shirikisho la soka nchini limemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha marcio maximo kuendeleza libebbeke la kuinoa taifa stars. mkataba wake wa awali wa miaka miwili unamalizika mwezi ujao. yeye kakataa kuongeza miaka miwili kwa sababu za kifamilia. ila imewekwa wazi kwamba endapo stars itafuzu kombe la dunia na mataifa ya afrika ataongeza wa pili. wadau mnaizungumziaje hatua hiyo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. HUYU MJASIRIAMALI ANANIFURAISHA SANA . AMETUELIMISHA TUWE NA MAfIGA MENGI KATIKA KAZI TUSITEGEMEE MOJA TUU. PIA TUSIIBE NDIO TUWE WAJASIRIAMALI TUTAFUTE MALI KWA HAKI ILI IDUMU MILELE NA VIJUKUU NA VITUKUU VILE MATUNDA KAMA TOYOTA, SONY NA WENGINE

    ReplyDelete
  2. HUYU MJASIRIAMALI ANANIFURAISHA SANA . AMETUELIMISHA TUWE NA MAfIGA MENGI KATIKA KAZI TUSITEGEMEE MOJA TUU. PIA TUSIIBE NDIO TUWE WAJASIRIAMALI TUTAFUTE MALI KWA HAKI ILI IDUMU MILELE NA VIJUKUU NA VITUKUU VILE MATUNDA KAMA TOYOTA, SONY NA WENGINE

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2008

    Anaondoka huyo baada ya huo mwaka mmoja alioongezewa,hapo 'ametutega' tu.Nilikuwa na pumba nyingi za kumwaga hapa lakini kuna "blogger" mmoja ananifuatafuata humu hadi nimeanza kuogopa kukolimbwa(Kidding).

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2008

    Waheshimiwa mimi sio mtalaamu wa soka ila kwa akili ndogo nilizonazo naona huyu Makisimo akae miaka mmoja, miwili haisaidii.
    Mabadiliko ya soka nyumbani yatahitaji kuwekeza kwa muda mrefu zaidi, miaka kidogo ya kuanzia iwe mitano mpaka kumi. Uwekezaji uwe kwenye vijana wadogo wenye vipaji vya soka. Tena kama inawezekana Chama cha soka kisiwe chini ya serikali, kiwe huru.
    Vinginevyo ndugu zangu siku zote sisi tutakuwa watu wa kushangilia mataifa mengine, so so sad

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2008

    Hiyo ndio raha ya watanzania, tumetoa sare na Cameroun tumeridhika na udhaifu wote wa kocha umefutwa. Wenzetu wote wameshinda timu kubwa ktk michezo ya nyumbani, Malawi wamewafunga mabingwa wa Africa Misri na bado hawashangilii. Baada ya muda aliopewa Maximo kuisha ndipo tutagundua tumeliwa na tutakuwa tumechelewa na kupoteza raslimali nyingi kama ilivyo ktk mambo yote. Wajinga ndio waliwao, idumu TFF!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2008

    Maximo mjanja, amesoma ALAMA ZA NYAKATI.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2008

    Nilimsikia leo asubuhi Leodgar Tenga wa TFF akitoa maelezo kwamba walimwomba Meximo aendelee kufundisha Taifa Stars kwa miaka mingine miwili kutokana na kuridhishwa na utendaji mzuri wa Ukocha wake,Lakini yeye mwenyewe akakataa na kuomba apewe mwaka mmoja tu na iwapo timu yetu itafanikiwa kusonga mbele katika Kombe la Dunia basi atakubali mkataba mwingine wa miaka miwili zaidi!What a good natured Coach!Napendekeza Maximo apewe Miaka mingine KUMI ili tuweze kufikia kiwango cha Brazil na tuwe tishio barani afrika!Maximo ametutoa mbali jamani mpaka tumeweza ku draw na Cameroon?Siyo mchezo Babaaakee!Watanzania wazuri jamani!Peace and Love!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2008

    hivi huyu maximo mbona haonekani kama mbrazil?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2008

    KUONDOKA LAZIMA ATAONDOKA,ILA ANAONDOKA KWA STAILI GANI,AKIONDOKA TUTAMKUMBUKA KWA HISTORIA ALIOIWEKA, KUIPANDISHA CHATI,NA KUFANYA VIZURI KWA TIMU YETU YA TAIFA KWA KIPINDI KIUPI TU,NA AKIONDOKA ANAWEZA AKAJA KOCHA BOMU,NAKUANZA PROGRAM YAKE MUPYA,KWAJINSI HIYO KILA SIKU TUTAKUA TWAANZA KWA KIPA,KWAKUKOSA UVUMILIVU WABONGO,MWISHO TIMU TUTAIRUDISHA KWA MTAALAAM JAMUHURI KIWELU (JULIO).HAPO NDIPO TUTAKAPO UTWAA UBINGWA WA DUNUIA KWA DOMO.BIG UP MAXIMO ATA UKIONDOKA WAPENDA SOKA WA KWELI TUTA KUKUMBUKA DAIMA NA HONGERA SANA UMEJARIBU AMIGO.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2008

    Sasa wadau wote waliokuwa wanataka maximo hafukuzwe tunawapa kazi ya kutafuta kocha kuanzia leo ambae atachukuwa nafasi ya maximo mwakani.mda mnao wakuja na kocha mzuri zaidi mna mwaka mmoja.kazi kwenu.na kumbukeni maximo alikuwa kaongezewa miaka miwili sema yeye mwenyewe ndio kaamua kuchukua mwaka mmoja kuwapa nafasi makocha wengine.
    Mdau mzawa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2008

    HUYU ANACHOSEMA NI KWAMBA AMEHAKIKISHA KWAMBA TUNA TAMBAA, TUKISHA SIMAMA TUMTAFUTE WA KUTUWEZESHA KUTEMBEA HALAFU TUTAFUTE WAKUTUWEZESHA KUKIMBIA.

