafu mnalalama eti Maximo hajui kufundisha.
ReplyDeleteHizi nguvu za kushabikia vitu vya ulaya tungezielekeza nyumbani basi tungekuwa mbali.
Ama kweli haya ni mawazo ya kitumwa!
Aa! Makubwa maana hadi mnasheherekea kama ni wapenzi wa kweli si muwe mnaomba visa kwenda kuangalia mechi msimu ukianza?
ReplyDeleteHongereni na huyo anony wa 11:51 hapo juu.
Mzalendo (Yanga Damu)
BIG PHIL SCOLARI KOCHA CHELSEA, MTAKOMA!! KUTESA KWA ZAMU.
ReplyDeleteNdugu yangu mpendwa wa June 11, 2008 11:51 PM,Je unanufaika kimapato cha hao wapiga mateke wa gozi la pumzi??sidhani yakhe...,kwa hiyo hebu jirekebishe kifikra na jikomboe kutoka kile kinachojulikana kama'INFERIORITY COMPLEX'
ReplyDeleteNaona hapa kunatatizo la uelewaji.Manunited kama Team nyingine ulaya zimeundwa na wachezaji kutoka nchimbali mbali duniani na mpira wa miguu umedevelop beyond contry League.Labda kwa kuongezea kuna proposal in Premium league right now kuwa kila team lazima icheze game at least one out of england,do you know why?
ReplyDeleteMimi sishangai kuona Big party kufanywa bongo kusheherekea team bora Manunited.
Mwisho mimi na pinga kusema kushabikia team nje ya nchi ni utumwa,ila ni dalili mpira umegrow kuwa global sports compared 1960's.
Nadhani tusiwalaumu wenzetu huko Tanzania, watafanya nini sasa zaidi ya kushabikia mipira? Nchi inakwenda down south, uchumi wa nchi unakuwa kwenye makaratasi lakini mifukoni mwa watanzania unakuwa na negative speed.
ReplyDeleteHakuna kingine muhimu zaidi ya kushangilia mipira. Jamani kama mnaweza fungueni matawi ya basketball pia, wekeni Lakers au Celtics au Rockets.
Big up sinza boyz. hao wapenda netball wanasubiri tuwe na mchezaji wakibongo man u ndo waanze ushabiki. tuko kwenye nchi huru na yenye demokrasia kula kitu roho inapenda bora usivunje sheria.
ReplyDeleteje hao ma hipocrity wanajua ukiristo na uislamu siyo dini za africa??? wajiulize hilo kabala ya kutukanyaga . manu u is my religion. wakati sisi tunapanga timu msimu ujao chelsee ndo kwanza wanatafuta kocha then tukijashinda kwa pont mbili mwisho wa ligi wanajiuliza ilikuwaje?? glory dayz glory man u united. na hakuna mtu mkubwa kuliko club tutamuozesha bench au twaweza chukua hizo million 80 tukanunua ronaldo wengine watatu big up sir alex.
Uchumi hauwezi kukua mifukoni mwa watu kama hawa. hata huko ulaya na Amerika watu wanafanya kazi sana ili wapate pesa na siyo blaa blaa.
ReplyDeleteKinachotakiwa hapa ni kuwaambia wabongo wajitume kwa kufanya kazi bila kuchagua ni kazi gani ili wajiongezee vipato vyao na siyo kubaki kuilaumu serikali tu. Mimi nawashangaa watanzania wenzangu hasa waliopo nje ya nchi kwani nao ni miongoni mwa watu wanaoilaumu serikali kwa kila kitu huku wakiwatetea watu wasiopenda kufanya kazi (wazembe) ambao kazi zao ni utapel, kushaini pamba na kutafuta mademu tu. Ninawalaumu kwa sababu najua wabongo wengi waliopo huku japo wapo wenye elimu nzuri lakini wanafanya kazi zisizo na hadhi kwa elimu zao na zingine za kutia kinyaa lakini wanazifanya ili wapate pesa za kuishi na hawazilaumu serikali za nje kwamba maisha yao ni magumu. Kwa mfano huu kama kila mtanzania angetafuta shughuli endelevu ya kufanya kama vile kilimo, ufugaji (siyo kupiga debe na umachinga) n.k na siyo kukaa vijiweni na kuilamu serikali nadhani watu wangepiga hatua na nchi ingesonga mbele. Ni kweli serikali ina makosa yake lakini kinachoonekana sasa kila mtu anataka maisha bora bila kutoka jasho, waambieni ukweli kwamba mliopo ulaya mnatoka jasho hivyo wasisubiri vya kupewa tu wakati ana uwezo wa kulima mchicha na kupata pesa. Watanzania tubaki masikini kama tutaingojea serikali ifanye kila kitu
Kila mtu ana haki ya kufanya atakalo, hakuna anayevunja sheria, kama wanataka kushabikia Pamba ya Mwanza Lukusa.
