Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumatano, Juni 11, 2008) amerejea nyumbani kutoka London, Uingereza ambako alihudhuria mkutano wa Kamati Maalum ya Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola kuhusu mageuzi katika taasisi za kimataifa.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam, Rais Kikwete amelakiwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ali Shein na viongozi wengine wa Serikali.

Rais Kikwete ni miongoni mwa wakuu 10 wa nchi za Jumuia ya Madola ambao wameombwa na Jumuia hiyo kubuni na kupendekeza namna Jumuia hiyo inavyoweza kushiriki kwa ubora zaidi katika uhamasishaji na uchangiaji wa kuleta mageuzi katika taasisi za kimataifa.

Taasisi zinazolengwa ni zile za kimataifa za fedha na hasa Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia; Umoja wa Mataifa na jinsi ya kulifanya suala zima la mazingira kuwa sehemu ya utawala bora duniani.

Viongozi hao 10 walifanya kikao chao cha kwanza cha siku mbili mjini London kuanzia Jumatatu. Rais Kikwete aliondoka London mara tu baada ya kumalizika kikao hicho jana (Jumanne, Juni 10, 2008) mchana kurejea nyumbani.

Mkutano huo ulifanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown na kuhudhuriwa pia na viongozi kutoka Uganda, Ghana, Sri Lanka, Guyana, Trinidad na Tobago, Tonga, Visiwa vya Maldives na Malaysia.

Mara tu baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam na kupokelewa na Dk. Shein, Rais Kikwete alikwenda moja kwa moja kwenye eneo la Airwing la Jeshi la Wananchi kwenye uwanja huo kutoa pole, rambirambi na kuaga miili ya marehemu ambao wamepoteza maisha katika ajali ya helipokta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania iliyotokea Jumatatu asubuhi katika eneo la Oljoro, Arusha.

Kwa zaidi ya saa moja, Rais Kikwete aliwaongoza viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa kutoa rambirambi kwa wafiwa.

Rais Kikwete alibakia kwenye eneo hilo hadi ndege mbili zilizobeba miili zilipoondoka kwenda Mwanza na Iringa kusafirisha miili ya marehemu kwa ajili ya mazishi.

Waliofariki katika ajali hiyo ni aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo, Kanali Wekete na msaidizi wake, Luteni Kirunga, fundi wa helikopta Meja Sinda na fundi mwenzake Private Maande. Wengine ni Irene Nkande Jitenga, mke wa Brigedia Jenerali Jitenga na Tamary Elangwa Mziray, mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HAPO KUNA KAZI WANAMCHOSHA SANA MZEE INAMAANA VIJANA WA IT HAPO WAMESHINDWA KUMWEKA MZEE KWENYE VIDEO-CONFERERECE.SI HAKI JAMANI. SAS HII SEREKAALI KIELECTRNIC INAYO ANDALIWA ITAKUWA NI VIRTUAL TUU (YA TASWIRA) NA SISI TUNAO KUWA NA WASI WASI PALE AMBAMBO MYWIFE ZETU WANAPOKUWA KAZINI SHETANI ASIWATOKEE PAMOJA NA BOSI WAKE, SIO LAZIMA WAENDE KAZINI PHYSICAL ATAFANYA KAI ZOTE KWENYE COMPUER ON LINE WATAKUTANA NA BOSI MARA CHACHE SANA. NAFIKIRI KAZI MHIMU ZA KUWA SITE NI KAMA UJENZI. HII ITASAIDIA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI BARAARANI NA MSONGANI WA NDEGE HEWANI. KUNA VIJANA WETU WAMESHA NYAKUA HIZI PHD ZA TRANSPOTATION KAMA VILE DC,VM ,TI , WENGINE SOON KAMA WM.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2008

    what are you going on about?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...