septemba 1, 2007: mchezaji wa nyota wa zamani wa taifa stars na pia yanga na simba kwa nyakati tofauti maulid dilunga akiwa msimamizi wa mchezo wa kirafiki kati ya stars na uganda neshno.wadau wengi wamesema iko haja ya kutafuta njia ya kumuenzi mareehemu dilunga ambaye alifariki dunia siku ya jumanne na kuzikwa jana huko kwao kisarawe. alikuwa na umri wa miaka 62.
wamesema kusimama na kupewa heshima kabla ya mchezo wa stars na cemeroun siku ya jumamosi kama ilivyotangazwa na tff hakutoshi bali kuna haja ya hata kuipa sehemu moja wa uwanja mpya wa neshno jina lake, huku sehemu zingine zikipewa majina ya kina gibson sembuli, omar mahadhi bin jabir na wengine walioleta sifa nchini kwa kabumbu safi.
kwa wanaokumbuka dilunga awali alikuwa anaitwa eusobio akifananishwa na mchezaji wa msumbiji wa enzi hizo aliyetamba huko ureno, na baadaye akapachikwa jina la kuitwa mexico baada ya yeye na omar mahadhi bin jabir kuteuliwa mwaka 1994 kujiunga na timu ya kombaini ya afrika kwenda kucheza huko mexico.
mola aiweke mahala oema roho ya marehemu dilunga peponi - AMINA


Ni kweli kwamba marehemu Maulid Dilunga (Mwenyezi Munge amrhemu) alikuwa mchezaji mahiri na kusema itengwe sehemu ya uwanja ipewe jina lake, huku sehemu nyingine wakipewa kina marehemu Sembuli na wengine waliopita labda itafikia wakati kila kiti uwanja wa taifa kitapewa jina na pengine navyo visitoshe. Pili, kusema kwamba Eusebio alikuwa mchezaji wa Msumbiji aliyetamba Ureno ni sawa na kusema kuwa Zidane ni mchezaji wa Algeria aliyetamba Ufaransa au Vieira ni mchezaji wa Senegal aliyetamba Ufaransa au Barack Obama kuwa mwanasiasa wa Kenya aliyetamba America. Yote si sahihi. Mtu aliyetoka kwao akiwa mdogo au mwenye asili ya nchi moja bila kuwa mchezaji alikotoka hakumfanyi mchezaji wa nchi hiyo.
ReplyDeleteKaka michuzi, naomba utuoneshe ni yupi huyo al marhum Dilunga wengine hatuna mtambuya.Ni yupi kati ya hao.
ReplyDeleteInna lillahi wainna ilaihi raajiuun. Mwenyeezi mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. ameen.
ReplyDeleteNingepependa kusahihisa kidogo kuwa huo mwaka walioteuliwa akina dilunga kwenda kucheza mexico haukua 1994, bali ni 1974. Pia kuna profile kubwa sana ya Dilunga kama wataifuatilia vizuri. Mwaka 1974 Dilunga alikua mchezaji bora katika fainali za kombe la africa huko ghana.
naungana na AL MUSOMA SAID, kisha Dilunga akuchaguliwa mwaka 1994 ila ni mwaka 1974 kaka misupu
ReplyDeleteni huyo mwenye suit myeusi mkono wa kushoto unapoangalia au wa kulia wa waamuzi
ReplyDeleteMwenyeenzi Mungu mlaze mahali pema peponi.
ReplyDeleteUMEULIZWA NI YUPI KATI YA HAO?SASA WAKAA KIMYA KWA NINI?.MICHUZI MIMI NITAENDELEA KULA NA WEWE,MAELEZO YAKO KWENYE PICHA YANAKUWA YA KULIPUA.HAYATOSHI,UNAFANYA KUSUDI?
ReplyDeleteRAMBIRAMBI:NATOA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA,NDUGU,NA JAMAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU DILUNGA.
JUMAMOSI:1 MINUTE SILENCE NDIYO INTERNATIONAL 'SIMBO' KWA MISIBA YA NAMNA HII,HAKUNA HAJA YA KUTOA KIPANDE CHA UWANJA NA KUKIPATIA JINA LAKE
Kwa Vijana wetu wa leo,Maulid Dilunga ni huyo mwenye Suti Nyeusi.Mimi binafsi nilipata bahati ya kumshuhudia akilisakata kandanda la hali ya juu sana uwanjani.Bila hiyana kwa kweli Dilunga alikuwa na kipaji na uwezo sawa kabisa na ule aliokuwa nao Pele Nascimentos wa Brazil ambaye hadi hii leo amepewa heshima kubwa sana na FIFA pamoja na mataifa mbalimbali.Alikuwa na uwezo kufunga goli kutoka katika Impossible Angle yoyote ile huku akikabwa na maadui.Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kupiga chenga na kupangua mabeki(defense).Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusoma timu ya maadui na kupanga mashambulizi.Huyu ndiye aliyekuwa nguzo ya Timu ya Yanga katika mashambulizi.Ni jambo la kusikitisha sana kwamba hata Klabu yake mwenyewe ya Yanga haikujitokeza kidete kumkweza Mchezaji huyu mahiri na shujaa wa Taifa letu katika kabumbu la soka.Nakubaliana kabisa na wewe Michuuz kwamba wakati sasa umefika wa kuwaenzi wachezaji mahiri kama Dilunga waliloliletea Taifa letu sifa kubwa katika medani ya soka ulimwenguni.Lakini viongozi wetu walikuwa vipofu mno katika siasa na kusahau umuhimu wa nyota kama marehemu Maulid Dilunga.Uwanja mojawapo mahiri wa soka hapa nchini upewe jina lake kutunza na kuenzi kumbukumbu yake kwa Taifa letu.Vyuo mbalimbali vya michezo,Kumbi za Michezo na Burudani na sehemu zinazo fanana na hizo zipewe majina ya wachezaji nyota wa soka na ikibidi hata riadha katika kuwaenzi hawa majemedari wetu.Mungu ailaze pema peponi roho ya huyu ndugu yetu Maulid Dilunga.R.I.P.-Rest In Peace.Amen.
ReplyDeleteNDUGU michuzi,katika maswala ya soka,kidogo unatuchanganya,kumbukumbu za soka tanzania,tunashindwa kuzipata,katika riadha,the greatest athlete of them all,to come out of tanzania,is undisputable a certain mr filbert bayi.sasa katika soka tunaomba utupangie list moja mpaka kumi,tujue hii roll of honour of our ten best football players of all time
ReplyDeleteRIP DILUNGA.
ReplyDeleteilikuwa sio mwaka 1994 wala 1974 bali ilikuwa 1972 ndio marehemu dilunga alichaguliwa kwenda mexico, 1974 dilunga mpira ulikuwa unaisha na hakucheza nyamagana dhidi ya simba, mwishoni 1974 alijiunga na simba, 1975 alijiuzulu kucheza, sidhani kama tutaweza kupanga all time list kwa sababu wachezaji wazuri walikuwa wengi bongo miaka ya sabini na themanini, uwanja hautatosha majina yao.
ReplyDelete