hinya hinya la kumsaka mrithi wa miss tz 2007 richa adhia limpamba moto kila kona ya nchi na tarehe 20/10/2008 siku ya ijumaa ni zamu ya kitongoji cha morocco ambapo warembo watachuana kuwania tiketi ya kushiriki fainali za mkoa wa dar na hatimaye kumpata mwakilishi wake katika miss tz mwaka huu. mwandaaji wa miss morocco da'vicky kaiambia globu hii ya jamii kwamba kutokana na ukali wa washiriki wa kitongoji chake hana wasiwasi kwamba taji la mkoa litapatikana na mmoja wao na kwamba siku hiyo fm academia watakuwepo kutia ngwasuma kali kwenye usiku huo wa kukata na shoka. kazi kwenu wadau wa morocco na vitongoji vingine vya jiji hili la maraha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2008

    Sasa mnaweka picha ya Ciara ili iweje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...