    ReplyDelete
  12. ish, mshkaji ana vitara ya mtumba? alafu makanika mwenyewe? hakyanani huyu kaweza kujimix bongo utazani nanihii.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2008

    we peggy acha ushamba wewe,eti gari ya mtumba,unajua bei yake wewe???

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 20, 2008

    aongezewe tu,kwani hakujakuwa na maendeleo tangu aanze kusimamia timu?!?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 20, 2008

    Tena we mshenzzi huna adabu ya mtumba?!!!! si ajabu we hata huna gari kama hilo.watu wakiishi kama nyie mnawasema akiishi maisha ya juu anakula pesa za TFF,watu hamna jema

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 20, 2008

    ndio wadau wenzangu.Nashangaa sana watanzania juzi walikua wakipiga kelele Moximo atufai,lakini leo anafaa naomba kabla atujachukua maamuzi tufikirie kwa makini!!kihistoria soka la bongo tumejaribu mara nyingi kulifufua lakini mafanikio atuyaoni,atakama yapo basi ni kidogo.Nachojua ni kwamba kila kitu kina msingi,ukijaribu kuangalia tunang'ang'ana na timu ya taifa,kwenye club akuna uboreshaji wowote!tunategemea kama atutaanza kuboresha kwanza vilabu tutatoa wapi wachezaji wenye vipaji?Kingine ni namna wachezaji wa timu ya Taifa wanavyobalishwa mara kwa mara tunaomba mchezaji apate muda wakutosha wa kukaa kwenye kikosi akishindikana ndio uamuzi wa kutoa ufanywe na kamati ya ufundi ya timu,sizani kama ndivyo timu nyingine za taifa zinavyofanya tuige pia tujifunze kutoka kwa wenzetu.Jambo jingine timu yetu ya taifa tunapenda sana kukomaa na yale mataifa makubwa kutaka ushindi,uku zile timu za mataifa madogo tukizembea,matokeo yake tunapoteza mechi rahisi na kudroo mechi ngumu!kama mechi zilizopita tulikua na uwezo wakushinda lakini ndo kama yalivyotokea!Moximo peke yake si kigezo cha kupandisha soka la bongo tunaitaji kujipanga zaidi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 20, 2008

    nyie mnaomtukana mtoa hoja ya gari ya mtumba hamjaelewa hapo. mwenzenu anamsifia maximo kwa kuishi maisha ya kawaida, oil anapima na kutia mwenyewe na nyie mnamlipukia na matusi. magari ya mitumba ni jambo la kawaida kabisa kila sehemu duniani humu. acheni asila

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 20, 2008

    It will be very dificut to leave just now because Taifa Stars now play international foootball not continentale because of supot from Tenga and Chikwete.Now play no fear big names like Etoo and Drogba!Zey Play same same standard.If Stars dont win remain matches zey will angry everybody even myself will go back to Brazil!Some players no disiplin,Zey want to play but no trial matches!When I refuse, Zey begin saying Maximo no good Coach!Ripota wa interview hii bado kalazwa Muhimbili kwa kuteguka Mbavuuz!tehe tehe!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 20, 2008

    mimi naona ni sawa apewe muda huo halafu tuangalie. wanaosema afukuzwe kutokana na udhaifu kidogo 2 wakumbuke kuwa yy sio Mungu kusema anaweza kufanya 100% sawa, cha msingi toka kaishika timu imesogea kiubora au laa. kama haijasogea hatufai lakini wenyewe tunaona.... kwa hiyo tumpe muda zaidi.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 20, 2008

    Sio kwanba anaweza sana ila amekuja wakati mzuri na amewezeshwa vya kutosha, pia back up ya serikali, TFF na Wadau. Ingekuwa enzi zile angechemsha, in short he is the only one. so one yr is better as we can re-evaluate this guy

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 20, 2008

    Maximo anataka kutu-Scolari atimkie Chelsea. Hivi anataka kutumia mwaka mmoja huu kujiongezea sifa kwenye wasifu wake.
    Ukweli uko pale pale, ameinua soka la bongo. Tulikuwa tunapigwa 5-0 na Kenya mwaka 2002 tu hapa. Sasa hivi Kenya wakiambiwa wacheze na sisi Taifa wanakuja kujihami, hawana hamu.
    Mkuu wa nanihii anzisha mada ya nani aje kumrithi Maximo. Vigezo ni uwezo wa kutufikisha tunakotaka kwenda na kutojali kuendesha gari ya mtumba akiwa nchini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...