MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY NDUGU ABDULRAHAMANI A. ABDALLAH KWA NIABA YA JUMUIYA ANAWATANGAZIA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NA WATANZANIA WOTE HAPA ITALY NA HUKO NYUMBANI KUWA NDUGU YETU OMARY JAFFARI NGWAYA aka 50 cent au SALUM LONGA AMEFARIKI LEO ASUBUHI KATI YA SAA KUMI NA SAA KUMI NA MOJA ASUBUHI KWA AJALI YA GARI.


AJALI HIYO ILITOKEA SEHEMU YA ISCHITELLA/LAGO PATRIA MJINI (NAPOLI)BAADA YA DARAJA.


NAE KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA NAPOLI ANAWATANGAZIA WATANZANIA WOTE KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO LEO SAA KUMI JIONI PALE MABEMBEANI,WOTE MNATAKIWA KUFIKA BILA KUKOSA ILI KUWEZA KUFANIKISHA MIPANGO YA MAZISHI. KWA WALE WOTE WALIO NJE YA NAPOLI TUNAOMBA MICHANGO YENU KWA ILI TUWEZE KUFANIKISHA MIPANGO YA MAZISHI HARAKA NA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI TANZANIA.


KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA KUWAKILISHA MCHANGO WAKO PIGA SIMU YA OFISI YA JUMUIYA

+39 081 3340635

FAX + 081 3340624



Marehemu amecha watoto wawili huko Tanzania.


REST IN PEACE LONGA!


PICHA ZA AJALI NAMAELEZO ZAIDI YAPO KATIKA BLOG YETU www.tnzncommunity.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2008

    INNALILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN
    M/MUNGU aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi amin.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2008

    inna lillahi wainna ilahii rajiuun,
    salum longa mshikaji wangu wa migo migo, mtoto wa magomeni kondoa. haya jamani tuliobaki tuna pumua juu ya ardhi huu ni ukumbusho tosha kwamba any time Allah atatuita, so get yourself prepared, kuwa na uhusiano mzuri na Allah na viumbe vyake hapa suniani then you will be fine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2008

    poleni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...