ReplyDeleteHongera vijana wa sinza.... next time tunaomba nasi mashabiki wa man utd tabata mtukaribishe tu sherekee pamoja...Man utd daimaaaaaaaa
ReplyDeleteNimeota vibaya leo eti Cameruni 7 stars 0.kipindi cha kwanza eti tukaweka mpira kwa pani
ReplyDeletehongereni wapenzi wa man u...acheni wjinga waongee wakichoka watanyamaza kwani tumejitahidi kusherehekea soka letu la bongo hamna kitu na sisi tunapenda soka sasa tufanyeje...penda kitu roho inapopenda utaenjoy milele
ReplyDeleteMWANACHAMA[MANCHESTER UNITED]
FROM UK-MANCHESTER
Hongereni sana mashabiki na wapenzi wa Man U achaneni na hao wasafisha vinywa hawana jipya ndo kazi yao hiyo,big up ma u
ReplyDeleteHabari zenu ndugu zanguni, hasa wale ambao wanaipenda Man Utd na wale ambao hawipendi lakini kwa namna moja au nyingine wameweza kutu-support kwa kufanya party yetu.
ReplyDeleteSasa narudi kwa wale woote ambao wametukashifu na kutoa maneno ya kejeli kuhusu party yetu, kwanza kabisa napenda kuwakumbusha kuwa hii ni Tanzania huru, hivyo basi mtu yeyote anaweza kufanya chochote atakacho ili mradi tu asivunje sheria zilizowekwa kwa mujibu wa katiba na taratibu zake, hivyo basi ni mapenzi yetu kwa Man Utd na hakuna yeyote aliyekuwa na uwezo wa kutufunga minyororo tusifanye tulichokusudia kama hivi tulivyofanya na tutaendelea kufanya kufuru zaidi ya mwaka huu iwapo mwakani mambo yatakuwa mazuri tena hilo ndilo azimio letu sisi.
Kingine nawatakia hongera sana wana Man Utd duniani kote najua blog hii inapatika popote penye uhai wa binadamu, homngereni sana kwa kusheherekea popote mlipo.
Kingine tena sisi kama wana Man Utd tumedhamilia kuanzisha umoja wa wana-Man Utd hapa Dar na sasa tupo kwenye mchakato mkubwa kujipanga kujua tutawezaje kufikia malengo yetu, kuna wanaoshangaa sisi kushabikia Man Utd mbona Kenya na Uganda nimepata habari ambazo bado sijazithibitisha kama ni kweli wameanzisha umoja wa timu wanazozipenda, kama wmefanikiwa hongera zao pia.
Nawaomba wana Man Utd popote hasa ndugu yangu wa Tabata si mbali lakini pia unaweza kutumia e-address hii japh232000@yahoo.com tubadilishane mawazo ikiwezekana tushirikiane kuunda umoja wa wapenzi wa wana-Man Utd Bongo Land.
Kibonzo cha mwisho kwa wale wanaotucheka na kushangaa wamwambie Bro. Issa Michuzi na yeye pia aache kuanzisha umoja wa wana-Liverpool Bongo au bwawa la maini kama anavyopendelea kuita kaka michuzi kama atawaelewa.
Asaaaaaalaaaaam.
Mdau wa Man Utd, Sinza Madukani.